Mjadala - Kitabu cha unyama wa Paul Kagame: Behind the Presidential Curtain: Inside Out of real Paul Kagame

Mkuu tuna appreciate moyo wako wa kuweza kusoma na kutudadavulia hapa .Big Up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mleta uzi ni muhimu kusoma hicho kitabu ukiwa na Akiba ya jicho la tatu. Haifai kuweka hapa maandishi na simulizi na madai ya huyo mwandishi ukasema ndio ukweli na kuanza kumhukumu Kagame. Tungepata vitabu kadhaa vya pande mbili au hata pande 3 tujue ukweli umelala wapi. Lakini kumsikiliza huyu bodyguard mmoja sikubaliani nayo kabisa. Hata mimi nitakitafuta kitabu hiki nikisome na kuendelea kufanya utafiti Zaidi kuhusu Kagame, lakini ukweli ni kwamba kwenye kuongoza haswa unapotaka kuweka mambo sawa hutakosa maadui huo ndio ukweli. Kuna mengi mazuri na mabaya mengi tunasikia kuhusu Kagame lakini pia tunasikia Rwanda inaendelea vizuri sana kiuchumi sasa labda Wanyarwanda watuambie kama Kagame amesaidia nchi au la. Kwenye kuongoza nchi na kuleta mabadiriko ya jamaa mengi sana mabaya hupitiwa hakuna taifa lilifanikiwa duniani bila kupita kwenye wakati ambao sio wa kujivunia soma nchi za Ulaya, Marekani, Asia wenzetu walipita vipindi vibaya sana lakini leo wako wapi…? Hebu tuwe na akili ya mtu mzima.
 
"lakini pia tunasikia Rwanda inaendelea vizuri sana kiuchumi"
Stori za Uchumi mzuri wa Rwanda ni propoganda tupu za viongozi wachache wa magharibi walioshindwa kushughulika vizuri na mauaji ya kimbari na mashirika ya maendeleo yanayotaka kuonyesha kwa kulazimisha matokeo mazuri ya misaada. Nenda kaangalie data zake ulinganishe na mataifa mengine,ni ya kawaida sana.
 

Jamaa anatumia genocide kama political tool for silencing his opponents. I don't like that.... Wapo wahutu Wengi waliokufa wakipinga genocide. PK hataki kusikia hilo. Poor him!
 
Aaaaah senior officer acha povu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuwafanya wakina Blair na Clinton wamuunge mkono sababu ya kushindwa kwao kushughulika na genocide ipasavyo.
He is also a master in propoganda and PR
Jamaa anatumia genocide kama political tool for silencing his opponents. I don't like that.... Wapo wahutu Wengi waliokufa wakipinga genocide. PK hataki kusikia hilo. Poor him!
 
Your point then...?
 
Kuna Genocidals humu yaani hawatulii bila kuleta negative threads za Kagame na Rwanda.
Ukisoma threads humu JF utasema Rwanda hakukaliki kumbe stori zinaishia humu humu...uzuri wanyarwanda wengi JF hata hawaifahamu na kiswahili hawaelewi hivyo kelele zote hizi hazina impact yoyote kwa wahusika..
Unadhani adui ataandika nini zaidi ya kutunga hadithi!!
Hiki kitabu pamoja na vingine havina ukweli wowote ni propaganda za maadui wa Kagame..
 
Hulazimishwi kufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alianza mauaji ya kimbari kwa Wahutu kabla ya haya tuliyoyajua baadae. Sasa akituhumiwa kuwa haya makubwa ni muendelezo wa aliyoyaanzisha, anakuwa mbogo na nafikiri anatamani aue watu wote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…