Mizimu

Mizimu

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,097
Reaction score
1,457
MATATIZO YA IMANI ZINAZO PENDWA

Je wale wanao amini kuwa mwanadamu (roho) anajitambua baada ya kifo wanaweza kukataa kile kitakacho onekana kuletwa kwao na hiyo roho??

Imani kwamba roho za wafu zinarudi kuwahudumia walio hai inafungua mlango kwa ajili ya imani ya kisasa ya mizimu.

Ikiwa wafu wanapata fursa ya kuwa na maarifa yanayozidi yale waliokuwa nayo wakiwa hai, kwa nini wasirudi duniani ili wawafundishe walio hai?

Ikiwa roho za wafu huvinjari juu ya rafiki zao duniani, kwa nini zisiwasiliane nao jamaa zao walio hai?

Je ni kweli watu walio kufa wapo mbinguni wakitazama yale tunayotenda? Luka 16:19—21

Karibu wakristo wote huamini kuwa mara baada ya kifo ‘roho’ huenda mbinguni, pagatori (mahari pa kutakasia dhambi ndogo) ama mahali mahali wapaitapo kuzimu au ahera (peponi). Kwahiyo, watu wengi wanajaribiwa kufikiri kuwa wapendwa wao walio kufa wapo mbinguni. Na kama haitoshi, wanafikiri kwamba baada ya kifo, wapendwa wao wanayo fursa kuona kila linaloendelea kwa marafiki na familia walizoziacha.

Fundisho kwamba roho haifi ndiyo msingi wa imani kwamba waliokufa wapo mahali Fulani wanatutazama, tunaweza kuwaendea wakatutatulia shida zetu (umizimu). Hii dhana ya kuwa ‘roho’ yaweza kuishi yenyewe nje ya mwili halipo kabisa katika biblia. Dhana hii ililitwaliwa kutoka kwa wapagani wa kale wanafalsafa wa Kimisri na Wayunani na mwisho likapenyeza katika theolojia ya Kikristo.

HALISI AU MFANO: Luka 16:19—21

Watu wanaoamini kwamba roho haifi na kwamba yapo maisha baada ya kifo hutumia Luka 16: 19 –21 kama uthibitisho. Je hilo ndiyo fundisho halisi la mfano huo?.

  • Mfano huu ni wa mwisho katika mfululizo wa mifano mitano (luka 15 na 16) ambayo Yesu alikuwa akijibu malalamiko ya Mafarisayo kwamba ni kwa nini alikula pamoja na wenyedhambi. Kila mfano ulilenga kulaumu kiburi na unafiki uliokuwa umeshamiri kwa viongozi wa dini kwa kuwaambia ‘ufalme wake ulikuwa zaidi ya sherehe; ulikuwa ni kujumuika pamoja Mungu na wanadamu (questions on Doctrines uk 549)
  • Katika mfano huu Yesu hakuwa anafundisha habari za roho na wafu. Husichanganye madesa kujasitifai anijasitified.Angalia mfano huu jinsi unavyofanana na tabia za Mafarisayo ambao waliamini wanastahili upendeleo toka kwa Mungu. Uzima wa milele ulikuwa kwa watu kama Lazaro.
  • Fundisho la imani haliwezi kujengwa katika mfano; Kwa vile mfano ni ufafanuzi kuhusu ukweli Fulani.
Fungu jingine lenye utata ni ‘ufunuo 6:9

Hii ni lugha ya picha (symbolic language) Vitabu vya ufunuo na Danieli vimeandikwa kwa lugha ya picha. Utapoteza maana ukitumia tafsiri ya moja kwa moja (Direct translations). Kwa nuru ya Mhubiri 9:5, Hapawezi kuwepo ‘roho za wafu’ zinazo oongea mbinguni, ama roho zinazo mlilia Mungu. Sikia Luka 20:38 ‘ Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake’’

Ukweli ni huu

  • Mungu pekee ndiye hasiyekufa. Ndiye pekee anaishi milele, na kwake hapana uharibifu ama kifo 1Tim 1:17 na 1Tim 6:16
  • Tutapokea kutokufa kupitia Yesu tukifika mbinguni (uzima wa milele) Ufunuo 21: 4, 1Kor 15: 53,54
 
