Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive


YAni hawa jamaa wanajifunza sheria za BUNGE kwa miaka mi-5!!what about half pay,or no pay at all for that time as well?!!

these people are not serious at all,TANZANIANS should LOOK at HAITI,it has been independent for over 2 centuries(over 200 years!!)now,BUT STILL VERY POOR.with these rate of current leaders,we are going to break the record for independence/development curve!

it is time that Tanzanians understand the party that brought them independence is not necessarily going to give them development.

with this kind of arrogance,a leader saying he is supposed to be given five years to study parliamentary laws and regulations,we will not get anywhere.
 
- I am not against ukomo wa wabunge bungeni, lakini someone atuelimishe jinsi hii inavyoweza kutunufaisha taifa kwa sababu naona bado tunalikwepa tatizo la uwezo mdogo wa viongozi wetu,

- Tunahitaji a built in system katika politics zetu ambayo itawatema viongozi wanaonyesha uwezo mdogo, kama kule Carlifornia gavana Davis alionyesha uwezo mdogo wa uongozi, wananchi wakakusanya signatures zinazotakiwa kisheria, wakamuondoa kwenye nafasi.

- Ukomo wa viongozi peke yake hautoshi, tunahitaji more than that!

Respect.

FMEs!
 
Siamini chochote asemacho kuhusu mali zake kwani hakuna namna yeyote ile ya kuthibitisha. Ingekuwa kama wanavyofanya Marekani na kufile taxes hapo kidogo tungeweza kuweka imani ktk ayasemayo

OPP, umeongea point kubwa sana kuhusiana na kufile taxes kila mwisho wa mwaka na kuonyesha mali zote za muhusika zilizo ndani na nje ya nchi. Utaratibu huu Tanzania hatuna na hivyo mheshimiwa anaweza kabisa kudanganya kuhusu mali zake na hakuna namna ya kuthibisha mali alizozitaja ni kweli ndiyo hizo tu au kuna nyingine kwa makusudi hakuamua kuzitaja ili kutoonekana ana utajiri wa kupindukia.

Kwa maoni yangu hakuna ubaya wa kiongizi kuwa tajiri kama utajiri huo kaupata kwa njia za halali.
 

Mkuu Invisible......umeona hiyo hapo juu?


Mkuu Invisible.....umeona mediocre type of wabunge kama huyu Kijiko........yaani mijitu inagombea ubunge lakini haina hata vision/malengo ya kuwatumikia wananchi......yaani inaingia bungeni 5years za kwanza anajifunza matatizo!!.....yaani mtu mpaka unakuwa mbunge unakuw ahujui matatizo ya wananchi husika?......DAMN!.........do we really these type of people.........

Watu waelewe kuwa uongozi ni KUJITOLEA KUWATUMIKIA WANANCHI ili wafikie malengo ya maendeleo yao kwa kipindi fulani............na sio kuhodhi uongozi ukitgemea fadhila za Chama na Rais akuteue............Tena napendekeza term iwe moja tu.....mtu akishindwa/akiweza kutimiza yale aliyoahidi at least 75%.......aruhusiwe kugombea tena baada ya term moja kupita............sio mijitu inang'ang'ana tu bungeni huku hai-perform........

Mtu lazima ajue matatizo ya wananchi wa sehemu anayotaka kugombea......na aainishe/aweke mkakati ni kwa jinsi gani atatatua matatizo hayo within 5years term.........akishindwa apigwe chini..........

Kule Rombo.......wananchi walimpa kura tena Mramba kwa sharti moja......."tunataka barabara ya lami + Maji"....PERIOD.........na jamaa (Contractors) wanashughulika sasa hivi kule.....sijui ile miradi imeishia wapi.........
 
UAMUZI wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kutangaza mali zake, sasa ni mtego wa kisiasa kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye amekaa kimya tangu aingie madarakani mwaka 2005.


Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanaeleza kuwa kiasi cha utajiri mdogo alionao Pinda unaweza kuwa kikwazo kwa Rais Kikwete na viongozi wengine kutangaza kwa vile wengi wao wamejilimbikizia mali.


