Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Hili la mbunge kuangukia chama kingine na rais chama kingine ni jambo la kawaida kabisa! Binafsi, sikumpigia Lowassa kwa sababu ambazo tayari nilishazieleza hapa jamvini lakini hata hivyo ubunge na udiwani nilipigia upinzani! Kuna bro wangu yeye ni mtu wa kawaida kabisa... I hope unanielewa namaanisha nini! Yeye nilipomuhoji akasema wazi kwamba Urais amempigia Magufuri lakini ubunge na udiwani akampigia mtu wa UKAWA!

Tukirudi kwenye matokeo kwa ujumla hapa tusisahau kwamba CHADEMA walitumia nguvu kubwa sana kujijenga Kanda ya Ziwa na kwa kweli walifanikiwa. Ukichukua mikoa 4 ya kanda ya ziwa; Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga; watu ambao walijiandikisha walikuwa 3.8 million. Huu ni mtaji mkubwa sana kwa chama chochote. Hao watu 3.8 million ni sawa na waliojindikisha Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Manyara ambazo ndio nguzo za CHADEMA. Hata hivyo, Mbeya sio maeneo yote. Kwa bahati mbaya, kura za mikoa (hiyo 4) ambayo ni ngome ya CHADEMA zikawa dissolved na kura za ngome nyingine ya CHADEMA, yaani kutoka Kanda ya Ziwa ambao waliamua kumpigia kura mtu wa kwao! Kwahiyo investment ambayo CHADEMA waliifanya kwa miaka kadhaa ndani ya kanda ya ziwa ikapotea mara moja tu baada ya CCM kumpitisha mtu wa kanda ya ziwa. Kwa tabia za Kiafrika, ni ngumu sana watu waache kumpa kura za urais mtu wa kwao.

Ukiondoa hiyo mikoa 4, CHADEMA wangeweza kufurukuta tu Mara na kidogo Kagera lakini mikoa mingine yote ambayo ilibaki ilikuwa ni ngome ya CCM except for Dar es salaam at least kwa uchaguzi uliopita. Kwa bahati mbaya, kama unavyofahamu watu wa Dar es salaam kwa kujifanya wapo bize, nilipiga hesabu za haraka haraka na kukuta waliojitokeza kupiga kura ni around 55-57%!

Binafsi nilipokuja kuona kumbe Tabora, Tanga, Dodoma na Morogoro kwa ujumla wao wana wapiga kura wengi kuliko Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mbeya kwa ujumla wake tayari nikaona ugumu walionao UKAWA huku kanda ya ziwa ikiwa inatafuta nani wa kui-dissolve!

Hivyo basi, waliosaliti UKAWA ni watu wa kanda ya ziwa ambao waliamua kumpigia mtu wa kwao na Dar es salaam ambao hawakujitokeza kwa wingi!
Tathmini ya uchaguzi mwaka huu ni ngumu sana.

Sheria ya takwimu imefanya kazi , sheria ya mitandao imefanya kazi

Ni ngumu kwasababu hapo juu tumeuliza, je uchaguzi huu ulikuwa na integrity na credibility?

Kama hatuwezi kusema hayo yalikuwepo, tutawezaje kufanya tathmini ya uchaguzi kwa uhalisia?

Tunaweza kwenda kwa namba za NEC, namba zilizopatikana katika mazingira ya kushangaza kidogo.

Hivi tunaweza kuamini kuwa wilaya moja huko mikoani au jimbo moja linaweza kuleta matokeo kabla ya Ilala au Temeke?

Kwa hali ilivyo sasa, mtu wa kawaida kabisa anaweza kufanya mawasiliano na Tanzania nzima kwa muda mfupi sana.

Tumeona watu wakifanya organization za mambo haraka kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Sasa inapotokea tunapata matokeo reja reja halafu siku moja, nchi nzima ikaleta na kutangazwa inatia shaka na kuhoji kuna integrity na credibility?

Tumeona matokeo yakitangaza na kuwekwa hadharani, imekuwa ni haramu watu ku compile matokeo yale yale yaliyoko hadharani. Nini kinafichwa?

Kwa mfano, kuna taasisi zimeingiliwa na computer kuchuliwa, sasa hapo kuna nini hasa kinaogopwa.

Na yote hayo yanafanyika kwa kutumia sheria za takwimu na cybercrime

CCM walitangaza kupata takribani majimbo 188 kabla ya matokeo.

Leo tukiangalia hawakuwa mbali na ukweli. Je, wao waliwezaje kupata takwimu hizo na kuzitangaza kabla ya tume?

Na kwanini tume haikuchukua hatua dhidi ya waliovunja sheria za kutangaza matokeo? integrity na crefibility ipo wapi

Tumeshuhudia malalamiko kuhusu kura za wakala na matokeo halisi.

NEC haijatoka na ku clarify ukweli ni upi. Je, hapo integrity na credibility ipo wapi?

NEC kikatiba inapaswa kuwasiliana na ZEC mara kwa mara. Tumesikia tamko la mwenyekiti wa ZEC.

Hatujasikia lololte au chochote kuhusu kauli ya NEC

Hii maana yake, yale mawasiliano ya mara kwa mara ya NEC na ZEC yalikuwepo kikatiba ni rahisi kwa baadhi ya wananchi kuhisi tamko la mwenyekiti wa ZEC lina 'baraka' kwa upande wa pili kwasababu hatujasikia kauli yoyote kutoka NEC

Haya yote yanafungwa katika mwamvuli moja wa uzembe wa Wapinzani.

Si kuwa walishindwa uchaguzi, wameshindwa kusimama na kuona uchaguzi unafanyika katika mazingira huru na ya haki

Hapo juu tumeonyesha kifungu cha katiba kinachosema, Rais ndiye atakayeteau tume ya uchaguzi.

Kumbuka Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ndiye anayeteua tume.

Halafu kifungu hicho kinaendelea kusema, mjumbe wa tume ataondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo tabia mbaya

Tabia mbaya ni ipi, haikuanishwa. Kwamba, mtu au watu wanaweza kusema tu, huyu bwana ana tabia mbaya kwasababu hakubaliani na maywka yao.

Hata watoto wetu wanapokuwa hawakubaliani na kile wazazi wanachosema, kwa kawaida hupakwa jina la tabia mbaya ili kuhalalisha adhabu

Kosa kubwa la wapinzani si uchaguzi, ni kwenda katika uchaguzi wakijua wazi uwanja una mabonde na goli lao ni pana.

Kuna integrity na credibility ?

Hatusemi kuna aliyepaswa kushinda au kushindwa, tunachouliza, je uchaguzi wetu una integrity na credibility?

Haya ya wapinzani waliyataka. Maandalizi ya sheria za haraka haraka waliyaona.

Kilichopaswa kwao ilikuwa kutoendelea na uchaguzi. Na mwaka huu walikuwa na public support, wakaiacha fursa hiyo

Hata hivyo, kwa hali ilivyo ni ngumu sana kufanya tathmini. Hatuna habari nyingine isipokuwa zile za NEC

Tathmini itakuwa ni ya NEC, Sasa tukikubaliana kuwa takwimu za NEC ndizo pekee, na kwa mujibu wa sheria ndivyo ilivyo, hatuna sababu za tathmini kubwa.

Swali je tutakuwa tumezitendea akili zetu haki?
 
Kuna gazeti la Tanzania nimelisoma jana (silikumbuki ni lipi) ambalo linazungumzia Kahama (wilaya) kuwa ndipo Uraisi ulifahamika. Kwa mujibu wa gazeti hili, Magufuli alipiga kura Jumapili akiwa nyumbani kwake Chato. Kesho yake akisafiri kwa barabara, msafara wake ulifika Kahama na mahitaji ya kuchimba dawa yakatokea. Waliposimama hapo Kahama, ilikuwa Jumatatu Oktoba 26 mida ya saa nne asubuhi.

Walipoondoka Chato, Magufuli alikuwa amekaa mbele na dereva kama kawaida. Walipokuwa wamesiama Kahama saa nne asubuhi, mfumo na mchakato wa msafara na usalama ukabadilika. Watu wa Usalama wakashika hatamu, Magufuli akahamia kiti cha nyuma, gari yake badala ya kuwa gari la mbele, ikawa gari la tatu katika msafara na kukawa na nyongeza ya magari ya usalama na ulinzi wake.

