YANATIMIA TARATIBU
MBEGU TULIYOSEMA IMESHAOTA, INASUBIRI TU KUMWAGILIWA
Katika mabandiko mengi tumesema nchi yetu imagawanyika. Kwamba, uchaguzi uliojaa kampeni chafu umeacha makovu makubwa. Umeamsha vidonda na utaratibu mzima umezaa matatizo zaidi ya uchaguzi
Inaendelea...
Rais ameshapatikana kuendelea na malumbano ya uchaguzi iwe mitaani au katika vyombovya sheria ni kuendelea kulitia taifa ganzi na kuligawa zaidi.
Ni kupalilia chuki zilizotokana na uchaguzi ambazo zitazidi kulipooza taifa achilia mbali kuligawa
Tusemezane
Tumeshuhudia kampeni za kutuhumiana kuhusu upuuzi wa kibaguzi na chama tawala kikionekana kupoteza kabisa ukongwe au uongozi dhidi ya vile vya upinzani katika kukemea!
Kampeni zimeanza kuzaa matunda, na hakika ni wakati muafaka viongozi wajitokeze na kukemea
YALIYOTOKEA ZANZIBAR
Mabango yanayosema ' Machotara Hizbu ZNZ ni ya Waafrika' ni hatari sana.
Yametolewa viongozi wote wa kitaifa wa serikali na CCM wakiwa wanashuhudia wazi na mchana
Tuna uhakika mwallimu angekuwepo asingevumilia upuuzi ule
Mwalimu alikataa ubaguzi na kutumia sehemu kubwa sana ya uongozi wake kupinga hilo
Tunajua alivyosaidia ukombozi kwa wale waliokandamizwa.
Akaenda mbali kuunga mkono vyama vingine kama PLO na hata kuingilia kati mzozo wa Biafra
Sifa moja ya Mwalimu ilikuwa kupinga ubaguzi hata pale masilahi ya nchi yalipotatizwa
Leo viongozi waliobaki wametulia katika mazulia mekundu wakiona mbegu mbaya inachanua
Hatudhani mapinduzi yalilenga kubagua watu. Kinyume chake, chanzo cha mapinduzi ni kuondoa ubaguzi, kusimamia utu na heshima ya wananchi bila kuwabagua
Kilichoonekana ZNZ ni kudhihaki mapinduzi na kuondoa ile maana yake halisi.
Waliopoteza maisha wakitetea mapinduzi leo wapo makaburini 'wakigeuka kwa uchungu na hasira'
Laiti wangerudi, wasingeamini rangi imekuwa kigezo cha utaifa.
Hata mabepari wamekubali hilo, Raia wa Wazanzibar weusi na weupe, machotara na washihiri wamekimbilia nchi za magharibi na kupewa hadhi za Uraia huko.
Nani asiyejua 'michenzani' UK? Huko Canada na kwingineko ?
Walipokelewa kwasababu ya kulinda utu na ubinadamu wao, si kwasababu ya rangi zao
Laiti rangi ingekuwa kigezo, wale weusi tii wanaosema Zanzibar ni ya kwao wasingepewa passport ya Mwingireza, Mdanish, Msweden au Mcanada
Hii dhana iliyoasisi na CCM ni mbaya. Imeasisi na CCM kwasababu mabango hayo yametengenezwa chini ya usimamizi wao, yakapita langoni na kuingia uwanjani wote walikuwepo wakiyaona ni 'hate crime'
Hakuna aliyethubutu kusema hili halifai. Viongozi hawakuhamaki wala kukemea katika hotuba zao
Tunaona taarifa ya CCM ikitolewa na kada wa chini kana kwamba ni jambo dogo tu
CCM WANAWAJIBIKA
Kwa hili hakuna namna CCM inaweza kujiondoa isipokuwa kwa njia moja tu.
Mwenyekiti wa CCM ajitokeze na kulaani kitendo hicho mbele ya umma.
Rais wa JMT ajitokeze na kulaani kitendo hicho
Rais wa ZNZ ajitokeze na kulaani ubaguzi huo
Marais wastaafu waliokuwepo wajitokeze na kulaani ubaguzi huo
Ni hayo tu ndiyo yatakayolioponya Taifa. Na wale waliohusika watafutwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Hili ni kosa la kibaguzi likichochewa na ubaguzi 'hate crime'
Polisi na vyombo vya usalama vinahitaji ushahidi gani zaidi?
Vingenevyo, yanayoendelea ZNZ na uchaguzi yatahusishwa na tukio hilo.
Jumuiya ya kimataifa haitatuelewa. Tutakuwa tumepoteza thamani yetu ya utu na kupoteza heshima yetu katika uso wa dunia
Tuna nafasi ya kujirudi, vingienvyo tutakemea vipi uhutu na utusi huku tukiwa na 'Uhutu na utusi katika nyumba yetu?''
Tusemezane