Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

hiii hutegemeana huwa kuna matatizo mengi tu yanayoweza sababisha gari kukosa nguvu, moja wapo ni mafuta kidogo, hewa ndogo inayoingia kwemye combustion chember
 
Kwa kiasi kikubwa inawezekana fuel pump yako imechoka hasa kama gari haiwezi kuaccelerate. Vinginevyo, inawezekana air filter yako imeshaziba, inabidi uibadilishe. Kwa jumla matatizo ya gari kuishiwa nguvu ni ama hakuna mafuta au hewa ya kutosha kwenye combustion chamber. Utaiona wakati mweingine inatoa moshi mweupe.
 
Sababu nyingine inawezekuwa 'catalytic converter' imeziba.

kutokana na maelezo yako inaonesha engine inakosa nguvu baada ya kuendesha umbali fulani. kama mafuta hayachomwi yote kwa muda unaotakiwa kwenye chemba basi mafuta hayo yataendelea kuungua baada ya kutoka kwenye engine (yaani kuungua ndani ya bomba la moshi). Moto huo mkali huyeyusha 'materials' zilizoko kwenye 'catalytic converter' ambazo huziba moshi usitoke nje (muffler).

DSC_2850.JPG


Sasa unapowasha gari kwa mara ya kwanza (asubuhi), 'pressure' katika bomba la moshi huanza kuongezeka kwasababu haina pa kutokea na kadiri unapoendesha ndiyo 'pressure' inazidi. Mwishowe inafika karibu na 'engine' (exhaust manifold) ambapo hukinzana na 'gases' nyingine mpya zinazotoka kwenye engine. Ni kama vile kujaza hewa kwenye tube ya baiskeli, mwanzoni ni rahisi lakini baadae inakuwa ngumu kujaza. Sasa 'pressure' hii huzuia engine kutoa 'exhaust gases' ambapo hupunguza nguvu ya 'engine'.

Sasa kujua kama hili ndo tatizo unatakiwa kupima 'temperature' kabla na baada ya 'catalytic converter' kwa kutumia 'non contact thermometer'. Kama baada ya 'catalytic converter' (kushoto kwenye picha) ni baridi kuliko kabla ya converter wakati 'engine' imepata joto basi lazima kuna mahali pameziba. Kwa kawaida joto baada ya converter linatakiwa liwe juu (150 degrees Celsius)

Baada ya kugundua hilo tatizo inabidi ubadilishe 'catalytic converter' au uweke 'straight pipe' (you didn't hear this from me) lakini inabidi pia utatue tatizo la emission (Kwanini mafuta hayachomwi yote?).
 
Kwa kiasi kikubwa inawezekana fuel pump yako imechoka hasa kama gari haiwezi kuaccelerate. Vinginevyo, inawezekana air filter yako imeshaziba, inabidi uibadilishe. Kwa jumla matatizo ya gari kuishiwa nguvu ni ama hakuna mafuta au hewa ya kutosha kwenye combustion chamber. Utaiona wakati mweingine inatoa moshi mweupe.
Umejibu kitaalam
 
Wandugu habari za mchana. Naomba msaada wa kiuzoefu na ufundi. Nina gari yangu Nisan Serena, from no where ilianza kukosa nguvu na hatimaye ikawa haichanganyi kwa maana ya kutomaliza resi.

Nmewaleta mafundi wengi na kukaribia kumaliza tatizo ila kilichonifanya niombe msaada hapa ni kwamba gari ikiwa haijafunikwa bonet inamaliza resi vizuri, ukifunika tu tatizo linarudi palepale. Mafundi wote niliowaleta, wamepima kwa mashine lakini tatizo liko palepale.

Ebu nisaidieni, nn cha weza kuwa tatizo na wapi au nani anaweza saidia.

Natanguliza shukrani
 
Umeandiia kama mlevi,tulia kwanza andika vizuri ili mtu akuelewe
 
Mmecheki mfumo wa gear uko vizuri?....
Je ukifunika bonnet temperature inapanda?...
Hebu cheki na hayo
 
Mmecheki mfumo wa gear uko vizuri?....
Je ukifunika bonnet temperature inapanda?...
Hebu cheki na hayo
Mkuu tumecheki na hakuna tatizo, temperature iko normal haipandi
 
Back
Top Bottom