Mkuu, hebu soma CPA Section 10(4)
(4) Utakuwa ni wajibu wa afisa polisi kabla ya kumhoji mtu kumweleza mtu huyo kuwa anawajibika kuyajibu kwa ukweli maswali yote yanayohusiana na kesi atakayoulizwa naye na kwamba hawezi kukataa kujibu swali lolote kwa sababu tu swali hilo lina mwelekeo wa kumhatarisha wazi katika shitaka la jinai, adhabu au kunyang'anywa mali yake.
kwa nini ukatae kuhojiwa? au kila siku uwe unaenda polisi, ikiwezekana unyimwe dhamana mpaka utakapokuwa tayari kujibu maswali ya mpelelezi. maana utakuwa unataka ugomvi na sio kutafta haki tena
MKUU upo sahihi. lakini soma pia kifungu cha 53 halafu tujadili na hicho pia.
53. Where a person is under restraint, a police officer shall not ask him any questions, or ask him to do anything, for a purpose connected with the investigation of an offence, unless–
(a) the police officer has told him his name and rank;
(b) the person has been informed by a police officer, in a language in which he is fluent, in writing and, if practicable, orally, of the fact that he is under restraint and of the offence in respect of which he is under restraint; and
(c) the person has been cautioned by a police officer in the following manner, namely, by informing him, or causing him to be informed, in a language in which he is fluent, in writing in accordance with the prescribed form and, if practicable, orally–
(i) that he is not obliged to answer any question asked of him by a police officer, other than a question seeking particulars of his name and address; and
(ii) that, subject to this Act, he may communicate with a lawyer, relative or friend.
CPA YA KISWAHILI IMEANDIKWA HIVI
53. Pale mtu anakuwa kizuizini, afisa polisi hatamuuliza maswali yoyote, au kumtaka kufanya chochote, kwa madhumuni yanayohusiana na upelelzi wa kosa, isipokuwa kama:–
(a) afisa polisi amemwambia jina na cheo chake;
(b) mtu huyo amejulishwa na afisa polisi, katika lugha ambayo anaielewa, kwa maandishi na, kama inawezekana, kwa mdomo, kwamba yuko kizuizini na kosa ambalo kwalo yupo kizuizini; na
(c) mtu huyo ameonywa na afisa polisi katika hali ifuatayo, yaani, kwa kumjulisha au kusababisha kujulishwa, katika lugha anayoielewa, kwa maandishi kwa kufuata fomu iliyowekwa na, iwapo inawezekana, kwa mdomo kwamba –
(i) halazimiki kujibu swali lolote atakaloulizwa na afisa polisi, tofauti na swali linalotafuta habari kuhusiana na jina na anuani yake; na
(ii) kwa kuzingatia Sheria hii, anaweza kuwasiliana na mwanasheria, ndugu au rafiki.