Kwa waandaaji walidhamiria kupeleka mziki wa injili kwa hao watu, na ilikuwa target nzuri sababu mnawakusanya pamoja afu mnawapiga nondo za Injili
Na pia walitaka kunufaika pia kwa kuleta ladha ya tofauti kwa mashabiki wao
Kwa Mwimbaji nae pia hilo ndo lengo, pamoja na kuhakikisha kuwa wimbo wake unawafikia walengwa wake, Wimbo wake huu mpya, umeimbwa kuwalenga wakristo walio kengeuka, ambao wakiwa kanisani wanasinzia, ila wanapenda kuparty na kwenda kunywa beer, Wimbo una lengo la kuwafanya wakumbuke wanachofanya kuwa si sawa afu watafakari mienendo yao na wamuombe Mungu awasaidie.Hawa sio wakristo ambao ungewapata kokote kule kwa wingi ,zaidi ya kwenye TigoFiesta. Na wamejaa mtaani.
Na piaaa, kuhoji hili suala unakuwa hauna tofauti Na Mafarisayo walio hoji kama ni halali kwa Yesu kwenda Kula nyumban kwa Zakayo Mla Rushwa na mtoza Ushuru na kuhoji kama ni halali kwa kupakwa mafuta yule mama kahaba.
Jibu la Yesu lilikuwa simple kuwa wenye njaa ndo wanaohitaj chakula, wagonjwa ndo wanaohitaji kumuona Daktari.
Huyo mwanamziki ndo mwanamziki pekee ambae nimeona had sasa aliefanikiwa kuifikisha injili kwa walengwa.
Wengine wanapeleka injili kwa wachungaji, Injili peleka kwa walevi huko