Mizimu

Mizimu

Kila binadamu aliyepo duniani ana watangulizi wake.. Baba, Mama, Babu, Bibi na kuendelea.. Watangulizi hawa wanaacha alama kwa kizazi chao kinachofuata.. Unaweza ukawa na sura yao, tabia zao, Jina lao na hata kufanana kwa makundi ya damu.. Watangulizi hawa wanaweza kukuachia alama ambazo huwezi kuziona kwa macho wala kufananisha.. Mfano kutembea na hata kucheka au kutabasamu..

Watangulizi hao ambao tunawaita mizimu kawaida wana uhalali mkubwa sana kwetu na wana nafasi kubwa sana katika maisha yetu hapa duniani.. Wewe uliyepo hapa duniani huna nafasi ya kuishinda mizimu ya kwenu mpaka pale utakapovunja muunganiko wako na mizimu hiyo..(hili sitaliongelea)

Binadamu anapozaliwa moja kwa moja anakuwa mali ya mizimu hiyo.. Mizimu ina uwezo wa kuzuia mafanikio yako.. Mizimu inaweza kikupa mafanikio.. Mizimu inaweza kukuchagulia kazi ya kufanya na pia inaweza kukuzuia kufanya kazi fulani.. Mizimu inaweza kukuepusha na majanga na pia kukuletea majanga.. Hii itatokana na ufahamu wako kuhusu mambo hayo..

Kutokujua habari za mizimu sio suluhisho la wewe kuokoka na nguvu za mizimu.. Naahirisha kwa kusema kuwa mizimu ipo na ina nguvu kubwa sana katika kuathiri maisha ya mtu aliye hai..

NTAENDELEA

Endelea mkuu umeshusha facts
 
Endelea mkuu umeshusha facts
Mizimu inawatesa wengi
1: wengine wamevaa bangili za chuma mikononi sababu ya mizimu
2: kuna watoto wameacha shule, kila wakienda shule hawaoni ubaoni, wanaona mauza uza kisa mizimu
3: Mizimu ni Upagani moja ya Tamaduni za asili ya Mwafrika, hazina uhalisia katika Ukweli wa Biblia
4: Mizimu ipo tangu enzi ya Kuandika kea Biblia lakini Biblia inazifunua kama ushetani, ushirikina na Upagani (Soma Isaya 8 mlango wa 19 na 20)
 
Kumbe hii mibangili ni ushirikina wa kimizimu, unakuta mtu kavaa bangili kubwa limepauka kiasi kwamba halionyeshi utanashati wowote zaidi ya kumfanya mtu aonekane kama mganga wa kienyeji.
 
Soma kitabu cha Ayubu, wafu hawana kumbukumbu lolote duniani..........watoto wake watapata taabu au hata kufanikiwa yeye hajui lolote. Hiyo inayoitwa mizimu ya mababu ni roho chafu au majini ambazo zinavaa uhusika wa wale marehemu waliotangulia ili ziabudiwe na ziwasaidie kupata mafanikio, ndo maana zinatolewa sadaka kama hizo za pombe, mazao na wakati mwingine kuna kafara za wanyama na watu.

AYUBU: MLANGO 14. 10 Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? 11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; 12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini. 21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.​
kwahyo kila kabila lina majini yake ? maana utakuta kabila hili wanafanya hivi na lile vile kwenye mambo haya.

Je kweli kama majini yanavaa uhusika wa watu hao majini huwa yanakunywa pombe na kutumia vitu vingine ambavyo tunajua kwa majini ni ngumu kuvitumia?
 
