Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

There is a difference between having critical negative opinion and having a purely negative attitude. Kadri hii thread inavyoenda i see more of the later from Nguruvi, i might be wrong and i hope i am.
Mkuu unaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wako, lakini hatuwezi kuwa sahihi kwa mitazamo yetu kwa wengine
Niko entitled kwa maoni na ninasema ninachokiona kwa mtazamo wangu. Msomaji ataamua na ni haki yake

Tunachokataa wengine ni kitu kidogo sana. Tunataka Tanzania iliyofanikiwa.

Tunataka viongozi wanaowajibika

Hatuwezi kuwapima kwa siku 30 kwasababu huko nyuma tulifanya makosa yakatugharimu miaka mingi sana ya maendeleo. Hatuwezi kupima matokeo ya kazi ya mtu tukijua mfumo anaofanyia kazi umeoza

Tunasema hivi, hatua anazochukua hatuna shida nazo ikiwa tu zimelenga kutoa dawa ya ugomjwa na si kupunguza homa. Kinachotakiwa ni kwenda mbali zaidi ya hapo

Wapo wanaosema kwa siku 30 afanye nini, nasi tunasema mna mpimaje kwa siku 30 kutuaminisha anawajibika
 
Mkuu unaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wako, lakini hatuwezi kuwa sahihi kwa mitazamo yetu kwa wengine
Niko entitled kwa maoni na ninasema ninachokiona kwa mtazamo wangu. Msomaji ataamua na ni haki yake

Tunachokataa wengine ni kitu kidogo sana. Tunataka Tanzania iliyofanikiwa.

Tunataka viongozi wanaowajibika

Hatuwezi kuwapima kwa siku 30 kwasababu huko nyuma tulifanya makosa yakatugharimu miaka mingi sana ya maendeleo. Hatuwezi kupima matokeo ya kazi ya mtu tukijua mfumo anaofanyia kazi umeoza

Tunasema hivi, hatua anazochukua hatuna shida nazo ikiwa tu zimelenga kutoa dawa ya ugomjwa na si kupunguza homa. Kinachotakiwa ni kwenda mbali zaidi ya hapo

Wapo wanaosema kwa siku 30 afanye nini, nasi tunasema mna mpimaje kwa siku 30 kutuaminisha anawajibika

Pamoja mkuu...
 
GlaxyS3anauliza je, kingefanyika nini kabla ya haya tunayoona ya timua timua.
Jibu letu ni rahisi sana, kukaa chinikama watu wenye akili na kuangalia mfumo mzima

Hakuna shortcut katika hili. Maelezo yake ni mengi,tujaribu kwa uchache kuonyesha
Kwanza,lazima kuwe na intelligence kwa maana yakupata, kutahmini na kufanyia kazi habari za kijasusi kwa minajili ya ima kijeshi, kisiasa au kiuchumi

Kitengo kiimarishwe ili kufikia malengo tarajiwa. Kwasasa,intelligence yetu inaonekana kama kukimbizana na wanasiasa badala ya mambo ya usalama kama uchumi.

Tumesema mara nyingi sana, dunia ya leo usalama na uchumi havitenganishwi

Ni kitengo kinachotakiwa kuwa na uhuru kwa kiasi kikubwa ili kifanye kazi. Intelligence ndiyo moyo wa Taasisi nyingine

Pili,Jeshi la polisi liimarishwe kwa kubadili muundo. Jeshi liondoke katika muundo wa maguvu na kukumbatia utaalamu
Jeshi la Polisi liwe na uhuru wa kufanya kazi zake

Tatu, nyadhifa kama za PCCB, DPP na DCI ziwekewe uzio. Kwamba, wakishateuliwa wawajibike kwa mamlaka zingine ili kuwabana wafanye kazi zao na kuwapa uhuru wa kutenda bila kuingiliwa

Nne, kazi za kisiasa zitenganishwe na za kitaalaamu.

Tano, mamlaka za nchi zipewe udhibiti katika muundo wa checks and balances

Sita, madaraka ya Rais yapunguzwe ili kumwezesha kuwajibika na kuliangalia Taifa kwa ujumla na si vitendea kazi

Saba, Mihimili ya dola itanganishwe na kupewa uhuru. Jaji ateuliwe na chombo kingine, Bunge lisihusishwe na shughuli za serikali. Vyombo hivyo viwe huru na vifanye kazi kwa kutegemeana lakini kwa uhuru

Nane, turekebisha na kuweka mifumo ya nchi. Kwamba, utawala unaoingia madarakani unakuta Taifa likiwa na values zake zisizobadilika. Kwasasa ni ngumu sana kujua nini values za Taifa letu

Tisa, utendaji na watendaji waangaliwe namna wanavyopatikana au kuteuliwa. Vetting system

Kumi, maadili na miiko iwe sehemu muhimu ya maisha yetu na kwamba kukiuka ni kuvunja taratibu

Kumi na moja, tuangalie structure nzima ya utawala kama tunahitaji watu kama DC wanaoleta urasimu bila kazi za lazima

Orodha inaendelea...

Haya yote hayawezi kufanyika kwa reja reja kwa kutambua yanagemeana.
Ukibadilisha muundo wa watendaji kama DCI , DPP, Mhakama n.k. unagusa sehemu nzima ya muundo uliopo.

Huwezi kupeleka mswada wa kubadilisha kimoja, kingine kikabaki salama.
Kutakuwa na overlap ya shughuli na kuleta mvurugano zaidi

Njia rahisi ni kufumua mfumo mzima. Na hilo ni kupitia katiba kama tulivyoona rasimu ya Warioba

Ndio msingi wa kusema, kinachofanyika sasa hivi ni kusafisha vidonda si kutibu ugonjwa unaoleta vidonda

Well, kusafisha ni immediate measures, muhimu ni long term measure Hatuna budi kurudi katika blue print

Uliuliza blue print ni ipi, nasema ni kukaa chini kama Taifa na kujadiliana tunakwendaje mbele.

Si kukaa chini na kuamuliwa na kamati ya watu wachache corrupt na waliofeli na kuliangusha Taifa

Blue print ni katiba mpya itakayofumua mfumo mzima na kuusuka upya

Tusemezane
 
Sasa tunaelewa KUKAA CHINI na KUSUKA HESABU. Maendeleo si Bahati nasibu kama za kuitegemea CDM mlizozitumain.
Anaita.
 
Afanyacho Dr ni sahihi, kwa maana ya kucheza na kilichopo. HESABU tuzitakazo si fupi, 30 dayz!!? Si wakat wa kusema yote
 
TUTAJIFUNZA LINI

TUTAACHA LINI KBEBA MANYANGA, NJUGA NA MAKUYAMBA NA KUTUMIA AKILI ZETU


Kwa muda sasa tumerudia kauli kuwa matatizo yetu hayahitaji ufumbuzi wa zimamoto.