Protocol nzima ilibadilika walipofika Kahama na status ya Magufuli ilibadilika kutoka kuwa Mgombea na kuwa Mteule huku bado kura zikiwa zinahesabiwa, kujumuishwa na kukusanywa.

Je ni nani alikuwa na majibu yote ya Urais jumatatu ya Oktoba 26 saa nne asubuhi? ikiwa NEC na Lubuva jumatatu hiyo walitangaza majimbo 11 mengi yakiwa ya Zanzibar, kwa nini Protocol ilibadilishwa ghafla saa nne asubuhi na Matokeo rasmi yalianza kutangazwa tarkibani kuelekea jioni ya Jumatatu Oktoba 26?

Tuchemshe Bongo!
 
Come on Rev.

Let's keep it 100 here.

Was the outcome ever in doubt?

Mimi sikuwa na shaka lolote kwamba NEC ya CCM eti somehow ingeweza kumtangaza mgombea asiye wa CCM kuwa ndo mshindi.

Na kamwe haitotokea hiyo NEC ije imtangaze mgombea asiye wa CCM kuwa ndo mshindi.

Tanzania kiuhalisia hatuna demokrasia ya vyama vingi.

Tuna maigizo tu ya demokrasia ya vyama vingi [ambayo mimi naiita ni demokrasia ya chama kimoja].
 
Hiki ni sawa na ile Ze Comedy nyingine ambapo Rais JK alioenekana kumpongeza Mteule na picha zikapigwa nyingi!

Rev Nape aliposema CCM itashinda kwa goli la mkono alimaanisha hivyo.

Tena aliposema NEC ilikaa kimyaa! haikuwahi kumkemea

Kama alivyosema Nyani Ngabu , yaani kilichofanyika ilikuwa ni dhihaka

Wananchi wana resentment, unaweza kuona nchi haina raha, hakuna ile felicity

Jambo kubwa ambalo wapinzani wanatakiwa kuanza nalo ni katiba. Kwasasa wana support kubwa sana ya umma

Kazi ya Wapinzani ni ku kuunganisha nguvu za umma kudai katiba kwanza. Hilo ndilo wanatakiwa kulipa kipaumbele

Na wananchi waache kuhuzunika au kulalamika. Wasimame kudai katiba yao si ile ya CCM, wadai yao inayokidhi matakwa yao.

Wasidanganywa na hizi habari za kufukuza kazi watu hazina majibu kwa matatizo yetu.

Kwa mfano, walikuwa ndani ya baraza la mwaziri lililoidhinisha ununuzi wa magari kwa mamia.

Hawakuwahi kuuliza Muhimbili wanalala vipi, leo anaonekana shujaa kumfukuza mkurugenzi.

Hayo yote ni kutaka kusahauslisha wananchi machungu waliyo nayo kutokana na uchaguzi.

Wananchi hawatakiwi kushangilia CT scan mbili, wanatakiwa washangilie mfumo utakaohakikisha hadi wilayani zipo na zinafanya kazi.

Mkurugenzi wa Muhimbili hajawa tatizo la X-Ray Wilayani.

Hizi zote ni kutuondoa katika kuhoji demokrasia na bao la Nape, kutuondoa katika hoja za kutaka katiba yetu.

Tupate katiba yetu si ile aliyoshiriki kuiandika Dodoma Mheshimiwa akiwa sehemu ya BMLK na serikali na CCM, tunataka ya wananchi.

Si wakati wa kulishwa peremende, tunataka katiba

Mkurugenzi wa Muhimbili si tatizo, tatizo ni mfumo tena ule ule waliutumikia miaka mingi wakiwa sehemu yake

Ubovu wa Muhimbili ulifanywa na serikali , walikuwa sehemu ya serikali miaka 20, nini wasichokijua kuhusu Muhimbili?

Anasimamisha safari za nje, wakati alikuwa sehemu ya mfumo huo huo tena kumwagia sifa kwa kazi nzuri.

Hatuhitaji political stunt tunataka mfumo ubadilike ili tuwe na mamlaka ya wananchi, kuendesha na kuchagua viongozi.

Wananchi kuwawajibisha viongozi na kuamua hatma ya taifa lao. Hatma ya taifa inahitaji fikra si Bao la mkono

Tatizo si haya tunayojiuliza, ni mfumo mzima usioweza kuwajibisha wananchi na viongozi

Mfumo usio na majibu ya matatizo yetu, na hapo ndipo pa kuanzia. Kubadili mfumo kwanza, haya ya MRI yatafuata
 
Come on Rev.

Let's keep it 100 here.

Was the outcome ever in doubt?

Mimi sikuwa na shaka lolote kwamba NEC ya CCM eti somehow ingeweza kumtangaza mgombea asiye wa CCM kuwa ndo mshindi.

Na kamwe haitotokea hiyo NEC ije imtangaze mgombea asiye wa CCM kuwa ndo mshindi.

Tanzania kiuhalisia hatuna demokrasia ya vyama vingi.

Tuna maigizo tu ya demokrasia ya vyama vingi [ambayo mimi naiita ni demokrasia ya chama kimoja].

right on!
 
Hivi kuna ulazima wa kupiga kura kila baada ya miaka 5??

upinzani ukigomea kupiga kura, tatizo litakuwa ni nini?

kwa nini upinzani hauchukui hatua ya kukataa uchaguzi wowote mpaka TUME IWE HURU?? hivi akili zenu/zetu za kufikiri kuna jambo jipya inatokea wapi?

Hivi elimu zetu zinasaidia nini hapa? KAMA MIAKA 5 IKIFIKA UCHAGUZI UKAGOMEWA ACHA DUNIA IJUE KUWA NI UCHAGUZI WA CCM WENYEWE KWA WENYEWE...kama tume siyo huru, mnataka nini?

Ndio maana vita yangu, mawazo yangu,nguvu zangu,akili zangu, na hasira zanguhuwa ninazipeleka kwa wapinzani.....! HAWAKO strong enough, hawana logic? KWA NINI umpe mwananchi FALSE HOPE kuwa eti kuna uwezekano wa kuingia ikulu?? kwa hii tume huru?

Hao akina mbowe kweli wako serious kuingia ikulu? kwa TUME hii hii?

KUBADILI tume haihitaji katiba yote ibadilishwe, ni marekebisho ya katiba, MUUNDO NA MFUMO WA TUME SIYO MSAAFU UNABADILISHIKA!

atoke mwanasias mmoja jasiri, aweke proposal ya katiba apeleke mjadala bungeni!!!

wengine huwa tunashawishika kusema kuwa wapinzani ni WAPIGAJI HELA TU,huwezi kuwa mbumbumbu au mjinga kiasi gani kujua kuwa urais hautakuja kuwa wa upinzani kwa TUME HII

2010 slaa alilalamika, 2015 EL analalamika

fun enough akina EL, Sumaye na kingunge wanajua kila kitu na siri zote za ushindi wa CCM

CCM wamejisafisha sana na kupumbaza ulimwengu

ATOKE MTU ANAYEJIITA ANA AKILI TIMAMU ASEME NAMNA YA KUINGIA IKULU UPINZANI

huwa ninasemaga muwe genuine!!! utumbo wa upinzani mnaufumbia macho,kama na sawa kabisa na wale wa CCM

huku mnataka kujadili tathmini ya uchaguzi

hii aibu ya kuwa na logic mfu kama hizi tutaiweka au tunaiweka wapi?? where is our logic of great thinking??

kweli mtu na akili zako unaweka hope ye EL kushinda?? that was totally unafair kuwadanganya watanzania kiasi kile

Nguruvi ebu amkeni wakuu, taifa tunalipeleka pabaya kwa kutokuwa wakweli katika vitu ambavyo vinahitaji ukweli??

kwa nini mahaba, mapenzi, hisia na wishful thinking vinatuongoza??

ukisoma comment ya Nyanu Ngabu haina chenga; kama kuna mtu aliwaza kinyume na hapo hana uhalisia na HANA AKILI TIMAMU

comment kama hizi tumezitoa 2011, tunazitoa 2015...NA 2020 UPINZANI huu mnaouona una maana na unataka mabadiliko utaingia tena kwenye uchaguzi na tume ile ile; AKILI AU MATOPE??

samahani
 
Waberoya

Nadhani upo hapa siku nyingi. Hakika hakuna kipya wala hakuna aliyetarajia jipya kwa sisi wengine

Kama utakumbuka, tuliwapigia sana kelele walipokwenda Ikulu na nyuzi zipo zaidi ya 100.

