Mjadala huru: Je ni heri kutoboa ujanani, ukubwani au uzeeni

Mjadala huru: Je ni heri kutoboa ujanani, ukubwani au uzeeni

Kutoboa kwa maana ya kujipata.. Ni umri upi sahihi?
Faida zake ni zipi?
Hasara zake ni zipi?
Je una mifano hai?
Karibuni kwa mjadala huru..!

Tumia mfano wa aliyekuwa Mheshimiwa Amina Chifupa.

Nafikiri asili au hatma ya mtu anayo muumba. Na siku tunaingia hapa duniani huwa tunaingia na hatma zetu viganjani ni vile tuu ufahamu unakuwa bado hatujaupata.

Wako wanaofanikiwa wadogo kutokana na familia (bakhresa, MO)

Wako wanaofanikiwa wenyewe wenyewe tuu wakiwa bado vijana na wanadumu na mafanikio yao hadi uzeeni.

Wako wanaochelewa kufanikiwa yqani baada ya kustaafu anakuwa tajiri balaa hadi anakufa.

Wako wanaofanikiwa in their mid age 40s and 50s na wanazeeka na utajiri wao.

Wako wanaozaliwa na mafanikio toka kwa wazazi wao, wazazi wakifa wanabaki maskini wa kutupwa.

Wako wanaojitafuta ujanani wanafanikiwa kisha wanafilisika au wanapotea mapema au wanazeeka maskini...

Ni maisha tuu hapo katikati kuna mengi watu wanapitia, husda, wivu, fitina, macho ya watu.... ukiyavuka hayo unazeeka na mafanikio yako.
 
Aisee kutoboa ujanani ukikosa hekima na usipokuwa na hofu na Mungu unakufa mapema sana cause starehe na anasa zitakufanya upite kama upepo

Kwanza kupoteza ulichonacho vyepesi sana usipokuwa na hofu na mungu na ikikosa busara mifano ipo wazi kwenye jamii yetu so kufulia dakika sifuri tu


MY TAKE
Mafanikio yaje kidogo kidogo kulingana na umri unapofika umri 50 + huwezi tetereka ukiwa umejipata cause huwezi babaika na chochote kile

Mfano mdogo tu

Kipindi upo masomoni either chuo au sekondari kuna vitu vingi ulitamani uwe navyo ili uwanyooshe watu miaka imepita leo upo mtaani vitu ulivyotamani unavyo je unawanyoosha watu si unaona kawaida tu so the same na mafanikio katika maisha yaje kwa hatua
 
Aisee kutoboa ujanani ukikosa hekima na usipokuwa na hofu na Mungu unakufa mapema sana cause starehe na anasa zitakufanya upite kama upepo

Kwanza kupoteza ulichonacho vyepesi sana usipokuwa na hofu na mungu na ikikosa busara mifano ipo wazi kwenye jamii yetu so kufulia dakika sifuri tu


MY TAKE
Mafanikio yaje kidogo kidogo kulingana na umri unapofika umri 50 + huwezi tetereka ukiwa umejipata cause huwezi babaika na chochote kile

Mfano mdogo tu

Kipindi upo masomoni either chuo au sekondari kuna vitu vingi ulitamani uwe navyo ili uwanyooshe watu miaka imepita leo upo mtaani vitu ulivyotamani unavyo je unawanyoosha watu si unaona kawaida tu so the same na mafanikio katika maishs yaje kwa hatua
True,na haya ya kunyoosha watu yapo Africa thus Mungu uwapa wengi uzeeni tofauti na wenzetu weupe wao wanajua kutofautisha utu na kutoboa.
Mswahili hajui kutofautisha
 
True,na haya ya kunyoosha watu yapo Africa thus Mungu uwapa wengi uzeeni tofauti na wenzetu weupe wao wanajua kutofautisha utu na kutoboa.
Mswahili hajui kutofautisha
Unakufa mapema au unafulia mapema tu mifano ipo wazi ngoja tutumie watu wenye majina kuna Msanii MR NICE tunambiwa kipindi chake alikuwa anatembea na pesa kwenye mfuko leo zipo wapi, kuna kijana wetu idriss alipata si chini ya milion 500 kibongo bongo ukituliza kichwa tobo tayali hilo ila yupo wapi mifano ni mingi mingi sana kuna uyu kijana wetu pendwa anavuma balaa kimuziki na tunaona uwezekaji wake save hii comment in five years later asipomshika mungu na kuwa na hekima tunamkuta soba house
 
KUTOBOA UKUBWANI NI VIZURI zaidi unakuwa na maturity nzuri na unaweza kujisimamia kwa uimara zaidi, ujana maji ya moto, utarukaruka sana ila lazima yakuunguze.

