Mizimu inaweza 'kukuona' ukiwa kwenye faragha:"

Huo sio mzimuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Kijana anafanya masihara πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Uzuri ni kwamba haya mambo yapo sana na yakiamua kukuvaa ndio utajua.

Kuna jamaa alikuwa ni bitoz nyangema na ana undugu na boss fulani wa zamani wa TISS yamemvaa haya mambo inatakiwa awe mzee wa kilinge.

Mambo yote ya kidunia hayaendi ameamua kuanza kujifunza Uganga sasa hivi na baada ya hapo hata baadhi ya mambo yamekubali
 
Ni roho za watu waliokufa, hususan mababu au wahenga, ambao kulingana na itikadi na tamaduni nyingi za Kiafrika wanaaminika kuendelea kuishi katika ulimwengu wa roho baada ya miili yao ya nyama kufa

Siku nyingine ukiwa na mizimu tupigie selfie....just to remind you, shetani ambaye ni baba wa uongo, ana vibweka vingi sana.

Na anajua kucheza na akili za wanadamu
 
Siku nyingine ukiwa na mizimu tupigie selfie....just to remind you, shetani ambaye ni baba wa uongo, ana vibweka vingi sana.

Na anajua kucheza na akili za wanadamu
Mambo ya mizimu, maono, au viumbe wa kiroho mara nyingi yamejaa mafumbo na changamoto kubwa ya kutofautisha ukweli na udanganyifu, hasa kwa sababu akili ya mwanadamu inaweza kushawishiwa au kudanganywa kwa urahisi kupitia hofu, matamanio, au mambo yasiyoelezeka.
 
Napenda kujipongeza kua karibu n mizimu y ukoo wng maana inanipa maisha. Faida naona mno
Kazi ni kipimo cha utu
Mkuu ni uhakika mizimu inasaidia kwa namna fulani

Nakumbuka mwaka 2007 kuna mtu wangu wa karibu sana alinitegea dawa za kichawi ili nikiruka zile dawa nipotee au niwe msukule yeye awe na hela

Usiku ule jamaa alichezea bakola za kutosha mpaka akasema alikuwa anataka kunitoa kafara apate utajiri. Nini kilisababusha WAZEE πŸ€—

Kuna kipindi fulani tena kuna jamaa aliniwekea sumu kwenye Azam Cola ile nife lakini kwa siku tatu alikuwa halali akizima taa tu anatokewa na joka 🐍 kubwa linamwambia kwanini unataka kumuua fulani ? Amekukosea nini ? Nenda kamuombe msamaha

Haya ni kweli wala sidanganyi
 
Sio kwenye faragha tu, hata ukiwa na mpango wa kuingia kwenye faragha na mtu, inaweza ikakuambia huyo mtu ni nani, kama ni muuzaji, mchawi, kaumia nk
 
Mzimu ni nini?
1. Roho za Wafu: Hizi ni roho, nafsi, au vivuli vya watu (hasa mababu au ndugu) waliofariki dunia zamani.
Katika imani za jadi, inaaminika kuwa mwili pekee ndio unaokufa, lakini nafsi inaendelea kuishi katika ulimwengu wa kiroho na inaweza kuathiri maisha ya waliobaki duniani.

2. Mahali pa Kutambikia:
Neno hili pia hutumika kutaja eneo maalum ambapo watu huenda kufanya matambiko, kutoa sadaka, au kuwasiliana na roho za waliokufa.
Maeneo haya mara nyingi huwa chini ya miti mikubwa (kama mbuyu au mkuyu), kwenye mapango, au makaburini.

3. Kivuli cha Sura ya Marehemu: Hali ya kutokea kwa sura au taswira ya mtu aliyefariki dunia, ama kupitia ndoto au maono
 
Braza umenikata stimu aisee utalipa nakwambia!
 

Kuna watu wengi wametapeliwa na kuliwa na hawa jamaa
 
Pia kwa ndugu zetu waroma (RC) huwa wanawakumbuka mizimu Yao kwa kutumia neno mtakatifu (st)mfano st Peter (Huu ni mzimu) na mifupa yake inakuwepo pale mbele kabisa kwa ajili ya ibada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…