Changamoto zangu nyingi nazikabili mwenyewe na wanafamilia wangu kwasababu ya kwa uhalisia watanzania tulio wengi tu wanafiki, waongowaongo, matapeli, tuna roho mbaya sana, halafu tunafurahi mno! mwenzetu anapopata shida / taabu fulani.
Kwa mfano ; jirani yangu alikuwa na kazi yake nzuri tu ya kumuingizia kipato, nyumbani kwake akafungua biashara ya duka. Bahati mbaya yakatokea ya kutokea kazini akafukuzwa kazi, duka likayumba na kuporomoka hadi likafa. Baadhi ya watu walifurahia hali hiyo kwasababu eti mkewe alikuwa anaringa sana mambo yalipokuwa mazuri na sasa anakoma mambo yameenda kombo.
Sipendelei kuanika mambo yangu hadharani isipokuwa inapolazimu mno! kufanya hivo