Mizani yote ya kupima magari asilimia kubwa sensor zinazimwa makusudi

Mizani yote ya kupima magari asilimia kubwa sensor zinazimwa makusudi

halfcastmangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2023
Posts
605
Reaction score
1,644
Kuna suala linawaumiza kichwa sana madereva walio wengi wanaondesha vyombo vya moto vyenye uzito kuanzia tani 3.5 au zaidi,

Labda nianze kwa kusema mizani mingi sana Tanzania iliwekwa sensa na foleni ktk mizani kwa kiasi kikubwa ilipungua, ila baada ya kifo cha mpendwa wetu Hayati Magufuli shida imerudi tena kubwa, foleni kubwa hata gari ikiwa na nusu ya uzito taa inawaka gari iingie mizani, hata saa ingine ikiwa haina mzigo taa inawaka iingie mizani, inaudhi sana.

Sasa swali ni hili, kama serikali iliwekeza fedha nyingi katika mizani kwanini wananchi wateseke? Kuna mizani sugu na ina sensa, vigwaza, tanangozi, mpemba na mingine wadau wataongezea.

Waziri mwenye dhamana, tunaomba fuatilia hili kwa usiri, pana rushwa kali sana ktk mizani. Kuzimwa taa ya sensa na kadhalika.
 
Ungefuatilia vizuri kwanza.

Kuzima censor maksudi ndio kufanyaje sasa!.

Hiyo censor(kihisishi) inasoma kwa uzito ambao gari linaweza kuzidi vipimo, ndiyo linaamuliwa liingie mizani kupima.

Sasa ulisema wanazima censor ili magari yasiyostahili yaingie kupimwa hiyo haieleweki.

Ukizima censor maana yake haitasoma, na siyo kwamba itasoma gari liingie kupima.
 
Naweza nikakubaliana na ww ila naomba nisaidie ktk hili, inakuwaje gari yako GVM ni 40,000 ukipakia mzigo ukiwa na GVM 47 sensa inakuruhusu upite ila kwa gari hiyohiyo ukiwa empty siku ingine taa nyekundu inawaka ukapime?
 
Hivi unajua GVM mwisho ni 50,000. Kwa semi trailler.

Inakuwaje uwe na GVM 47,000 sensa ikuruhusu upite bila kupima wakati kuna uzito wa excel?

Unaweza ukawa na GVM ya 47 lakini ukazidi kwenye excel.
 
Back
Top Bottom