Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Haya mambo ni mazito!, unajua hata madawa huwa ni lazima ya testiwe ili yaonekane kuwa yapo effective na yana reasonable impact ktk uponyaji wa ugonjwa uliokusudiwa kuponywa na kama yakionekana hayafai baada ya vipimo basi they have to be abandoned, tatizo langu ni kwamba nikisikia tu mtu analeta ushuhuda lakini siye yeye ndiye mlengwa huwa napoteza uhakiki na consistency ya habari. Sasa tunataka mtu aliyeponyeshwa azungumze mwenyewe na isiwe hizi bedtime stories za ati rafiki yangu alipona au mfanyakazi mwenzangu alipona na kwa sababu hii i am sorry to cunclude that bado sioni kama babu ni mponyaji due to unreliability and lack of evidences.
 
Kwamba, hali hiyo ilisababisha wagonjwa waliokuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi kupungua idadi yao, na halmashauri ikalazimika kutuma Mratibu wa Ukimwi wa wilaya upande wa afya kwenda kuonana na babu Mwasapile kumshauri asitishe dawa yake.
"Hiyo ilikuwa Juni 2010 lakini hata baada ya kurejea watu ndiyo walizidi kumiminika kwa mchungaji huyo, hivyo halmashauri ilibidi ikae na mkuu wa wilaya ili kuona namna ya kumzuia babu huyo, maana wengi walikuwa wakikatiza dozi," alieleza.
Alisema hata hivyo hawakuweza kwani ilibidi kurudi tena kwa Mchungaji Mwasapile Juni 26, 2010 na kumuomba awasaidie kuwaambia wagonjwa hao wasiache kutumia ARV's pindi wanapokunywa tiba hiyo ambayo mti wake kwa Kimasai unajulikana kama Lawa.
"Kama SIMAC tulikaa na mkuu wa wilaya na kumuelezea hofu yetu ya watu kukatiza tiba za ARVs tukimwomba hasimamishe huduma za mchungaji huyo lakini ilishindikana, kwani usafiri ukawa shida baada ya watu kugundua kuwa halmashauri ina mpango wa kuzuia," alisema.

Tanzania tuna kazi. Yani wanataka mtu asimamishe huduma yake ile watu waendelee na dawa!! Halafu hapo wanafanya bila kuwa na takwimu zozote zile zinazoonyesha negative effect. Huu ujinga tutauondoa lini? Hawa mananga wanaofanya hizi kazi huko wilayani watakuwa wamezuia maendeleo kwa kiasi gani?
 
Babu amefanya tusahau Dowans,katiba maandamano mpaka turudi mda utakuwa umesogea.
 
Inawezekana ni kweli na jinsi wengi wetu tulivyo wasahaulifu!!
 
Watanzania Bana.. eleweni hakuna DAWA YA HIV!! Dawa ni KUACHA NGONO ZEMBE!! BASI.!! ... hata chinese Herbs ambazo zipo advanced na kujulikana dunia nzima .. Bado ahzitibu ukimwi.. huyu babu ni msanii.
angesema magonjwa kama kisukari, b.p.. ningekubali lakini ukimwi BADO!

you have a point
 
it might b, siku zote imekua hivyo, panapokuwa na hoja nzito kuna upepo fulan wa kupumbaza hupita na kutusahaurisha yote! Yawezekana kweli.
 

With this data, its clear now ..an objective scientific follow up can be carried out!!

A group of HIV patients from a well know hospital should be taken to Babu ... and clear management be done ...according to Babu's instruction ..and medical DR .... get it clear and make a follow up ...and we want feedback!!!
 
Haya mambo ni mazito!, unajua hata madawa huwa ni lazima ya testiwe ili yaonekane kuwa yapo effective na yana reasonable impact ktk uponyaji wa ugonjwa uliokusudiwa kuponywa na kama yakionekana hayafai baada ya vipimo basi they have to be abandoned, tatizo langu ni kwamba nikisikia tu mtu analeta ushuhuda lakini siye yeye ndiye mlengwa huwa napoteza uhakiki na consistency ya habari. Sasa tunataka mtu aliyeponyeshwa azungumze mwenyewe na isiwe hizi bedtime stories za ati rafiki yangu alipona au mfanyakazi mwenzangu alipona na kwa sababu hii i am sorry to cunclude that bado sioni kama babu ni mponyaji due to unreliability and lack of evidences.

