Pre GE2025 Miundombinu ya Barabara na Madaraja: Wanasiasa na Hila za Kukarabati Kipindi cha Uchaguzi

Pre GE2025 Miundombinu ya Barabara na Madaraja: Wanasiasa na Hila za Kukarabati Kipindi cha Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Tunaelekea Mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani

Kadri tunavyokaribia mwaka wa uchaguzi mkuu, tutashuhudia mengi kutoka kwa viongozi walioko madarakani na hata wale wanaotaka kuonyesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa kawaida, kuna tabia za viongozi fulani — wabunge na madiwani — waliokaa madarakani kwa miaka mitano tangu kuchaguliwa na wananchi, lakini hawakutekeleza majukumu yao kikamilifu. Hawa ni wale ambao, kwa kipindi chote cha uongozi wao, hawajashughulikia changamoto za msingi kama miundombinu ya barabara na madaraja, ambayo mara nyingi imekuwa mibovu sana. Lakini sasa, ghafla wanajitokeza wakiwa na ahadi tele au kuanza miradi ya dharura ya kuchonga barabara au kukarabati vikaravati vya mitaa.

Hili ni jambo la kushangaza na la kusikitisha — ni sawa na danganya toto! Ni hila ya kuwarubuni wananchi ili wapate nafasi nyingine ya kubaki madarakani, huku lengo lao likiwa ni kuendeleza maslahi binafsi na familia zao.

Kwa mfano, katika mtaa ninaoishi, barabara zimekuwa mbovu kwa muda mrefu sana. Hakuna aliyechukua hatua yoyote ya kuzifanyia kazi, lakini sasa, kwa ghafla, wameanza kupima ili wachonge barabara za muda, kama "rafu road." Mimi naiita hii ni ujinga wa hali ya juu na siwezi kuvumilia uongo wa aina hii. Ni jukumu letu, kama wananchi, kutambua hila hizi na kufanya maamuzi sahihi zaidi kwa maslahi ya muda mrefu.

Wananchi Wenzangu, Huu Ndio Muda wa Kuwa Makini

Sasa ni wakati wa kupima kwa umakini kila ahadi na kila hatua wanayochukua wanasiasa hawa, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi. Tusirubuniwe na maneno matamu au miradi ya dharura inayoanza kuonekana ghafla kwa sababu ya uchaguzi. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunawachagua viongozi wanaojali maslahi ya wananchi kwa dhati na si wale wanaojali tumbo lao pekee.

Tujifunze kutoka kwa uzoefu wa miaka iliyopita, tusikubali kupotezwa tena, na tuwe makini katika kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wa jamii yetu na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom