Mjadala: Haki ya kutoa maelezo Polisi

Nilichofurahi ni wewe haukuwa makini kusoma nani anacomment nini, pengine ni wewe ulinichoza kuniita polisi asijua kazi yake, mara sijui mahakama zilipo na zaidi kuuliza account yangu ina ina nini.Lakini pia mwanzoni nilijibu gently ila ulikuwa too harsh ndio nikajibu vile.
 
Mkuu Hute nitake radhi
Mimi hauwezi kuniweka kundi la hao.
Mi toka nakua naona kwenye vibanda vya video mtu akikamatwa lazima aambiwe haya:
1.You have the right to remain silent till you are in the court of law.
2. Whatever you say or explain will be taken as evidence in the court of law.
3. You have the right to be represented by your lawyer.
Sasa inamaanisha Askofu na wakala wake hawakuyajua yote haya kweli?
Hawakuangalia hata picha za action kama sisi udogoni na sasa?
Au ni wewe tu unajifanya mjanja na wao unawafanya wajinga mkuu Hute?
 
Last edited by a moderator:
pole. haujui kitu. na sitajadili hii topic kwasababu haina faida (topic ya taskforce) na haikuwa moja ya hoja za thread. bye.

Ndio maana sikutaka kutaja watu ila kama kuna mtu atakuja na ushahidi kuwa taskforce ilianza kabla ya 1998 katika ule ulipuaji wa ubalozi wa marekani basi narudi chekechea. Accidentally nikutajie .........peke yake?
 
kama walikuwa wanayajua, hasahasa faida ya kukaa silent, kwanini hawakukaa silent? ok, tunaweza kusema kuwa siku ya kwanza walipitiwa kwasababu hawakuwa wanajua wanaenda kuhojiwa kwaajili ya kumtusi pengo au mambo ya usajili wa kanisa na umiliki wa mali. je? juzi tarehe 9 waliporudi kwanini hawakujipanga akafika pale akasema nimeamua kuremain silent, sitatoa maelezo tena kama mnaona nina kosa nitajieleza mahakamani wakati wa kujitetea....hapo lazima kuna maelezo ya nyoongeza yameshaandikwa kuhusiana na umiliki wa mali namna sadaka zinavyotumiwa na mambo mengi na polisi wanatafuta sababu ya kumpachika na kosa either la money laundering au drug trafficking....sawa wao hawakuwa na knowledge hiyo, na walikuwa na muda mrefu sana wa kujipanga kabla ya tarehe 9 waliyorudi tena na kupewa hiyo list ya vitu vya kuleta. hauoni kama kulikuwa na uzembe upande wa mwanasheria kweli hapo?

kama wewe ni lawyer mzoefu, unajua madhara ya kujianika kwa polisi kwamba ukijianika tu unazalisha kosa lingine la kuchunguzwa, ametoka arusha siku ile kwanini hakujipanga na mteja wake kabla hata hajafika kwamba ukifika sema hivi?
 
Hute;

Mkuu, hebu soma CPA Section 10(4)

(4) Utakuwa ni wajibu wa afisa polisi kabla ya kumhoji mtu kumweleza mtu huyo kuwa anawajibika kuyajibu kwa ukweli maswali yote yanayohusiana na kesi atakayoulizwa naye na kwamba hawezi kukataa kujibu swali lolote kwa sababu tu swali hilo lina mwelekeo wa kumhatarisha wazi katika shitaka la jinai, adhabu au kunyang'anywa mali yake.

kwa nini ukatae kuhojiwa? au kila siku uwe unaenda polisi, ikiwezekana unyimwe dhamana mpaka utakapokuwa tayari kujibu maswali ya mpelelezi. maana utakuwa unataka ugomvi na sio kutafta haki tena
 
Last edited by a moderator:
mimi pamoja na uelewa wangu mdogo nafahamu kesi haiwezi kwenda mahakamani bila mtuhumiwa kuhojiwa.nimesoma comment hizi hapa kwenye thread kwa makini nimegundua kwenye kutoa ushauri watu wanatumia jabza sana ambaye anajua kidogo hataki afundishwe zaidi.
 
MKUU upo sahihi. lakini soma pia kifungu cha 53 halafu tujadili na hicho pia.

53. Where a person is under restraint, a police officer shall not ask him any questions, or ask him to do anything, for a purpose connected with the investigation of an offence, unless–
(a) the police officer has told him his name and rank;

(b) the person has been informed by a police officer, in a language in which he is fluent, in writing and, if practicable, orally, of the fact that he is under restraint and of the offence in respect of which he is under restraint; and

(c) the person has been cautioned by a police officer in the following manner, namely, by informing him, or causing him to be informed, in a language in which he is fluent, in writing in accordance with the prescribed form and, if practicable, orally–
(i) that he is not obliged to answer any question asked of him by a police officer, other than a question seeking particulars of his name and address; and

(ii) that, subject to this Act, he may communicate with a lawyer, relative or friend.

