kuna miti kama upo dar imepandwa pembezoni mwa barabara iendayo mwenge tokea Moroco ni mizuri sana kwa kivuli na inakuwa haraka- marawi yake yanakuwa kama ngazi ngazi hivi!
Tatizo la miti hiyo ni kuwa haiishi miaka mingi.
Ni vizuri kupanda miti ya vivuli inayosurvive kwa miaka mingi, mfano kuanzia babu anatumia kivuli chake mpaka mjukuu na kitukuu.
Ila miti ya hivyo huchukua muda mrefu kuwa mkubwa na kutoa kivuli.
Mimi katika maisha yangu yote naamini miti mizuri sana ni
"Jacaranda Mimosifolia" au mjakaranda kwa kiswahili.
Ukienda Arusha maeneo ya uzunguni na hata monduli utakuta Mijakaranda iliyopandwa pembeni mwa barabara enzi za ukoloni na wazungu na hakuna mwaka inaacha kutoa maua mazuri na kivuli mujarabu
Pia mti kama muembe nyonyo ina kivuli kizuri na bado inatoa matunda yaliwayo so ni mzuri.
Hizi zingine za kisasa ni za artificial na nyingi zinatoka ulaya, huwa ni nzuri kwenye garden ila haidumu muda mrefu, uwe tayari kuipanda na baada ya miaka 10-15 uibadilishe kwa kupanda mingine.
Pia ni vizuri kupanda miti ambayo mbali na kivuli inaweza kuconvice ndege kujenga viota vyao hapo utapafurahia sana.
Kingine ni vizuri upande miti isiyodondosha sana matawi yake yanayochafua mandhari.
Mijohoro ni mizuri na ndio miti ya kivuli yenye kuni nyingi sana na inastahimili ukame.
Muarobaini nayo ni mizuri sana kwani pia inatoa dawa lakini kuna wadudu wanapenda sana kuishambulia ikiwa midogo.
Mimi pia napenda sana miti na nimekuwa mpandaji tangu udogo wangu.
Wabillah Tawfiq,