Kwa habari ya mizimu nahisi wanatheolojia wengi hawajapata kukutana na tukio la marehem kuongea kupitia mtu hai.
Hata kimakabila kuna ambao hawakutani na hali hii.
Lakini kwa wahaya hasa ukimwambia marehem hawezi kuongea kupitia mtu (enchweke), ni suala tu la kuamua kugomea fact.
Tunachoweza kujadiliana ni uwezo na mipaka ya roho hiyo.
Binafs mimi ni mbishi sana kuhusu hizi habari labda kutokana na iman yangu ya kikristo na elimu dunia iliyoongezwa. Lakin kuna tukio la macho yangu niliishia kusema..iiiii bado sijaelimika vyema, au ni ukorofi wa kutokukubali nisichokiamin!
Yan marehem ninayemjua alimwingia binti yetu. Sauti yenyewe. Mkao wa marehem wenyewe. Hadi upumuaj wenyewe. Ujumbe unagonga kwenye hali halis ambazo aliyeingiliwa hata hajui. Na ubish wangu nikajisemea .kweli kuna maarifa hatupewi vizuri.
Elimu za wazungu nazo zina ukomo taarifa aisee, maana wanakosa uzoefu au wanalazimisha tuamini wanachokiamini
 
Kwa habari ya mizimu nahisi wanatheolojia wengi hawajapata kukutana na tukio la marehem kuongea kupitia mtu hai.
Hata kimakabila kuna ambao hawakutani na hali hii.
Lakini kwa wahaya hasa ukimwambia marehem hawezi kuongea kupitia mtu (enchweke), ni suala tu la kuamua kugomea fact.
Tunachoweza kujadiliana ni uwezo na mipaka ya roho hiyo.
Binafs mimi ni mbishi sana kuhusu hizi habari labda kutokana na iman yangu ya kikristo na elimu dunia iliyoongezwa. Lakin kuna tukio la macho yangu niliishia kusema..iiiii bado sijaelimika vyema, au ni ukorofi wa kutokukubali nisichokiamin!
Yan marehem ninayemju alimwingia binti yetu. Sauti yenyewe. Mkao wa marehem wenyewe. Hadi upumuaj wenyewe. Ujumbe unagonga kwenye hali halis ambazo aliyeingiliwa hata hajui. Na ubish wangu nikajisemea .kweli kuna maarifa hatupewi vizuri.
Elimu za wazungu nazo zina wa ukomo taarifa aisee
Kwa kifupi una maanisha wafu Wana weza kuongea kupitia wengine Isaya 38:18, Mhubiri 9:5
 
Watu wakifa hawawi mizimu. "Mizimu" ni mashetani ya kijini yanayokuja kwa wajihi wa watu ambao walishakufa na watu wakadhani ndio wenyewe. Unakuta mtu anamuona mtu wake wa karibu kama baba, mama, mke, mume, mtoto, dada, kaka, sheikh wake au rafiki ambaye kashafariki au kusikia sauti yake kabisa, akadhani ni mzimu, kumbe ni shetani wa kijini anamchezea tu na kutaka kumdanganya na kutaka kumpoteza. Mizimu ni Majini.
 
Kwa kifupi una maanisha wafu Wana weza kuongea kupitia wengine Isaya 38:18, Mhubiri 9:5
Ndugu yang siwezi kuchallenge chanzo chako cha maarifa yan biblia.
Ila tu nataman hali ile itokee ukiwepo ili tuanzie hapo.
Niseme tu wewe unayo quote ni kujifungamanisha na data zilizoingizwa kwako.
Kuna mambo hamwezi kupata hitimisho sawa endapo mnatofautiana vyanzo vya maarifa. Ndipo hutokea makubaliano ya kutokukubaliana.
Mf. Niliimuuliza padre rafik yangu nini maana ya mambo hayo marehem kumuingia mtu akatoa ujumbe?
Akajibu , ni mkanganyiko wa taarifa kujirudia rudia aliye hai akiamin marehem angesema au kufanya hivi!
Huku nikijua amewai kushikwa asiyejuana na marehem nikajisemea. Kweli Biblia haijatoa majibu ya hali halis.
 
