Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Usiombe uchaguliwe kwenye kamati ya harusi ndo utapatwa na hasira mara mbili maana wakati wa ahadi ukisema mimi nitatoa lakimoja wanakamati wote wanaguna aaaaaaaaaaaah!
 
tatizo usipochanga unatengwa na marafiki, siku ukipatwa na matatizo wansema huyo siyo mwenzetu! mbona huwa changii? mfano hivi karibuni maeneo ya kawe mama mwenye nyumba alimpa mpanagaji wake notice kisa hajachangia birth day ya mtoto
 
Mi sielewi kabisa watu wanaoana wao kisha nichangie mie WHAT THE HECK!!Sherehe ni jambo la hiari na ukitaka sherehe kubwa unatakiwa uwe na uwezo wa kuimudu gharama zake sio kutafuta kuwapa watu lawama...
Msibani kutoka mchango wa rambirambi ni poa lakini harusi no no :nono::nono:,sichangii mtu na sina haja ya kuchangiwa na mtu PERIOD!!
 
Hiyo si Kama ushirika wa pombe kwenye bar? Marafiki watakunywesha mpaka ushindwe kukumbuka nyumbani kwako, lakini muombe akusaidie japo sembe ya Siku hiyo atakwambia "....brother pombe nkunyweshe na mkeo nkulishie?......"

well said, na iyo michango ya harusi wanakamati wanahakikisha inaisha hapo hapo bwana na bi harusi wanaanza moja.
 
tatizo usipochanga unatengwa na marafiki, siku ukipatwa na matatizo wansema huyo siyo mwenzetu! mbona huwa changii? mfano hivi karibuni maeneo ya kawe mama mwenye nyumba alimpa mpanagaji wake notice kisa hajachangia birth day ya mtoto
Hii siyo kweli hata kidogo, kutengwa na kundi la wajinga is good reddense & Great relief.

Kutengwa na dhehebu lako la dini ndio kitu angalau unaweza ukajali lakini siyo genge la wajinga wanaoona kuchangishana pesa nyingi kwa ajili ya kulewea siku moja kwa gear ya harusi huku wakiwaacha maharusi na ufukara wao ni ujinga zaidi.
 
kati ya hizo mkuu kuna kadi mbili wameandika kabisa mchango sio chini ya laki moja,kuna raia wengine sijui huwa wanafikiria kwa kutumia ma------?

Si chini ya laki moja? Mchango mtu anatoa anachoweza ya nini kuwekeana viwango? Huo sio mchango wa harusi bali ni ada/kodi ya harusi. Tatizo letu ni kupenda sifa/ufahri. Si vibaya kufanya harusi za kifahari ila sehemu kubwa ya gharama itoke kwa wahusika wenyewe badala ya kuzihamishia hizo gharama kwa watu wengine.

Nakushauri usifuate hicho kiwango chao bali uwachangie kwa kiwango unachoweza.
 

msibani ni sawa kusaidina pale mchango unapohitajika,likini hii mikiki mikiki ya michango ya harusi ni hiari tu,tatizo wahusika hawaelewi hilo
 

mkuu matola tena sio rafiki,hadi ndugu wanakutenga.wao wanaamini wewe unao uwezo wa kuchangia kumbe hawajui ratiba zako na bajeti yako
 
Mimi nilishaacha kuhudhuria vikao vya harusi na sitaki kadi yoyote ya mchango kwani kipato changu haitoshelezi kwa familia yangu, sembuse kuchangia harusi!
 
Big up mhaya wangu kakataa katukatu japokuwa alikuwa mchangaji mzuri yetu haina michango ila watu 50 wenye bahati watajumuika nasi kwa dinner,kuchangisha ni lawama kwanza inabidi ujitahidi kuwaridhisha wageni wachangaji(japo ni ngumu)ila kama hujamchangisha mtu ukamuita aje ajumuike nawe labda dinner au lunch atachokikuta ndo uwezo wako sio atoke hapo ooh nimechanga laki nimeambulia bia moja??hhaaa ila kuna watu wanapenda kujitutumua jamani unakuta ana dhiki kibaoo ila anavyohangaika na visherehe mara birthday ya mtoto mara kipaimara tubadilike maisha yanabana sana unaoa kwa harusi yakifahari unasifiwa ukishaanza maisha ya ndoa mnaanza kulipa madeni akha haihusu
 

Mkuu kama umekuja kulalamika huku wala sitaki unichangie tena. Baki na hizo cent zako
 
Easy sana, na wewe oa peleka kadi kwa wote mnaofahamiana...baada ya hapo utawapata wachache wa kuwachangia
 
sikuchangisha na sikufanya hayo masendoff/kitchen party sababu yakukwepa kero hizo jinsi ninavyokwazika sitaki mtu nimkwaze
message ninazotumiwa ni nyingi watu wengine ni majirani tu hata hatuna uhusianao ila nasema sichangii ,mshahara wenyewe huu,mwisho wa mwaka huu! ada january kichwa kishaanza kuniuma kwa kweli nichangie maharusi ada hakuna mtu atanisaidia bora lawama kuliko fedheha ya wanangu kubaki nyumbani bila ada.kuna mtu alitaka mchango wa harusi na kparty yaani shangazi yangu na mimi ile june nimebanwa na ada za watoto second term,mpaka leo huyu shangazi ameacha kuwasiliana nami kabisaa ila nilimwambia nina watoto wakulipia ada na nitachangia sherehe wanangu wabaki nyumbani au nifanyeje ??bora lawama kuliko fedheha
 
juzi kuna mtu kaja ananiambia dada naomba ndoo 2 tu za rangi nipige kule kwangu niamie nikase hawa ndio watu kuliko nichangie harusi bora nimpe huyu
 

Wish I cud give u more than 1 like.
 
Kwa upande wetu kuna unafuu afadhali. (zanzibar) sana sana wanaochangia ni wanafamilia tena wa karibu sana tena wala hamna kupewa kadi ya mchango.
Ukienda kwenye arusi Unajua kama hii wenyewe wanajiweza na hii ni ya watu wa wastan tu. Mtu anafanya kwa uwezo wake.
 
mie sharti langu moja tu....

Kama nilikuchangisha niletee kadi ya mchango...


Kwa raha zangu

Na hivi sikuchangisha zaidi ya familia kunipiga tafu

Naziangalia tu kadi zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…