Yes -- bedtime stories! Na kama serikali kupitia Wizara yake ya afya inamsapoti Babu huyu na tiba yake, basi iwasaidie Watanzania, na hasa hao wagonjwa wenye maradhi sugu kama vile ukimwi -- kwa kuwapa imani kwamba tiba hiyo ni ya kweli. Wizara ifanye hivyo rasmi kwa kuratibu baadhi ya wagonjwa kwa kuwapima kwanza kama wana HIV na wakisha pata tiba ya huyo Babu wawapime tena ili kuona effect ya dawa. Hapo Watz wengi wataamini, kuliko hizi cock-and-bull stories zisizokuwa na uthibitisho wowote rasmi.


 
Yes -- bedtime stories! Na kama serikali kupitia Wizara yake ya afya inamsapoti Babu huyu na tiba yake, basi iwasaidie Watanzania, na hasa hao wagonjwa wenye maradhi sugu kama vile ukimwi -- kwa kuwapa imani kwamba tiba hiyo ni ya kweli. Wizara ifanye hivyo rasmi kwa kuratibu baadhi ya wagonjwa kwa kuwapima kwanza kama wana HIV na wakisha pata tiba ya huyo Babu wawapime tena ili kuona effect ya dawa. Hapo Watz wengi wataamini, kuliko hizi cock-and-bull stories zisizokuwa na uthibitisho wowote rasmi.




Kweli kabisa mkuu Zak: Bila ya kufanya hivyo itakuwa ni rumours tu kwamba tiba inaponyesha! Lakini nadhani serikali haiwezi kufanya hivyo kwa kujua fika kwamba itapata negative results -- maana wakipata positive results (yaani kikombe kimoja cha hiyo dawa inaponyesha magonjwa yote sugu sugu yaliyotajwa) basi medani za sayansi-tiba ulimwenguni itapata mtikisiko mkubwa kutoka Tanzania! Na serikali ya TZ ikubali consequences zake na isije ikaonekana inaendekeza sana masuala ya tiba za imani kuliko zile za kawaida!
 
si mnakumbuka ishu za popo bawa?, si mnakumbuka ishu za mtu kupotea salender bridge?. na sasa babu wa loliondo, hivi hizi ishu hazipikwi na usalama wa taifa kudivert mijadala nchini?
 
Mimi nadhani serikali ya CCM inatafuta namna ya kulifanya suala lote hili -- ambalo linaonekana kuwa popular -- kuwa mradi wake katika kujijenga upya baada ya pigo kubwa la kukubalika na wananchi lililotoka kwa PIPOOOOOZ!
 
Amini utapona na usipoamini huwezi kupona hata kipindi cha Yesu walikuwepo wasio na imani kwa hiyo wengi wataamini nakupona na wengi hawatapona kwa kutoamini kwao
 
Mimi nitawalaumu wanaotupa habari na taarifa mbalimbali. Siamini kuwa usalama wa Taifa ndiyo wanawapumbaza watu kwa style hizo alizotoa mtoa mada ila ni ushambenga biashara za magazeti na vyombo vya habari hapa nchini. Usitake kuniambia kuwa yaliyotokea japan ni mpango wa kijasusi kuwasahaulisha wamagharibi yanayoendelea huko arabuni.

Siku zote media zetu zinapenda kucheza na akili za wako kwa hali na mali wakijua ukimwambia mtu fulani anasaidia watu kupata fedha au mali watu wengi watajitokeza kumfuata, ukisema fulani ni mchawi, dowans na matatizo ya kifisadi nchini, sita kasema hivi, lowasa kasema hivi, rostam kasema vile, dr. slaa aamua hivi, serikali yanywea kwa babu loliondo; basi kila mtu atanunua gazeti au atafualilia vyombo vya habari ili kupata habari au ufafanuzi zaidi. Sasa media inakoelemea ndiyo huko watu wanapoelemea kama media iking'ang'ania mambo ya muhimu katika nchi kusingekua paradigm change in the media.

Kwa upande mwingine nikuunge mkono kuwa serikali haipaswi kusaidia au kupeleka misaada mingi kule ila tu kiasi kidogo kama miundo mbinu na kuangalia usafi wa mazingira kama ilivyodesuri ya kulinda watu afya zao na mali zao. Maana itasaidia waganya wangapi? Mbona hawamsaidii Joe David pale Tanganyika peckers, Kakobe, wanamaombi wengine pale Jangwani na kwingineko kunapokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu na wengine watakaokuya kwa kufuata nyayo za babu wa loliondo?

