Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Jamaa alikuwa na xtrail anadai tubadilishane na Toyota Rush aniongeze na 2m.
 
Kama unayapenda unaweza kununua ila kwa ushauri tu yale magari hayana faida zaidi ya hasara maana ni kama mayai tuu
 
Naona watu siku hizi magari haya ya Nissani Extrail wananunua sana.

Je wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu.
Magari mabovu tena....? Unajua mpaka gari inatoka ipelekwe kwenye soko inakua ishapitia sehemu kibao na wameiona inafaa na waipa star yake either ni star 1, 2, 3, 4 au 5.....sasa wewe unapokuja kusema ni mabovu sijui automobile skills kama unayo
 
Mafundi hapo ndo huwa wananichosha..huwa wanakisia tu mambo! Mi kuna fundi alinitia hasara sina hamu mpaka leo!!
 
Mafundi hapo ndo huwa wananichosha..huwa wanakisia tu mambo! Mi kuna fundi alinitia hasara sina hamu mpaka leo!!
Kuna fundi anaitwa Mikidadi yupo Ilala Machinga Complex ni mpuuzi kuliko mafundi wote niliowahi kukutana nao yaani ni yy ndo alifanya nichukie xtrail mazima gari ilizima ghafla barabarani kuja kucheki anadai sensor tukaenda kufix ile nimechukua gari sijafika hata karume imezima tena nampigia kaja anadai tubadilishe injini (kwa lugha rahisi tu).
 
MAFUNDI WA TZ HAWATAKI KUJIONGEZA....NISSAN XTRAIL NI GARI NZURI SANA ILA INATAKA NIDHAMU YA MATUNZO....SERVICE SI KUMWAGA OIL NA KUBADILI FILTER.....INATAKA CHECK UP KWA KILA PART HASA RADIATOR....WA TZ TUMEZOESHWA TOYOTA KWA SABABU KUNJUNGA SPARE NA MAFUNDI WENGI WANAJUA MIFUMO YA TOYOTA...
 
Bora ununue Rava4
 
Naona watu siku hizi magari haya ya Nissani Extrail wananunua sana.

Je wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu.
Usinunue,
Kwanza ni front exel, na kwa ukubwa ule lile ni tatizo, manufature hakuwaza sana.

Pili, spea zake utadhani za ki China, zinachoka ki urahisi na kibaya zaidi zina bei ghari kama spea za Uingereza (UK)

Tatu injini yake ilivyotengenezwa ikishafika kilometa 150,000 inaisha kama suruali ya kodrai ikianza matatizo mpaka uweke nyingine.

kwa hiyo, kama unafanya vitu kwa kufuata ushauri, bila kushoboka huo ndio ukweli wa hiyo mikweche.
 

NimekuPM mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…