Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Mpaka sasa motandao ya Youtube, TikTok na Signal imeliwa kichwa, haipatikani mpaka utumie VPN, yote hii ikiwa ni kuzuia wananchi kupata taarifa wakati muhimu kabisa wa uchaguzi ambao wananchi wana haki na wanastahili kupata taarifa kujua kinachoendelea katika siku muhimu inayoenda kuamua hatma ya Watanzania.
Hata baada ya kumwaga askari katika maeneo mengi ya Dar na kutuambia karibu kila dakika hali ni shwari bado wamechukua hatua hii mbaya ya kuzima mitandao! Wanatka kuficha nini?
Wanataka dunia isijue udhalimu unaoendelea nchini? Mpaka unafikia kufanya haya ni dhahiri kuwa hakuna anayekutaka, badala ya kutumia nguvu kubwa hivi si bora urudi zako nyumbani kucheza na wajukuu, maana hata ufanye nini mwisho wa siku utaanguka tu! Hakuna majibu mengine, labda uturoge Tanzania wote tukupende, vinginevyo hutoboi!