Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Gamba la Chuma

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
1,243
Reaction score
342

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Gari ninayotumia ni Chaser GX100.

Nimesafiri nayo kutoka Dar kuja Iringa na ninatarajia kuitumia kurudi Dar.

Imetokea ghafla steering imekuwa nzito (stiff) ie unatumia nguvu kidogo kukata kona.

Hakuna kelele za belt kwisha, hakuna leakage kwenye steering fluid, na hydraulic ipo level.

Wataalamu wa magari naombeni msaada wa kujua tatizo na kama naweza kuitumia kurudi Dar.

Natanguliza shukrani !
---
---

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
---
---
---
---
---
 
Mkuu ni vema ukawahi gereji nzuri maana umesema unategemea kurudi Dar, chukua tahadhali haraka kabla mambo hayajawa magumu.
 
Pole mkuu, unaweza tu kurudi nayo mpaka DSM utakapoipeleka kwa fundi. Inawezekana inapoteza nguvu na hii inatokana na hydrolic nyingi tunazoweka hazina kiwango.

Muhimu iwe haivuji na inasukuma hapo unatembea by the way ukiwa speed itakua laini na utafika.
 
Angalia BALL JOINT zinataka kuchomoka (hapa kama sijaelewa mkuu)
 
gamba
la Chuma,
Pole sana mkuu, mi nilikua na SV50 ikawa nipo dodoma gafla ikafa stering power nikafos kurud Dar ivo ivo, lalala kufika dar tu stering rake.

inavuja, feni belt imekrek sana haifai tena, nikaenda kwa BADI mpemba 0657617671 pale shauri moyo ilala akaniuzia vyengine, mpigie atakutumia.

hana tabu na wewe tu uwe muaminifu milielekezwa na ndugu yangu akanipa namb ya badi ndo nikampigia. mpigie kabla stering rake haijaanza kuvuja.
 
Ushauri nasaha. Tafuta mnyalu mwenye pesa akuvue huo mkweche uje mjini ununue gari jengine. Hata m 5 mpe huo ni wembe ukizidi kuuchezea utalia.
 
Ushauri nasaha. Tafuta mnyalu mwenye pesa akuvue huo mkweche uje mjini ununue gari jengine. Hata m 5 mpe huo ni wembe ukizidi kuuchezea utalia.

Mkuu mbona unawatania shemeji zangu. Cc OLESAIDIMU.
 
Last edited by a moderator:
Hilo mbona tatizo la.kawaida hapo iringa wapo mafundi usikubali kurudi nayo dar bila kuhakikisha iko sawa. Sio vizuri kutake risk ya namna hiyo.
 
Angalia BALL JOINT zinataka
kuchomoka (hapa kama cjaelewa mkuu)

Najaribu kumwelewesha ni hivi kwenye tairi za mbele kuna vitu vinaitwa BALL JOINT sasa hizo zikichoka zinafanya usukani wa gari unakuwa mgumu, ni uzoefu maana nishakutana na hali hiyo.
 
Turufuu,
ulikosea mwana ilitakiwa utoe mkanda ule then utumie mechanical tu japo stering ingekua ngumu ila ungefika bila tabu
 
Nna gari aina ya Suzuki Samurai, ambayo ki ukweli iko kiuchumi kwenye ulaji wa mafuta na hata bei ya spea zake. Tatzo imeanza kusumbua, naiwasha vzr naondoka, baadae inaanza kumiss, then inapoteza nguvu na kuzima.

Nikiiwasha tena kwa muda uleule haikubali mpaka engine ipoe kdg, ndo inawaka tena. Nmezunguka sana, kwa mafundi wa mtaani, ambao mpaka wamenishauri nibadilishe spea kama starter, ignition coil na fuel pump, na kugundua kumbe vilikua vizima, mana tatzo limebaki palepale.

Naomba ushauri juu ya ufumbuzi wa tatizo hili kwamba linatatuliwaje hili mana mafundi wa uswazi wamenichosha.
 
Kupata taarifa unayohitaji kwenye search engine huwa pia inahitaji ujue key words za kutumia. Kama mleta thread hujafanikiwa ku-identify kwa usahihi tatizo la gari yako sio rahisi Google ikupe solution. Tena basi information nyingi kwenye mtandao zinahitaji maneno sahihi ya kiingereza,

Vitu kama mfano "rejeta" havijulikani! Nashauri uachane na gereji bubu za mtaani zinazotengeneza magari kwa trial and error na badala yake ukubali gharama uende gereji nzuri zipo nyingi,tena ukiweza utafute kabisa Dealer wa SUZUKI maana hii ni model ya zamani kidogo, hakika matatizo yake mengi si mageni kwa wazoefu.

Kila la kheri.
 
@SofiaKitwana,
Asante sana sister mana kama kugoogle nmegoogle sana tu, bila kupata jb sahh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…