Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

This is true, i buy your idea too! ila wasi was wangu ni kuwa isije ikawa na ww umechnagisha baada ya kumaliza mambo yako sasa unakimbia something wwhich is not good!otherwise i conquer with u good folk.

This is true, i buy your idea too! ila wasi was wangu ni kuwa isije ikawa na ww umechagisha baada ya kumaliza mambo yako sasa unakimbia something wwhich is not good!otherwise i conquer with u good folk.

This is true, i buy your idea too! ila wasi was wangu ni kuwa isije ikawa na ww umechnagisha baada ya kumaliza mambo yako sasa unakimbia something wwhich is not good!otherwise i conquer with u good folk.

Ukweli ni kwamba, Mimi binafsi ni mtu wa daraja la kati, uwezo wa kufanya sherehe ya mil 6, 7 mimi mwenyewe ninao. Ila nilitaka kufikisha ujumbe huu kwa jamii, mimi nilienda kanisani na mke mchumba wangu (sasa mke wangu) jumamosi moja miaka mitano iliyopita, nikafunga ndoa na baada ya hapo tukarudi nyumbani. Sikumchangisha mtu na wala mimi mwenyewe sikutumia hela yoyote zaidi ya shela , suti na pete. Mimi na mke wangu tunaishi kwa amani, nina watoto watatu,

kwa kweli hata mimi michango inanikera sana. yaani unajikuta mtu huwezi kuserve hata laki kwenye account. alafu usipochanga jamii inakutenga, ivi kwa mwendo huu tutafika. wenzetu wakenya wanachangiana ada za shule, sisi ukiomba uchangiwe ada, watu wanaleta roho mbaya eti " mi wangu hawajafika university kwa nini nikuchangie wewe'

Yani hilo ndo tatizo, inakuwa ngumu kufanya jambo lolote. Mtu unakuta upo bize na michango ya harusi, unacompromise hata na mahitaji ya msingi ya familia. na mbaya zaidi wanaweka viwango vya chini vikubwa mno!!

Ndugu JF hebu tujadili ni kwa namna gani tunaweza tukaliokoa taifa letu kutoka kwenye hiki kitanzi.

Wengi mnaopinga michango ni wale ambao tayari mmeshaoa.
Zakwenu mlichangisha bila aibu, za wenzenu mnaona kero

Tunachanga,after 1 or 3 years unasikia watu wameachana.NAUNGA MKONO HOJA.

Wengi mnaopinga michango ni wale ambao tayari mmeshaoa.
Zakwenu mlichangisha bila aibu, za wenzenu mnaona kero

Wewe ukubali au ukatae, michango ya haruc inabaki kuwa ni mwiba!!

Mimi nimeshindwa kumtambulisha mchumba wangu kwa kuwa naamini nikifanya hivyo tu, dingi ataanza kuwakwida rafki zake ambao alishirikiana nao kufanikisha sherehe za wanao. Anasubiria ya kwangu, nahisi kama nina mpango wa kumharibia, Japo natanguliza samahani kwa kuwa najua itamuuma sana.

Nitakachokifanya.
1. Nitaenda/tuma watru kwenda kwao na wife kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kukubaliana mahali.
2. Nitatafuta mahali hiyo japo hata nusu kama watadai kubwa sana, nyingine watanidai ambayo sitalipa kwa namna yoyote ile.
3. Nitawajulisha kuwa nawatangazia kuwa na mke rasmi siku fulanai katika kanisa ambalo nitalichagua kwa ajili ya kupata CHETI cha ndoa. Nasema kuwatangazia kwani nilishaoa kitambo kwa kulala naye, wengi hasa wazazi wetu hawajui kama sisi tuko kwenye ndoa kutokana na kufanya ndoa kwa siri kubwa. Hivyo nitawatangazia rasmi.
4. Siku ya harusi, itakuwa ni kuapa na baadae kwenda kupata chakula cha pamoja, picha za kawaida na kadhalika kisha kila mtu atarudi nyumbani kwake mapema kabla ya 12 jioni.

Nimechangia wengi, nahisi mimi sitaki kuchangiwa kwa kuwa ni mke wangu si mke wa watu wanaonichangia

wewe ukubali au ukatae, michango ya haruc inabaki kuwa ni mwiba!!
hii kitu ni mwiba mkali mno zaidi ya kodi ninayo lipa serikalini. Just imagine kwa uchache nimechangia 200000 kwa mwezi huu unaoisha leo na maisha inabidi ya endelee kama vile top up money za ada za wadogo zetu vyuo vikuu n.k hapa juu ya meza kuna kama tatu hivi zote zahitaji mchango!!!!!

Umeongea vema, kuna jamaa ni twinces wanaoa pamoja wanasumbua hao kudai michango najuta kuwafahamu.

Hapa nina kadi sita, kati ya hizo nne za watu wangu wa karibu, mbili hata siwafahamu. Halafu eti wanaweka na minimum amount eti 50,000/- huku si kuumizana....???

Yaani hii michango inaumiza kweli Mrembo..

Wangapi wanaangalia mikanda ya video ya harusi zao at least kila mwaka? This is debatable.

Pili, watu wengi wanasema, hatuchangii kwa kupenda, bali kufuta lawama tu. This is also debatable?

ulijipendekeza.kwanini usikatae?? Aibu zenu zinawasuta eeehhhh. Koma

Wewe ukubali au ukatae, michango ya haruc inabaki kuwa ni mwiba!!

Naunga mkono hoja.Hii kitu ni kero na naona inazidi kuwa mzigo kadiri siku zinavyoenda.Binafsi nilishaacha kuchangia,so nikipata msg ya mchango I just ignore,mambo yangu ya msingi hayaendi,ndiyo nichangie anasa?Sijui nani katuroga watanzania.Mwingine utakuta hamjawasiliana miaka miwili iliyopita lakini akiwa na harusi ndo anakumbuka kwamba na wewe upo,utashangaa msg kwenye simu zako zote!!Inakera sana

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…