Ipo hivi, Pesa zinalipwa huko youtube kwa sababu ya matangazo, Narudia tena "MATANGAZO", mimi, wewe na makampuni makubwa iwapo tuna huduma au bidhaa tunazotaka zitangazwe tunaweza kutangaza kupitia Youtube ili bidhaa zetu zijulikane na watumiaji wa youtube.
Tukipeleka Tangazo letu youtube, Itabidi youtube tumlipe ili tangazo letu liwafikie watumiaji wa youtube.
Youtube yeye kama yeye ni kampuni tu inayoturuhusu kupandisha video, Video zinazowekwa youtube sio za youtube bali ni za wasanii, waandishi wahabari, n.k youtube hawezi kufanya chochote kwenye hizo video.
Sasa youtube tunapompa fedha atutangazie biashara zetu mimi na wewe kwa watumiaji wa youtube ina maana ya kwamba watumiaji wayaone matangazo hayo wanapotizama video za youtube
Youtube hawezi kuweka tu tangazo kwenye video za watu, Inabidi aombe ruksa ya kufanya hicho kitu kwa wasanii kama kina Diamond platnumz.
Sasa tuchukulie kwamba ndio youtube na diamond wanongea, mawasiliano yapo hivi (ni mfano tu, Diamond katumika kama mfano):,
Youtube: " Bwana diamond, kuna kampuni inaitwa jamiiforums wametengeneza app yao, wametupa tangazo lao tuwatangazie youtube liwafikie watanzania, sasa bwana Diamond tunaomba ruksa yako tuweke tangazo la jamiiforums liwe linaonekana kabla video yako haijaanza kucheza ama pembezoni, We unasemaje?"
Daimond: "Sawa, nimekuelewa Bwana youtube, matanmgazo yao nikiyaruhusu yaonekane kwenye video zangu basi itabidi na mimi mnilipe kiasi kadhaa kwenye hio pesa mliopewa,"
Youtube: "Ondoa shaka, wala usihofu kijana, wewe utachukua asilimia 55 na mimi ntabaki na asilimia 45, kwa hio kama jamiiforums walitulipa kwa kigezo cha elf 5 kwa kila watu elf 1 wataoliona tangazo wakicheki video yako wewe utachukua 2,750 na sisi tutabaki na 2,250"
Basi ndio mkataba huo unaanza kutekelezwa hapo ndipo unapoendaga kutazama video za wasanii huko youtube unakumbana na aina ya matangazo yale ambayo yanaanza kucheza kabla video uliyotaka kuicheki haijaanza na kuna kitufe cha kuruka tangazo (skip ad) ama aina nyingine ni matangazo yale ambayo yanakuaga pembeni mwa video, n.k
Jambo lingine ni kwamba watu wanaotaka kutangaziwa biashara zao kwa youtube huwa wanaseti kabisa tangazo lao liwafikie watu wa tanzania ama nchi flani, sisi watazamaji wa bongo tunayaonaga matangazo mengi ya kina vidacom ama tigo, Nao wenye biashara marekani huwa wamelenga watazamaji wa huko na ulaya.
Sasa endapo video za msanii zikitazamwa Marekani, Ulaya, Canada, n.k basi msanii anaweza kulipwa hata elfu 10 akipata views elf 1 kutoka majuu, hii ni kwasababu makampuni ya huko yanayotaka kutangaziwa biashara yana ni makubwa na pesa nyingi tu, wanaweza kulipa hata elf 20 kwa views elf 1 youtube wakachukua elf 9 msanii akabaki na elf 11, views za wabongo elf 1 msanii anaweza akabaki hata na buku tu kwasababu tangazo tutaloliona mimi na wewe tukiwa hapo buza litakua labda ni la kampuni ya ufugaji wa kuku ambayo bado ni changa