Mizengo Pinda: Mwalimu alikataa kuwa 'dictated' na watu kutoka nje kwa sababu ya misaada

Mizengo Pinda: Mwalimu alikataa kuwa 'dictated' na watu kutoka nje kwa sababu ya misaada

Je Marekani ametengwa na nani hata pale Trump alipolalamikia kanuni za uchaguzi kulalamikiwa?

Je hukuona kwa mara ya kwanza maandamano hadi kwenye Bunge la nchi hiyo kubwa Duniani na hata baadhi ya wabunge kutekwa na waandamanaji?

Nani anaikemea Marekani?

Uongozi thabiti wa nchi ya kiafrika sio mpaka usifiwe na wazungu.

Wasomi wa sasa hivi ndio mmekariri kuliko mahitaji yenu.

..kama Magufuli alikuwa anaamini Donald Trump ameibiwa kura basi alitakiwa kukataa kumtambua Joe Biden.

..Nyerere alikataa kuzitambua serikali za Rhodesia na Afrika Kusini kwasababu aliamini hazikuchaguliwa kihalali.
 
Tatizo letu kubwa ni mambo muhimu kuamuliwa na mtu mmoja.
 
Wazee wa kula kwa urefu wa kamba yako wanahisi wanasemwa wao. Hawataki mtu yeyote kutoa maoni yake. Wanataka tu kulamba asali.
 
Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mizengo Pinda akiwa kwenye kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa Taifa, hayati Mwl. Nyerere ameongelea misaada na masharti yanayokuja nayo. Pinda amesema mwalimu alikataa katakata misaada yenye masharti yasioendana na Maslahi ya Taifa.

========

Mizengo Pinda: Kwenye uchumi pamoja na mambo mengine yote, vita ya Uganda na vinginevyo lakini wale mnaojua kilichokuwa kimetokea, nilipenda mimi binafsi, jeuri yake alikuwa anakataa kuwa 'dictated' na watu kutoka nje just because kuna misaada anataka akupatie. Mwalimu alikuwa mgumu sana, alikataa kabisa. Bora nikafe na umasikini wangu lakini hilo unalotaka nifanye siwezi.

Leo wangapi, tukibanwa na mambo hayo mazuri yanayotaka kuja na hili na lile, how many of us wako tayari kutoa masharti ambayo unaona hayaendani maslahi ya Taifa? Lakini yeye aliweza na nakumbuka mzee Mwinyi alipoingia kama Rais wa pili alikutana na hilo jambo, sasa ikawa ngombo. Mwalimu alikuwa na uwezo wa kulibeba hata kama hamjui litaishaje lakini tutafika huko.

=> Kuhusu Mkapa, Pinda amesema pamoja na kuleta 'Ukapa' alipomaliza miaka kumi watu walitamani aendelee.
Sawa alikataa kuwa dictated,atuambie basi miaka 25 ya mwalimu ilikuwa na tija ipi kiuchumi kwa Tzn ukilinganishwa na waliokuwa dicteted kwa ajili ya misaada?
 
Huyu naona ana mawazo Kama ya Kabudi na jiwe...
Ukiwauliza masharti yenyewe ni yapi wataanza kukuambia kuruhusu ushoga, kwa hiyo nchi inapewa msaada Sasa hivi kwa sababu imeruhusu ushoga?

Wakataka waongoze nchi kwa ukatili wa kuua na kutekwa watu, kubaka demokrasia Kisha wakikemewa wanakimbilia kusema Hawa wanataka turuhusu ushoga.
Umewambia ukweli hawa viroboto!
 
Sawa alikataa kuwa dictated,atuambie basi miaka 25 ya mwalimu ilikuwa na tija ipi kiuchumi kwa Tzn ukilinganishwa na waliokuwa dicteted kwa ajili ya misaada?
Hata mama inabidi umwambie uchumi haujengwi kwa pesa. Cash do not build neither structure our economy.
Pesa haijengi uchumi.
 
Maoni ya kizamani kwenye Zama mpya.
Wakae kimya wale pensheni zao na wajukuu zao.
Watuache bhana....

Hawawezi kuwaacha hivi sasa kazi yao ni kuwasimika watoto wao ili warithi vyeo vyao!! Mtoto wa Pinda nae ni Mbunge na ni naibu Waziri!!!
 
Sawa alikataa kuwa dictated,atuambie basi miaka 25 ya mwalimu ilikuwa na tija ipi kiuchumi kwa Tzn ukilinganishwa na waliokuwa dicteted kwa ajili ya misaada?
Mbali ya uchumi, Mwalimu alikuwa na kazi ngumu sana kuliunganisha Taifa kuwa moja na ukabila ukafutika, hiyo ilikuwa kazi ya kutukuka sana, Cha ajabu, ikaharibiwa ndani ya kipindi kifupi tu cha m iaka 6.
 
Mwalimu atakumbukwa kwa kuleta umoja wa kitaifa ila uchumi alivurunda.
 
Back
Top Bottom