Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Richman,
kama walivyokushauri wadau, tatizo hapo linasababishwa na "Throttle Position Sensor" TPS Sensor. Nilishakuwa na Suzuki yenye tatizo kama lako na nikabadilisha TPS Sensor tatizo likaisha.
 
Angalia fuel pump yako. Inaonekana iko harijojo. Unapowasha inawaka sababu bado haijapata moto. Ikishapata moto inakausha mafuta na ndiyo maana haiwaki
 
Tafuta fundi acheki sensa nilishakutana ugonjwa hu kwenye suzuki v6 nilipoteza zaidi ya milioni 1 badae ikaja kugundulika ni sensa nikatibu kwa sh120000 unaweza ukakuta ghafla inapoteza nguvu na ikirudi kama inastuka kuwa makini sana unapoiendesha
 
Richman,
Ndugu hilo limewahi tokea kwa Suzuki carry ya hapa home ikatutesa kununua spea kibao ila tatzo likawa palepale.

Kuchemsha, mwendo kasi kushuka na kukosa nguvu ya kujongea haraka ila baadae ikajagundulika ni pump zilizo katika radiator na baada ya kuzifanyia usafi na kufungwa upya.

Sasa gari inatembea kama awali. Katika radiator waligundua kuna kutu iliyopitiliza na kuifanya gari kupumua kwa shida na hii hutokana na maji chumvi.
 
Huenda ikawa sio gari maana vijana wa kisasa wana lugha zao hilo gari yawezekana ni kukosa nguvu za kiume nyie mnang'ang'ana kusema gasket Mara valve kazi kwelikweli
 
Aisee hio gari usiitembeze mpk utakapobadiri mfumo wakuupoza engine.. Hio gari ina heat na hatimae utaunguza silinda head gasket na mwishowe head itapinda upate hasara zaidi..
Anzia mfumo wa radiator itakuwa chafu na gari haipozi vizuri engine.. Ilishanitokea..
 
Chunguza tank la mafuta na pump ya mafuta. Ni ugonjwa kwa magari mengi kwa kuwa mafuta yanachajachuliwa. Kwa dar ndiyo zaidi.
 
Richman,
Check kama mafla inatoa moshi, mafla ni sehemu ya maungio kati ya engine na bomba la kutolea moshi. Nishawahi pata hilo tatizo. Cjui km nawe itakua ni hiyo k2 au tofauti.
 
Vipi kuhusu maji ya kupoza injini (coolant) yanapungua kwa kiwango kipi??
 
Back
Top Bottom