Mkuu, naona nimekuja late.
Nissan X-trail zipo za aina mbili, zile zilizoundwa kati ya mwaka 2001-2007 na zile za tokea 2007 hadi sasa.
Hizi za 2001-2007 zinaweza kupata tatizo la engine kuunguruma kwa muda mrefu na kulifanya gari kama liwe linajivuta. Hii husababishwa na sensors kuanza kulegea hivyo kukosekana mawasiliano kati ya engine, sendors na engine management system.
Mara nyingi utaona taa ya njano kuashiria tatizo hili.
Tatizo lingine ni la camshaft ambapo timing belt inakuwa imechoka hivyo kuanza kuwa loose na kusababisha ku-jam na kupelekea pia brakes kushindwa kufanya kazi.
Nissan X trail lililoundwa kati ya mwaka 2000 na 2007
Pia kuna tatizo la mafuta kuvuja kwa X-trail za kati ya mwezi june mwaka 2000 - na November mwaka 2007 ambapo ule mpira wa kuingizia mafuta kwenda kwenye tank ya mafuta unakubali kutu kutambaa kwa kasi ya ajabu na kuleta uwezekano wa mafuta kuwa yanaishia hewani.
Hivyo kama unanunua gari hili la 2001- 2007, basi inakupasa uwe na fundi wako ambae ataangalia masuala haya mawili.
Kuhusu Nissan X-trail za mwaka 2007 hadi sasa nazo zina tatizo la steering control ambapo steering shaft inaanza kulegea na kusikika ikipiga kelele wakati wa kukata kona hivyo kupelekea siku moja dereva kushindwa kulidhibiti gari na kusababisha ajali mbaya sana.
Matatizo mengine ni kama yafutayo:
Turbo chargers kuanza kupiga kelele na moshi kuanza kuonekana kwenye engine na hii ni kwa yale magari ya Diesel.
Diesel filter kwa X-trail za diesel huwa zinajaza uchafu mapema Zaidi kuliko kawaida na hii hutokana na uharaka wa kuipiga moto engine na kutaka kuanza kuendesha wakati huohuo na kushindwa kuliacha gari lipige moto na engine ipate joto linalotakiwa.
Baadhi ya X-trail za kuanzia 2007 na kuendelea zina tatizo la umeme ambapo vifaa muhimu kama muziki , madirisha na dashboard kwa ujumla zinakuwa hazipati umeme wa moja kwa moja kutokana na hitilafu na wiring.
Hivyo basi , wakuu unapotaka Nissan Xtrail ya nguvu basi uzingatie matatizo hayo na uhakikishe anekununulia amefanya ukaguzi wa kueleweka kabla hajakabidhi mpunga uliouhangaikia.