Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

alipooteshwa na Mungu amemwambia kuna meli mbili zinakuja na watu kutoka ulaya watakapoisha tu watu hao na dawa itaisha nguvu so watu waende kwa wingi wawahi maana meli zinakaribia kufika.Kuna habari nimezipata kuwa Mkwere alipokuwa kwenye zoezi la kufukua nyayo alipita kwa mchungaji na kupewa dawa mwenye macho haambiwi tazama na masikio haambiwi sikia na ****** haambiwi kujamba kila mwenye tatizo aende aapate tiba!

we ndo utafanya watu wasiende kudanganywa tena coz umemtaja mdanganyika mkuu kuwa naye kaenda. kama unataka kudanganya watu waende kudanganywa tafuta bac catalyst anaendana, achana na mkwere, kwanza alikwenda huko aliomba ruhusa kwa shehe yahya amtabirie kwanza??!!! teh teh teh jamani mbavu zangu, nchi hii jamani!!!!! du! hiv kama prezdaa anaongoza nchi kwa rada za kishirikina itakuwa laymen n women kudanganywa kulishwa uchafu etii ni dawa ya ngoma??? haya fungueni zipu zenu bac eti kuna dawa muone moto wake..wafuasi wa kinjekitile nyie!! haya semeni majiiiii na risasi haitaingia.....teh teh teh teeeeeee, uuuuwi, apaaa wandeeee, zama hizi za dot com bado tu tunashoiya jaman????!!!! je tutafikaaa?? chambeche mzee wangu makwaia wa kuhenga!
 
Is this material from the septic Tank?...
Lengo lako nini kuandika takamwili hizi?
Unashangaa mawaziri kwenda huko...my hairs!..Hivi kuumwa kuna uwaziri?
Kwanini usimshangae mkwere aliyekuwa wa kwanza kwenda?

umeshasema "mkwere" sasa tushangae nini tena!!!! mbona hatukushangaa wakti Shehe Yahay anampa rada za kuwaongoza wadanganyika kuwatoa dunia ya tatu kuwapeleka ya saba!!!

tafuta mfano mwingine unaoweza ku-fuel huu ujinga, huo uliotoa utafanya wadanganyika wastuke haraka....comed mpooooo, dili la kutuvunja mbavu hilo hapoooooo peupeeeeeeee!!!
 
Mkuu inaonekana umeshtuka sana uko njiani unakwenda? Kilichoshtusha sana ni the way of thinking ya watu wetu. Lengo langu hasa ni kuhimiza watu kuthink reasonable na ninashangaa mawaziri kwa kua ndio wasimamizi wa taifa sasa kama hivi ndivyo wanavyofikiri tunadhani kua kutapatikana ufumbuzi wa changamoto tulizonazo

ndugu yangu ukishangaa ya musa utayaona ya firauni...wewe wawashangaa mawaziri wakati aliewateua anaongoza nchi kwa rada za shehe yahya??!!..mtashangaa sana mwaka huu!!
 
jamaa hesabu yake nzuri, amejua akiweka bei juu maswali yatakua mengi. Vuna baba wa loliondo, ujanja si lazima ukae twn
 
Jamani, nasisitiza umakini katika jambo hili, watu wengi wamelizwa na waganga!, mganga hakubali kushindwa, yaani utashindwa wewe lakini si yeye!.

Mti mzuri utaujua kwa matunda yake!. Tuvute subira tuone mwisho wa haya. Isije ikawa Shetani anataka kudanganya watu kwamba wamepona virusi, matokeo yake wakaacha ARV, na wengine wakaanzisha maambukizi mapya kwao wenyewe na kwa wale wasio na virusi!.
 
huu ni ushirikina na usanii tu .Hakuna atayepona hii ni DECI part II ni mradi wa wakubwa, kumbukeni katika utawala wa JK kila uchaguzi unapokamilika kunaibuka miradi ya kitapeli tulianza na DECI leo tuna Loliondo.Mimi nasema SIDANGANYIKI.Kesho mtanikumbuka ninayosema leo.Kuna mafisadi watatu wamejificha hapo:
  1. Yule babu mganga
  2. Kile kijiji kinacho-host kwani kuna ushuru wa shs.20,000 kwa kila mgonjwa
  3. Wenye vyombo vya usafiri
Hebu fikiria kuna kadiriwa watu 5000 wamekwisha fika (watu 5,000 x shs.20,000) Tayari kijiji kimejikusanyia shs.100,000,000
Kwa yule mganga atakuwa ameweka kibindoni shs.2,500,000