Tukawaambia juisi za maembe na mengine siyo muhimu kama wao kutaka mfumo ubadilike

Bandiko 42 hapo kuna mahali tumesema hivi '' Haya yote yanafungwa katika mwamvuli mmoja wa uzembe wa wapinzani''

Kabla ya uchaguzi, tuliwaambi wazi uchaguzi wetu haupo katika kura , tulisema ''Uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura''

Nakubaliana nawe kabisa na wengi watakubaliana nasi kuwa upinzani una uzembe. Hili halikuhitaji diploma kulitambua

Tena umeongezea jambo moja muhimu. Hawa waliokuwa CCM wanajua mbinu.

Wanajua kuwa haitatoke ikatangazwa tofauti na inavyotakiwa iwe.

Nape aliwaambia ukweli, hata goli la mkono lazima. Bulembe akasema Ikulu 'Ngo'

Na yote hayo yalisikika na tume, haikufanya lolote kwasababu inajua ukweli

Sasa kuna pande kadhaa kuhusu hili suala

1. Wapinzani watamke wazi kuwa hawataenda katika uchaguzi mkuu mwingine na katiba au tume iliyopo

2. Kuna umuhimu wa wapinzani kubadili uongozi. Watu wale wale waliofanya yale yale kwa miaka 20 hawawezi kuja na jambo jipya isipokuwa marudio. Na kwa hili wapinzani wabadili uongozi mzima wa Upinzani bungeni

3. Hoja ya kwanza wanaotakiwa kusimama nayo ni kubadili mfumo. Wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote
Umma unaona na kuwaunga mkono. Hii ni fursa isiyotakiwa kupotezwa kama ilivyokuwa nyuma

4. Sisi wananchi tuna shea yetu. Tunadhani hili ni suala la wapinzani tu.
Tumesahau kuwa ni suala letu.Leo tunaona ubabaishaji, kwamba watu wale wale waliokuwa katika mfumo ulele na wakishirika kufanya yale yale wanaonekana wanakuja na mapya. Kwamba, wamekuwa malaika usiku mmoja tu!

Hakuna anayeomba radhi kwa madhila ya nyuma kwasababu wote ni sehemu ya mfumo ule ule.

Haiwezeakani wakaukana mfumo uliowafikisha hapo. Kama hatusimama na kutaka mabadiliko ya mifumo yetu tutabaki kuhuzunika na kulalamika.

Nguvu ya umma ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa mchakato. Kwa bahati mbaya sana, wapinzani hawakuwa na maono licha ya tahadhari zote tulizowapa.

Na sisi wananchi tukaridhika kudanganywa na mchakato tukijua haukuwa na udhibiti wetu.

Leo wamekaa wanataka kurudisha katiba ile ile iliyoandikwa na CCM

Watafanikiwa kwasababu hatukuwauliza wakati wanapita katika mikutano yao.

Walikaa kimya wakisubiri wapewe 'rungu' waaanze kufanya yao.

Tukiendelea kukaa kimya wataendelea kutupumbaza. Tuwaambie wazi hatuhitaji mabadiliko ya sura za wakurugenzi.

Tunahitaji mabadiliko ya mfumo mzima wa kujitawala.

Mfumo utakaotupa sisi sauti zaidi ya kujiendesha kama taifa na si kikundi cha watu au mtu

Hatuhitaji 'one man show' tunahitaji mass participation. Tumeishi na one man show na kubaki taifa la omba omba.

Sasa si wakati wake, ni wakati wa sisi kutaka mabadiliko ya mifumo yetu mibovu

Tunaona mifumo mibovu inavyotuletea matatizo.

Wiki ijato bunge la JMT linaanza kukiwa hakuna wajumbe wa BLW znz.

Hawapo ndani ya bunge lakini tunaambiwa ni la JMT. Tunaambiwa mfumo ni kamili

Leo tunaona NEC na ZEC zikiwa vyombo viwili tiofauti kabisa. Katiba inatuelekeza ni vyombo vinavyofanya kazi kwa ushirikiano. Uhalisia umetimia tunaona yale ya katiba ni maandishi tu kumbe nchi inaongozwa tofauti

Tumeambiwa Rais wa JMT ndiye mkuuwa taifa la Tanzania.

Tunaona Rais akiwa kama mtazamaji wakati sehemu ya nchi ikiwa na tatizo.

Tumeona nguvu moja ikifanya kazi kama taifa kwamba, nguvu za nchi zipo kwa mtu na si timu au watu

Haya yote tunapaswa kuyaona kama matatizo. Hayo ya MRI ni matokeo ya kuwa na mfumo mbovu

Sasa wapo wenye platform, na wapo wenye sauti, wakasimama na kusema hapana au ndiyo sauti yao itafika nyikani.

Itasikika kwa mfalme aliye juu akiangalia nyika kwa chini. Mfalme atatupa haki za kufikiri, kupanga na kuchagua, si kwasababu anataka bali mfumo utamlazimisha. Huko ndiko tunakotaka kwenda si sura za Wakurugenzi
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna ulazima wa kupiga kura kila baada ya miaka 5??

Kwa mazingira ya sasa mimi binafsi sioni kabisa ulazima uliopo. Ni bora mara mia hizo hela zinazotumika kwenye hayo maigizo yanayoitwa 'uchaguzi' zikatumika kununulia mashine za CT-Scan na MRI kwenye hospitali zote za serikali.

upinzani ukigomea kupiga kura, tatizo litakuwa ni nini?

Ni kama ulikuwepo kichwani mwangu. Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiwaza kwamba, ingekuwa ni juu yangu mimi basi hakuna chama cha upinzani ambacho kingeshiriki hayo maigizo.

Mahesabu yangu ni kwamba, kutokushiriki kwao kungeondoa au kupunguza uhalali wa 'ushindi' wa CCM na kuwa moja ya shinikizo la kuleta katiba mpya ambayo itaweka mazingira sawa kwa washindani wote katika chaguzi zijazo.

kwa nini upinzani hauchukui hatua ya kukataa uchaguzi wowote mpaka TUME IWE HURU?? hivi akili zenu/zetu za kufikiri kuna jambo jipya inatokea wapi?

Daah Wabe utadhani uliwahi kuwepo sehemu ambayo nilikuwa nimekaa na washikaji nikiwapa hilo darasa la wapinzani kususia kushiriki hizi chaguzi chini ya mazingira sasa.

Ulichoandika ndicho mimi nimekuwa nikijaribu kuwaelimisha watu hususan nje ya hapa JF. Lakini nikiri pia kuwa ni wachache mno ambao hunielewa. Hapo ndo unapata taswira ya jinsi watu wengi walivyo kifikra.

Hivi elimu zetu zinasaidia nini hapa? KAMA MIAKA 5 IKIFIKA UCHAGUZI UKAGOMEWA ACHA DUNIA IJUE KUWA NI UCHAGUZI WA CCM WENYEWE KWA WENYEWE...kama tume siyo huru, mnataka nini?

Exactly! Uchaguzi ukisusiwa hata uhalali wa CCM utakuwa wa mashaka. Sijui kwa nini tu watu hawalioni hilo.

Kwa sababu, mara tu unapokubali kushiriki kwenye uchaguzi ambao unajua kabisa 'the odds are stacked against you' kwa sababu ya mazingira mabovu, maana yake ni kwamba umekubali kushiriki mchezo chini ya sheria 'mbovu' zilizopo.

Sasa kwa nini ufanye hivyo? Huo nao ni uwendawazimu tu. Ingekuwa juu yangu ningegomea mpaka pale tutakapokuwa na mazingira mazuri na yasiyompa 'undue advantage' mshiriki yeyote yule.

