GE2025 Mitandao ya YouTube, TikTok na Signal imeliwa kichwa kama X na Telegram. Facebook, Instagram na WhatsApp kufuatia?
Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu,

Mpaka sasa motandao ya Youtube, TikTok na Signal imeliwa kichwa, haipatikani mpaka utumie VPN, yote hii ikiwa ni kuzuia wananchi kupata taarifa wakati muhimu kabisa wa uchaguzi ambao wananchi wana haki na wanastahili kupata taarifa kujua kinachoendelea katika siku muhimu inayoenda kuamua hatma ya Watanzania.

Hata baada ya kumwaga askari katika maeneo mengi ya Dar na kutuambia karibu kila dakika hali ni shwari bado wamechukua hatua hii mbaya ya kuzima mitandao! Wanatka kuficha nini?

Wanataka dunia isijue udhalimu unaoendelea nchini? Mpaka unafikia kufanya haya ni dhahiri kuwa hakuna anayekutaka, badala ya kutumia nguvu kubwa hivi si bora urudi zako nyumbani kucheza na wajukuu, maana hata ufanye nini mwisho wa siku utaanguka tu! Hakuna majibu mengine, labda uturoge Tanzania wote tukupende, vinginevyo hutoboi!:BearLaugh::BearLaugh::BearLaugh:
Kaandamane mbwa wewe kwani hiyo mitandao mnaandamana nayo?
 
Naona Airtel wao wameamua kuzima kabisa. No Internet
 
Mwisho wao ndio umeeanza leo, wananchi leo wamejua kumbe inawekana
 
Back
Top Bottom