Mitume na manabii tishio kwa Kakobe,Gamanywa na Fernandes ndio maana wanalalama

Mitume na manabii tishio kwa Kakobe,Gamanywa na Fernandes ndio maana wanalalama

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Mwenge kakobe alikuwa peke yake akiwika Ghafla akakuta Mtume mwingira huyo kaingia hatua chache toka alipo na maelfu ya waumini akimiliki.hadi ndege na television ujogoo ukaisha ghafla

Gamanywa na Fernandes walikuwa ndio majogoo mbezi Ghafla bin vuu wakakuta Mtume Mwamposya huyu hapa hatua chache toka walipo na anavuma kuliko wao.na kusomba watu kibao Hadi sehemu za kukaa hawana .Wengine kasomba waumini wao

Hi ndio sababu kuu yao wao kuanzisha Vita na mitume na manabii lakini ukweli Ni kuwa Ni frustrations za kuona wamepitwa Ghafla na vijana wa juzi juzi tu

Kifupi wajiandae kwa surprise zaidi .Kanisa Ni dynamic sio static Ukiona wewe umefika kesho utashangaa mtu hata hujui katokea wapi huyo anaku overtake.Ni Kama Daudi alivyo mu overtake Sauli na kuchukua ufalme.Mrithi wa Mfalme Sauli kawaida angekuwa mtoto wa Sauli lakini akakuta Daudi huyo kitoto toka porini hicho kinapeta
 
Hela huleta chuki eti watu wa Mungu nao wameanza bifu.KAKOBE ATULIE ZAMU YAKE KUPIGA HELA IMEISHA SASA NI ZAMU YA KINA MWAMPOSA NA SUGUYE.
 
Vita ya manabii wa kizazi kipya iyo.Ni ngumu sana
Sio mchezo mfano umoja wa makanisa Nigeria yote TB Joshua aliopoanza walitoa matamko wazi kabisa kuwa hawamtambui,hajulikani alikotokea,hajasomea dini kabisa na haeleweki aliyemleakidini Nani Yaani baba yake wa kiroho. Na miujiza yake haileweki kimantiki ya Biblia!!!!!

Yeye hakujali.Sasa hivi ndie kiongozi wa dini pekee Nigeria anayeongoza kuiingizia Nigeria pesa za kigeni kuliko dini yeyote kupitia wageni toka dunia nzima wanaoenda kule.
Anaheshimiwa na viongozi wengi wakuu wa nchi Duniani wakiwemo wastaafu na waliopo ikiwemo Tanzania.

Ndilo kanisa pekee Duniani ambako.maraisi ,mawaziri wengi toka mataifa mbalimbali Duniani huenda kusali.

Ana TV ya kurusha matangazo dunia nzima kwa lugha kubwa zote za dunia akirusha toka kwao Nigeria

Hawa waafrika wapya sio rahisi kivile .Ni new Afrikans breed ambao Hadi watu wa ulaya na Marekani wanawashangaa uwezo wao.
 
Si waende mahospitali waliko na wagonjwa

Kama bwana wangu Yesu !!!...

Hawa ni wahuni
acha hizo Yesu hakuwahi kwenda hospitali kuponya mtu yeye alienda tu kule aliitwa kuponya hata kufufua hakwenda makaburini kufufua watu ila akiitwa akafufue alienda Mfano kwa Lazaro na alimfufua kwa hiari yake Wala hakuna aliyemuomba alijisikia kufufua akafufua.
 
Yesu na mbwembwe zoooote, alifufua mfu mmoja tu.... hii ni jeuri na kutokujali au matumizi mabaya ya talanta.
 
Point of Correction hakuna kanisa hata moja hapo hayo uliyoyataja yote ni huduma za maombezi za watu binafsi kwa kifupi makanisa ni machache sana i.e Roman Catholic,Lutheran,Anglican,Morovian,Pentekoste, na Assemblies of God (hapa bila kutenganisha EAGT na TAG) hizo zilizobaki zote ni huduma za maombezi..
 
Kondoo wa Mungu wapo tu, hakuna haja ya kuwagombania, bali ni mbinu ya kuwaita na kuwachunga.

Tuliona viongozi wa kidini Bongo kujipa nyadhifa za mtume wakawapiku manabii.

Bahati nzuri aliyejiita yesu aliishia Nyayo., na DC rockcity kumpiga marufuku huyu mfalme (ke) mungu wa zumaridi. Vinginevyo kwa hizi nyakati za mwisho tutashuhudia mengi
 
Yesu na mbwembwe zoooote, alifufua mfu mmoja tu.... hii ni jeuri na kutokujali au matumizi mabaya ya talanta.
acha hizo Yesu hakuwahi kwenda hospitali kuponya mtu yeye alienda tu kule aliitwa kuponya hata kufufua hakwenda makaburini kufufua watu ila akiitwa akafufue alienda Mfano kwa Lazaro na alimfufua kwa hiari yake Wala hakuna aliyemuomba alijisikia kufufua akafufua.
Someni Yohana 5:1-15

Kiswahili ni lugha yetu, mnashindwa
kutofautisha KUPONYA na KUTIBU
 
Someni Yohana 5:1-15

Kiswahili ni lugha yetu, mnashindwa
kutofautisha KUPONYA na KUTIBU

Hoja yangu ni tofauti kidogo na uponyaji wa vipofu, ni kuhusu ufufuo wa wafu.... mbwembwe zoote zile kufufua wangapi..?
 
Back
Top Bottom