Ndio maana vita yangu, mawazo yangu,nguvu zangu,akili zangu, na hasira zanguhuwa ninazipeleka kwa wapinzani.....! HAWAKO strong enough, hawana logic? KWA NINI umpe mwananchi FALSE HOPE kuwa eti kuna uwezekano wa kuingia ikulu?? kwa hii tume huru?

Nakubaliana nawe mia kwa mia. Vyama vya upinzani navyo vinastahili kabisa lawama kwa kubariki na kukubali katika chaguzi za kilaghai.

Hao akina mbowe kweli wako serious kuingia ikulu? kwa TUME hii hii?

Wanacheza hao. Hivi hujagundua tu kwa nini CCM haina sana shauku ya kutaka katiba mpya na kupata tume huru ya uchaguzi?

KUBADILI tume haihitaji katiba yote ibadilishwe, ni marekebisho ya katiba, MUUNDO NA MFUMO WA TUME SIYO MSAAFU UNABADILISHIKA!

Naam, hilo ni kweli. Lakini pia haitokuwa vyema kuwa na tume huru halafu itokee chama kingine kishinde uchaguzi halafu nacho kiendelee kutawala kwa kutumia katiba hii hii ya hovyo tuliyo nayo.

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi are way long overdue. Hivi vilitakiwa viwe ndo vitu vya kwanza kabisa kufanywa pindi tulipoamua kuingia kwenye siasa za vyama vingi.

Na kusema ukweli hata tume ya Nyalali ilipendekeza hivyo lakini CCM kwa kutumia ujinga wa walio wengi kwa manufaa yao, wakaliepuka kabisa hilo suala na sasa tunaona jinsi wanavyonufaika kwa kutokuwa na katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi.

Nikupe tu mfano wa Afrika Kusini. Baada ya kuamua kuondokana na utawala kibaguzi, waliandika katiba ya wakaa [interim constitution] ambayo ilitumika katika kipindi cha mpito na baada ya uchaguzi wa 1994 wakaandika katiba mpya kwa kuwashirikisha wananchi wote.

Hiyo katiba iliidhinishwa na mahakama ya katiba mnamo tarehe 4 Disemba 1996 na ikasainiwa na rais Mandela tarehe 10 Disemba mwaka huo huo na ikaanza kutumika tarehe 4 Februari 1997.

Katiba ya Afrika Kusini inakubalika kuwa ndo moja ya katiba bora kabisa duniani.

Sasa hebu fikiria kwa mfano ANC wangeendelea kutawala kwa kutumia ile katiba ya zamani ya Makaburu na labda kwa kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale.

Hivi unadhani kungekalika huko?

Ndo maana huwa nasema kwamba na sisi tulitakiwa kuanza huu mfumo wa vyama vingi na katiba mpya kabisa ambayo ingepunguza madaraka ya rais na ambayo ingeunda taasisi huru kama vile tume huru ya uchaguzi na kadhalika.

Tungekuwa tumefanya hivyo pengine labda kusingehitajika rais kuvamia vamia maofisi kukagua utendaji wa kazi.

atoke mwanasias mmoja jasiri, aweke proposal ya katiba apeleke mjadala bungeni!!!

Na afanye hivyo kwa dhati kabisa na si kwa sababu ya kutafuta kiki tu.

wengine huwa tunashawishika kusema kuwa wapinzani ni WAPIGAJI HELA TU,huwezi kuwa mbumbumbu au mjinga kiasi gani kujua kuwa urais hautakuja kuwa wa upinzani kwa TUME HII

2010 slaa alilalamika, 2015 EL analalamika

fun enough akina EL, Sumaye na kingunge wanajua kila kitu na siri zote za ushindi wa CCM

CCM wamejisafisha sana na kupumbaza ulimwengu

ATOKE MTU ANAYEJIITA ANA AKILI TIMAMU ASEME NAMNA YA KUINGIA IKULU UPINZANI

huwa ninasemaga muwe genuine!!! utumbo wa upinzani mnaufumbia macho,kama na sawa kabisa na wale wa CCM

huku mnataka kujadili tathmini ya uchaguzi

hii aibu ya kuwa na logic mfu kama hizi tutaiweka au tunaiweka wapi?? where is our logic of great thinking??

kweli mtu na akili zako unaweka hope ye EL kushinda?? that was totally unafair kuwadanganya watanzania kiasi kile

Nguruvi ebu amkeni wakuu, taifa tunalipeleka pabaya kwa kutokuwa wakweli katika vitu ambavyo vinahitaji ukweli??

kwa nini mahaba, mapenzi, hisia na wishful thinking vinatuongoza??

ukisoma comment ya Nyanu Ngabu haina chenga; kama kuna mtu aliwaza kinyume na hapo hana uhalisia na HANA AKILI TIMAMU

comment kama hizi tumezitoa 2011, tunazitoa 2015...NA 2020 UPINZANI huu mnaouona una maana na unataka mabadiliko utaingia tena kwenye uchaguzi na tume ile ile; AKILI AU MATOPE??

samahani

Mimi nimeshasema kamwe wapinzani hawataiona ikulu kwa kadri tume ya uchaguzi itakavyoendelea kuundwa na CCM.

I mean, it's a joke. Mwenyekiti wa CCM ambaye ndo rais anaunda tume ya taifa ya uchaguzi ambayo kazi yake kuu ni kuratibu, kuendesha, na kusimamia shughuli za uchaguzi ambazo CCM nayo inashiriki.

Mbona mgongano wa kimaslahi ni dhahiri kabisa hapo?

So why even bother taking part in such elections?

Foolishness.
 
Ile siku Rais mteule alipomtemblea Rais Ikulu niliangua kicheko sana. Nilicheka sana

Mwnyekiti wa CCM ambaye alikuwa kwenye kampeni na mgombea wa CCM, wamekutana Ikulu si kama CCM bali Rais Mteule na Rais wa nchi. Kwamba, muda tu ndio unabadilisha nyadhifa zao.

Halafu mwenyekiti wa CCM aliyekuwa ana kampeni kwa mgombea wa CCM ndiye Rais anayeteua tume ya uchaguzi na amepewa nguvu za kikatiba kumuondoa mjumbe wa tume kama ana tabia mbaya

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anatoa maombi ya fedha za kazi za uchaguzi kwa mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wakati wowote hata akiwa kwenye kampeni.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anaomba resources kama ulinzi n.k. kutoka kwa m/kiti wa CCM ambaye ni Rais na Amir jeshi mkuu popote alipo hata kama yupo kwenye kampeni za CCM.

Wapinzania wanategemea m/kiti- CCM a.ka. Rais mwenye upendo, huruma na maadili meema atakayeganisha kazi za Chama na Urais.

Wanategemea m/kiti wa tume awe huru kabisa ingawa resources zake zinatolewa kwa idhini ya mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais

Miaka 20 wametegemea ujio wa malaika atakayeweza kusimamia uchaguzi. Leo wakiangalia nyuma hawajagundua tatizo

Mabadiliko hayaletwi na vyama, yanasukumwa na wananchi kwa vyama, yaanze na mmoja mmoja, kwa wingi na kwa umoja.

Hatuwezi kutegemea CCM waliopata taabu sana mwaka huu wakubali dhiki nyingine miaka 5 ijayo.

Waatengeneza sheria za 'voda fasta' kama ya takwimu na cyber crime wafanye surprise suprise!

Tuache hadithi nyingine zote za sura za wakurugenzi, spea za VX, NOAH, MRI na chaki za shule.

Tusimame mfumo huo ufike mwisho. Pakuanzia ni hapo tuliposema

Wapinzani, hakuna hoja nyingine mnayotakiwa kuzungumzia isipokuwa mabadiliko ya mfumo, na uchaguzi ni mwisho hadi mabadiliko

Wapinzani, miaka 20 kwa watu wale wale wanaosubiri malaika waje kutusaidia umetosha, sasa apatikane kiongozi na timu ya Upinzania bungeni (KUB) na timu mpya itakayokuja na mwelekeo mpya. Waliodumuza na kuwaomba wakae pembeni. Tuanzie hapo

Halafu si kuchagua tuwaachie tu kazi, nasi pia tuseme huu ni wakati wa kutengeneza mfumo, si kupita garage kuangalia difu za magari ,welding machine, Microscope, wala Chaki ni nyeupe kama zinafanya kazi

Ni wakati wa kuanza kutengeneza mfumo ambao Mkurugenzi atawajibika bila kumuona mtu.Utawala wa wananchi si wa mtU/ watu.