Ni matatizo ya kimfumo ambayo utatuzi wake ni kufumua mfumo mzima na kuusuka upya ili kuendana na mazingira yaliyopo


Mfumo wetu wa utawala hautoi nafasi kwa watu wenye nia njema na Taifa hili kutenda yaliyo mema.

Huo ndio msingi wa kusema kinachotokea sasa hivi si kitusu stainable bali ni excitement tu


Tumehoji sana kama kumuondoa kamishna wa TRA ndio ufumbuzi. Tulisema vipi kama alipewa vimemo? Angefanya nini?

Tukahoji iweje akae na majina akijua anahatarisha ugali wake?

Tukahoji,vyombo vya umma vilikuwa wapi? Je havikujua hujuma za kodi , ubadhirifu na ufujaji?

Soma habari hii kwa hisani ya gazeti la Raia Mwema utapata majibu

Utaelewa kwanini tunasema mfumo kama haubadiliki hakuna kitakachobadilika.

Tatizo letu si mkurugenzi wa shirika , taasisi n.k.


Tatizo letu mfumo wetu unaruhusu madudu tena kwa sheria halali kabisa.

Ndio mfumo uliopo na kama hatutabadilika tutakuwa Taifa la kushangilia


Tulianza na ufagio wa chuma kwa wasiowajibika . Tukaja nauwazi na ukweli. Mwisho tukaimba nguvu mpya ari mpya na kazi mpya.

Huko kote hatukujifunza tunadakia ghani nyingine hapa kazi tu


Hatujifunzi!

Soma Raia Mwema - Siri ya Kikwete TRA yaanikwa


Tusemezane
 
MGOGORO WA ZNZ WALIATHIRI TAIFA

TULIONYA MAPEMA, HILI NI SUALA LA TAIFA SI ZNZ

MIRADI ILITAFUTWA KWA GHARAMA KUBWA, KUKWAMA NI HASARA KWETU

Kama mtakumbuka, mapema sana katika jamvi la duru tulionya kuhusu mgogoro wa ZNZ na athari zake kitaifa

Tulisema, kwa muundo wa muungano, Rais wa JMT ndiye mwenye dhamana ya ulinzi na usalama na ni taswira ya nchi

Bodi ya MCC imesitisha msaada kwa Tanzania. Ikumbukwe, awamu ya 4 ilitumia muda mwingi kutafuta msaada huo

Aidha,serikali ya CCM imesifia safari za nje kwa kuonyesha MCC kama sehemu ya mafanikio ya ziara hizo

Inapotokea Taifa likakosa misaada likiwa limekeza muda na rasilimali, ni upotevu wa nguvu na rasilimali bila sababu

Awamu ya 5 nayo ilisema mgogoro utapatiwa ufumbuzi, kitu kinachoonekana hakikuwa na uhalisia

Mgogoro wa ZNZ ni wa sehemu ndogo sana ya Taifa. Madhara yake yanawagusa watu wasiohusika, inasikitisha

Hatuoni sababu za Watanganyika kubeba mzigo wa matatizo yanayosababishwa na mgogoro wa ZNZ
Hili ni sawa na kutoa 'kafara' ya watu takribani milioni 44 kwasababu tu ya wapiga kura laki 3

Lakini pia mgogoro huu hautokani na wapiga kura wa ZNZ.
Kazi yao ilikamilika, na wengi wakiwemo wa CCM walikubali matokeo.

Tatizo linatokana na wahafidhina wasiozidi 20 wa CCM waliogomea matokeo hayo kwasababu tu za kihistoria

Hivyo Taifa limewekwa rehani na kikundi cha watu ambao wanaungwa mkono na CCM. Hili linasikitisha sana

Swali la kujiuliza, kikundi hiki cha wahafidhina kina umuhimu gani katika Taifa hili kiasi cha kuliweka Taifa njia panda

Hoja ya kwamba, hatutaki misaada haina mashiko. Kama tulijua hivyo, kwanini tuliwekeza sana katika MCC siku za nyuma?

Kuna umuhimu wa kurudi katika katiba, tuandike utaratibu utakaolinusuru Taifa na majanga kama haya

Wakati Tanganyika ikibeba mzigo mzito wa kuhudumia muungano na sehemu ya SMZ , sasa inajikuta inalipa gharama zaidi kutokana na mgogoro wa ZNZ ambao kiuhalisia hauna masilahi na mwananchi wa Tanganyika

Kilichotokea ni kuwatwisha Watanganyika mzigo zaidi licha ya ukweli kuwa wamebeba muungano mzito tayari

Watanganyika wanabebeshwa mzigo huu na CCM iliyoshindwa kukabaliana na wahafidhinaa pengine hawazidi 20

CCM inaweza kuwekwa rehani na wahafidhina kama chama, lakini ni makosa makubwa wahafidhina kuvuka mipaka na kuliweka Taifa rehani.

Haya ni matokeo ya kutumia maguvu na wingi wa CCM kuliko maarifa katika masuala yanayowagusa wananchi.

Tutaendelea hivi hadi lini?

Tusemezane
 
KAULI YA JAJI BOMAN ‘INAFIKIRISHA'

MZIGO WA MGOGORO WA ZNZ KaTWISHWA MAALIM SEIF

CUF WAINGIA 18, WAJIFUNGA KAMBA

Tumezungumzia katika uzi huu na mwingine kuhusu mgogoro wa ZNZ na athiri kwa Taifa

Tulieleza kwa mbinu zinazotumika kutaka matokeo yawe kama ‘inavyotarajiwa '

Mengi yamepita katika hatua mbali mbali, ni vema tukayarejea kwa uchache ili kueleweka

CCM haina malalamiko ya uchaguzi. Matokeo ya majimboni yalisainiwa na mawakala.
Hesabu zikafanyika kwa nusu ya kura . Matokeo yakasitishwa na Mwenyekiti na si Tume

Yakatolewa madai na Mwenyekiti wa tume yapatayo 9.

Yote hayakutokana na Tume bali mwenyekiti.

Wajumbe wa Tume wamekana kuwepo kwa kikao chochote

CCM ikaanza kutumia hoja za mwenyekiti wa Tume kujenga hoja zao.
Katika hoja zote , hakuna yenye mashiko.


Vikao vya siri vinaendelea kutafuta suluhu na si kura za wananchi

Rais aliyeko anaendelea na kazi kana kwamba hakuna kilichotokea

Majuzi , waziri mmoja wa SMZ amesema hakunawaangalizi wa ndani au nje watakaoruhusiwa uchaguzi utakaporudiwa
Hoja ya kurudia uchaguzi imetumika na CCM bila sababu za kisheria

Wakati mazungumzo yanaendelea jitihada za kuaminisha umma kuwa

uchaguzi utarudiwa zinaendelea kwa kasi

Tukawauliza CUF, mazungumzo gani ikiwa tayari kuna harakati za kurudia uchaguzi zinazofanywa na waliokaa meza moja nao?

