Mitume na manabii tishio kwa Kakobe,Gamanywa na Fernandes ndio maana wanalalama


Yeyote anayejiita mtume au nabii hapati airtime kwangu. Hawa ni matapeli wanaojificha nyuma ya kichaka cha injili. Bahati nzuri, Biblia ilishatutahadharisha juu ya kuibuka kwa manabii wengi wa uongo katika siku za mwisho.

Gospel consumer beware!
 
Mkuu, kosa la kwanza la Yesu ni kujiita mfalme wa wayahudi huku akijua mtawala ni mrumi,
Hebu wacha kichekesho... Ulichokiandika ni kwamba hakuna uhusiano...Nadhani hujui mfumo mzima wa jinsi serikali ya kirumi (kikoloni) na tawala za mahali ambapo lilikuwa lina exercise koloni lake...Ni bora ukae kimya...
. Kosa jingine dhidi ya wayahudi ni yeye kujiita mwana wa Mungu, hayo mawili yalitosha kupata adhabu aliyopata.
HApo umesema ni kosa dhidi ya Wayahudi...Sasa Serikali ya Kirumi inaingiaje hapo...? Hivyo walimhukumu Yesu auawe ni nani...?? WArumi walikuwa ni wapagani na wala maswala ya kujiita mwana wa Mungu yalikuwa hayawahusu kamwe...

Usijitoe ufahamu kama Tahira au katika familia yenu na ukoo wenu mna historia ya kuwa na matahira... hizo Elimu mnazozipata ziwafanye muwe mnafikiria kidogo....NDIO MAANA MIMI NIKAWAITA wALOKOLE WOTE DUNIANI NI GENGE LA WATU WAJINGA WALIOJIFICHA KWENYE MWAMVULI WA DINI....
 
kuna tengenezo moja tu linalofanya na waumini wake wanajitahidi kufanya mapenzi ya MUNGU,mafundisho yao yanabase kwenye Bible, hawana michango ya kukabana koo wanachojali umjue Mungu, ndo tengenezo ambalo kadri miaka inavyokwenda wanazidi kuongezeka.
yahitaji utulivu kuwajua katika dunia hii ya mvurugano, YESU alisema barabara zipo mbili tu , ya uzima wa milele na ile ya upotevu unahitaji hekima sn kuijua barabara sahihi ni ipi huku ukiwa na Bible yako pemben ikikusaidia kuwajua WAPI ni sahihi.

Nao ni Mashahidi wa YEHOVA pekee
 
Vita ya manabii wa kizazi kipya iyo.Ni ngumu sana kujua mkweli ni yupi?.mwisho wa siku nmewaweka kundi moja la wapiga dili
Ngumu vipi kujua mkweli ni yupi ! Wakati wewe umeweza tayari kuwajua maana hapo hakunaga mkweli ni wapigadili tu ,ukianza kutafuta mkweli ni yupi tayari wewe umesha ingizwa chaka la wapumbaavu
 
Kwani alikosea nn??
 
Ukiona hivyo ujue ulokole ni kama umalaya leo kule kesho huku
Sio walokole tu wanaohama wakatoliki,walutheri ,Angilicana nk sababu kubwa ni kuwa kiwango Cha elimu za watu Kiko juu kwa Sasa .Ile mtu kusema ndiyo,ndiyo kwa kiongozi wa dini haipo.Zamani watu walikuwa elimu hawana kwa hiyo kiongozi ndiye alikuwa msomi peker mkubwa mtaani au kijijini mtu unakuta anaapa kufia dini.Enlightment ya watu ikiongezeka kupitia elimu dini inakuwa mhanga wa kwanza kuumia.Mfano kipindi Cha enlightment ulaya na Marekani ndipo watu walianza kuhoji mambo ya dini zikaibuka dini kibao ukatoliki ukaanza keambaratika kuzaa madhehebu kibao Kama ulutheri,Anglikan nk.
Kwenye kuhama Hama hakuna kanisa linalonusurika kwa Sasa halipo hata moja Wawe wakatoliki au walokole.Sababu kubwa ni kuongezeka kwa elimu.Hivyo mwenye convincing power kubwa ndiye Ana win .Mtu kwa Sasa kuikubali dini so kwa zile cheap reasons za zamani kuwa ohh abudu kwetu sisi ndio dini ya kwanza!!! Au ohh abudu kwetu sababu sisi hatutumii mafuta ya upako!!
Unatakiwa ujenge hoja hasa.
Mfano wewe unasema watu wanahama sababu Ni Kama Malaya hivi unaona mtu aweza kukuona kuwa una akili si atakuona mjinga tu.Mfano mtu anayebadilisha biashara moja kwenda nyingine kutafuta faida zaidi utamuita Ni Kama Malaya?
Ukosefu wa ujengaji hoja Kama wako ndio hufanya watu wengi zaidi kuendelea kuhama sababu wanasema reasoning ya kiongozi wa dini nilipo iko chini na Yuko hopeless.
 
Tatizo mnapenda matusi hata pasipostahili, hivi ungeandika kawaida tu ukasema unachokijua bila matusi nini kingeharibika? Umesoma vizuri nilichoandika mkuu? next time acha matusi na utakuwa mtu mzuri kabisa.
 
Kuna Yule wa Winners Chapel International. Yule ni shida mkuu
 
Tatizo mnapenda matusi hata pasipostahili, hivi ungeandika kawaida tu ukasema unachokijua bila matusi nini kingeharibika? Umesoma vizuri nilichoandika mkuu? next time acha matusi na utakuwa mtu mzuri kabisa.
Ni lugha ya kawaida kabisa hiyo.... Hebu nioneshe tusi hapo...?
 
Vita ya manabii wa kizazi kipya iyo.Ni ngumu sana kujua mkweli ni yupi?.mwisho wa siku nmewaweka kundi moja la wapiga dili
Mkweli ni Neno la Mungu pekee. Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
 
Yesu alisema hiki ni kizazi cha nyoka kinachotaka ishara ni miujiza naye akasema hakitapata ishara au miujiza isipokuwa ni muujiza kama ule wa Yona wa kumezwa na samaki. Ndio maana mnapigwa ili muone muujiza lazima mununue maji ya upako. Mnatembea na michanga na udongo kwenye mifuko na mikoba yenu. Kizazi cha miujiza na ishara ni shida sana.

Hivi kuna watu ambao Mungu aliwafanyia miujiza mikubwa kama wana wa Israel jangwani? Kuna ile miji miwili korzani na Bethaida Yesu alitenda miujiza mikubwa ila hawakumwamini akatoa ole kubwa sana. Miujiza ni kwa ajili ya kuvuta wasioamini ila Neno huwajenga watu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…