Huu ni wizi mkubwa
 
Kuhusu huyo Askofu hakuna ubishi anatibu na watu wanapona. Mahita alipata dawa na alipopona akarudi na familia nzima. Mtoto wa Ndesamburu alitua kwa helicopter akiwa na mkuu wa mkoa wa Musoma. Magufuli alipata dawa huku akizuga amekwenda kukagua barabara. Kikwete alifika na mkewe akafuatia. Mufti mkuu ameshapata dawa na kama huamini hebu kajionee waislamu walivyo wengi kuliko wakristo. Wanaotoka huko wote wanakiri kupona bila kuzingatia imani zao. Babu hapokei zaidi ya sh.500 na hataki zawadi kama shukurani baada ya kupona. Amekataa gari na nyumba toka kwa muhindi na pia amekataa kuhamishiwa Dodoma na kudai Loliondo ni katikati ya dunia na kazi yake si kwa Tanzania tu bali dunia nzima. Kikubwa ni kwa serikali kusaidia kujenga vyoo kwani kuna hatari ya kilichopo kujaa. Pia chakula ni tabu kwani kuna hatari ya njaa kwani kuna uwezekano wa kusubiri dawa hadi siku nne na zaidi. Nina ndugu yangu amepona vidonda vya tumbo kabisa na kwa kumjaribu tumetia pilipili kibao ila sisi ndio tumeshindwa kula chakula.

NABII HAKUBALIKI KWAO.
waislamu ni wengi huko kwa sababu wana "KITI". KITI amewaruhusu waende huko. ila mwanangu kiti wakti mwingine anakuwa-ga mkaliiii...akisema mimi KITI nimesema stokiii na hatoki kweli mpaka mchinje jogoo wa kijani. kama huna toa milioni moja wapewe waungwana...teh teh teh teh!
 
Picha za pilikapilika za watu wakijaribu kupata tiba za magonjwa sugu maeneo ya Loliondo:
GARI%2BLA%2BMANISPAA%2BNDANI%2BYA%2BMCHUNGAJI.JPG

magari%2Bwakinywa%2Bdawa.jpg

PICHA%2BMAGARI.JPG

Picha hisani ya Mzee wa Mshitu

Mungu babaeee watu wako wanaangamia kwa kukosa maarifa Baba wa Mbinguni!!!! kweli Ujinga na Umaskini ni kitu mbaya sana..CCM imejua kweli ni vip waendelee kutawala wadanganyika..wape ujinga na umaskini...kwishnee khabari yao
 
Nikweli unachosema, I once when was pregnant of my first born outside the country..Sasa nikaambiwa kuwa nitoe history ya ndugu zangu wakti wa uzazi na 50% wenye maumbile kama yangu walikuwa wamepasuliwa. Me on my side nilishajiambia sitaki kupasuliwa so ili kuondoa biase ya Dr. nikaandika hakuna hata mmoja aliyepasuliwa wote wana deliver normally. Dr. akanipima baadaye akaniambia it seams wewe hutaweza kudeliver normal...akasema itategemea your choice though ila tutaweka hii note wakati wa kujifungua ikitokea tatizo tutakupasua..Then kabla ya my time siku moja nimeenda clinic Dr. kunipima nikaona anachukua simu akaita tax nikaambiwa nisiende nyumbani moja kwa moja niende referal hosp...Nikaenda kufika kule duuh nikawekwa ma machine mengi mengi then nikauliza kwani tatizo nini wakaniambia we suspect the baby is dead...nikamwambia dr. my baby can never die! Akaona huyu mgonjwa anajipa moyo...akasema yes its good to think that way but also its gud to prepare your mind incase we find out its dead...nikamwambia tena I choose not to prepare my mind for the lose but to believe is alive for christ is also alive and have never left me alone...Dr. akaona hii argument siyo nzuri akaendelea na vipimo..So akasema I cant feel the beats and you see you can read from your side there is graph nikamwambia I dont believe the graph give me time...Basi wakaniambia okay then we will examine you after 15 min. naona alinikubalia ili asiniumize..Then after 15min they examined wakakuta mapigo kwa mbali...nikaambiwa nipumzike na nilale kwa ubavu kila baada ya 5 min wananichunguza mapigo yakapanda mpaka normal... Then wakasema wanipeleke theatre pindi ile enxiety ikiondoka nikamwambie dr. I dont want that way i will deliver normally...So dr. akaniangalia akasema please its risk for me I understand what you mean my darling na kuni pet pet kwingi..Nikamwambia I will sign and will bear all the consequences! Wakaniacha day one niko salama na mtoto mzima then wakasema kama ndivyo basi tuna initiate labour lakini kama contraction hazitakuwa nyingi then tunakupasua nikasema sawa...Wakanianziashia put the cathetor and kuniwekea maji ya uchungu huku waki monitor progress ya mtoto..and the thing went on mpaka nikapata baby boy normal bila kupasuliwa alive until todate Glory to God!