Tuliwakumbusha CUF kuwa hoja zao zinabadilishwa na kuelekezwakule CCM inapotaka au kuona kuna mwanya

HOJA ZA CCM

Ni kwamba, mgombea wa CUF ametangaza matokeo kabla.

Hoja zingine zimeonekana kutobeba uzito isipokuwa hiyo moja. Tuliwakumbusha CUF , huko ndiko CCM wanataka waelekee

KUPITISHA MUDA

Vikao vyote vinavyoendelea havinamwisho, agenda wala ajuaye ninikinazungumzwa.

Hizi ni kura za wananchi wanahaki ya kujua hatma ya Taifa lao na kura zao za Oktoba 25

Ni katika hali ya kupitisha muda ili dunia na wananchi wasahau mambo ya uchaguzi. Baada ya hapondipo shutukizi litakapotokea




CUF Waingia 18, wajikaanga

Inaendelea……..




 
BOMANI ANENA

Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali na Mzee mwenye kuheshimika ametoa kauli juu ya uchaguzi kama ilivyonukuliwa hapa

http://www.dailynews.co.tz/index.php/home-news/45185-find-solutions-to-election-irregularities-zec-urged

Katika maelezo yake, Jaji Bomani anamsihi mgombea wa CUF maalimakubali kushiriki uchaguzi wa Marudio.

Moja yasababu anazotoa ni ukikukwaji wa taratibu za uchaguzi kama ilivyoelezwa na NEC, na Jaji anasisitiza NEC ifanyie kazi kwanza mapungufu hayo kabla ya kuandaa uchaguzi

Jaji Bomani anasema, uchaguzi uharakishwe ili kupata serikali halali

Nakwamba Maalim Seifa asiogope uchaguzi kurudiwa kwavilewaliompigia kura watampigia na kama ni ushindi ataupata

http://www.ippmedia.com/?l=87163

Jaji amesisitizwa kuundwa kwa jopo la wataalamu likaomaliza mgogoro na kuendelea na kazi hadi uchaguzi wa marudio utakapokamilika

Mzee Bomanianasema, suala la ZNZ ni la kikatiba na limalizwe kisheria


MAONI YETU KUHUSUKAULI ZA Mzee Bomani

Kwanza,ni wazi Mzee Bomani ameshakubaliana namaoni ya kurudiwa kwa uchaguzi.

Hakueleza kwanini uchaguzi urudiwe.

Ukimsoma kwa undani, Jaji ameridhika na madai ya Tume ya uchaguzi.


Na amejiridhisha kuwa iliyofuta uchaguzi ni tume si mwenyekiti

Hapa maana yake , Jaji keshachukua upande.
Kukubali tu kuwa kulikuwa na matatizo na Tume iyarekebishe , nikujiridhisha kuwa yalikuwepo matatizo.


Je, ni kweli yalikuwepo? Nani alilalamika?

Nakwanini baada ya matokeokuhesabiwa Mwenyekitialitoweka kutanagaza mwenyewe?

Je, Tumeya ZEC ni mwenyekiti au ni wajumbe?

KwaniniJaji aone uhalali wa Mwenyekiti kuwa ndiye Tume nzima?

Je,amewasiliana na wajumbe wengine kuwasikiliza kama anavyomsikiliza mwenyekiti wa tume?

Pili,Jaji anaposema uchaguzi urudiwe, ni kwa kutumia kigezo gani?

Akiwa mwanasheria , je, ni kifungu gani cha sheria kinacho kinachoplekea uchauzi urudiwe?

Ni msingi upi unaomshawishi Jaji kuwa ni muhimu uchaguzi kurudiwa

Kwanii asisitize matokeo yatangazwe,amejielekeza katika kurudia uchaguzi?

Je,makosa ya uchaguzi yanatokana na upande gani kwa maoni yake?

Jajianaposema uchaguzi urudiwe Seif asihofie,je, anajua kwanini kuna hofu?

Haki ipi itapatikana ikiwa waliogomea matokeo ndio watakaosimamia uchaguzi?

CCM bara naCCM visiwani ndio wenye vyombo vya dola kwa sasa.Hki ipoi?

Kwanini Jaji amshwishi maalim Seif na si Dkt Shein?

Ukisoma habari yake, ingawa ameongea kama Mzee wa jamii kauli zake zinatosha kueleza msimamo wake kwauhalisia bila kupepesa macho

Inaendelea..

 
‘CUF WAIINGIA18' WAJIFUNGA KAMBA WENYEWE
Kwamuda mrefu CUF wameacha hoja zao kufinyangwa ili waelekee kule CCM walipotaka. Ndicho kinachotokea. Hoja za CUFzilikuwa wazi kabisa

Kwanza,aliyefuta uchaguzi ni nani, Tume au mwenyekiti?
Ushahidi wa Tume kufuta uchaguzi upo wapi.
Mamlaka ya Tume aumwenyekiti katika hilo yapo wapi!


Pili,matatizo ndani ya tume yameathiri vipi uchaguzi vituoni

Tatu,nani anayelalamika kuhusu matokeo.
Chama gani kilifikisha mlalamiko katika tume kabla ya kura kuhesabiwa?


Nne,endapo Maalimu alitangaza matokeo kabla, sheria inasemaje kuhusuhilo.
Ni kufuta uchaguzi au kumfikishakatika sharia?


Orodhainaendelea

CUFwakavutwa kwenye mazngumzo na wale wanaowalalamikia.
Mazunguzoambayo hakuna anayejua yanahusu nini


Wakati mazungumzo yanaendelea, kampeni za kurudia uchaguzi zinaendelea.
CUFwalitakiwa wajiulize,


kama kuna ‘hukmu'ya kurudia uchaguzi , maongezi yanahusu nini na yana maana gani?

CUFwalitakiwa wajiulize, ni kitu gani hasa kinachohtaji mazungumzo? Katibaya ZNZ inatoa nafasi kwa serikali ya umoja wa kitaifa, leo mazungumzo yanahusu nini?

CUF wametoa nafasi CCM iliyohitaji, muda. CCMZNZ wanaelewa nguvu kubwa ipo bara, na kutokana na hali ya uchaguzi wa bara, ilihitajika muda nguvu kuelekezwavisiwani

Kauli kama za Jaji Bomani zinaonyesha muda walioutaka unatimia

Pili, walichokitaka ni kufikia mahali iamuliwe uchaguzi urudiwe

UCHAGUZI KURUDIWA
CCM namakada wengine wakiwemo watu maarufu wanataka uchaguziurudiwe. Hili linasisitizwa sana na kufunika hoja ya kwanini urudiwe

Uchaguzi ukirudiwa, CUF watashindwa kinyume na anavyosema Jaji Bomani. CUF watashindwa kwasababu nyingi

Moja,wanachama wao watakuwa ‘demoralized' na kukata tamaa ya kupiga kura

Pili, nguvuya CCM kutoka bara itaelekezwa visiwani. Kila mbinu itatumika ili kufikia lengo

Tatu, CUFhawana vyombo vya dola. CCMwatatumia vyombo vya dola kuhakikisha nguvu ya CUF inapunguzwa kwa kila namna.

