Miti kwa ajili ya kivuli

Miti kwa ajili ya kivuli

Wakuu naomba mnijuze aina ya miti ya kupanda kwa ajili ya kivuli ambayo inakua haraka

Sent using Jamii Forums mobile app

...Kama lengo lako kuu ni kivuli tuu na ukipate kwa miti itakayokua kwa muda mfupi basi nakushauri upande: 1. Muarobaini (Azadirachta Indica) - bei ya miche haizidi 1000, na inasitawi maeneo mengi except nyanda za juu na zenye baridi sana. 2. Mjohoro (Senna Siamea) - maelezo yake ni kama huo mwingine.
 
nenda kwenye wataalam wa mambo ya kilimo wanatoaga ushauri mzuri miti mingine ni hatari kwa udongo inaweza leta magonjwa hata MAUA yasiote kwa arusha wapo kule tengeru au usariver wanauza miti ya maembe, mapera, parachichi, papai miti ya vivuli na haina madhara
 
Panda miembe mifupi mkuu. Au mikomamanga.

love thé love or hâte thé love.....
Aende pale SUA au nane nane atapata mbegu ya maana

brain is the beautiful part of the body.
 
kuna miti kama upo dar imepandwa pembezoni mwa barabara iendayo mwenge tokea Moroco ni mizuri sana kwa kivuli na inakuwa haraka- marawi yake yanakuwa kama ngazi ngazi hivi!
Tatizo la miti hiyo ni kuwa haiishi miaka mingi.

Ni vizuri kupanda miti ya vivuli inayosurvive kwa miaka mingi, mfano kuanzia babu anatumia kivuli chake mpaka mjukuu na kitukuu.

Ila miti ya hivyo huchukua muda mrefu kuwa mkubwa na kutoa kivuli.

Mimi katika maisha yangu yote naamini miti mizuri sana ni

"Jacaranda Mimosifolia" au mjakaranda kwa kiswahili.

Ukienda Arusha maeneo ya uzunguni na hata monduli utakuta Mijakaranda iliyopandwa pembeni mwa barabara enzi za ukoloni na wazungu na hakuna mwaka inaacha kutoa maua mazuri na kivuli mujarabu

Pia mti kama muembe nyonyo ina kivuli kizuri na bado inatoa matunda yaliwayo so ni mzuri.

Hizi zingine za kisasa ni za artificial na nyingi zinatoka ulaya, huwa ni nzuri kwenye garden ila haidumu muda mrefu, uwe tayari kuipanda na baada ya miaka 10-15 uibadilishe kwa kupanda mingine.

Pia ni vizuri kupanda miti ambayo mbali na kivuli inaweza kuconvice ndege kujenga viota vyao hapo utapafurahia sana.

Kingine ni vizuri upande miti isiyodondosha sana matawi yake yanayochafua mandhari.

Mijohoro ni mizuri na ndio miti ya kivuli yenye kuni nyingi sana na inastahimili ukame.

Muarobaini nayo ni mizuri sana kwani pia inatoa dawa lakini kuna wadudu wanapenda sana kuishambulia ikiwa midogo.

Mimi pia napenda sana miti na nimekuwa mpandaji tangu udogo wangu.


Wabillah Tawfiq,
 
Dr. hiyo mitiki faida zake nini... ninapenda miti saana... nimeshazoea mitope tope miparachichi stafeli michungwa ambayo mwisho wa siku napata matunda.
Lalashe hiyo pia inaitwa Mibunduki

Hakuna mti wenye mbao ngumu kama hiyo

Ndiyo iliyotengenezewa meli ya MV Liemba

Na imeitwa mibunduki kwakuwa huwa inatengenezewa vitako vya bunduki, na kama ujuavyo inaishi miaka mingi mnoo bila hata kufubaa.

Ni zaidi ya chuma.

Arusha pia ipo, nitakuelekeza panapouzwa.
 
Dr. hiyo mitiki faida zake nini... ninapenda miti saana... nimeshazoea mitope tope miparachichi stafeli michungwa ambayo mwisho wa siku napata matunda.
Lalashe hiyo pia inaitwa Mibunduki

Hakuna mti wenye mbao ngumu kama hiyo

Ndiyo iliyotengenezewa meli ya MV Liemba

Na imeitwa mibunduki kwakuwa huwa inatengenezewa vitako vya bunduki, na kama ujuavyo inaishi miaka mingi mnoo bila hata kufubaa.

Ni zaidi ya chuma.

Arusha pia ipo, nitakuelekeza panapouzwa.
 
Kuna hii miti impepandwa kituo cha mwendo kasi gerezani. inaitwaje? Nimeipenda sana inaota haraka na inatanda.
 
Lalashe hiyo pia inaitwa Mibunduki

Hakuna mti wenye mbao ngumu kama hiyo

Ndiyo iliyotengenezewa meli ya MV Liemba

Na imeitwa mibunduki kwakuwa huwa inatengenezewa vitako vya bunduki, na kama ujuavyo inaishi miaka mingi mnoo bila hata kufubaa.

Ni zaidi ya chuma.

Arusha pia ipo, nitakuelekeza panapouzwa.
Asante lalashe
 
Nafikiri mitiki ni mti ghali kuliko miti yote kwani ubao wake mkuu daby unatumika kutengeneza vitako vya bunduki na kutengenezea meli ni miti ambayo inafaida sana ukilima ekari moja unauuga umasikini.
Sehemu nyingi inastawi.......ila zaidi kwenye mvua za kutosha, joto la wastani na udongo wenye kina kirefu. Mashamba makubwa ya Teak yapo Tanga (Longuza), Morogoro (Turiani, Ifakara etc). Kazi kwako.....ukipata kijitabu cha mbegu cha Tanzania Tree Seed Agency kimeorodhesha maeneo kwa ufasaha zaidi.
Mimi binafsi nimeipanda kwangu na shambani japo si kwa wingi.
Mkuu ubao wa teak huwezi kuununua its very expensive na endapo ukilima hata ekari moja lazima mabenki waje wakubembeleze uwauzie.
Siyo kweli
 
Miembe ya kisasa ya ku badi inaweza kulete kivuli?
 
Ni mawazo yang kwa hivyo unahaki ya kukubali au kukataa mkuu.
Lakini pia wewe unaweza kutwambia mti ambao ni ghali zaidi maana umepinga bila kutoa hoja.
Sina jibu la moja kwa moja ni mbao gani ni GHALI zaidi duniani, kuna mbao nyingi zinazouzwa ghali kuliko hizo teak. Bubinga ni mfano mzuri, ni ubao aghali sana na upatikanaji wake si rahisi, nina wiki mbili sasa natafuta slab 100 za 2x12 Tanzania sijazipata, nimepata quote kutoka Congo simchezo na usafirishaji juu yangu! Hebu jaribu kuulizia ubao wa 2x8 wa mpingo halafu uje tena useme mtiki ndiyo expensive!!!
 
Panda miembe mifupi mkuu. Au mikomamanga.

love thé love or hâte thé love.....
Mwembe mfupi waweza ukakaa chini yake ukapata kivuli??
Maana first priority ya mleta mada ni kivuli.
 
Back
Top Bottom