MATATIZO YA IMANI ZINAZO PENDWA
Je wale wanao amini kuwa mwanadamu (roho) anajitambua baada ya kifo wanaweza kukataa kile kitakacho onekana kuletwa kwao na hiyo roho??
Imani kwamba roho za wafu zinarudi kuwahudumia walio hai inafungua mlango kwa ajili ya imani ya kisasa ya mizimu.
Ikiwa wafu wanapata fursa ya kuwa na maarifa yanayozidi yale waliokuwa nayo wakiwa hai, kwa nini wasirudi duniani ili wawafundishe walio hai?
Ikiwa roho za wafu huvinjari juu ya rafiki zao duniani, kwa nini zisiwasiliane nao jamaa zao walio hai?
Je ni kweli watu walio kufa wapo mbinguni wakitazama yale tunayotenda? Luka 16:19—21
Karibu wakristo wote huamini kuwa mara baada ya kifo ‘roho’ huenda mbinguni, pagatori (mahari pa kutakasia dhambi ndogo) ama mahali mahali wapaitapo kuzimu au ahera (peponi). Kwahiyo, watu wengi wanajaribiwa kufikiri kuwa wapendwa wao walio kufa wapo mbinguni. Na kama haitoshi, wanafikiri kwamba baada ya kifo, wapendwa wao wanayo fursa kuona kila linaloendelea kwa marafiki na familia walizoziacha.
Fundisho kwamba roho haifi ndiyo msingi wa imani kwamba waliokufa wapo mahali Fulani wanatutazama, tunaweza kuwaendea wakatutatulia shida zetu (umizimu). Hii dhana ya kuwa ‘roho’ yaweza kuishi yenyewe nje ya mwili halipo kabisa katika biblia. Dhana hii ililitwaliwa kutoka kwa wapagani wa kale wanafalsafa wa Kimisri na Wayunani na mwisho likapenyeza katika theolojia ya Kikristo.
HALISI AU MFANO: Luka 16:19—21
Watu wanaoamini kwamba roho haifi na kwamba yapo maisha baada ya kifo hutumia Luka 16: 19 –21 kama uthibitisho. Je hilo ndiyo fundisho halisi la mfano huo?.
- Mfano huu ni wa mwisho katika mfululizo wa mifano mitano (luka 15 na 16) ambayo Yesu alikuwa akijibu malalamiko ya Mafarisayo kwamba ni kwa nini alikula pamoja na wenyedhambi. Kila mfano ulilenga kulaumu kiburi na unafiki uliokuwa umeshamiri kwa viongozi wa dini kwa kuwaambia ‘ufalme wake ulikuwa zaidi ya sherehe; ulikuwa ni kujumuika pamoja Mungu na wanadamu (questions on Doctrines uk 549)
- Katika mfano huu Yesu hakuwa anafundisha habari za roho na wafu. Husichanganye madesa kujasitifai anijasitified.Angalia mfano huu jinsi unavyofanana na tabia za Mafarisayo ambao waliamini wanastahili upendeleo toka kwa Mungu. Uzima wa milele ulikuwa kwa watu kama Lazaro.
- Fundisho la imani haliwezi kujengwa katika mfano; Kwa vile mfano ni ufafanuzi kuhusu ukweli Fulani.
Fungu jingine lenye utata ni ‘ufunuo 6:9
Hii ni lugha ya picha (symbolic language) Vitabu vya ufunuo na Danieli vimeandikwa kwa lugha ya picha. Utapoteza maana ukitumia tafsiri ya moja kwa moja (Direct translations). Kwa nuru ya Mhubiri 9:5, Hapawezi kuwepo ‘roho za wafu’ zinazo oongea mbinguni, ama roho zinazo mlilia Mungu.
Sikia Luka 20:38 ‘ Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake’’
Ukweli ni huu
- Mungu pekee ndiye hasiyekufa. Ndiye pekee anaishi milele, na kwake hapana uharibifu ama kifo 1Tim 1:17 na 1Tim 6:16
- Tutapokea kutokufa kupitia Yesu tukifika mbinguni (uzima wa milele) Ufunuo 21: 4, 1Kor 15: 53,54