lord commander
Member
- Feb 2, 2024
- 23
- 104
Katika miaka kadhaa ambayo watanzania tumeizoea mitandao basi tunakutana na watu mbalimbali katika posts zao ama comments ambazo ukizisoma unaweza patwa na hasira kwa jinsi alivyoandika upuuzi.
1.Kuna hawa wanaoandika kuhusu siasa, kuunga mkono juhudi, kutukana wapinzani, kusifia mambo yasiyoeleweka. Sio lazima kujibizana nao.
2.Kuna hawa wadau wa michezo.
hapa kila mtu yupo na hisia zake, kuna watakaoanfika matusi, pumba, na kila aina ya upuuzi ili tu kujifurahisha kuhusu timu zao. Hapa ndio kabisa hakuna haja ya kujibu.
3.Mashabiki wa miziki.
Huwa nashangaa sana watu wanajibizana nini katika hili, watu wanaingia studio kufanya kazi zao za kujipatia riziki, lakini utakuta kuna watu mitandaoni wanatukana msanii husika kwamba eti "muda wako umeisha", "umechuja", na kauli nyingi kama hizo, tena hususani kwa hawa wadau wa vizazi vya diamond na alikiba. Hakuna haja ya kuwajibu.
Kitu ambacho wengi huwa tunakisahau tunapoingia mitandaoni ni kwamba huku tunakutana na watu wenye akili tofauti, ufahamu tofauti, umri tofauti, na hata watu waliokulia kwenye malezi tofauti, unaweza kumaliza nguvu zako ukaanza kujibizana na jitu ambalo hata mama yake mzazi lilimshinda kulielewa.
Anyway, TUJENGE TAIFA.