Akitangaza mali zake Alhamisi iliyopita jijini Dar es Salaam, Pind
a alisema ana Sh25 milioni kwenye akaunti yake, nyumba tatu za kawaida zilizo Dar, Mpanda na Dodoma na gari alilolinunua kwa mkopo.


Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema: "Na kikubwa ambacho mimi nasema kwa nafasi hizi (za uwaziri), pengine mimi sielewi unataka utajiri ili ufanye nini,". Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu ni utaratibu mzuri unaoweza kuweka wazi mali za viongozi ili wasije kupotoka kimaadili.

"Ninajitahidi kujaza fomu za sekretarieti ya maadili kila mwaka na ninazipeleka huko na kwa sababu sijaulizwa napenda niamini kwamba sijagombana na tume," alisema Pinda ambaye alianzia naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na baadaye waziri kamili kabla ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu mapema mwaka juzi.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17368
 
kusema ukweli kama Pinda anasema ukweli bila shaka ni mfano wa kuigwa,naye mkuu wa kaya afuate nyayo zake!!!!!!!!!
 
Hofu yangu si kuishia kutangaza, je ataendelea ku maintain hali hiyo ya usafi kama ambavyo anatuaminisha au yatakuwa ni yale yale kama Ben?kama hata maintain huo usafi, ni bora awe kama muungwana ambaye hajatangaza na hatatangaza daima na milele!Amina.
 
Kikwete hawezi kutangaza mali zake, kama alishindwa wakati anaingia madarakani leo hawezi, maana ile gharama ya ujenzi kwenye mradi wa CHALINZE inatia shaka kua nani anafadhili ama amepata wapi cash yakujenga ule msululu wa majengo yale.
 
Kikwete hawezi kutangaza mali zake, kama alishindwa wakati anaingia madarakani leo hawezi, maana ile gharama ya ujenzi kwenye mradi wa CHALINZE inatia shaka kua nani anafadhili ama amepata wapi cash yakujenga ule msululu wa majengo yale.

Ni kweli kabisa ile mijengo imesimama pale si mchezo, huwa nikipita pale naishia kugugumia kwa maumivu ya uzalendo wa nji hii umebaki wapi?
 
Pinda ni mnafiki sana kwa hakika,hawezi kuwa na mali kidogo hivi huu ni uongo kabisa.Kwa kuwa amekuwa katibu wa bunge kwa miaka 30 ambayo kila wiki analipwa sitting allowance mbili za juuu kabisa ambazo ni za level ya cabinet....amekuwa miaka yote hio akienda bungeni dodoma na kupata allowance kama supportive staff wa serikali na kuwa anapata posho kubwa...analishwa na serikali na kupewa mahitaji yote akiwa ndani na nje ya ofisi na huku analipwa perdiem ya serikali ambayo hana cha kuitumia kwa kuwa kila kitu kinalipwa na serikali kabisa............kwa maisha alioishi huyu shushu waserikali ni vigumu kuwa na hela ndogo hivi.
 

Mzee Bubu, Heshima mbele Mkuu,

Wakati mwingine inaniwia vigumu kuelewa ni njia zipi halali ambazo kiongozi anaweza kuzitumia kupata utajiri. Kwa mfano ukichukua viongozi walio kwenye nafasi za uongozi kwa miaka 15 sasa i.e. tangu mwaka 1995 wakati Rais Mkapa anaingia madarakani ni wangapi walikuwa matajiri wakati huo? Kama hivi sasa ni matajiri wameupataje utajiri huo na kwa njia zipi halali?

Kwa maoni yangu, concept ya kiongozi katika nchi maskini kuwa tajiri haina mantiki.
 

Akina Lusekelo ndio waandishi waliobobea! Alichoandika kinaweza kumtoa mtu machozi kutokana na lugha aliyoitumia ambayo inaelezea hali halisi ya nchi yetu ilivyo. Aidha ameichora picha halisi na sahihi ya jinsi Pinda alivyo.

Well done Mzee Lusekelo, naona akili ya uandishi haijastaafu!
 