Sense ya hapa ni hii; Upagani umejengwa juu ya mizimu, kwa hilo upo sahihi
Ukija katika usahihi wa Maandiko matakatifu umizimu ni Upagani na ndo ma'ana Sauli mfalme enzi za Waezrael alimwendea yule bibi mchawi Ili amwinulie Sauli: Msimamo wa Biblia ni Huu Isaya 8 :19-20 " Je haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao??
turudi hapo kwa Sauli kuinuliwa roho ya Samwel je kilichoinuliwa ni nini?

kuna haja gani ya kusema hayapo wakati hata biblia inatoa kabisa mfano sahihi wa kuinuliwa roho ya Samwel? na tunaona kitu kinatendeka.
Mimi hapa nionacho ni doctrine, lkn kusema sijuh majin sijuh nini hapa tunadanganyana, mizimu ni mizimu na majini ni majini.
 
kwahyo kila kabila lina majini yake ? maana utakuta kabila hili wanafanya hivi na lile vile kwenye mambo haya.

Je kweli kama majini yanavaa uhusika wa watu hao majini huwa yanakunywa pombe na kutumia vitu vingine ambavyo tunajua kwa majini ni ngumu kuvitumia?
Nimeshakwambia hizo ni roho chafu, kwa kizungu zinaitwa evil spirits......nisome vizuri unielewe.
 
turudi hapo kwa Sauli kuinuliwa roho ya Samwel je kilichoinuliwa ni nini?

kuna haja gani ya kusema hayapo wakati hata biblia inatoa kabisa mfano sahihi wa kuinuliwa roho ya Samwel? na tunaona kitu kinatendeka.
Mimi hapa nionacho ni doctrine, lkn kusema sijuh majin sijuh nini hapa tunadanganyana, mizimu ni mizimu na majini ni majini.
Soma vizuri kisa cha

Soma vizuri 1 Samweli 16: 14----"Roho wa BWANA akamuhacha Sauli, Roho mchafu akamwingia--- Mizimu, mizuka, majini wote ni mawakala wa shetani!
Haijalishi mizimu ukiitumia inafaida, ni mlinzi, anatoa njozi utabiri nk ,ukweli ni kwamba ni Roho zinazotokana na shetani
 
kwahyo kila kabila lina majini yake ? maana utakuta kabila hili wanafanya hivi na lile vile kwenye mambo haya.

Je kweli kama majini yanavaa uhusika wa watu hao majini huwa yanakunywa pombe na kutumia vitu vingine ambavyo tunajua kwa majini ni ngumu kuvitumia?
Swali zuri, aje atoe majibu
 
Kumbe hii mibangili ni ushirikina wa kimizimu, unakuta mtu kavaa bangili kubwa limepauka kiasi kwamba halionyeshi utanashati wowote zaidi ya kumfanya mtu aonekane kama mganga wa kienyeji.
Hiyo ni mizimu, kama Tatizo limetokana na mizimu ya ubabani unavalishwa bangiri mkono wa kulia.
Ikiwa Tatizo limetokana na ukoo wa ujombani(umamani) unavaa bangiri mkono wa kushoto
 
Mimi nilifikiri hawa watani zangu elimu imewakomboa, kumbe bado wanajenga vibanda vya mizimu wanaweka pombe na kahawa......shomilee!
 
Kwa habari ya mizimu nahisi wanatheolojia wengi hawajapata kukutana na tukio la marehem kuongea kupitia mtu hai.
Hata kimakabila kuna ambao hawakutani na hali hii.
Lakini kwa wahaya hasa ukimwambia marehem hawezi kuongea kupitia mtu (enchweke), ni suala tu la kuamua kugomea fact.
Tunachoweza kujadiliana ni uwezo na mipaka ya roho hiyo.
Binafs mimi ni mbishi sana kuhusu hizi habari labda kutokana na iman yangu ya kikristo na elimu dunia iliyoongezwa. Lakin kuna tukio la macho yangu niliishia kusema..iiiii bado sijaelimika vyema, au ni ukorofi wa kutokukubali nisichokiamin!
Yan marehem ninayemjua alimwingia binti yetu. Sauti yenyewe. Mkao wa marehem wenyewe. Hadi upumuaj wenyewe. Ujumbe unagonga kwenye hali halis ambazo aliyeingiliwa hata hajui. Na ubish wangu nikajisemea .kweli kuna maarifa hatupewi vizuri.
Elimu za wazungu nazo zina ukomo taarifa aisee, maana wanakosa uzoefu au wanalazimisha tuamini wanachokiamini
Hio ni michezo ya shetani.Shetani anavaa mwili wa mtu yeyeto wa zamani aliyehai na kujifanya yeye kwa kukopi KILA kitu, kumbuka Mzimu unaishi hadi miaka elf 6 so unazo taarifa zote za mtu tangu yupo tumboni na atakuwa nani hadi atakapokufa.Generation nzima ya familia tree yako kuanzia chimbuko la ukoo au kabila fulani unao.
 