Nne, Waziri na SMZ ikiwemo NEC yabara wamesema waangalizi mwisho . Waziri wa SMZ amesemahakutakuwepo na waangalizi wa ndani au nje katika uchaguzi wa marudio. Yaani ni ‘free style'' Je CUF wana ubavu wa free style?


Katika hili,kutatokea kile kinachoitwa ‘votersuppression'' Vitisho, vitimbwi n.k.vitatumika , kwa bahati mbaya CUF hawanafursa katika hilo
MzeeBomani anapomsihi Maalim akubali kushiriki uchaguzi wa marudio, tayari inaonyeshauchaguzi utakuwepo.

Hoja nikumtaka Maalim ashiriki kama vyamavingine

Kwamantiki hiyo, CUF wamejibebesha mzigo wenyewe.

Hoja iliyopo ni kumtaka Maalim ashirikiuchaguzi wa marudio.

Mzigo huo ametwishwa Maalim ili aongee na wanachama wake.

Hakunahoja nyingine zaidi ya kurudiwa uchaguzi, zile mita 18 walizotaka CCM na ambazo CUF wameingia bila kutarajia zimetimia

Maalim sasaana mzigo mzito wa kueleza, mazungumzo yalihusu nini

Na jeuchaguzi wa marudio kama CCM wanavyotaka utakuwepo?

Hatuoni CUF wanaweza kupindua kauli hiyo bila kubebeshwa dhamana ya ‘utulivu na amani'

Shemuya mwisho inafuata







 

Tumalizie kwa kusema kuwa, mgogoro wa ZNZsi wa kisheria ni wa kutengenezwa


Ni wa kijamii zaidi, kwamba, kundi moja linaamini lina haki ya kutawala Kundi hilo ni la watu wachache sana wenyenguvu katika vyama

Linaweza kuiwekaZNZ na Tanzania rehani ilimradi matakwa yatimizwe. Limefanikiwa kuteka watu wenye heshima katika jamii.

Inapotokea wajuzi wa sheria wanasimama na kusema tu bilasababu inaeleza mengi


Kwamba, ushauri ni kuundwa kwa jopo la watu nje ya NEC na vyama visani kukubali matokeo

Mbona hilo lipo katika sheria za nchi, ZEC n.k.? Kwanini watu wanataka kukwepa ukweli kwa kuingiza yasiyo na maana?


Taifa lina changamoto nyingi ikwemo
ombwe la watu wenye hekima.

Wazee tuliowataraji wanapanda majukwaani na kuporomosha mitusi, malofa n.k.

Umasikini ni chanzo cha ombwe la watu wenye busara.

Wazee wanatumika kwavile tu wanahitaji kuishi. Wamekuwa ‘mateka' wakifungia vyeti makabatini, uzoefu wao kwenye magodoro na wanazugumza kama watu wa mitaani.

Kauli za wazee zilenge umoja, kusimamia haki na kutoa mwongozo. Kamwe zisitoe hisia au kuhalalisha ‘uhuni' kwa njia za mkato zisizojibu hoja



CUF watambue katika hili kuna pande mbili. Hakuna upande wa tatu.

Hivi karibuni tumeona majaji na wasimamizi wa vyombo kama tume za chaguzi waliostaafu wakiwa na kadi za vyama vya siasa mifukoni


Kwa hili CUF wamejifunga kamba za mikononi. Wanategemea ‘mbwa mwitu' anaweza kugeuka kuwa mbuzi mzuri


Nasi wananchi tutambue Taifa lina ombwe la watu wenye busara.
Tufkirie kwa manufaa yetu sote na vizazi vyetu.

Tukiendekeza njaa kama wanavyofanya wazeewetu tutarithisha vizazi vyetu ombwe labusara

Asiyetaka kusema kijiko ni kijiko na siyo chepeo huyo ni wa kuogopa kama ukoma

Tusemezane
 


MGOGORO WA ZNZ

WALICHOFANIKIWA CCM

Ukisikiliza kauli za viongozi wa CCM –ZNZ hoja yao imebaki moja kati ya zile alizoorodhesha mwenyekiti wa Tume kama sababu za kufuta uchaguzi

Hoja inayotawala vichwani na katika maongezi ni ‘Tume imefuta uchaguzi'

Wanachokwepa kusema ni ‘Mwenyekiti wa tume amefuta uchaguzi'

Hakuna kifungu kinachompa uwezo Mwenyekiti wa tume kufuta uchaguzi.

Kukwepa hilo kauli ya ‘Tume..' inatumika

Hata hivyo bado kuna tatizo. Inaposemwa tume imefuta uchaguzi swali lipo pale pale.
Tume ina uwezo gani kisheria kufuta uchaguzi?


Maswali hayo hayana majibu. Kinachofanyika ni kutumia uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuaminisha kuwa tume ndiyo imefuta matokeo.

Wanafahamu kurudia hilo jambo mara nyingi, linaaminika


KULIKUWA NA ULAZIMA GANI ‘BUNGENI''

Tulishuhudia mtafaruku wakati wa kufungua bunge. Wabunge wa

‘UKAWA' walipinga uwepo wa Rais wa SMZ katika shughuli hiyo

Zome zomea hadi bunge likaingia dosari ya kutoka kwa wapinzani

Katika vikao vya karibuni vya CCM , Makamu mwenyekiti ZNZ hakuonekana(labda kama hatukuona sawa sawa).

Juzi , katika kikao cha baraza la mawaziri la JMT kiti cha Rais wa ZNZ kilikuwa wazi

Hapa kuna mambo ya kujiuliza. Iweje CCM waone lipo tatizo la kumwalika Rais wa ZNZ kukiwa na mgogoro unaofukuta, na Bunge la JMT lisione tatizo hilo?

Kulikuwa na ulazima gani wa kumwalika Rais wa ZNZ wakati huo, huku

vikao vingine vinavyomhusu vikaacha kiti wazi, kuanzia vya chama hadi serikali?

Busara zinatumika wakati gani ?

Ulikuwepo ulazima wowote wa kuwalika Rais wa ZNZ Bungeni na kuzua mtafaruku?