In a question and answer session with editors held in Dar es Salaam this noon, Mr Pinda also said that he has only one private car."
Kauli na majibu ya Anna Makinda wakati akihojiwa ni ya kibabe na ya kumkosea heshima Waziri Mkuu. Kutokana na taarifa zilizoandikwa magazetini hatujaambiwa kwamba Waziri Mkuu aliitisha mkutano wa Waandishi wa Habari kwa madhumuni ya kutangaza mali zake. Hata kama alifanya hivyo si kitu cha ajabu kwa Pinda kutangaza mali zake. Katika kipindi hiki ambacho viongozi wanashutumiwa kutumia nafasi zao kwa manufaa yao, Anna alipaswa kumsifu Pinda kwa kutangaza mali zake badala ya kutoa kauli ya kuli-dismiss jambo hilo kama halina faida ama maana yoyote. Nadhani ile sifa aliyowahi kupewe Anna Makinda huko nyuma ya kuitwa ‘iron lady' inamlevya!

Tatizo linalojitokeza kwa viongozi wa CCM waliokaa kwenye nafasi za uongozi (Ubunge n.k.) kwa muda mrefu ni kujiona kwamba wao ni bora kuliko wengine. Hoja ya Ndugu Pinda kwamba Wabunge wakae vipindi vitatu tu Bungeni na baada ya hapo wawapishe wananchi wengine wanaotaka kuingia kwenye uongozi ina mantiki. Hii Tanzania ni ya wote na kila mmoja aliye na sifa zinazohitajika anayo haki ya kugombea na kuchaguliwa kuwa kiongozi. Hakuna mwenye 'hatimiliki' ya uongozi!


Usalama wa Taifa, Idara ambayo inaendeshwa na WATU, ndio inayoliwezesha Taifa kuwa na Amani na Utulivu. Kwa hiyo kusema kwamba watu wa Usalama wa Taifa ni hatari na waoga ni uzushi. Wangelikuwa hatari Tanzania pasingelikalika! Mkapa kamzidi nini Pinda? Kwa mtazamo wangu Pinda ni msomi, mzalendo na anaweza akawa na vision itayaoweza kulikwamua Taifa hili kutoka kwenye ufisadi uliokithiri kushinda Mkapa. Ndio maana Pinda ameweza ku-declare mali zake na kudhihirisha usafi wake amidist manyang'au waliolihujumu taifa na wanaoendelea kuhujumu ambao hawako tayari kuwa wakweli wakijua kwamba wamelitendea dhambi taifa.

Wakati mwingine Watanzania tunajidhalilisha wenyewe kwa kudharau historia yetu bila sababu za msingi. Ule ‘ujima'/ujamaa uliokuwepo ambao leo unadharauliwa na kuzungumzwa kwa kejeli ndio uliozaa Usalama wa Taifa hili. Naam, enzi za ‘ujima'/ujamaa kuwa na mali ambayo hukuitolea jasho, mali iliyotokana na kulihujumu Taifa ilikuwa ni uhaini dhahiri ua ulipigwa vita kwa nguvu zote kwa manufaa ya Taifa. ‘Kupanga ni kuchagua' kama mtu haoni mantiki ya kubana matumizi kwa kutovaa suti, wapo wanaoona mantiki hiyo. After all, wavaa suti katika nchi yenye joto kama hii yetu wanaonekana kama ‘clowns' tu hususan mbele ya wale waliolibuni vazi hilo kukidhi mahitaji yao katika hali ya hewa ya baridi ya nchi zao.
Lini Watanzania tutazinduka na kuacha ushamba wa kuiga mambo at the expense of our own true development? Tungeokoa fedha za kigeni kiasi gani na kuiletea nchi yetu maendeleo kwa kutumia vitu vyetu wenyewe kama walivyofanya Wachina? Wachina walivaa uniform za vimao huko nyuma na kujinyima kwa kila hali ndio maana leo wanatishia dunia kiuchumi!
 