So second born at Aghakhan dr akaniambia nipeleke report ya yule wa kwanza kusoma akasema huyu ceasarian session kama kwenye excelent centre mambo yalikuwa hivi sisi hatutake risk...nikanyamamza maana dr wetu collaboration na mgonjwa unatakiwa kuwa makini they know almost everything even against your will...So was praying God to make my day of delivery before that date nakweli ikawa a week before na dr. aliyekuwepo akasema aah huyu mwacheni mbona anajifungua kawaida ila mwekeeni maji ya chungu and thats how I got my second born. Why all this kuwa chosha no but to tell you siyo kila kitu science inaweza kujibu na mjue kuwa kama ni hiyo science hata mimi naifahamu inside out lakini haijatawala maisha yangu iko applicable to a limited extent for me science without faith is empty!

Good account but is caesarian session a normal delivery?
 
Kama ni kweli, Serikali na taasisi husika zifanye jitihada za kiutaalamu ili dawa zake zitambuliwe na TFDA na WHO (ila WHO wanamizengwe sana). Hii itawezesha makampuni yanayotengeneza dawa kufanya naye kazi kwa mkataba ambao utamwezesha yeye kupata faida kubwa na pia itawezekana kusaidia watu wengi zaidi, kupitia mass production ya dawa hizo na huduma sehemu mbalimbali. Au zinamasharti ya kiza?

TATIZO WHO hawafanyi kazi kwa kuoteshwa. watu wamejifungia labaratory wanafanya testing saa hizi wewe ukalete mambo yako ya kuoteshwa nani atakuskia?? kinjekitike at work. wewe risasi ikipigwa sema majiiiii na risasi itageuka kuwa maji na tutamshinda jerumani.....tatizo lilikuja pale jerumani katili alipoaanza kuwamiminia risasi...du!du!du, kilichoonekana ni uharo tuuuu, na hiyo ndo dawa ya kubwa jinga
 
babu anasema mtu mwingine akichuma au chimba huo mzizi wa dawa hawezi pona mpaka achimbe yeye....sasa swali je?, kuna nguvu za giza?

ndo manakee, pigia mstari, unauliza mtori uchagani?? weee vip??

pia jiulize akifa leo na dawa imekufa au??
 
kwanza wana jf mfahamu kuwa huyu si mganga wala nabii bali ni mchungaji
kumbuka mungu huwainua wanyonge kutoka mavumbini na kuwaketisha na wakuu,huyu ni umchungaji mdogo tuu na wala si askofu,ametumwa na mungu kuokoa wanyonge na wenye hofu.sisi tulio arusha tumeshuhudia na tumepona mnataka tuamini kipi?dawa za kizungu ambazo unatumia mpaka kufa.

wale wasio amini hawaumwi kabisa,kumbuka kama una dada au kaka anangoma unadhani utamwacha nyumbani?
acheni kubeza bwana acheni watu wapige glass zao
wapone

hiv yule wa uganda aliyewakaanga wenzake kama mishkaki naye alikuwa mchungajieeeee???!! ok, well......
 
Juzi hapa kuna wana JF walienda huko sasa wamefikia wapi kuhusu hayo mambo maana hapa tunataka more pics na habari zaidi maana so far habari ni zile zile....tupeni more news guys.....
 
Watu wataambukizana ukimwi huko huko

natabiri huko mbeleni babu atakuja kubadilisha masharti. lazima aipake dawa kwenye nanii yake alafu akuingizie. kwa kina Hawa haitakuwa tabu, tatizo kina Adamu sasa!!!! Lazima ubong'oe....hapo chacha hapo!!!
 
Ni juzi tuu mkuu mmoja wa serikali alitangaza kua ugonjwa kama wa kisukari hauna dawa kabisa, leo gazeti la Mwananchi linatoa taarifa kua kuna mchungaji anatibu kisukari, ukimwi na magonjwa mengine sugu. Kinachishtusha sana ni kuona akili za waTanzania wengi namna gani zinaweza kukinaishwa maramoja.

Ugonjwa kama ukimwi kisukari nafikiri sio ugonjwa wa mtu kupewa kikombe kimoja cha dawa na kufika kwenye conclusion kua mtu ameshapona, tunaribu kua reasonable, hivi ni vitu vinahitaji muda kidogo ili kujua kua kweli dawa hiyo inatibu.

