Mitt Romney akalia kuti kavu GOP baada ya Usaliti, hata USA usaliti not allowed!

Mitt Romney akalia kuti kavu GOP baada ya Usaliti, hata USA usaliti not allowed!

Bavaria,

..samahani.

..sikusoma vizuri na kuelewa majibu yako.

..nimerekebisha post yangu.

..Niwie RADHI.
 
Rommney aliunga mkono jambo la msingi sana: kwamba Senate iridhie kuwa watu waliozuiliwa na serikali kuhojiwa na baraza la wawakilishi sasa waitwe mbele ya Senate. Republicans hawakutaka kwa sabsbu walijua Rais ataendelea kuvuliwa nguo.
 
Hawezi kufukuzwa chamani. US sio shithole country, hizo ni siasa tu.

Kwenye uchaguzi wa Marekani 2008 Collins Powel na Condolezza Rice pamoja na kuwa Republicans lkn walimuunga mkono Obama na hawakufukuzwa chamani.

Hii inaitwa, "A highly developed democracy", wanaheshimu mawazo ya mtu tofauti na huku uswahilini ambapo woote mnatakiwa kuwa na philosophy ya Manyumbu.
 
Hujaelewa aliposema mitt anaitwa msaliti. Kama siyo msaliti kwanini wanamuandama? Jiulize haitakiwi degree haka kama una elimu kama ya Msukuma utajua anashambuliwa kwaajili ya kukisaliti chama chake. Trump anataka Mitt afukuzwe kwenye chama sasa wewe kama kweli umelewa tuambie sababu za Trump kuomba Mitt afukuzwe chamani
Nasubiri Mitt apigwe risasi 38.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani impeachment ilifanyika kwenye congress(democrat ni majority) kilichokuwa kinafanyika jana senate(republican ni majority) ni conviction.

Umechanganya kidogo hapo, Senate pia ipo ndani ya Congress, usahihi hapo kwenye bluu ni house of representatives.
 
Kwa hiyo uhuru wa mtu kuamua na kuchagua ndio kwako unaona usaliti? Hiyo ndio maana halisi ya demokrasia. Uhuru wa kuamua na kuchagua kwa kadri nafsi yako inakuelekeza na si kwa matakwa ya ya mwengine. Usilazimishe mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo ni tweet ya mtoto wa Trump! Pia umeshaambiwa Trump Sr sio mwenyekiti wa chama hana uwezo wa kumfukuza Romney chamani hata kama angependa iwe hivyo!
 
Mitt Romney ni republican Senator pekee aliyekuwa upande wa Democrats kutaka Raisi D.Trump awe ,, impeached”, sasa baada ya Seneti linaloongozwa na Republicans kukataa kumvua Uraisi D. Trump, wamemgeukia Mitt Romney na kutaka afukuzwe Uanachama GOP kwa Usaliti, ...

Acha kutia chumvi,be professional in reporting.
 
Mitt Romney ni republican Senator pekee aliyekuwa upande wa Democrats kutaka Raisi D.Trump awe ,, impeached”, sasa baada ya Seneti linaloongozwa na Republicans kukataa kumvua Uraisi D. Trump, wamemgeukia Mitt Romney na kutaka afukuzwe Uanachama GOP kwa Usaliti, ...

Sijaona popote huyo "masaliti" alipotishiwa kuuawa.

Na ungeelewa maana ya "usaliti" usingethubtu kabisa kuleta mada hii JF.

Tatizo letu kwenye jukwaa hili la JF, kila mwenye takataka zake anaruhusa ya kuzirusha tu mradi anapendezwa yeye kufanya hivyo.

Yaani hata kujua watu wanavyosimamia mambo wanayaoyaamini, kama alivyofanya huyo Romney, bado huelewi chochote?

LOoo, samahani. Kumbe ni wewe?
Sikusoma jina kabla ya kujibu. Samahani sana, unaweza kughairi kila kitu nilichoandika hapo juu.
 
Mitt Romney ni republican Senator pekee aliyekuwa upande wa Democrats kutaka Raisi D.Trump awe ,, impeached”, sasa baada ya Seneti linaloongozwa na Republicans kukataa kumvua Uraisi D. Trump, wamemgeukia Mitt Romney na kutaka afukuzwe Uanachama GOP kwa Usaliti, ...

Sasa baba wa demokrasia hiyo ndio demokrasia ambayo wanatushupalia tuifuate?
 
Shetani atakupa mamilioni ya sababu, ili utende dhambi, ila mjue mwanamme wa halisi ameshaweka shoka shinani, nyie endeleeni kuua,kuonea na kuteka watu tu, ila mida ikifika itakuwa ni kulia na kusaga meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mitt Romney ni republican Senator pekee aliyekuwa upande wa Democrats kutaka Raisi D.Trump awe ,, impeached”, sasa baada ya Seneti linaloongozwa na Republicans kukataa kumvua Uraisi D. Trump, wamemgeukia Mitt Romney na kutaka afukuzwe Uanachama GOP kwa Usaliti, ...

Senate haina mamlaka ya kum impeach rais. Kazi hiyo ilishafanywa na wakina Pelosi. Maamuzi ya Senate ya kukataa kumvua urais hakubadilishi status yake ya kuwa alikuwa impeached. Donald Trump Jr ni domo kaya. Hana mamlaka yeyote kwenye chama cha Republican. Kingine ni kuwa mtu hahitaji kuwa mwanachama wa chama chochote ili awe Senator. Republicans wakimvua uanachama itakula kwao maana kwa miaka minne ijayo ataendelea kuwa Senator na bila shaka watahitaji kura yake katika masuala mengine. Mwisho ni kuwa Romney anaheshimiwa sana na Mormons wenzake na kwa kufanya alivyofanya ndio kabisa kawaloga maana amethibitisha kuwa wao ni watu wenye msimamo. Kwa hali iliyopo sasa hakuna Republican Utah anayejitambua ambae atadiriki kum challenge kwenye primaries za mwaka 2024. Na mwaka huo, hata kama Trump atashinda mwaka huu, atakuwa bata kilema.

Amandla.......
 
Kuna mtu kaniita mjinga humu nilipoifananisha CCM ya Magufuli na Republican ya Trump. Kuna vilaza humu hawasomi habari za kimataifa wamebaki tu kumsema Magufuli
Wewe kweli ni mjinga.Tena kabisa.Hizo habari za kimataifa unazosoma bado huzielewi.Hata unachoandika hakieleweki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaelewa aliposema mitt anaitwa msaliti. Kama siyo msaliti kwanini wanamuandama? Jiulize haitakiwi degree haka kama una elimu kama ya Msukuma utajua anashambuliwa kwaajili ya kukisaliti chama chake. Trump anataka Mitt afukuzwe kwenye chama sasa wewe kama kweli umelewa tuambie sababu za Trump kuomba Mitt afukuzwe chamani
Wewe jamaa ni mpumbavu kweli, unataka kulinganisha siasa za US Na huku Shithole kwetu?!
 
Back
Top Bottom