Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Gari nzuri zisizoongelewa sana na wabongo
Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana, ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa watanzania.

Gari hizi zinavitu vingi sana ambapo gari nyingine kama Toyota huwezi pata hasa ukilinganisha bei yake.

Mitsubishi outlander 2006 - 2015
1.Ni gari inakuja na charging system ya laptop, yaani unaweza kuchomeka switch sockate na ukaweka charger yako vizuri... Kwa kifupi
Gari hili linabadili umeme wa dc kwenda ac.
Kwa watu wanaopenda kutumia laptop wakiwa safari hii gari unaweza kutumia laptop toka Dar mpaka Mwanza, bila kuizima unafanya kazi tu au unaangalia series.

2.Gari hii inakuja na kifridge kidogo kuweka vivywaji uwapo safarini.

3.Gari hii ina option ya 4WD

4.Gari hii inakuambia muda wa kupumzika ukichoka safarini.

5. Gari hii inakuja na mziki mziti yaani subwoofer isiyojaza buti.

6.Gari inakuja na seat 7.

7.Gari hii ina option ya manual na automatic.

8. GARI hii ina gear 6, inaifanya itumie mafuta kidogo.

Hii gari bei yake ipo chini ya kina harrier, kulger na Vanguard. Kitu ambacho hivi vitu vyote vingekuwa kwenye hizo gari bei zake zisinge shikika.
Asante kwa hii taarifa. Nlikuwa nakosa ushawishi wa kutosha. Natafuta mteja wa Xtrail Rider DTX nihamie Outlander ya 2012 kwenda juu cc2000
 
Difference kubwa hv
Unapata mkuu ukiwa fresh wacheki jamaa wa Autocom Japan wanabei nzuri. Mfano Mitsubishi Outlander ya 2010 ukiikuta Befoward bei inakuwa tofauti na Autocom kwa tofauti ya $ hata 800 au 1000 ni vile maraia wamekariri Befoward na kwingine
 
Tatizo letu Watanzania tunajifanya tunajua kila kitu, hakuna gari iko comfortable kama hiyo! Achana na toyota zinazovibrate dashboard! Unaweza kuta mtu hapa anachangia kwamba sio gari nzuri wakati hakuwahi kumiliki hata boxer pikipiki!!
Acha uboya, Toyota ina vibrate dashboard sababu mounting haziko sawa. Weka mounting zote ziwe sawa uone kama kuna mtetemo wowote utaupata. Au nenda Yard yeyote kawashe Carina Ti uone kama itakuwa na mtetemo.
 
Acha uboya, Toyota ina vibrate dashboard sababu mounting haziko sawa. Weka mounting zote ziwe sawa uone kama kuna mtetemo wowote utaupata. Au nenda Yard yeyote kawashe Carina Ti uone kama itakuwa na mtetemo.
Oyaaaa mbona unamfokea?[emoji1787][emoji1787]
 
We jamaa acha uchawi.
Mimi nina Mitsubish na gereji hawanijui.
Zaidi ni service za kumwaga oil na service za tairi.
Ni gari ngumu mno.
Waswahili bana huwa tunapokezana taarifa nyingine hata zisizo na uhakika.

Hivi kweli kwenye ushindani wote wa soko Kampuni kubwa kama hiyo itengeneze Gari dhaifu ili iweje? hii hata haingii akilini.

Nilichojifunza ni kuwa huwa kunakuwa tu na kasumba au tabia ya Jamii kuamini Gari za aina fulani, wakati mwingine kigezo kinakuwa ni bei au kuigana tu.

Kwa mfano kuna Nchi moja kule Asia ukienda utashangaa Magari ya KIA yalivyo mengi na maisha yanaenda....sasa muombe ushauri Mbongo kwamba unataka kununua KIA uone atakavyoziponda.
 
Back
Top Bottom