Mjadala: Je, ruzuku ya bilioni 100 kwenye mafuta itapunguza bei ya mafuta kwa kiasi gani? "Jambo letu hatarini"

Mjadala: Je, ruzuku ya bilioni 100 kwenye mafuta itapunguza bei ya mafuta kwa kiasi gani? "Jambo letu hatarini"

Ndugu zangu,

Leo siku ya jumanne tarehe 10.05.2022 Ndugu Januari Makamba, Waziri wa Nishati akiwa bungeni ametangaza uamuzi wa serikali kutoa ruzuku ya takribani bilioni 100 za kitanzania.

Nikirejea uamuzi wa Waziri Makamba miezi michache iliyopita wa kuondoa tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta ulisababisha Serikali kukosa mapato zaidi ya bilioni 100 ikabidi Rais Samia abatilishe nafuu hio na kurudisha tozo hiyo.

Kwa hesabu za haraka haraka ni dhahiri ruzuku ya bilioni 100 huenda isiwe na unafuu wenye tija kwa lita ya mafuta ambayo kwa sasa yanauzwa angalau shilingi 3,200 kwa lita moja kwani wakati Makamba akitangaza nafuu hii itakayoanza tarehe 01.06.2022 pia amesema bei ya mafuta itaendelea kupaa.

Je,ruzuku hii ya bilioni 100 itaweza kumeza ongezeko la bei ya mafuta kiasi cha kuleta ahueni kwa mwananchi? Kimahesabu jibu ni hapana.

Bila Serikali kuwa kali na makini katika usimamizi wa "mnyororo" wa biashara ya mafuta ruzuku hii ni kazi bure.Mnyororo wa biashara ya mafuta unaanzia kwenye ununuzi wa mafuta kutoka ng'ambo hadi kumfikia mtumiaji wa mwisho.Hili ndilo jukumu la msingi kwani ruzuku sio "sustainable".

Serikali ikumbuke kuwa Rais kaahidi wafanyakazi nyongeza ya mshahara sasa kupunguza matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na kutumia kama ruzuku itasababisha kutokuwa na bajeti ya nyongeza ya mshahara.

Nawasilisha.
Hizi ruzuku zinatolewa kwa utaratibu wa aina gani? Tanzania kila kitu ni fursa ya wajanja kupiga
 
Suluhisho hapa ni kupunguza tozo katika Lita Moja ya mafuta yanayouzwa kwa Lita nitakribani sh 900
 
Itapigwa tu kama itatolewa kweli na mafuta yatapanda. Tupo hapa. Kuna watu wako bar wanagongesha cheers wakiisubiria kwa hamu kama itatoka.
 
Nawezaje kuhamia zanzibar, natokea NANJILINJI?
 
Jibu ni inategemea na muda ambao serikali itaSubsidize..

Kumbuka: Subsidy iko fixed yaani Tsh 100 Billioni.

Quantity to be subsidized: Variable

Tanzania inatumia Mafuta jumla lita Million 400 kwa mwezi.

Hivyo basi, kama serikali itasubsidize kwa muda wa mwezi mmoja, bei itapungua kama ifuatavyo:

Punguzo, P1 = Tsh100 Billioni / 400 Million litres

P1 = Tsh 250 per litre for 1 month

Pia, kama serikali itasubsidize kwa muda wa mwaka mmoja, bei itapungua kama ifuatavyo:

Punguzo, P12 = Tsh100 Billioni / 4.8 Billion litres

P12 = Tsh 20.8 per litre for 1 year.

Hitimisho: kiwango cha bei ya mafuta itakayopungua kutokana subsidy iliyoweka serikali itategemea na distribution timeframe, kwa maana kwamba kama muda utakuwa ni kwa mwezi mmoja, bei itapungua Tsh 250 kwa kila lita ya mafuta..ila kama distribution itakuwa kwa mwaka mzima then bei ya mafuta itapungua kwa Tsh 20.8 kwa kila lita..
Duh
 
Ni muhimu ikajulikana ili isije kuwa faida tu kwa wauza mafuta
 
Back
Top Bottom