Upande mwingine ni ule wa mtu kudai kua ana mawasiliano na God hili nalo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kinachoshtusha zaidi ni kusikia watu ambao tunawaamini kua ndio viongozi wa taifa letu kama wabunge mawaziri wanamiminika huko na mkuu wa mkoa anaiomba serikali ifacilatate mazingira ya watu kwenda. Hii ndio Tanzania yetu. Mungu ibariki dunia, Afrika na Tanzania
Yesu alitema mate kwenye udongo, akafanya tope na kumpaka kipofu, na mara akaona.
Je wewe waweza fanya hivyo na kipofu akaona?
Je kuna maelezo scientific ya kueleza tukio hilo?
Huyu mchungaji wanasema alioteshwa na Mungu dawa hii, sasa nyinyi mnataka scientific explanation! Fikiria dawa ni moja tu kwa magonjwa yote hayo! (haya kisayansi ni magonjwa tofauti kabisa - ukimwini virus, kisukari si virus wala bacteria, kansa hivyo hivyo nk.
Mti wenyewe siyo siri amewaonyesha watu wote, ila mtu mwingine akichemshahiyo dawa maji yanabaki meupe tu ila akichemsha mganga maji yanageuka rangi na kuwa kama chai - shangaa hapo!
Kuna testmony za watu waliotumia na kupona; muanzisha thread anasema mzee wake alikuwa na kisukari na sasa kapona kabisa na wako wengi wanaokiri hivyo katika thread hizi; mwataka nini zaidi? Asiyeamini asiende anayeamini aende.
Hata wakati wa Yesu wapo ambao hawakumwamini; hata wakati wa gharika kuu wapo wengi waliokaidi, na wakati wa sodoma na gomora hivyo hivyo na wa mwisho aligeuka nguzo ya chumvi! MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
 
Sasa we unaona kipi bora waendelee na dozi huku wakifa taratibu, au aamini apone kabisa na kuendelea na enjoyment ya muda wa maisha yao uliobaki? hata kwenye biashara risk averse remain poor na risk takers wanachance ya kubwa ya kuuaga umskini milele..So my friend let them choose what they want; au nawewe unaogopa utakosa wateja wa kuja kukupa consultancy fee na pesa za dose?
Nakubaliana nawewe;
mganga hajamwambia mtu aache dozi yake ya kila siku? Wewe endelea nayo na ya mganga kunywa halafu kapime upate majibu current.
 
muulize jeikei maana amekwishaitumia kama unataka namba yake nibeepu nikupigie uongee naye

huyu alishatabiriwa na shehe yahya kuwa akilogwa tu akala dawa za hospitalini Dr Slaa anampindua hapo hapo. ameambiwa dawa yake ni ya kienyeji(sema kiafirika) na itatoka kule kung'aapo nyota ya maji ya bahari nako ni kule kuliko ule unyayo wa mtu wa kale zaid dunia umzolopagaaaaaz wa nyota ya urari, hakika ni kaskazini mashariki ya tanganyika kule walipomwaga ile damu ya Wana Wa Nchi kwa ajili ya chakula cha jini makata
 
Yesu alitema mate kwenye udongo, akafanya tope na kumpaka kipofu, na mara akaona.
Je wewe waweza fanya hivyo na kipofu akaona
?
Je kuna maelezo scientific ya kueleza tukio hilo?
Huyu mchungaji wanasema alioteshwa na Mungu dawa hii, sasa nyinyi mnataka scientific explanation! Fikiria dawa ni moja tu kwa magonjwa yote hayo! (haya kisayansi ni magonjwa tofauti kabisa - ukimwini virus, kisukari si virus wala bacteria, kansa hivyo hivyo nk.
Mti wenyewe siyo siri amewaonyesha watu wote, ila mtu mwingine akichemshahiyo dawa maji yanabaki meupe tu ila akichemsha mganga maji yanageuka rangi na kuwa kama chai - shangaa hapo!
Kuna testmony za watu waliotumia na kupona; muanzisha thread anasema mzee wake alikuwa na kisukari na sasa kapona kabisa na wako wengi wanaokiri hivyo katika thread hizi; mwataka nini zaidi? Asiyeamini asiende anayeamini aende.
Hata wakati wa Yesu wapo ambao hawakumwamini; hata wakati wa gharika kuu wapo wengi waliokaidi, na wakati wa sodoma na gomora hivyo hivyo na wa mwisho aligeuka nguzo ya chumvi! MWENYE MASIKIO NA ASIKIE

kwanza nieleze vizuri nijue yesu ni nani/nini!! mimi ni mhindu ila wazazi wangu walikuwa wabudha

pili hilo la yesu tumeliskia jee kinjekitile alipowa-corn babu zetu waseme "majiiiiii" unajua kilichotokea jeruman alipokunya risasi zake???.......ilikuwa ni uharo tu kwa ku-go front

na kibwetere je unajua aliwafanyia nini wale wajinga wa kule uganda????........halafu bwana kibwetere sku hizi naskia yupo sehemu flan(spataji mtaenda mkamata nyie wafitini) anakula wine yake kimyaaaaaa baada ya kuwa resitisha in peace wale jamaa kwa kuwapeleka mbinguni kinamna.....kweli wajinga ndiyo waliwao!!!
 
Back
Top Bottom