Watu wakifa hawawi mizimu. "Mizimu" ni mashetani kijini yanayokuja kwa wajihi wa watu ambao walishakufa na watu wakadhani ndio wenyewe. Unakuta mtu anamuona mtu wake wa karibu kama baba, mama, mke, mume, mtoto, dada, kaka, sheikh wake au rafiki ambaye kashafariki au kusikia sauti yake kabisa, akadhani ni mzimu, kumbe ni shetani wa kijini anamchezea tu na kutaka kumdanganya na kutaka kumpoteza. Mizimu ni Majini.
Imani ya kuwa Roho hazifi, mtu anapokufa Roho zinaendelea kuishi inadumisha upotofu wa dini!
Mizimu ni mashetani wanaojitokeza katika sura ya wapendwa wetu waliokufa
 
Ndugu yang siwezi kuchallenge chanzo chako cha maarifa yan biblia.
Ila tu nataman hali ile itokee ukiwepo ili tuanzie hapo.
Niseme tu wewe unayo quote ni kujifungamanisha na data zilizoingizwa kwako.
Kuna mambo hamwezi kupata hitimisho sawa endapo mnatofautiana vyanzo vya maarifa. Ndipo hutokea makubaliano ya kutokukubaliana.
Mf. Niliimuuliza padre rafik yangu nini maana ya mambo hayo marehem kumuingia mtu akatoa ujumbe?
Akajibu , ni mkanganyiko wa taarifa kujirudia rudia aliye hai akiamin marehem angesema au kufanya hivi!
Huku nikijua amewai kushikwa asiyejuana na marehem nikajisemea. Kweli Biblia haijatoa majibu ya hali halis.
Imani ya kimizimu ipo kea wingi katika familia za kiafrika, india na latin America.
Watu wa maeneo haya wanaheshimu makaburi, na kwao kaburi ni kitu cha thamani na cha pekee sana.
Wanaamini wakienda makaburini ikiwa wanatatizo basi litapata ufumbuzi
Umizimi = ushetani= upagani = ulimwengu wa Roho
 
Imani ya kuwa Roho hazifi, mtu anapokufa Roho zinaendelea kuishi inadumisha upotofu wa dini!
Mizimu ni mashetani wanaojitokeza katika sura ya wapendwa wetu waliokufa
Imani ya kuwa Roho hazifi, mtu anapokufa Roho zinaendelea kuishi inadumisha upotofu wa dini!
Mizimu ni mashetani wanaojitokeza katika sura ya wapendwa wetu waliokufa
Roho hazifi. Roho zinaendelea kuwepo zikitenganishwa na kiwiliwili na zinaendelea kuneemeshwa au kuadhibiwa mpaka zitakaporudishwa katika viwiliwili tena siku ya kufufuliwa.

Na Allah anajua zaidi.
 
Roho hazifi. Roho zinaendelea kuwepo zikitenganishwa na kiwiliwili na zinaendelea kuneemeshwa au kuadhibiwa mpaka zitakaporudishwa katika viwiliwili tena siku ya kufufuliwa.

Na Allah anajua zaidi.
Na hii ndo base (foundation) msingi wa umizimu.
Hii imani ya kimizimu inatenda kazi sana katika imani za wanaojiita wanafanya kazi katika ulimwengu wa Roho!
Utasikia mchungaji anasema " nilikuona katika ulimwengu wa Roho nilioneshwa katika ulimwengu wa roho
 
Hapana katika Imani ya Uislam hizo roho ziko katika maisha mengine kabisa yanaitwa Barzakh. Kuna kizuizi kati yao na walio hai. Hawana mawasiliano yoyote.

Ama hizo taswira za watu waliokwishakufa zikaonekana miongoni mwa watu na kuzungumza nao hao ni majini tu. Ndio watu wakasema ni mizimu au sijui roho zinazotangatanga. Hao ni majini.

Hivyo watu wanaoabudia makaburi na kuwaomba wafu, wakatokewa na taswira za hao watu waliokufa na kudhani wametokewa na hao waliokufa "mizimu", hao wanadanganywa na kupotezwa na mashetani.
 
Back
Top Bottom