Ushauri wangu kwa serikali yetu. Waziri wa Afya atoe statement akiwaeleza wananchi kuwa watu wanywe dawa ya babu kwa imani zao na serikali haihusiki na wala haitahusika na matokeo yoyote ya dawa tajwa. Hii itasadia hata yakijatokea ya kina kibwetere serikali isilaumiwe kwa lolote na wala siasa isijeingizwa hapo.

Ushauri kwa wananchi. Kama hujanywa dawa ya babu tafadhali usidhubutu kunywa na washauri ndugu jamaa na marafiki wasinywe dawa hiyo. Lakini hapa nashauri kiimani maana dawa yenyewe ni ya kiimani. Nakumbushia mengi ambayo yalishatokea kwa style hiyo mfano Mbeya, Moshi vijijini na bio disc.
 
USHUHUDA zaidi umezidi kueleza kwamba tiba inayotolewa Loliondo na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (78), inaponya magonjwa mbalimbali sugu yakiwamo magonjwa ya ukimwi na kisukari.
Taarifa za kiushuhuda zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili kwa zaidi ya wiki moja sasa kutoka kwa maofisa wa serikali wilayani Ngorongoro na baadhi ya wagonjwa walioeleza kuinywa dawa ya mchungaji huyo maarufu kwa jina la Babu, zimesema tiba hiyo inatibu kwa imani na kwamba tayari wapo wagonjwa kadhaa wa ukimwi waliopimwa hospitalini baada ya kuitumia dawa hiyo na kuonekana hawana virusi vya ugonjwa huo tena.
Mmoja wa mashuhuda wa uponyaji wa tiba hiyo inayotolewa katika Kijiji cha Semunge wilayani humo, ni Mollel Lucas, ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya jamii.
Kwa mujibu wa Mollel, yeye na baadhi ya watendaji wenzake ndio waliokuwa wa kwanza kushuhudia uponyaji wa dawa hiyo baada ya mwanakikundi mmoja kilicho chini ya kamati ya halmashauri kuinywa dawa ya babu huyo na baadaye kupimwa hospitalini na kuonekana hana tena virusi vya ukimwi alivyokutwa navyo awali.
Akifafanua zaidi ushuhuda wake huo, alisema katika halmashauri yao kuna kamati inayoitwa SIMAC inayofanya kazi za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kamati hiyo pia ina kikundi cha kuwasaidia watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo kwa kuwapa misaada mbalimbali.
Alisema taarifa juu ya tiba hiyo iliwafikia kupitia mwanachama mmoja wa kikundi hicho aliyekuwa amefiwa na mumewe na ambaye baada ya kupima katika hospitali za wilaya na mkoa aligundulika kuwa ameambukizwa virusi hivyo.
Alisema dada huyo alikuwa pia akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs) lakini hali yake haikuwa nzuri, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo hatimaye alianza kujisikia vizuri na hatimaye kubaini kuwa amepona.
Bahati nzuri huyo dada anakaa karibu kabisa na mchungaji huyo kwa hiyo aliweza kupata tiba ya Mwasapile ni mmoja wa watu wa mwanzo kabisa kutibiwa, tunamjua vizuri.
Baada ya kutumia tiba hiyo hali yake ilibadilika na kurudi kama zamani ndipo aliporudi kwa mchungaji Mwasapile na kumuelezea kuhusu afya yake na Mwasapile alimtaka akapime kwa mara nyingine ili kuona kama ugonjwa huo umekwisha, alieleza.
Alisema aliporudi katika hospitali aliyofanyia kipimo mara ya kwanza madaktari walistaajabu kukuta hana virusi vya ukimwi lakini waliamini kuwa walikosea vipimo vyao na kumtaka akapime hospitali za juu zaidi.
Alipopima katika zahanati ya Digodigo ambapo kuna huduma hiyo aligundulika hana virusi hivyo, wakaamua kumwandikia ili kupata uhakika katika hospitali teule ya Waso, ambayo ilikuwa imemuanzishia dozi ya ARVs lakini nako walipompima hawakukuta virusi hivyo, alisema na kuongeza:
Taarifa za dada huyo ambaye ni mwanachama wa kikundi cha halmashauri zilizagaa kila kona hata baadhi ya wanachama wengine wakalazimika kwenda kunywa dawa hiyo.
Kwamba, hali hiyo ilisababisha wagonjwa waliokuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi kupungua idadi yao, na halmashauri ikalazimika kutuma Mratibu wa Ukimwi wa wilaya upande wa afya kwenda kuonana na babu Mwasapile kumshauri asitishe dawa yake.