CPA YA KISWAHILI IMEANDIKWA HIVI

53. Pale mtu anakuwa kizuizini, afisa polisi hatamuuliza maswali yoyote, au kumtaka kufanya chochote, kwa madhumuni yanayohusiana na upelelzi wa kosa, isipokuwa kama:–

(a) afisa polisi amemwambia jina na cheo chake;

(b) mtu huyo amejulishwa na afisa polisi, katika lugha ambayo anaielewa, kwa maandishi na, kama inawezekana, kwa mdomo, kwamba yuko kizuizini na kosa ambalo kwalo yupo kizuizini; na

(c) mtu huyo ameonywa na afisa polisi katika hali ifuatayo, yaani, kwa kumjulisha au kusababisha kujulishwa, katika lugha anayoielewa, kwa maandishi kwa kufuata fomu iliyowekwa na, iwapo inawezekana, kwa mdomo kwamba –

(i) halazimiki kujibu swali lolote atakaloulizwa na afisa polisi, tofauti na swali linalotafuta habari kuhusiana na jina na anuani yake; na

(ii) kwa kuzingatia Sheria hii, anaweza kuwasiliana na mwanasheria, ndugu au rafiki.
 
jaribu kusoma hapa

53. Where a person is under restraint, a police officer shall not ask him any questions, or ask him to do anything, for a purpose connected with the investigation of an offence, unless–
(a) the police officer has told him his name and rank;

(b) the person has been informed by a police officer, in a language in which he is fluent, in writing and, if practicable, orally, of the fact that he is under restraint and of the offence in respect of which he is under restraint; and

(c) the person has been cautioned by a police officer in the following manner, namely, by informing him, or causing him to be informed, in a language in which he is fluent, in writing in accordance with the prescribed form and, if practicable, orally–

(i) that he is not obliged to answer any question asked of him by a police officer, other than a question seeking particulars of his name and address; and

(ii)that, subject to this Act, he may communicate with a lawyer, relative or friend.

CPA YA KISWAHILI IMEANDIKWA HIVI

53. Pale mtu anakuwa kizuizini, afisa polisi hatamuuliza maswali yoyote, au kumtaka kufanya chochote, kwa madhumuni yanayohusiana na upelelzi wa kosa, isipokuwa kama:–

(a) afisa polisi amemwambia jina na cheo chake;

(b) mtu huyo amejulishwa na afisa polisi, katika lugha ambayo anaielewa, kwa maandishi na, kama inawezekana, kwa mdomo, kwamba yuko kizuizini na kosa ambalo kwalo yupo kizuizini; na

(c) mtu huyo ameonywa na afisa polisi katika hali ifuatayo, yaani, kwa kumjulisha au kusababisha kujulishwa, katika lugha anayoielewa, kwa maandishi kwa kufuata fomu iliyowekwa na, iwapo inawezekana, kwa mdomo kwamba –

(i) halazimiki kujibu swali lolote atakaloulizwa na afisa polisi, tofauti na swali linalotafuta habari kuhusiana na jina na anuani yake; na

(ii) kwa kuzingatia Sheria hii, anaweza kuwasiliana na mwanasheria, ndugu au rafiki.
 
10(4) It shall be the duty of a police officer before examining a person to inform him that he is bound to answer truly all questions relating to the case put to that person by him and that he may not decline to answer any question on the grounds only that the question has a tendency to expose him to a criminal charge, penalty or forfeiture.hebu angalieni kwenye red. maana ya subsection hii ilikuwa ni nini?

je? alikuwa anamaanisha kumtaka suspect akiamua kujibu maswali analazimika kuyajibu kwa ukweli (he is bound to answer truly all questions) au alikuwa anamaanisha kuwa analazimika kujibu maswali yote, hawezi kukataa kujibu?, ukimaliza kusoma hapa nenda kasome section 53(c)(i)
 
Hute;

Je baada ya kufika ndugu au mwanasheria akigoma kuhojiwa inakuwaje atalazimishwa .
 
Last edited by a moderator:
Je baada ya kufika ndugu au mwanasheria akigoma kuhojiwa inakuwaje atalazimishwa .
wakifika hao ndipo atapewa haki ya kutoa maelezo kwa hiari. kama hawakuwepo wakifika that means polisi anaanza mwanzo kabisa kwa kujitambulisha, kutaja cheo chake, kumpa haki kuwa halazimishwi kutoa maelezo na kumpa alart kuwa maelezo yatakayoandikwa siku moja yanaweza kuja kutumika kama ushahidi dhidi yake mahakamani, theni anaendelea kuanzika maelezo. sasa kama suspect atahiari kutoa maelezo yote analazimika kuyatoa ya kweli yasiyo ya uongo kwasababu akitoa ya uongo anaweza kushitakiwa.
 
labda kuna kitu tunapishana mtu akikataa kuhojiwa kabisa polisi akata ushahidi wake akatoe mahakamani inaruhusiwa .
 
labda kuna kitu tunapishana mtu akikataa kuhojiwa kabisa polisi akata ushahidi wake akatoe mahakamani inaruhusiwa .
ndicho tunachoongea tangu mwanzo hapa, na mjadala umesimamia hapo. isipokuwa atatakiwa kutaja jina lake na address yake tu, ila kuhusu kuongelea kosa ambalo anatuhumiwa nalo anaweza kuamua asiseme chochote. soma icho kifungu 53 uelewe. na sheria nimeattach hapo juu haujaona? au hujadownload ili uzisome?nimeweka CPA ya kiingereza na CPA ya kiswahili. hiyo ya kiswahili haijatoa tafsiri halisi ya lengo ya hicho kifungu nafikiri watafisiri kule law reform (ambao ndio wanaotafisiri kwenda kiswahili) hawakuweka neno zuri kama ilivyo kwenye CPA ya kiingereza. try to download and compare.
 
nimesoma nimeshakuelewa kwa hiyo kwenye kesi ya Gwajima kuna kosa alifanya mwanasheria wake ndo maana wanachezewa rafu hivi nimejifunza kitu kwenye hili.
 
nimesoma nimeshakuelewa kwa hiyo kwenye kesi ya Gwajima kuna kosa alifanya mwanasheria wake ndo maana wanachezewa rafu hivi nimejifunza kitu kwenye hili.
huyo lawyer mwenzio hapo juu ndio mpaka sasaivi hajaelewa. sijui amesomea chuo gani? au open university masomo ya jioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…