Mizimu inawatesa wengi
1: wengine wamevaa bangili za chuma mikononi sababu ya mizimu
2: kuna watoto wameacha shule, kila wakienda shule hawaoni ubaoni, wanaona mauza uza kisa mizimu
3: Mizimu ni Upagani moja ya Tamaduni za asili ya Mwafrika, hazina uhalisia katika Ukweli wa Biblia
4: Mizimu ipo tangu enzi ya Kuandika kea Biblia lakini Biblia inazifunua kama ushetani, ushirikina na Upagani (Soma Isaya 8 mlango wa 19 na 20)
Tatizo la mizimu haitaki maendeleo hofu watu wakiendelea watoto watapa elimu na wakipata elimu awatokumbuka kutambika mizimu eti hili mambo yaende.
Zile ni bangili za shaba si ushirikina labda tu kama kuna kitu mtu kaweka.Kama ambavyo mnyama au binadamu apatani na kitu fulani mfano nyoka na mafuta taa,ndivyo ilivyo majini, wachawi nk kuna vitu navyo awapatani navyo so Ili kuwazuia wasikuvae unavaa unatumia vitu wasivyovipenda mfano miti,mimea, vyakula,kemikali,madini.
 
MATATIZO YA IMANI ZINAZO PENDWA

Je wale wanao amini kuwa mwanadamu (roho) anajitambua baada ya kifo wanaweza kukataa kile kitakacho onekana kuletwa kwao na hiyo roho??

Imani kwamba roho za wafu zinarudi kuwahudumia walio hai inafungua mlango kwa ajili ya imani ya kisasa ya mizimu.

Ikiwa wafu wanapata fursa ya kuwa na maarifa yanayozidi yale waliokuwa nayo wakiwa hai, kwa nini wasirudi duniani ili wawafundishe walio hai?

Ikiwa roho za wafu huvinjari juu ya rafiki zao duniani, kwa nini zisiwasiliane nao jamaa zao walio hai?

Je ni kweli watu walio kufa wapo mbinguni wakitazama yale tunayotenda? Luka 16:19—21

Karibu wakristo wote huamini kuwa mara baada ya kifo ‘roho’ huenda mbinguni, pagatori (mahari pa kutakasia dhambi ndogo) ama mahali mahali wapaitapo kuzimu au ahera (peponi). Kwahiyo, watu wengi wanajaribiwa kufikiri kuwa wapendwa wao walio kufa wapo mbinguni. Na kama haitoshi, wanafikiri kwamba baada ya kifo, wapendwa wao wanayo fursa kuona kila linaloendelea kwa marafiki na familia walizoziacha.

Fundisho kwamba roho haifi ndiyo msingi wa imani kwamba waliokufa wapo mahali Fulani wanatutazama, tunaweza kuwaendea wakatutatulia shida zetu (umizimu). Hii dhana ya kuwa ‘roho’ yaweza kuishi yenyewe nje ya mwili halipo kabisa katika biblia. Dhana hii ililitwaliwa kutoka kwa wapagani wa kale wanafalsafa wa Kimisri na Wayunani na mwisho likapenyeza katika theolojia ya Kikristo.