#UkubwaDawa
Na unakuwa umeshapata uzoefu wa kutosha kuhusu maisha, changamoto na starehe zake
 
Kutoboa uzeeni

Mfano Mzee Wassira sasa anakula mema ya nchi na huwezi kuamini kuwa 1990s alikuwa anafata machozi ya Simba by foot kule Msasani mwisho 😂
Mzee ameanza kubugia burugutu siku nyingi kule mitaa ya Manyamanyama na Ikizu.Long kitambo hadi ana golden card.
NB:Kuhusu uzi,Mimi ningependa kutoboa na kujipata ujanani.Uzeeni utajiri wa nini?
 
Kutoboa uzeeni

Mfano Mzee Wassira sasa anakula mema ya nchi na huwezi kuamini kuwa 1990s alikuwa anafata machozi ya Simba by foot kule Msasani mwisho 😂
Miaka ya tisini ipi hiyo mkuu?. Mbona umemdogosha Sana Made Wassira?

Miaka ya tisini, mzee Wassira tayari Ali kuwa babu mwenye wajukuu, na ameanza kuhudumu kwenye serikali tangu miaka ya sitini
 
Ukipata mafanikio ujanani ukiachana na Starehe, ukiweza kuvuka nguvu za husda, wivu, kurogwa, kusemwa vibaya utakuwa umetoboa.

Maana siku hizi kila anaetoboa kijana anapakaziwa freemason au mchawi

Na haya Huwa yanafanywa na ndugu wa karibu wanaojua namna ya kukushusha na kukuangamiza.

Ukitoboa ukiwa kijana unatakiwa uwe na akili iliyopevuka sana kuvuka hivyo vikwazo

Kutoboa ujanani ni Bora kuliko Uzeeni, wengi wanaotoboa Uzeeni wanakuwa limbukeni wa mafanikio
 
Mzee ameanza kubugia burugutu siku nyingi kule mitaa ya Manyamanyama na Ikizu.Long kitambo hadi ana golden card.
Wassira alikuwa kijana wa mwalimu hivyo aliishi kijamaa mno hadi alipozingua kwenye Ubunge wa Warioba ndio Mfumo ukamtupa nje kabisa

Ni wakati huo ndio akawa rafiki yangu pale Makangira pamoja na rip Mzindakaya

JK ndio alimfungulia mlango kabla Bulaya hajamzingua tena

Sasa ndio ametoboa rasmi 😄
 
Miaka ya tisini ipi hiyo mkuu?. Mbona umemdogosha Sana Made Wassira?

Miaka ya tisini, mzee Wassira tayari Ali kuwa babu mwenye wajukuu, na ameanza kuhudumu kwenye serikali tangu miaka ya sitini
Unaelewa maana ya kutoboa lakini

Enzi za Nyerere hatukuwa na swaga hizo bwashee 😂
 
Unakufa mapema au unafulia mapema tu mifano ipo wazi ngoja tutumie watu wenye majina kuna Msanii MR NICE tunambiwa kipindi chake alikuwa anatembea na pesa kwenye mfuko leo zipo wapi, kuna kijana wetu idriss alipata si chini ya milion 500 kibongo bongo ukituliza kichwa tobo tayali hilo ila yupo wapi mifano ni mingi mingi sana kuna uyu kijana wetu pendwa anavuma balaa kimuziki na tunaona uwezekaji wake save hii comment in five years later asipomshika mungu na kuwa na hekima tunamkuta soba house
Ndo maana nasema hili lipo kwetu sisi weusi kwa sababu hatufundishwi elimu ya pesa utotoni.
Ngono ndio umaliza sana pesa za weusi, wenzetu walishatoka huko.
Wote hao uliowataja wanataka kuchungulia kila mtu
 
Back
Top Bottom