Tusemezane


 


MAZUNGUMZO YASIYO NA UPANDE WA PILI

CHADEMA/UKAWA WALIJIFUNZA KWA NJIA NGUMU
Chadema ilipopinga miswada ya mchakato wa katiba , waliitwa Ikulu.
Tuliwaona wakinywa juisi za maembe.
Tuliwatahadharisha, mazungumzo yasiyo na nyaraka yasiyojulikana hayana mwisho mzuri


Mwisho wa siku waligeukwa na kuonekana kama tatizo mbali na tatizo lenyewe.
Hawakuwa na nyaraka yoyote iliyoonyesha nini walikubaliana Ikulu. Kibao kikaugezwa, CDM wanataka ‘kuvunja ‘amani na utulivu. Miswada ikapitawakiwa wamepoteza kuungwa mkono


Hililikuwa somo zuri sana kwa CDM na hatudhani kama wanaweza kurudia madudu yamfano ule tena. Kwamba, mazungumzo yawe na kumbu kumbu na yawe kisheria zaidi kuliko maongezi juu ya glasi za juisi

Halihainoenekani kueleweka kwa upande wa CUF.
Mkwamo uliopo tunausikia ukifanyiwa mazungumzo. Hakuna anayejua mazungumzo yanahusu nini


Tatizo laZNZ ni baina ya vyama viwili, CCM na CUF.
Ni kati ya wagombea Urais Wa vyama hivyo. Wakati CUF ikiwa na Maalim Seif , CCM ina Dkt Shein


Mazungumzo yanaendelea! Hata hivyo zimekuwepo kauli za viongozi wa CCM-ZNZzikionyesha msimamo wa CCM kuhusu marudio ya uchaguzi.

Katibu mwenezi wa CCM visiwani na waliokuwa mawaziri wamenukuliwa mara kadhaa wakisema hayo


Hatujamsikia mgombea wa CCM kwa upande wa ZNZ. Hatujamsikia mwenyekiti wa CC taifa.
Hawa ndio wadau wakuu wa maongezi wakiwa na washirika wao waCUF. Vipi leo wapo kimya?


Tunasikia Rais wa JMT akiongea na katibu mkuu wa CUF ambaye ndiyemalalamikaji.
Rais wa JMT ana sehemu yake kikatiba, lakinije, wahusika wakuu wa CCM wapo wapi?


Nakwanini viongozi wa CCM kitaifa hasikiki kukemea kauli za baadhi ya makada wa CCM-ZNZ?
Hii maana yake ni nini? Kwamba , viongozi hao wa visiwani wamepata Baraka za wakuu wao, au wameamua kukiuka tu taratibu za chama chao?


Maongezi yanayoendelea ni kati ya nani na nani? Yanahusu nini?

Pengine CUF wangejiuliza zaidi,wanaongea na upande upi?

Tusemezane

 
HOFU YA CCM-UCHAGUZI WA ZNZ

'Majadiliano' ya kutafuta muafaka wa uchaguzi yanaendelea kukiwa na hadithi mpya kila uchao

Wengi wamejiuliza kwanini CCM-ZNZ inakuwa na 'nguvu ' CCM makao makuu?Hatuwasikii wa CCM kwa ujumla, kulikoni!

Kuna hoja mbili zinazoenda pamoja. Kwanza, CCM inahofia kufutwa kwa matokeo ZNZ kutaweka doa uchaguzi mzima Wapo wanaosema uchaguzi wa Rais wa JMT na ule wa ZNZ vinaenda sambamba lakini si kitu kimoja

Kuna ukweli kuwa si kitu kimoja, hata hivyo, upo ukweli kuwa wapiga kura wa ZNZ ni wale wale wanaopiga kura JMT

Katiba ya ZNZ ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho 2010 inasema

124(1) mamlaka ya baadhi ya vyombo vya muungano
(2) (a)Mahakama ya katiba ya JMT (b)Tume ya Pamoja ya fedha ya JMT (C)Tume ya Taifa ya uchaguzi ya JMT

(3)Kwa madhumuni ya kifungu hiki, vyombo vilivyoainishwa katika kifungu (2)vitahesabika kama vyombo vya serikali ya mapinduzi Zanzibar katika shughuli zake hapa Zanzibar

Hadi hapo tunaona jinsi Tume ya uchaguzi ya JMT inavyoingia katika sakata zima kuhusiana na uchaguzi wa JMT

Kwa upande mwingine, CCM makao makuu inaunga mkono kimya kimya CCM-ZNZ kwa kuangalia mambo kadhaa

1) Katiba ya JMT inamtaja Rais wa ZNZ kama mjumbe wa baraza la mawaziri. Maana yake , Rais akitoka upinzani kisheria ni mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT. Je, hapa ni rahisi kumuona 'mbwa' mwitu ndani ya kundi la kondoo?

Lakini pia CCM inahofu ya kupoteza mamlaka visiwani kwa muda mrefu. Katiba ya ZNZ inasema

Kifungu (66) Rais wa SMZ atateua wabunge 10, wawili kati yao wakitoka upinzani
Maana yake kuna wabunge 8 wa chama anachotaka Rais

Kifungu (67) (1) na (2) vinaeleza jinsi ya kupata wabunge wanawake wa kuteuliwa ndani ya baraza la wawakilishi

Kwa siasa za ZNZ, vyama vya CCM na CUF vinatoa wajumbe wanaokaribiana sana ndani ya BLW.
Tofauti inaweza kuwa wajumbe 2 au 3. Hata hivyo, tofauti kubwa inatokana na wajumbe 10 wa kuteuliwa na Rais

Yote hayo yanatoa hesabu muhimu ya Uspika. Kwamba, Rais aliyeko madarakani chama chake kitatoa Spika wa BLW

Ndipo CCM wanapoona ukakasi. Kwamba, hawatakuwa na udhibiti au uchochoro wa kupitisha mambo yao wanavyotaka.

Tunasema hivyo kwasababu, yapo mambo ya muungano yanayohitaji kuridhiwa na BLW.
kumetokea mtafaruku wakati wa mswada wa sheria ya katiba mpya, CCM wakitaka mambo yaendelee bila kuridhiwa, CUF wakisema suala lipelekwe BLW

Kwa muundo wa sasa wa CCM, Spika wa BLW ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM.
Kwao, ni rahisi kutoa maagizo kwa serikali ya CCM-ZNZ na kupata mwanya wa kupitisha mambo yao kupitia BLW

Suala la muungano likiwa bado ni bichi, hali kwa upande wao inawalazimu wafanye 'jitihada na majadiliano' ya ziada

CCM ikipoteze Urais, itapoteza sehemu kubwa ya utawala, kuanzia BLW, Tume ya uchaguzi n.k.

Kinachowasumbua CCM ni , je, baada ya kuachia, kuna nuru siku za usoni au ndiyo kutesa kwa zamu?