Mtu au watu wawe wasimamie wananchi wanayotaka si wanayotaka wao.

Na pia wananchi waache uzezeta , kushangilia tu bila kujua kwanini.

Hivi kazi ya fundi gari si kuhakikisha ana spea na welding machine. Leo akinunua mpya hilo ni tukio kweli! Hilo ni la kushangilia
 
Kwa mazingira ya sasa mimi binafsi sioni kabisa ulazima uliopo. Ni bora mara mia hizo hela zinazotumika kwenye hayo maigizo yanayoitwa 'uchaguzi' zikatumika kununulia mashine za CT-Scan na MRI kwenye hospitali zote za serikali.

Ni kama ulikuwepo kichwani mwangu. Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiwaza kwamba, ingekuwa ni juu yangu mimi basi hakuna chama cha upinzani ambacho kingeshiriki hayo maigizo.

Mahesabu yangu ni kwamba, kutokushiriki kwao kungeondoa au kupunguza uhalali wa 'ushindi' wa CCM na kuwa moja ya shinikizo la kuleta katiba mpya ambayo itaweka mazingira sawa kwa washindani wote katika chaguzi zijazo.

Daah Wabe utadhani uliwahi kuwepo sehemu ambayo nilikuwa nimekaa na washikaji nikiwapa hilo darasa la wapinzani kususia kushiriki hizi chaguzi chini ya mazingira sasa.

Ulichoandika ndicho mimi nimekuwa nikijaribu kuwaelimisha watu hususan nje ya hapa JF. Lakini nikiri pia kuwa ni wachache mno ambao hunielewa. Hapo ndo unapata taswira ya jinsi watu wengi walivyo kifikra.

Exactly! Uchaguzi ukisusiwa hata uhalali wa CCM utakuwa wa mashaka. Sijui kwa nini tu watu hawalioni hilo.

Kwa sababu, mara tu unapokubali kushiriki kwenye uchaguzi ambao unajua kabisa 'the odds are stacked against you' kwa sababu ya mazingira mabovu, maana yake ni kwamba umekubali kushiriki mchezo chini ya sheria 'mbovu' zilizopo.

Sasa kwa nini ufanye hivyo? Huo nao ni uwendawazimu tu. Ingekuwa juu yangu ningegomea mpaka pale tutakapokuwa na mazingira mazuri na yasiyompa 'undue advantage' mshiriki yeyote yule.

Nakubaliana nawe mia kwa mia. Vyama vya upinzani navyo vinastahili kabisa lawama kwa kubariki na kukubali katika chaguzi za kilaghai.

Wanacheza hao. Hivi hujagundua tu kwa nini CCM haina sana shauku ya kutaka katiba mpya na kupata tume huru ya uchaguzi?

Naam, hilo ni kweli. Lakini pia haitokuwa vyema kuwa na tume huru halafu itokee chama kingine kishinde uchaguzi halafu nacho kiendelee kutawala kwa kutumia katiba hii hii ya hovyo tuliyo nayo.

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi are way long overdue. Hivi vilitakiwa viwe ndo vitu vya kwanza kabisa kufanywa pindi tulipoamua kuingia kwenye siasa za vyama vingi.

Na kusema ukweli hata tume ya Nyalali ilipendekeza hivyo lakini CCM kwa kutumia ujinga wa walio wengi kwa manufaa yao, wakaliepuka kabisa hilo suala na sasa tunaona jinsi wanavyonufaika kwa kutokuwa na katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi.

Nikupe tu mfano wa Afrika Kusini. Baada ya kuamua kuondokana na utawala kibaguzi, waliandika katiba ya wakaa [interim constitution] ambayo ilitumika katika kipindi cha mpito na baada ya uchaguzi wa 1994 wakaandika katiba mpya kwa kuwashirikisha wananchi wote.

Hiyo katiba iliidhinishwa na mahakama ya katiba mnamo tarehe 4 Disemba 1996 na ikasainiwa na rais Mandela tarehe 10 Disemba mwaka huo huo na ikaanza kutumika tarehe 4 Februari 1997.

Katiba ya Afrika Kusini inakubalika kuwa ndo moja ya katiba bora kabisa duniani.

Sasa hebu fikiria kwa mfano ANC wangeendelea kutawala kwa kutumia ile katiba ya zamani ya Makaburu na labda kwa kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale.

Hivi unadhani kungekalika huko?

Ndo maana huwa nasema kwamba na sisi tulitakiwa kuanza huu mfumo wa vyama vingi na katiba mpya kabisa ambayo ingepunguza madaraka ya rais na ambayo ingeunda taasisi huru kama vile tume huru ya uchaguzi na kadhalika.

Tungekuwa tumefanya hivyo pengine labda kusingehitajika rais kuvamia vamia maofisi kukagua utendaji wa kazi.

Na afanye hivyo kwa dhati kabisa na si kwa sababu ya kutafuta kiki tu.

Mimi nimeshasema kamwe wapinzani hawataiona ikulu kwa kadri tume ya uchaguzi itakavyoendelea kuundwa na CCM.

I mean, it's a joke. Mwenyekiti wa CCM ambaye ndo rais anaunda tume ya taifa ya uchaguzi ambayo kazi yake kuu ni kuratibu, kuendesha, na kusimamia shughuli za uchaguzi ambazo CCM nayo inashiriki.

Mbona mgongano wa kimaslahi ni dhahiri kabisa hapo?

So why even bother taking part in such elections?

Foolishness.

Asante NN

Kuna vitu vinauma sana, tunataka CCM itoke madarakani; we need strategy, hii mihemko,mishawasha au kupiga sana kelele kunakofanywa na mashabiki wa upinzani hakusaidii wala hakutusaidii sisi

Hela zilizotumika kwenye kampeni ya EL akafanikiwa kuvuna watu 6m, zingetumika kupigania tume huru...tungekuwa mbali; I mean kura 6m zimepotea tu bure, sana sana kuongeza wabunge wa viti maalumu ambao nao mmesikia matatizo yake

upinzani bado dhaifu, hauko serious; wao wanasiasa ni kazi zao full time kuyaona na kuyafikiria haya

Hoja ya tume huru iko wazi kabisa, itaeleweka kwa kila mwananchi, ina make sense, inajenga base au msingi wa taifa la demokrasia. hata wakisema waingie barabarani kuungwa mkono ni rahisi maana hoja inaeleweka wala haina complication

hawa wanasiasa wetu walipata muda wa kujadili katiba kwenye bunge la katiba; wakawa bize kujadili serikali mbili na serikali 3!!!

Kuna vitu unaogopa utatukana, ila umefika muda wapinzani wasilaumu wananchi.....wafanye jambo , tusiseme tu CCM watakataa; kwa pressure gani? Tanzania sio nchi ya CCM

Huwa nasema simba wakitaka kucheza na Yanga na wakawa hawana imani na refa.....simba wataomba TFF wabadili refa! Tume huru ni refa,

hata kama magufuli atafanya yote haya kuvuta au kutafutwa kupendwa, haibadilishi ukweli CCM inatakiwa kupumzika, they are just tired!, kuwaondoa tuweke miundo mbinu bora ya ushindani
 
Waberoya

Nadhani upo hapa siku nyingi. Hakika hakuna kipya wala hakuna aliyetarajia jipya kwa sisi wengine

Kama utakumbuka, tuliwapigia sana kelele walipokwenda Ikulu na nyuzi zipo zaidi ya 100.

