Mitazamo hasi ya wanajamii mtandaoni na katika maisha halisi, huwasababisha wengine kutokuwa wakweli

Mitazamo hasi ya wanajamii mtandaoni na katika maisha halisi, huwasababisha wengine kutokuwa wakweli

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Baadhi ya wanajamii husababisha raia wenzao kushindwa kusema ukweli unaowahusu. Hii husababishwa na mtazamo hasi kutoka kwa jamii husika.

Utakuta kwa mfano mtu anapitia changamoto fulani na angependa kuizungumzia ili kupata msaada au kuwasaidia wengine kujifunza; mtu huyo itambidi atumie nafsi ya mtu nyingine ili mradi tu afiche uhalisia.

Endapo atasema wazi kuwa ni yeye ndiye anayepitia/aliyepitia changamoto hiyo basi inawezekana akatengwa na jamii au pengine kusemwa vibaya.

Hii si sawa. Jamii inapaswa kufahamu kwamba watu hupata matatizo. Hivyo mtu yeyote awe huru kujizungumzia pasipo kutumia nafsi ya mtu mwingine.
 
Changamoto zangu nyingi nazikabili mwenyewe na wanafamilia wangu kwasababu ya kwa uhalisia watanzania tulio wengi tu wanafiki, waongowaongo, matapeli, tuna roho mbaya sana, halafu tunafurahi mno! mwenzetu anapopata shida / taabu fulani.

Kwa mfano ; jirani yangu alikuwa na kazi yake nzuri tu ya kumuingizia kipato, nyumbani kwake akafungua biashara ya duka. Bahati mbaya yakatokea ya kutokea kazini akafukuzwa kazi, duka likayumba na kuporomoka hadi likafa. Baadhi ya watu walifurahia hali hiyo kwasababu eti mkewe alikuwa anaringa sana mambo yalipokuwa mazuri na sasa anakoma mambo yameenda kombo.

Sipendelei kuanika mambo yangu hadharani isipokuwa inapolazimu mno! kufanya hivo
 
Uko sahihi kabisa. Watu wengi hupenda kuombeana mabaya yakukute ukose wa kukusaidia.

Kuna mtu alifukuzwa kazi ndugu zake wakafurahi sana. Akawa analalamika maisha magumu. Kumbe alikuwa anasogeza tu muda, hela alikuwa nazo. Baadae akaanzisha miradi na kujenga maghorofa. Sasa hivi ndugu hawana la kusema.
 
Back
Top Bottom