Tusemezane
 
TUJIFUNZE KWA YALIYOTOKEA ZANZIBAR
TUONGOZWE NA FIKRA BADALA YA JAZBA


Tumeona yanayotokea Zanzibar leo hii ikiwa ni Zaidi ya miezi miwili uchaguzi , uongozi na hatma ya nchi kwa ujumla

Rais wa Zanzibar Dr Shein , amevunja ukimya tangu mtafarauku utokee kwa kusema, ni Rais Halali wanaompinga waende Mahakamani.

Ameyasema hayo akiwa Pemba kukagua shughuli za maendeleo

Shein breaks silence, says he is legal leader

Dr Shein amewaambia wanachama wa CCM yeye ni makamu mwenyekiti wa CCM na kwamba ni kiungo cha mawasiliano ndani ya vikao vya chama

Dr Shein kasema kweli kwasababu Mahakama ndicho chombo cha kutafsiri sharia pale kunapokuwa na mgogoro.

Kwa upande mwingine, Wanaohoji uhalali wa Urais wake wapo sahihi pia

Wanaohoji wanahoja moja kubwa, kwamba, si Urais ulio na tatizo bali mchakato mzima wa yeye kubaki madarakani unaondoa uhalali

Ili kupata jibu la nani yupo sahihi katika hili , mahakama ndicho chombo pekee kinachoweza kuonyesha uhalali au kukosekana kwake.

Hapa ndipo tatizo linapoanza

Dr Shein anaamini Mahakama kwavile uteuzi wa chombo hicho upo mikononi mwake na ana haki ya kuamini aliowateua kufanya kazi hiyo

Wanaohoji na kukataa kwenda mahakamani wanasita kwa kuelewa madoa yaliyojitokeza na kuondoa credibility ya Mahakama(kuaminika).

Inapotokea mkuu wa tume ya uchaguzi ambaye alikuwa Jaji mkuu kuchukua fomu ya Urais wa chama bila maelezo ya lini alianza siasa, inaondoa Imani kwa akili ya kawaida kabisa.

Pande zote na Wazanibar kwa ujumla wamejikuta hapa walio kwasababu moja kubwa, walifanyia mabadiliko ya katiba yao ya 1984 kwa marejeo ya 2010 katika malengo mawili

1. Kuweka uwiano kati ya utawala miongoni mwa vyama viwili CUF/CCM kwa kuigiza serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa mitafaruku miongoni mwao

2. Kukabiliana na 'muungano' ili kuipa Zanzibar mamlaka yake. Waliamini SUK itaweza kupambana na ''hasimu' wao Tanganyika.

Inaendelea...
 
TUJIFUNZE KUTOKA ZNZ

Inaendelea...

Mamb0 2 tuliyoyasema hapo juu , SUK-ZNZ na kukabiliana na Tanganyika yaliwasukuma WZN kufikiria katiba juu ya hayo tu bila kufikiria athari zingne

Serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) ikawaunganisha kufanya mabadiliko ya katiba bila kushirikisha sehemu muungano yaani Tanganyika.

Wazanzibar waliamini SUK ni nta itawaweka pamoja

Hatua iliyofuata ni kuanza kupunguza nguvu za muungano.

Wakaunda taasisi zao, wakaziondoa nyingine katika bila majadiliano.
Wakakimbilia mafuta wakiamini Tanganyika itawadhulumu

Wazanzibar wakampa Rais wao nguvu, wakataja mipaka ya nchi yao na uwezo wa kuigawa n.k.
Kila walilofanya lililenga 'kuwakomoa' Watanganyika

Kuna mambo wakasahau. Kwamba, bado muungano ni muhimu kwao pamoja na kuudharau.

Kwamba, ulizi na usalama vilikuwa chini ya muungano ule ule waliouangalia kwa jicho upande.

Wakasahau, ndani ya muungano mbaya ni Tanganyika, wakibaki nje wana tofauti zao zilizojificha.

Ya kwamba, anayeficha tofauti zao ni Tanganyika

Kwasababu ya kuelekeza jicho kwa Tanganyika, hawakuangalia katiba yao kwa umakini.
Kuweka nadharia zote kama ikitokea tofauti.

Kwa maana kuwa katiba yao inaposema Rais mwisho wake ni siiku kadhaa, haikwenda kwa undani kwamba ikiwa ABCD nini kifanyike katika mazingira XYZ

Tunachoshuhudia sasa ni wapinzani kurudi katika serikali ya muungano kutaka msaada, na CCM kurudi katika muungano kutaka msaada, hakuna SUK tena

Wakashindwa kufikiria ipo siku mahakama yao ya juu itahitajika.
Kwamba, walipaswa kuweka mazingira ya mahakama kuwa chombo huru na cha kuaminika

Leo mgogoro ungekuwa mahakamani, wapinzani wakitaka haki, Rais na CCM wakitaka haki. Sivyo! kwasababu jicho lao lilikuwa dhidi ya Tanganyika tu, abadiliko ya katiba hayakulenga ustawi bali namna ya ''kumkomoa' Tanganyika

Zile tofauti zao zilizojificha zimekuwa wazi kwasababu Tanganyika kakaa pembeni.

Nini basi kilichopekea haraka ya mabadiliko ya katiba na kusahau mambo muhimu kwao kuliko kuiangalia Tanganyika ?

Makosa hayo ndiyo tunataka tuyarudie kwa katiba ya JMT.

CCM wanaamini tu katiba itakayowapa nafasi ya kuendelea kutawala.

Hawana fikra na mazingira mengine muhimu ya maendeleo au yenye kutishia usalama siku za mbeleni

CCM wanachoharikisha ni katiba mpya kwa lengo moja, kuwa muundo wa serikali uwe mbili.

Hawana fikra za mazingira mengine nje ya hapo kama ambavyo wazanzibar walikuwa na chongo na mabadiliko ya katiba yao. Ni kwa muktadha huo, leo hakuna anayejua hatma ya ZNZ kwa uhakika.

Tusipojifunza kutokana na matatizo ya ZNZ tutastahili adhabu siku za mbeleni

Tusemezane
 
Last edited:
DALILI ZA MAZUNGUMZO ZNZ'' KUKWAMA ''

Taarifa ya katibu mkuu CUF ambaye ni mgombea kiti cha Urais imetolewa na mwenyewe leo

Kuna kila dalili mazungumzo yaliyokuwa ya 'siri' yamekwama. Kauli ya Seif kuwa kurudia uchaguzi hakukubaliki inaeleza hilo

Kwa wale mnaofuatilia hapa duru, tumehoji mara nyingi sana, mazungumzo ni baina ya CUF na nani?

Tulihoji hivyo kwasababu kwa upande wa pili, CCM walikaa kimya. Ikawa mazungumzo kati ya CUF na Marais wastaafu

Tulihoji, marais hao walipitia mfumo ule ule wanawezaje kuwa neutral bila kuangalia masialhi mapana ya siku za nyuma na zijazo?