Tukawaambia juisi za maembe na mengine siyo muhimu kama wao kutaka mfumo ubadilike

Bandiko 42 hapo kuna mahali tumesema hivi '' Haya yote yanafungwa katika mwamvuli mmoja wa uzembe wa wapinzani''

Kabla ya uchaguzi, tuliwaambi wazi uchaguzi wetu haupo katika kura , tulisema ''Uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura''

Nakubaliana nawe kabisa na wengi watakubaliana nasi kuwa upinzani una uzembe. Hili halikuhitaji diploma kulitambua

Tena umeongezea jambo moja muhimu. Hawa waliokuwa CCM wanajua mbinu.

Wanajua kuwa haitatoke ikatangazwa tofauti na inavyotakiwa iwe.

Nape aliwaambia ukweli, hata goli la mkono lazima. Bulembe akasema Ikulu 'Ngo'

Na yote hayo yalisikika na tume, haikufanya lolote kwasababu inajua ukweli

Sasa kuna pande kadhaa kuhusu hili suala

1. Wapinzani watamke wazi kuwa hawataenda katika uchaguzi mkuu mwingine na katiba au tume iliyopo

2. Kuna umuhimu wa wapinzani kubadili uongozi. Watu wale wale waliofanya yale yale kwa miaka 20 hawawezi kuja na jambo jipya isipokuwa marudio. Na kwa hili wapinzani wabadili uongozi mzima wa Upinzani bungeni

3. Hoja ya kwanza wanaotakiwa kusimama nayo ni kubadili mfumo. Wasikubali kuburuzwa kwa namna yoyote
Umma unaona na kuwaunga mkono. Hii ni fursa isiyotakiwa kupotezwa kama ilivyokuwa nyuma

4. Sisi wananchi tuna shea yetu. Tunadhani hili ni suala la wapinzani tu.
Tumesahau kuwa ni suala letu.Leo tunaona ubabaishaji, kwamba watu wale wale waliokuwa katika mfumo ulele na wakishirika kufanya yale yale wanaonekana wanakuja na mapya. Kwamba, wamekuwa malaika usiku mmoja tu!

Hakuna anayeomba radhi kwa madhila ya nyuma kwasababu wote ni sehemu ya mfumo ule ule.

Haiwezeakani wakaukana mfumo uliowafikisha hapo. Kama hatusimama na kutaka mabadiliko ya mifumo yetu tutabaki kuhuzunika na kulalamika.

Nguvu ya umma ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa mchakato. Kwa bahati mbaya sana, wapinzani hawakuwa na maono licha ya tahadhari zote tulizowapa.

Na sisi wananchi tukaridhika kudanganywa na mchakato tukijua haukuwa na udhibiti wetu.

Leo wamekaa wanataka kurudisha katiba ile ile iliyoandikwa na CCM

Watafanikiwa kwasababu hatukuwauliza wakati wanapita katika mikutano yao.

Walikaa kimya wakisubiri wapewe 'rungu' waaanze kufanya yao.

Tukiendelea kukaa kimya wataendelea kutupumbaza. Tuwaambie wazi hatuhitaji mabadiliko ya sura za wakurugenzi.

Tunahitaji mabadiliko ya mfumo mzima wa kujitawala.

Mfumo utakaotupa sisi sauti zaidi ya kujiendesha kama taifa na si kikundi cha watu au mtu

Hatuhitaji 'one man show' tunahitaji mass participation. Tumeishi na one man show na kubaki taifa la omba omba.

Sasa si wakati wake, ni wakati wa sisi kutaka mabadiliko ya mifumo yetu mibovu

Tunaona mifumo mibovu inavyotuletea matatizo.

Wiki ijato bunge la JMT linaanza kukiwa hakuna wajumbe wa BLW znz.

Hawapo ndani ya bunge lakini tunaambiwa ni la JMT. Tunaambiwa mfumo ni kamili

Leo tunaona NEC na ZEC zikiwa vyombo viwili tiofauti kabisa. Katiba inatuelekeza ni vyombo vinavyofanya kazi kwa ushirikiano. Uhalisia umetimia tunaona yale ya katiba ni maandishi tu kumbe nchi inaongozwa tofauti

Tumeambiwa Rais wa JMT ndiye mkuuwa taifa la Tanzania.

Tunaona Rais akiwa kama mtazamaji wakati sehemu ya nchi ikiwa na tatizo.

Tumeona nguvu moja ikifanya kazi kama taifa kwamba, nguvu za nchi zipo kwa mtu na si timu au watu

Haya yote tunapaswa kuyaona kama matatizo. Hayo ya MRI ni matokeo ya kuwa na mfumo mbovu

Sasa wapo wenye platform, na wapo wenye sauti, wakasimama na kusema hapana au ndiyo sauti yao itafika nyikani.

Itasikika kwa mfalme aliye juu akiangalia nyika kwa chini. Mfalme atatupa haki za kufikiri, kupanga na kuchagua, si kwasababu anataka bali mfumo utamlazimisha. Huko ndiko tunakotaka kwenda si sura za Wakurugenzi

Asante Nguruvi

nadhani ajenda ya Tume huru, iwe endelevu hawa wapinzani tuwaaambie wajue tunajua exactly nini kinatakiwa

Nyani Ngabu na mimi tumeeleza kwa kina, kuna vitu kama wana mabadiliko lazima tuone aibu kabisa

Kuna vya kuanza, kama kujifunza tumejifunza in a hard way!

kama tungekuwa mabinti na CCM ni dume, mimba ya ngapi hii?? na kila muda tukipata ujauzito tunalalamika kwa jirani kuwa ilikuwaje? kuna mtu ataelewa? maana baada ya kuazaa mtoto tunaona CCM na UKAWA wanavyokuwaga marafiki mno!
 
Bwana P Coelho ansema ''Everybody is a politicalperson, whether you say something or you are silent. A political attitude isnot whether you go to parliament; it's how you deal with your life, with yoursurroundings''

Na maisha anayozungumzia ni kama yetu. Miaka 10 tuliambiwamaisha bora, leo maisha bora ndiyo yale tuliyoyaona Muhimbili. Mazingira yetuni haya ya mfumuko wa bei, maisha magumu , kushukakwa uchumi na kutamalaki kwa umasikini

Bwana Murphy anatukumbusha kuwa ''The politicalprocess does not end on Election Day. Young people need to stay involved in theprocess by continuing to pay attention to the conversation and holding theirleaders accountable for the decisions they make'

Na mazungumzo anayosema nikama haya tuliyo nayo. Kuwawajibisha viongozi ni jukumu letu sote maana sisindio wenye maisha na mazingiraaliyozungumzia Coehlo hapo juu.

Hapa ndipo tunasema wakati umefika viongoziwalioshindwa kubadilisha hali ya mambo wakae pembeni.ili tusiwe na Insanity

A.Einstern anatafsiri Insanity kwa kusema ''doingthe same thing over and over again and expecting different results''

Tumelalamika kuhusu tume na katiba over and over again, sasa tumepatwa naInsanity.

Hatuwezi kuishi kwa insanity ifike wakati tukatae na tujitibu.Matibabu yanaanza na wapinzani.

Tunahitaji mabadiliko katika safu ya kuongozajitihada za mabadiliko ya kweli.

Si mabadiliko ya sura au vipuri vya magari ,ni mabadiliko ya mfumo.

Mfumo uliopo umejengwa na kundi linalonufaika nao.Ni makosa kuwalaumu CCM maana huwezi kuacha mlango wazi, ukamlaumu mwizi. Kaziya mwizi ni wizi na anapofanya hivyo anawajibika

Tatizo ni pale wanaoibiwa wanaposhindwa kuwajibika.Hawa ndio tatizo si wanaoiba

Pamoja na hayo Marcus S anasema ''While I hold my own political views, it'simportant not to get too wrapped up in individual candidates and personalities,but instead to focus on the real issues''

Na real issue hapa ni hatma yetu kama taifa.Issue si mtu au watu ni issues zinazotugusa.

Moja ya hizo ni uwajibikaji, utawala bora naustawi wa jamii.

Hayo ndiyo yanatengeneza kile tunachoitamifumo, iwe ya kiuchumi, kisiasa au kiutamaduni

Real issues si tatizo moja moja, ni mifumoisiyolingana na wakati au haja ya nchi.

