Kweli kwa mitandao ya 4G Tigo hana mpinzani kwenye spidi ya Internet yake, hii ninaongelea kwa experience yangu hapa ninapoishi (Kama mtoa mada anavyoongelea eneo lake analoishi).
Kwenye peak hours (muda ambao watu wengi wametoka maofisini na wapo majumbani wanatumia Internet kwenye simu zao, tuseme kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 usiku hivi) internet ipo vizuri na inacheza kwenye 30mbps hadi 40 mbps
View attachment 2582573
Kwenye mida ya kawaida wasipokuwepo watu wengi tuseme usiku wa manane hadi mida ya saa 10 jioni tunacheza 60 mbps kukaribia 90 mbps.
View attachment 2582578