Mbona hawakutoka mapema na kueleza misimamo yao hadi tunasikia wameitwa katika vikao
Mazungumzo ya viongozi wa dini yaliishia wapi?

Tuliwaambia CUF, kinachofanyika huenda ni kuvuta muda na wangeshtukizwa wakiwa wametunduwaa

Seif anasema, upo mapngo wa kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi uliokuwa ufanyike January 14 kwa mujibu wake

CUF wangejiuliza, vikao vinane vinajadili nini ikiwa sheria zote zipo vitabuni?

Tulisema wapinzani hawajifunzi kutokana na makosa. Chadema waliitwa Ikulu katika ile hafla ya juisi ya maembe
Wakaambiwa wakae kimya kwasababu maongezi hayo yatayolewa taarifa ya pamoja.

Taarifa ilipotolewa Chadema wakabaki mdomo wazi. Miswada ikapelekwa bungeni wakisingiziwa kukiuka makubaliano

Yes, walikiuka kwasababu hakuna anayejua nini kiliongelewa hivyo taarifa iliyotolewa ndiyo ilionekana kuwa sahihi
Kosa la kisiasa ambalo linajirudia kila siku

Sasa haijulikani nini hatma ya Zanzibar kwasababu haionekani kama kuna mwanga mbele ya safari kwa maelezo ya Seif

Tusubiri kesho sherehe za mapinduzi na kauli zitakazotolewa. Huenda tukapata mwanga wa 'nini kinaendelea''

Tusemazane
 
YANATIMIA TARATIBU

MBEGU TULIYOSEMA IMESHAOTA, INASUBIRI TU KUMWAGILIWA

Katika mabandiko mengi tumesema nchi yetu imagawanyika. Kwamba, uchaguzi uliojaa kampeni chafu umeacha makovu makubwa. Umeamsha vidonda na utaratibu mzima umezaa matatizo zaidi ya uchaguzi
Inaendelea...

Rais ameshapatikana kuendelea na malumbano ya uchaguzi iwe mitaani au katika vyombovya sheria ni kuendelea kulitia taifa ganzi na kuligawa zaidi.


Ni kupalilia chuki zilizotokana na uchaguzi ambazo zitazidi kulipooza taifa achilia mbali kuligawa

Tusemezane

Tumeshuhudia kampeni za kutuhumiana kuhusu upuuzi wa kibaguzi na chama tawala kikionekana kupoteza kabisa ukongwe au uongozi dhidi ya vile vya upinzani katika kukemea!

Kampeni zimeanza kuzaa matunda, na hakika ni wakati muafaka viongozi wajitokeze na kukemea

YALIYOTOKEA ZANZIBAR

Mabango yanayosema ' Machotara Hizbu ZNZ ni ya Waafrika' ni hatari sana.
Yametolewa viongozi wote wa kitaifa wa serikali na CCM wakiwa wanashuhudia wazi na mchana

Tuna uhakika mwallimu angekuwepo asingevumilia upuuzi ule

Mwalimu alikataa ubaguzi na kutumia sehemu kubwa sana ya uongozi wake kupinga hilo

Tunajua alivyosaidia ukombozi kwa wale waliokandamizwa.
Akaenda mbali kuunga mkono vyama vingine kama PLO na hata kuingilia kati mzozo wa Biafra

Sifa moja ya Mwalimu ilikuwa kupinga ubaguzi hata pale masilahi ya nchi yalipotatizwa

Leo viongozi waliobaki wametulia katika mazulia mekundu wakiona mbegu mbaya inachanua

Hatudhani mapinduzi yalilenga kubagua watu. Kinyume chake, chanzo cha mapinduzi ni kuondoa ubaguzi, kusimamia utu na heshima ya wananchi bila kuwabagua

Kilichoonekana ZNZ ni kudhihaki mapinduzi na kuondoa ile maana yake halisi.
Waliopoteza maisha wakitetea mapinduzi leo wapo makaburini 'wakigeuka kwa uchungu na hasira'

Laiti wangerudi, wasingeamini rangi imekuwa kigezo cha utaifa.

Hata mabepari wamekubali hilo, Raia wa Wazanzibar weusi na weupe, machotara na washihiri wamekimbilia nchi za magharibi na kupewa hadhi za Uraia huko.

Nani asiyejua 'michenzani' UK? Huko Canada na kwingineko ?

Walipokelewa kwasababu ya kulinda utu na ubinadamu wao, si kwasababu ya rangi zao

Laiti rangi ingekuwa kigezo, wale weusi tii wanaosema Zanzibar ni ya kwao wasingepewa passport ya Mwingireza, Mdanish, Msweden au Mcanada

Hii dhana iliyoasisi na CCM ni mbaya. Imeasisi na CCM kwasababu mabango hayo yametengenezwa chini ya usimamizi wao, yakapita langoni na kuingia uwanjani wote walikuwepo wakiyaona ni 'hate crime'

Hakuna aliyethubutu kusema hili halifai. Viongozi hawakuhamaki wala kukemea katika hotuba zao

Tunaona taarifa ya CCM ikitolewa na kada wa chini kana kwamba ni jambo dogo tu

CCM WANAWAJIBIKA

Kwa hili hakuna namna CCM inaweza kujiondoa isipokuwa kwa njia moja tu.

Mwenyekiti wa CCM ajitokeze na kulaani kitendo hicho mbele ya umma.
Rais wa JMT ajitokeze na kulaani kitendo hicho
Rais wa ZNZ ajitokeze na kulaani ubaguzi huo
Marais wastaafu waliokuwepo wajitokeze na kulaani ubaguzi huo

Ni hayo tu ndiyo yatakayolioponya Taifa. Na wale waliohusika watafutwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Hili ni kosa la kibaguzi likichochewa na ubaguzi 'hate crime'

Polisi na vyombo vya usalama vinahitaji ushahidi gani zaidi?

Vingenevyo, yanayoendelea ZNZ na uchaguzi yatahusishwa na tukio hilo.

Jumuiya ya kimataifa haitatuelewa. Tutakuwa tumepoteza thamani yetu ya utu na kupoteza heshima yetu katika uso wa dunia

Tuna nafasi ya kujirudi, vingienvyo tutakemea vipi uhutu na utusi huku tukiwa na 'Uhutu na utusi katika nyumba yetu?''

Tusemezane
 
CUF: TULISEMA

Dr SHEIN WANANCHI WASHIKE LIPI?

KIMYA UBAGUZI UKITENDEKA MAANA YAKE NINI?


Mtakumbuka tumerudia mara nyingi kueleza kuhusu mazungumzo yanayoendelea
Tulisema, Maalim Seif anazungumza na nani ikiwa partner wake wa CCM hayupo?
Tukauliza maongezi gani wakati kila jambo la kisheria lipo wazi? Kwanini yanachukua muda mrefu
Tulimazilia kwa kusema, iweje CCM wanaotuhumiwa ndio waongoze majadiliano?

Tulitoa historia ya 'Juisi ya maembe' ya Chadema Ikulu wakati wa bunge la Katiba
Tulionyesha jinsi gani Chadema waliufungwa midomo na mwisho wakashtukizwa
Tumeeleza, CCM wana ujanja wa kuvuta muda wakifanya 'timing' na huko ndiko maalim anakwenda

Siku za karibuni tulieendelea kueleza, muda si mrefu CCM watamtwisha maalim mzigo
Yote yanayotokea sasa ni marudio tu ya picha nzima tuliyoieleza

Na mwisho tukasema CCM inataka uchaguzi urudiwe kwasababu nyingi na tulizieleza
Kurudiwa uchaguzi ni agenda muhimu kwao na jinsi wanavyogeuza kauli, kuaminika kwao ni kudogo sana

Jana Rais Shein ameutubia sherehe za Mapinduzi. Moja ya matukio ya kusikitisha ni lile la ubaguzi wa rangi
Rais alikuwa na nafasi ya kulikemea pale pale , hakufanya hivyo

Lakini kikubwa Zaidi ni jinsi hotuba yake ilivyokuwa na sura mbili

Sura ya kwanza , ni kuwapendeza wahafidhina au kutimiza lengo la CCM
Rais alisema uchaguzi utarudiwa, tarehe isubiriwe kwani taratibu zote za kufuta uchaguzi zimeshatolewa na gazeti la serikali. Kwamba uchaguzi utarudiwa.

Sura ya pili, Rais Shein anamalizia kwa kusema mazungumzo yanaendelea na taarifa ya pamoja itatolewa

Hapa kuna mchanganyiko mkubwa. Endapo tarehe ya uchaguzi ndiyo inayosubiriwa, mazungumzo yapi yanayoendelea ? Ni mazungumzo ya jambo gani zaidi ya lililotolewa uamuzi tayari kwamba uchaguzi urudiwe?

Na pili taarifa gani ya pamoja inasubiriwa kutolewa ikiwa tayari uamuzi wa kurudia uchaguzi umeshatangazwa?

Haya ni mambo yanayosumbua jamii kifikra, yanaweka jamii njia panda hasa katika wakati wa 'political tension' ni ya kiwango cha juu. Ni kuendelea kuwatia wananchi wasi wasi na kutia hofu wafanyabiashara

Leo wananchi wanajiuliza, uchaguzi utarudiwa? Na kama CUF wakikataa nini kitatokea?
Na nini kauli ya taarifa ya pamoja kuhusu mazungumzo ambayo tayari majibu yameshapatikana?

Ule makakati wa CCM wa 'kununua muda ' umefanikiwa.
Wakati mwafaka ulikuwa jana na mzigo wote sasa ameubeba mgombea wa CUF

Kitendo cha CCM na wazee wastaafu kukaa kimya ubaguzi ukitendeka kinatoa ujumbe tuliokuwa hatujui

Swali, mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhusu nini ikiwa tuna kila jibu kutokana na yanayoendelea?

Tusemezane
 
LAKUVUNDA HALINA UBANI

HISTORIA NI MWALIMU MZURI


Home

Mabandiko ya uzi huu tumejaribu kueleza nini kilitokea siku za nyuma na nini kinatokea. Turejee kwa ufupi

1. Tumeandika kuhusu CCM kubadili mwelekeo wa mgogoro wa ZNZ. Jitihada zilifanyika kuaminisha umma tume ndiyo imefuta matokeo si Jecha. Tukawaadharisha CUF uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka kuwa ukweli

2. Tukakumbusha CUF historia ya kushindwa muafaka wa kwanza inaweza kujirudia
Mwafaka huo ulichukua siku nyingi na mwisho wake ukafa, Komandoo akaendelea kutawala

3. Tukakumbusha Juisi ya Maembe Ikulu. Kwamba, CDM walidanganyika kwa kuambiwa yapo mazungumzo.

Hivi lini CCM wakawa wema wa kusikiliza wananchi? Chadema wakaambiwa wakae kimya, kilichofuata ilikuwa surprise, CDM wakapoteza. nguvu ya wananchi ilishapoa, hawakuwa na pa kushika,.CCM ikapeta

4. Tulimuuliza Maalim , huu mgogoro unahusisha vyama vya siasa.
Mbona hatusikii kauli ya mwenyekiti wa Taifa wa CCM? Seif anazungumza na nani?

5. Tukasema mazungumzo yanayoendeshwa huku mlalamikiwa akiwa mwenyekiti hayana dalili njema

6. Tukauliza, sharia zipo wazi vikao vyote ni vya nini? Nini kinatafutwa hadi kuchukua muda kiasi hicho?

7. Tukasema viongozi wastaafu waliokuwa mstari wa mbele ya kampeni za CCM.
Lini wameshukiwa na rehma za uadilifu kiasi cha kuwa neutral katika mazungumzo?

8. Tuliandika pia, CCM ni wazuri sana wa kununua muda. Walifanya hivyo si mara moja au mbili.
Walichokuwa wanasubiri ni kupoa joto la uchaguzi, dunia igeuze kisogo ili waje na surprise. Ndiyo imetokea

9. Tuliandika, CCM wanataka uchaguzi urudiwe kwasababu nguvu ya Bara itahamia huko.

Nguvu zote unazozifahamu zitatumika kisiasa na kiutawala. Kama wameweza kumshawishi mwenyekiti(siyo tume) afute matokeo nini kitawashinda uchaguzi mwingine?

10. Tulisema, itafika mahali wananchi wanachoka na kusahau na atakayepoteza ni Seif.
CCM wanachotaka ni kurudia uchaguzi ambao wana uhakika utafanikiwa tu !

Si kwasababu uliopita ulikuwa na matatizo la hasha, hakuna kumbu kumbu za malamiko kutoka majimbo, matatizo yanatoka wapi

11. Tukamalizia katika bandiko tulilosema CCM wamefanikiwa kubadili mada, Maalim ameingia 18 kwa vikao vya siri akiwa mwenyewe. Ile political base yake imekuwa disappointed na kwamba atarudi kuwaeleza nini wafuasi wake?
Kwamba, Mzigo umeondoka mabegani mwa CCM kwa kununua muda, Seif ameubeba

Historia ni mwalimu mzuri, na la kuvunda halina ubani.

Hakuna hata moja lililonje ya hayo. Maalimu kajitoa katika mazungumzo wakati wanasubiri taarifa ya pamoja.
Taarifa ambayo hatuoni kwanini ichukue wiki na wiki

Huu ulikuwa mtihani wa wazi (open book exam)

Tusemezane
 
Back
Top Bottom