Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Unawachangia halafu wanakaa mwezi 2 wanaachana, mm nakudai mchango yangu!
 
KHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
MI NILITOA TANGAZO HAPA OFISINI KUWA WASINILETEE KADI ZA MICHANGO YA HARUSI SITAKI MAANA KWENYE SALARY SLEEP YANGU HAKUNA KIPENGELE CHA MICHANGO YA HARUSI MAANA MTU MDOGO WAKE ANAOLEWA HUKO KISIJU HATA SIMFAHAMU ANANIPITISHIA MCHANGO '


HAPANA NO
 
Hatuishi ndani ya box tunaishi na jamii. Mchango kama watu wanajitolea kuna ubaya gani? Wapo watu wakiambiwa wachange wanakataa hamna kosa ni ombi, kuna wengine wanapenda kuchangia tu utakataa uwaambie sitaki michango yenu?
Kila mtu yupo huru kuishi atakavyo ndio maana hupangiwi matumizi ya pesa yako. Hata michango ya humu kila mtu anajaribu kuchangia mawazo yake kwa mtizamo wake. Kuna namna nyingi za kushirikiana katika jamii, sio lazima kwa kuchangia sherehe.
 
MI NILITOA TANGAZO HAPA OFISINI KUWA WASINILETEE KADI ZA MICHANGO YA HARUSI SITAKI MAANA KWENYE SALARY SLEEP YANGU HAKUNA KIPENGELE CHA MICHANGO YA HARUSI MAANA MTU MDOGO WAKE ANAOLEWA HUKO KISIJU HATA SIMFAHAMU ANANIPITISHIA MCHANGO '


HAPANA NO
Mkuu umefunika kwakweli
 
Mleta mada atakuwa ameshaoa sasa anapata uchungu kuchangia wenzake na ndivyo tulivyo wa tz.
 
Wapeni watu vitu kwani kipimo mtoacho ndicho kitakacho pimwa vifuani mwenu kiasi cha kusukwasukwa na kujaa haya aliyasema Bwana Yesu. Pia tusizimie katika kutenda mema maana tutavuna kwa wakati kama tusipozimia mioyo. Mtoa mada moyo wako umezimia unapaswa kubustiwa na Neno la Uzima kutoka kinywani mwa Kristo Yesu. Barikiwa.
 
We mtumishi vipi?. Sijui umekariri hilo neno ama? Unless if you are being sarcastic. Unajua hata yanayofanyika huko kwenye hizo harusi? Pombe, kuopoana, kujionyesha...

Yesu Alikuwa anazungumzia kuwasaidia wenye shida na siyo hawa wanaotaka anasa wakati uwezo hawana. Kama kweli unataka mibaraka ya kweli saidia ambao wana shida ya kweli (harusi kwangu hai - qualify kama shida) tena ambao hawakujui huko mahospitalini, mabarabarani, kwenye ma-orphanages n.k. Samahani kama nimekukwaza mkuu lakini kila mtu ana uhuru wa kufanya atakacho. Kama kupangiwa hii michango ya harusi is your cup of tea endelea tu kwani ni maisha yako na huvunji sheria yo yote.
 
Ivi kama hauna hela unaweka sherehe ya nin afu mnaoa kwa mbwembwe madem wenyewe wameshatumika hao, waliombaka bfore wanakuchora tu umevaa kisuti umeshika kadem kameng'aa kwenye sheraa chini kumechoka ka ndoo ya chooni, senzi. Uliwahi kusikia babu zenu waliweka harusi wakati wanawaoa bibi zenu acheni uzungu usio na tija kwa maisha ya sasa. Senziiii tena
 
mrejessho...nimepokea slary ila nimeshindwa kutoa kwa maana matumizi namipango naksidia wazazi madogo mtoto ni mengi...yani nimebakiwa nahela ambayokutumia haifiki siku kumi n atano...kw avileniko mwenyewe naishi kibishi kiume....sio kwamba kuchangii hatupenndi ila sina hela jamani nikifikia kipindi mfukoni haiwezi pungua elfu hamsini na account si chini ya milioni tano tena untouchable na siwazi ntakulanini basi ntachangia
 
 
Mfano wako hauendani na uhalisia. Nchi za Ulaya na hao sijui wasanii hawachangii mambo ya sherehe tena za kujitakia. Wanachangia watu wenye shida - njaa, magonjwa, maafa ya asili n.k. Usichanganye ukiona mafisadi wanapoiba pesa hizo za misaada na kuanza kuzitumbua ukadhani kuwa zililengwa kwa matumizi hayo.

Hatukatai kuchangia. Changia sana tu ukipenda hulazimishwi na mtu lakini hii tabia ya kushikana mashati mpaka na kuwekeana kiwango kabisa ni no no. Njoo kwangu kama una shida ya kweli mf. kuuguliwa, karo za watoto, dharura zingine n.k. lakini siyo kadi ya harusi halafu na kiwango umejipangia. Nitakutoa mkuku. Pesa hizo ni afadhali mara mia nizipeleke kwa wagonjwa mahospitalini au huko kwenye ma-orphanages. But again kila mtu na maisha yake. Tusilazimishane!
 


Ha ha ha ha utakuwa unaolewa wewe hivi karibuni, si bure
 

Umeongea maneno kuntu
 
Habari za leo,

Jamani hili swala la michango harusi naona limekuwa jipu, tena jipu lililoota kwenye paji la uso.
Mtu anakuomba mchango wa harusi, alafu anakuwekea kiwango cha chini kuchanga.
Mwisho wa mwezi huu wa tano imenitoka Tsh 950,000 kwa michango mbali mbali. Sasa najiuliza kwa mshahara upi enzi hizi za JPM??

Usipochanga, muomba mchango anajenga uhasama mbaya, hata salamu hapokei

Hivi kwa mwendo huu, na kwa kipato chetu kidogo, maisha yatakuwaje.

Jamani tubadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…