Miujiza: Atangaza kukimbia kutoka Kigoma hadi Dar kwa miguu ndani ya siku 18

Morg

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
1,301
Reaction score
1,788
Mkazi mmoja wa mkoa wa kigoma jina kapuni ametangaza kukimbia kutoka kigoma Hadi Dar kwa miguu kuja kutazama mechi ya Simba na Yanga tarehe 8 June mwaka huu

Huu ni muujiza anataka kutuaminisha nini huyu bandugu kukimbia kilometers 1088 na miles 676 kwa mguu ndani ya siku 18 ni maajabu. Nachokiwaza hapa huyu mtua atamaintain vp hizo kilometers ndani ya siku hizo 18 ili aweze kufika Dar .Kwa kiuhalisia nadhani ni jambo amabalo haliwez kutokea nadharia. Hii hakuna kbsàa

Wana jf unamsemaje katika hili je unadhani atauweza kwa kigezo kipi labda.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa Kigoma uwa ni wagumu mno,hasa kwenye michezo.hata wanasoka wanaotoka Kigoma wamedumu sana kwenye ligi ya soka wengine wamestaafu wakiwa kwenye viwango vyao bora.
Alafu ni wabishi sana.
 
Kama ni km 1088 ina maana kwa siku akimbie 60.4 kms.

Mathematically ni kitu kinawezekana mafano tumkadirie tu awe anamaintain speed ya 10km per hour hapo inamaana kwa siku atatumia takribani masaa sita (6) ku cover hizo km 60.4 (anaweza kutumia chini ya masaa 6 kama ana endurance)

Issue kubwa ni kuwa awe ni high performer kwa maana ya kuwa ana experience labda ni athlete au huwa anafanya sana mazoezi. Pamoja na hayo lazima awe amejiandaa vizuri kwenye suala la recovery kuanzia kwenye ku replenish energy aliyotumia (hapa namaanisha suala ya vyakula na vinywaji), kupumzika vya kutosha (kulala) na kutunza misuli na joint kutokana na mkimbio huo mkubwa (kuna mazoezi na njia za ku recover baada ya high intensity performances).

All in all ni kitu kinawezekana kama huyo mtu amejipanga. Kama amekurupuka tu atatema ulimi.
 
Hii Taarifa imeletwa kinafki nafki huyo ni Mwanariadha na hii ni mbio yake ya tatu , Na anataka kuvunja rekodi amewahi kukimbia kutoka Kigoma hadi Tabora kwa siku kadhaa
Safari hii ni mpaka Dar es salaam kwa siku hizo 18 na KIKUBWA ni hizo MBIO zake na sio YANGA.
 
Mpango ana kazi kweli kweli ...akili za ndugu zake hazina tofauti na dagaa wa lakeTanganyika !.. wee ona baba levo na mwijaku .. ndio wapo hivyo hivyo!
 
Machizi nchi hii ni mengi mpaka kero.
 
Kila jambo huanzia kwenye ubongo...lazima uliweze kwanza ndani ya nafsi yako ndio utatekeleza kwenye ulimwengu wa uhalisia
 
Kutoka kigoma mpaka Dar kwa miguu ni gharama kuliko angepanda gari.

Hii inafanya niamini kua ana chanzo cha pesa stable kabisa na kinatosheleza pia yeye ni mwanamichezo mwenye jopo la madaktari na wataalamu watakaosimamia lishe yake, kupumzika na kukimbia kwake kwa kipindi chote hichi.

Aliyeenda kuangalia kaburi la Magufuli kwa baiskeli ameshafika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…