Ili kufumua mifumo hiyo na kuisukaupya, agenda ya kwanza ni kuangalia nguzo zake.
Katiba ni nguzo muhimu kwavile ndani ya katiba yapo mambokama ya tume ya uchaguzi n.k.

Ili kutoa msukumo, tunahitaji madereva wapya,tunahitaji damu mpya yenye maono zaidi ya tuliyo yaona.

Tuanze na uongozi mzimawa Upinzani na si Spika wa bunge. Spika wa CCM atasimama na CCM kwasababuwenyewe husema, CCM ni ile ile. Tunahitaji watakaotusaidia tuiache CCM ilele iletufanye bora kwa ajili ya ustawi wa taifa letu, si vyama vya siasa bali taifaletu sote bila kujali itikadi zetu au falsafa za kisiasa , kiutamaduni n.k.

Itakuwa ni kupoteza muda kama wapinzaniwataanza kuongelea ujenzi wa madaraja, microscope na chaki za kufundishia.

Hayosi matatizo, ni matokeo ya matatizo ya mifumo yetu

Tunaweka agenda wazi kwa wapinzani, achenikuongelea dalili ongeleeni kiini cha tatizo.

Wananchi hawahitaji asprin,wanataka matibabu ya malaria. Ukiondoa malaria hutahitaji asprin.

Agenda iliyo mbele kama walivyosema wengine,Tume huru ya uchaguzi haraka, katiba mpya ya wananchi

Wakati Nguruvi akiwa katika sehemu ya pili ya hii tathimini, nilichangia kabla hata hajamaliza kwenye post # 3. Nikasema haya ni marudio, huu si uchaguzi wa kwanza na wala haya sio matatizo mapya. Yanafanyika yale yale eti kukiwa na tamaa ya kupata matokeo tofauti. Mkuu Nguruvi katika yote uliyaandika, post yako # 43 pekee ndio nimeona kuna kitu cha maana (hayo mengine yanaweza kuwa na maana kwa wengine ila kwangu mimi ni marudio tu ya malalamiko yale yale);

  1. Wapinzani watamke wazi kuwa hawataenda katika uchaguzi mkuu mwingine na katiba au tume iliyopo
  2. Kuna umuhimu wa wapinzani kubadili uongozi.
  3. Hoja ya kwanza wanaotakiwa kusimama nayo ni kubadili mfumo
  4. Sisi wananchi tuna shea yetu.

Natumani CDM wakimaliza kugombana kwenye viti maalum, na CUF wakishamalizana kule Zanzibar watayafanyia kazi hayo hapo juu. But i am not going to hold my breath!

Wabe ametoa mfano umenifurahisha sana. Hivi kweli Simba na Yanga zina viongozi wenye upeo kuliko hawa viongozi wa upinzani? Hukubaliani na refa bado unaingia uwanjani ukijua kabisa utaonewa halafu unatategemea dunia ikuelewe ukija kulalamika baada ya mechi kuisha??

Nyani Ngabu kasema foolishness!

NB: Ohh ohh..wait and see wakavyounda kambi ya upinzani bungeni. While i am praying kusiwe na CDM vs CUF conflict, i can feel it coming.
 
Atokee mpinzani... Wapinzani wafanye... Tumewashauri wapinz... wazembe..
Tunakwepa wajibu wetu bado tunajiita Wazalendo.
 
Mabadiliko ni HESABU si IMANI. Imani kwa Upinzani, japo umewaangusha mara zote, mna imani si HESABU nao. ILUSSION
 
Mkuu GalaxyS3

Mwanadamu hujifunza vema kwa experience kulikonadharia.

Na mwanadamu hujiufunza vizuri pale anapokuwa na matarajio asiyowezakuyafikia.

Haya tunayosema yamejadiliwa sana.

Tunachofanya si kipya ni kuyawekakatika muktadha wa vitendo baada ya Nadharia.

Ni kuwaonyesha kwa uhalisia wapi tulipotoka, tulipona tunapoelekea.

Kwa mfano, tukisema kuna tatizo tume, lazima tuonyeshe kwamifano.

Ukiangalia matokeo ya uchaguzi wa Bara na visiwani ni kama yalikuwayanasubiriana.

Kwamba pande zote ziwe on the ''same page'' katika ngazi ya Urais.

Ndio maana huku bara yalianza kutolewa kidogo kidogo kutoka pembezoniwakisubiri ZNZ kitatokea nini.

Kwasasa CCM msimamo wao ni marudio ya uchaguzi. Wapo,nasi pia tumesema watakachokifanya ni kufuta matokeo ya uchaguzi ili yarudiwekukiwa na ‘mazingira' mazuri kwani nguvu itatoka bara.

Kwavile Rais wa JMT ameshapatikana, kuhalalisha kuwayupo halali, CCM watasema kura za ZNZ hazitoshi kubadili matokeo.

Hapo unaonaumhimu wa takwimu

Hii si kwa mujibu wa sheria za nchi, ni kwa mujibuwa CCM.

Ikiwa wanataka uchaguzi ufutwe tu bila kuwa na kigezo cha sheria,hawashindwi kusema kura za rais wa JMT kutoka ZNZ si muhimu. Wao kubwa niushindi mambo mengine yatafuata

Hii maana yake ni nini. Maana yake ni kuwa hatunamfumo unaongoza nchi kwa sheria.

Tuna mfumo unaongozwa na watu kwa kutumia ‘sheria'

Ndipo tunasema, wananchi wasibabishwe na kukosekanavipuri garage, hoja ya kwanza ni kuweka mifumo imara isiyochezewa na watu walaisiyotegemea watu.

Ili kufikia hayo lazima kuwe na agenda. Agenda ndio hizotulizosema.

Kwanza wawepo watu upande wa upinzani watakaokuja namawazo na nguvu mpya.

Waliolifikisha taifa hapa wapunzike, haiwezekani kufanya jambo lile lile miaka 20 bila matokeo tofauti

Pili, wananchi nao wachukue sehemu yao. Waache kudanganywa na ukosefu wa vipuri, bawaba za mlgo au microscope. Wachukue dhima ya kuona mifumo inabadilika

Tatu, Wapinzani watamke kutoshiriki uchaguzimwingine hadi yawepo mabadiliko

Nne, wapinzani wawe na agenda moja, kubadili mfumona katiba

Sasa kuyaongelea haya kwa weledi inawezekanakuandika kwa mistari miwili.
Lakini je, hadhira itaelewa kama unavyoelewawewe?

Kwa msingi huo, tutaandika kwamifano na hoja na ni jukumu la wasomaji kuona cha ‘maana ' au upuuzi.

Muhimu ni kuwaacha wasome na watafakari wenyewe

Ukiangalia mtiririko wa matukio yanavyoendelea ndio unaanza kuelewa kwa nini watawala walikubali "kirahisi" hivyo tuingie mfumo wa vyama vingi 1992. Walifanya hivyo wakijua fika kwamba as long as bado wameshikilia mfumo uliopo na katiba inayotumika ni hii hii ya toka mwaka 1977 wataendelea kubaki madarakani hata miaka mia ijayo!
 
TATIZO LA ZANZ NI KUBWA

Tatizo linaloendelea ZNZ ni kubwa kuliko inavyodhaniwa. Ukubwa si tu kwa hali ilivyo, bali muungano kwa ujumla wake.

Viongozi wanalifumbia macho, mbele ya safari litajidhiri kwa namna nyingine kubwa zaidi

Mwaka 2010 ZNZ ilifanya mabadiliko katiba yake ya 1984 kwa kuleta mgongano na katiba ya JMT

Wengi waliliona tatizo hailo, viongozi wakalichukulia kwa wepesi na kwa mazoea tu ya 'ndivyo tunavyofanya'

Majuzi Rais Mstaafu alizungumzia hali ya ZNZ kwa kusema inamgusa

Akiwa Rais wa JMT hali haipaswi kumgusa bali yeye kuwa sehemu ya shauri.