HALISI AU MFANO: Luka 16:19—21

Watu wanaoamini kwamba roho haifi na kwamba yapo maisha baada ya kifo hutumia Luka 16: 19 –21 kama uthibitisho. Je hilo ndiyo fundisho halisi la mfano huo?.

  • Mfano huu ni wa mwisho katika mfululizo wa mifano mitano (luka 15 na 16) ambayo Yesu alikuwa akijibu malalamiko ya Mafarisayo kwamba ni kwa nini alikula pamoja na wenyedhambi. Kila mfano ulilenga kulaumu kiburi na unafiki uliokuwa umeshamiri kwa viongozi wa dini kwa kuwaambia ‘ufalme wake ulikuwa zaidi ya sherehe; ulikuwa ni kujumuika pamoja Mungu na wanadamu (questions on Doctrines uk 549)
  • Katika mfano huu Yesu hakuwa anafundisha habari za roho na wafu. Husichanganye madesa kujasitifai anijasitified.Angalia mfano huu jinsi unavyofanana na tabia za Mafarisayo ambao waliamini wanastahili upendeleo toka kwa Mungu. Uzima wa milele ulikuwa kwa watu kama Lazaro.
  • Fundisho la imani haliwezi kujengwa katika mfano; Kwa vile mfano ni ufafanuzi kuhusu ukweli Fulani.
Fungu jingine lenye utata ni ‘ufunuo 6:9

Hii ni lugha ya picha (symbolic language) Vitabu vya ufunuo na Danieli vimeandikwa kwa lugha ya picha. Utapoteza maana ukitumia tafsiri ya moja kwa moja (Direct translations). Kwa nuru ya Mhubiri 9:5, Hapawezi kuwepo ‘roho za wafu’ zinazo oongea mbinguni, ama roho zinazo mlilia Mungu. Sikia Luka 20:38 ‘ Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake’’

Ukweli ni huu

  • Mungu pekee ndiye hasiyekufa. Ndiye pekee anaishi milele, na kwake hapana uharibifu ama kifo 1Tim 1:17 na 1Tim 6:16
  • Tutapokea kutokufa kupitia Yesu tukifika mbinguni (uzima wa milele) Ufunuo 21: 4, 1Kor 15: 53,54
Illusion
 
Kwa habari ya mizimu nahisi wanatheolojia wengi hawajapata kukutana na tukio la marehem kuongea kupitia mtu hai.
Hata kimakabila kuna ambao hawakutani na hali hii.
Lakini kwa wahaya hasa ukimwambia marehem hawezi kuongea kupitia mtu (enchweke), ni suala tu la kuamua kugomea fact.
Tunachoweza kujadiliana ni uwezo na mipaka ya roho hiyo.
Binafs mimi ni mbishi sana kuhusu hizi habari labda kutokana na iman yangu ya kikristo na elimu dunia iliyoongezwa. Lakin kuna tukio la macho yangu niliishia kusema..iiiii bado sijaelimika vyema, au ni ukorofi wa kutokukubali nisichokiamin!
Yan marehem ninayemjua alimwingia binti yetu. Sauti yenyewe. Mkao wa marehem wenyewe. Hadi upumuaj wenyewe. Ujumbe unagonga kwenye hali halis ambazo aliyeingiliwa hata hajui. Na ubish wangu nikajisemea .kweli kuna maarifa hatupewi vizuri.
Elimu za wazungu nazo zina ukomo taarifa aisee, maana wanakosa uzoefu au wanalazimisha tuamini wanachokiamini
Imenikuta hii, mke wangu anahita jina langu akiwa amelala na sauti inayotoka ni ya kiume. Nikachukua simu nimrekodi ila naanza tu, akanyamaza. Nikamuamsha hata hajui kilichokuwa kinaendelea.
 
Back
Top Bottom