PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Nawasalimu kwa jina la JMT
Nimekaa nikawaza, kumbe kupitia mitandao ya simu Kama vile Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel, nk inaweza ikachochea maendeleo ya moja kwa moja kwa wateja wake bila shuruti, hii inawezekana kupitia mfumo TOZO Kama ilivyoanzishwa na serikali.
Tunajua kwamba, vijana wengi sana wakitanzania wamekuwa na changamoto ya mitaji ya kuendesha shughuri zao ikiwemo ujasiliamali. Siyo tu vijana, kwa ujumla watanzania wengi wanategemea kuishi kwa kupanga, yaani nyumba za kulipia kwa Kila mwezi, hii haimaanishi wanapenda nikwasababu wameshindwa kuwekeza pesa kidogokidogo mpaka wapate hela inayotosha kununulia kiwanja.
Lakini pia utakubaliana nami kuwa, matumizi ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya mitandao na kuweka au kurushiwa vocha yamekuwa ni rahisi nayanafanyika kalibia Kila siku, maana yake, mtanzania anatumia pesa nyingi sana kwa matumizi ya miamala na vocha,.Sipo hapa kuzungumzia hasara ama faida ya kutumia mitandao ya simu kufanya miamala na wateja wake bali nimeguswa na mfumo wa TOZO uliobuniwa na serikali na sote tumejionea kwa namna gani serikali inavyovuna pesa kutoka kwa wananchi wake, sizungumzii ni maumivu gani wanayoyapitia wananchi ila naangazia namna ya kuligeuza hili wazo ili liwe na manufaa kwa mwananchi au mtumiaji wa mitandao ya simu Tanzania.
NAMNA YA MFUMO UNAVYOWEZA KUFANYIKA
- Mitandao ya simu iongeze option inayomtaka mteja kujisajili kwa hiali kuingia kwenye mfumo wa TOZO HURU ambao utaainisha vigezo na masharti ambayo mteja hana budi kukubaliana nayo au la, miongoni mwa masharti ambayo mteja anapaswa kukubaliana nayo au la, ni Kama ifuatavyo:-
VIGEZO NA MASHARTI VYA KUJIUNGA NA MFUMO WA TOZO HURU
Bandiko hili linaweza kufanyiwa marekebisho pale itakapoonekana kuna/ hakuna UMUHIMU kwa usalama wa fedha za mteje
- Mitandao ya simu itakaa na kuona namna nzuri zaidi ya kulifanyia wazo hili
- Tozo hizi zitakuwa nje na mfumo wa serikali hivyo Mitandao itatoa elimu kwa wateja wake juu ya faida ya mfumo huu
Ahsante

- Lazima laini ya mteja iwe imeunganishwa na mfumo wa kifedha za mitandao ie, MOBILE MONEY ACCOUNTS kama vile, AIRTEL MONEY, M-PESA, TIGO PESA, HALOPESA nk
- Mteja hataruhusiwa kujitoa isipokuwa mpaka atimize mwaka mzima baada ya kujiunga na kutoa kiasi alichowahi kuweka kwa kutozwa kupia mfumo wa TOZO HURU
- Mteja atawasilisha namba 2 mpaka 3 za watu wa karibu ili baada ya mwaka mzima ikitokea mteja kufariki, basi watu hawa waweze kuifahamisha mitandao husika na kuweza kumlipa mteja wao stahiki zake zote
- baada ya mteja kuridhika na masharti yatakayopendekezwa( yataboreshwa zaidi) mfumo wa TOZO HURU uwe sawa sawiya na ule wa SERIKALI au tofauti kidogo( Kama pendekezo hili linavyoweza kufanyiwa uboreshaji)
- Mteja atakatwa pesa Kila awekapo ama kutoa pesa, ama anunuapo vocha.
- Kama mteja atakuwa na desturi ya kuweka, kutoa pesa, kununua vocha mara kwa mara, atakuwa na uwezo wa kuwekeza kiasi kingi cha pesa bila ya yeye kuumia zaidi.
- kuna uwezekano mkubwa wa mteja kutimiza mwaka au miaka 2 akawa na mtaji mzuri au fedha ya kununulia kiwanja pasipo kutumia nguvu kubwa
- Mteja hatoumia na makato maana yake mfumo utakuwa huru na ataona kiasi anachokatwa na kutunziwa Kila anapohitaj kujua kwa kuomba option ya kuangalia akiba ya TOZO HURU hii itampa bidii mteja katika kufanya miamala kwa njia ya mitandao.

Upvote
1