Ni Amir jeshi mkuu na hivyo kutuma wakuu wa vyombo vya usalama kuzungumza na wanasiasa linatia shaka ushiriki wake

Ameondoka na kumwachia Rais aliyepo tatizo. Madhara ya tatizo ni kuigusa JMT kama nchi na si Zanzibar tu

Mwaka 2001 yalipotokea matatizo tunayojua, taifa kwa ujumla lilibeba sura ya tatizo na wala haikuwa ZNZ pekee

Uchaguzi 2015 Rais wa JMT ametangazwa kukiwa na matatizo ZNZ, unazidi kuleta ufa katika muungano. Wanaliona?

Pamoja na hayo, uchaguzi unatufumbulia kitendawili cha rasimu ya Warioba

CCM walikataa rasimu kwa hoja rasimu kuelekea kuvunja muungano badala ya kuuimarisha

Kwa mazingira yaliyopo, mgogoro wa ZNZ unazidi kudhoofisha muungano badala ya kuimarisha.

Nguvu ya Rais wa JMT haionekani na ushiriki wa upande mmoja wa muungano unazua maswali kuliko majibu

Vumbi litakapotulia visiwani, kuna uwezekano ZNZ kuendelea na 'utamaduni' wa mwaka 2010 wa kukiuka katiba ya JMT, kwani kwao katiba ya JMT inapoteza nguvu kila uchao. Yale ya 2010 ya ZNZ kwenda ''solo'' yatajirudia bila kizuizi

Lakini pia, wabunge wa CCM wataelewa kwanini masuala utaifa ni mbele badala ya vyama.
Kile kilichokataliwa na wabunge wa CCM sasa kinaonekana.

Hali iliyopo ni uwepo usio rasimi wa Tanganyika na Zanzibar.

Tunasema hivyo kwasababu, haionekani kama ZNZ imeshirikishwa na tume ya uchaguzi ya JMT

Kama imeshiriki, NEC inapaswa kueleza umma ushiriki wa ZNZ ni upi katika hali ya sintofahamu inayoendelea?

Kuna mambo matatu yanayoweza kujitokeza

Moja, kama uchaguzi utamalizika na CUF kuongoza nchi kama inavyodaiwa, huenda SMZ kupitia BLW kufanyia marekebisho sheria kuepuka matatizo kama yaliyopO.Sura iliyopo inatoa nafasi ZNZ kuamua hatma yao na si JMT

Pili, uchaguzi utakapofutwa kwasababu za ukiukwaji wa taratibu kama inavyosemwa, kura za WZNZ hazitakuwa zimechagua Rais wa JMT. Hivyo , Wznz watakuwa na sababu za kuamini Rais wa JMT ni wa Tanganyika

Haya ni matatizo ambayo CCM inajaribu kuyaficha, mbele ya safari yatajidhihiri pengine kwa mgogoro mkubwa wa kikatiba

FUNZO

Yapo yanayojitokeza na kuleta funzo kubwa kwa Watanzania. Kwamba, kuishi kwa hisia na mazoe ni jambo la hatari

CCM imekumbatia katiba ya 1977 licha ya kuelezwa mapungufu yanayotokana na nyakati.

Kwa kuamini tu kuwa itatawala siku zote, hilo haliwashughulishi hata kidogo.

Tumeona uwezekano wa mhimili mmoja kumilikiwa na pande mbili sasa ni mkubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Hatujui hali ingekuwaje kama ingetokea hivyo

Tayari mgogoro wa ZNZ unaonyesha baraza la mawaziri la Serikali ya CCM kuwa na wapinzani.

Ikumbukwe, Rais wa ZNZ ni mjumbe wa baraza la mwaziri la JMT. Je tuna serikali ya umoja wa kitaifa kikatiba?

Lakini funzo kubwa ni lile linalosemwa ''success favors the prepared mind'

kwamba mafanikio ni zao la matayarisho ya kifikra.

Tuliyoyaona mwaka 2010 kutoka Baraza la wawakilishi, mwaka 2015 bunge la katiba na 2015 uchaguzi mkuu lazima tukiri hatujafanya maandilizi ya kifikra, na mafanikio yetu siku za usoni yatategemea majaaliwa na si mipango

Kama Taifa hatuwezi kuishi kwa njia za ramli au kamari. Lazima tuwe na prepared mind.

Tusemezane
 
YA ZNZ, MATAMKO YANAPOLETA MASWALI ZAIDI YA MAJIBU
SPIKA WA BLW, NA MSEMAJI WA SERIKALI NA KAULI ZA KURUDIA UCHAGUZI

MWANASHERIA ANENA KUHUSU MAHAKAMA, KASAHAU INTEGRITY AND CREDIBILITY

Timbwili la uchaguzi wa ZNZ linabeba sura mpya kila uchao.

Majuzi msemaji wa SMZ alisema uchaguzi utarudiwa.

Jana kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, Spika wa BLW naye karudia kauli hiyo
Spika alihudhuria kikao cha kamati kuu ya CCM hivi kilichopitia uteuzi wa jina la Spika na 'mengineyo'

Kauli ya uchaguzi kurudiwa inasemwa kana kwamba ni tatizo na zinaleta maswali zaidi ya majibu.

Kwanza, viongozi wanaposema uchaguzi urudiwe, nani mlalamikaji katika majimbo yaliyofanya uchaguzi?
Majimbo yote na mawakala wao wamesaini, vipi ZEC ndio iwe mlalamikaji, isimame upande wa pili kuwa mshauri?
Na upande wa tatu kutoa 'hukumu'?

Swali la Pili,moja ya malalamiko ya ZEC ni kutokuwa na tume iliyotengamana.
Kwamba, wajumbe walifikia mahali pa kutupiana makonde.

Kwa mantiki hiyo tume tayari ina matatizo. Hawa wanaosema uchaguzi urudiwe, utarudiwa kwa usimamizi wa tume ipi?

Iliyopo ndio chanzo cha matatizo, mbona hatuambiwi ni tume ipi nyingine iyakayohakikisha uchaguzi huru na wa haki?

Tatu, hawa viongozi wanaosema uchaguzi urudiwe, kwani uliopo umefutwa na nani?

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa ZEC , tamko ni kwa mamlaka yake, na kwa mujibu wa makamishina wawili hakukuwepo kikao, na kwa mujibu wa sheria hakuna nukuu za kikao chochote. Ni haki kusema kauli za m/kiti wa ZEC ni zake

Swali, wanaosema uchaguzi urudiwe, ni kwa mujibu wa ZEC ipi? Ile yenye wajumbe au ile ya Mwenyekiti peke yake?

Tunaona matatizo ya kauli za viongozi na zinavyoweza kuchanganya kuleta matatizo makubwa zaidi ya ya yaliyopo

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa gazet moja la kampuni ya IPP. mwanasheria wa ZNZ wa zamani anawataka wanasheria wanaoona lipo tatizo waende mahakamani akimaanisha wa CUF bila shaka

Mwanasheria huyo anashindwa kuelewa mambo yalivyo visiwani.

Kuna tatizo la kutotangazwa matoke. Lipo la tume kutoa tamko bila kuwa na wajumbe, lipo tatizo la SMZ kuwepo madarakani baada ya muda wake, lipo tatizo la muda wa BLW kuisha na hivyo kutokuwa na uwakilishi wa wananchi

Hayo ni matatizo tofauti na hayawezi kufanywa tatizo moja.

Endapo CUF wataenda kupinga uwepo wa Rais kwa vile muda wake umeskwisha kwa mjibu wa sheria, hilo linazungumzika mahakamani. Kama wataenda kuhoji uwepo wa mawaziri baada ya muda,inazungumzika.

Lakini, CUF hawana nafasi ya kuhoji maamuzi ya ZEC mahakamani.

Leo ZEC wangetangaza CCM wameshinda hakuna wa kuhoji mahakamani.

Ndivyo ilivyo huku bara ambako watu wananung'unika lakini Rais keshapatikana.

Hakuna anayeweza kwenda kuhoji matokeo mahakamani

Hivyo, mwanasheria huyo anapatoka kuwaelekeza CUF mahakani, anataka wakusanye matatizo yoote katika kau moja. Hapo ni rahisi mahakama kutoa maamuzi ya jumla yatakayoathiri matatizo tofauti.

Kwanini wanataka CUF iende mahakamani?

Inaendelea....
 
Back
Top Bottom