Kuna sababu maalum ya kuweka term limit kwenye nchi ambazo zinafanya hivyo especially the presidential position. Hila at the same time hawa wenzetu wanamakubaliano ya kutovunja programme za maendeleo ambazo zilianzwa na serikali ya awali hata kama walizipinga wakati wao walikua wapinzani. Hivyo umalizia projects iliyokua njiani kwa faida ya taifa, na labda kuibadilisha uendeshaji wake depending on the aim au cost effectiveness. Hii ni role ya central governments its practical kwa sababu at the national level na kuna so many bodies to implement the changes after the policy or even to implement the proposed plan. Lakini hii hoja ya kusema kuwe na term limit kwa wabunge its just absurd. Inamaana hata kama mbunge anawapigania watu wake kuwaletea maendeleo muda wake ukifika nae atoke. Tukumbuke kwamba mmbunge ni only a representative anaweza akawa na long term battle to achieve is goal. Sio kwa matakwa yake bali to convice the policy makers wafikirie jinsi ya kubadilisha anachotaka au kwenye orodha ya uduma anayotaka wapelekea watu wake. Hivyo it is unreasonable to set a time limit for these people kwa kuwa wao wako independently in most cases, umtoe mtu ambaye yuko mstari wa mbele as a fighter na ulete mwingine kisa eti muda umepita na hata kama watu wake bado wanamuitaji. Najua kuna tatizo la wabunge ambao hawafanyi kazi, hivyo the solution hapa ni kuwa na democrasia tu watu wachague yule anaewafaa. Na namna moja ni kuweka misingi itakayo ruhusu hiyo demokrasia watu wagombee nafasi na si wateuliwe au waonge no wachaguliwe na watu.
 
Lakini Pinda naye ni m'mbeya tu yeye ni waziri mkuu ana uwezo kabisa wa kisheria kumuwekea ngumu JK na kumwambia aache wizi wa pesa ya walipa kodi. Huyu ameona uchaguzi uko malangoni ndio anaanza kampeni zake za kimasikini sikini tu.
 
Ni kweli kabisa ile mijengo imesimama pale si mchezo, huwa nikipita pale naishia kugugumia kwa maumivu ya uzalendo wa nji hii umebaki wapi?


hapo kwenye mahekalu yake ya msata msimamizi wa ujenzi ni rafiki yake subash patel .....anayejenga pale Umoja wa vujuna...,hiyo ni cha mtoto amejenga upya nyumba yake ya mwanzo kule bwagamoyo na ile ya migomani street.....zote zimesimama si mchezo...ndani ya miaka 5...hapo bado akikaribia kumaliza miaka kumi yake au kama mwakani hatagombea kwa sababu yeyote ile atastahili kujengewa nyumba na serikali ..sasa sijuwi hiyo atajenga wapi na ameshajenga kote.....labda ajenge ukweni...!!

siku mkimpelekea microphone atangaze mali zake atakimbia kama kaona ukoma!!! maana mali zilizoota ndani ya miaka 5 ni hizo hata raia wa kawaida wanaziona..wengine vibarua wanaojenga huko..na kumuona akifika [ujenzi kote umekamilika]...je zile zisizoonekana???...maana gharama za miradi yote hiyo ni in terms of Billions!!!
 
nadhani kama pinda hakushauriana naye kabla ya kuwasha moto wa kuangaza mali ....basi kimoyo moyo atakuwa anatamani kumchapa bakora..!!
 

- Only in Tanzania tu, kumbe yale machozi ya kuona nyumba ya mtoto wa El na kuishia kumnyima umakamu wa CCM, yalikua ni machozi ya mamba! Halafu kuna wanaosema dhambi iko Haiti tu!

Respect.


FMEs!
 
- Only in Tanzania tu, kumbe yale machozi ya kuona nyumba ya mtoto wa El na kuishia kumnyima umakamu wa CCM, yalikua ni machozi ya mamba! Halafu kuna wanaosema dhambi iko Haiti tu!

Respect.

FMEs!

..na yeye anaweza kuwa zote ameandika majina ya watoto...sidhani kama atakuwa amejenga majumba yote hayo bila kujuwa pa kuchomokea ... nasubiri kwa hamu siku akitangaza ,,,ni bora waandishi wa habari wambane kwenye next press ...msichangae kusikia akisema yeye ni lofa zaidi...anamiliko lile shamba lake la mananasi ..na halina hata boy qoater....tutacheka sana!!
 

- Atakuwa amepata darasa kwa Rostam the master, maana the man hana mali hata moja yenye jina lake! I hope Pinda hana macho Ikulu!

Respect.

FMEs!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…