Hiyo ilikuwa Juni 2010 lakini hata baada ya kurejea watu ndiyo walizidi kumiminika kwa mchungaji huyo, hivyo halmashauri ilibidi ikae na mkuu wa wilaya ili kuona namna ya kumzuia babu huyo, maana wengi walikuwa wakikatiza dozi, alieleza.
Alisema hata hivyo hawakuweza kwani ilibidi kurudi tena kwa Mchungaji Mwasapile Juni 26, 2010 na kumuomba awasaidie kuwaambia wagonjwa hao wasiache kutumia ARVs pindi wanapokunywa tiba hiyo ambayo mti wake kwa Kimasai unajulikana kama Lawa.
Kama SIMAC tulikaa na mkuu wa wilaya na kumuelezea hofu yetu ya watu kukatiza tiba za ARVs tukimwomba hasimamishe huduma za mchungaji huyo lakini ilishindikana, kwani usafiri ukawa shida baada ya watu kugundua kuwa halmashauri ina mpango wa kuzuia, alisema.
Alisema wakati huo kutoka makao makuu ya Wilaya ya Ngorongoro mpaka kufika kwa Mchungaji Mwasapile nauli ilikuwa sh elfu tano, lakini ilianza kuongezeka kadiri watu walivyokuwa wakitoa taarifa za sifa ya tiba hiyo.
Molleli alisema katika kipindi hicho tiba hiyo ilikuwa ikidaiwa kutibu kwa siku 21 lakini hadi kufikia Desemba mwaka 2010 ilidaiwa kuwa inaponya ndani ya kipindi cha siku saba pekee.
Mwingine aliyeelezwa kuwahi kuitumia tiba hiyo ambaye alikuwa alidhaniwa angefariki dunia muda wowote kutokana na maradhi ya ukimwi ni mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Babati aliyekuwa mahututi lakini baada ya kunywa dawa hiyo alipona na kuendelea na kazi.
Ni wengi sana waliokunywa dawa hiyo na kupona hasa wanachama wa kikundi chetu, lakini ilipofika Desemba dawa hiyo ilijulikana zaidi kwa kuponya magonjwa mengi, ikiwamo kisukari na presha (shinikizo la damu), alisema.
Aidha, kuna taarifa pia zinazomhusu mtaalamu mmoja wa masuala ya maji katika wilaya hiyo, kwamba aliponywa ugonjwa wa kisukari na hivi sasa afya yake imeimarika huku akiwa na uwezo wa kutumia vyakula mbalimbali ambavyo mwanzoni alikatazwa kabisa kuvitumia.
Ushuhuda mwingine ulioelezwa ni wa kijana mmoja ambaye alikuwa akipewa dawa za ARVs kwa takriban miaka 18 lakini mara baada ya kutumia tiba hiyo sasa anaonekana amepona kabisa magonjwa nyemelezi yaliyokuwa yakimsumbua. (majina ya wote waliotajwa kupona kwa sasa yanahifadhiwa).
Hata hivyo, wapo mashahidi wengine waliojitokeza na kuwa tayari kuripotiwa kwa majina yao kuhusu uponyaji uliofanywa na tiba hiyo na miongoni mwao wamo maaskofu wa KKKT.
Kanisa hilo la Kilutheri limesharipotiwa likitoa msimamo wake kwamba: Linaitambua na kubariki dawa inayotolewa na Mchungaji wake mstaafu anayefanyia shughuli zake Loliondo, Ambilikile Mwasapile, huku baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wakithibitisha kwamba wamekunywa dawa hiyo na kuponywa.
Kwa nyakati tofauti, maaskofu wa kanisa hilo, Thomas Laizer wa Dayosisi ya mkoani Arusha, Dk. Martin Shao wa Dayosisi ya Kaskazini, walisema huduma inayotolewa na Mchungaji Mwasapile ni sahihi na imeanza siku nyingi na kwamba wao ni miongoni mwa watu wa mwanzoni waliowahi kunywa dawa hiyo na kupona.
Askofu Laizer alisema kwa mujibu wa imani na taratibu za KKKT, mchungaji huyo yupo sahihi na kwamba hawana mgogoro naye.
Ifahamike kwamba kazi ya utoaji dawa haikuanza jana, ilianza siku nyingi na mimi kama askofu niliyembariki Mchungaji Mwasapile, nililetewa taarifa na wachungaji wengine pamoja na wakuu wangu wa majimbo juu ya mafunuo ya mchungaji na ndipo tulipoanza kufuatilia na kufanya mahojiano naye na kanisa likagundua kwamba tiba yake ipo sahihi, alisema Askofu Laizer.
Askofu Laizer alisema binafsi alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na shinikizo la damu kwa muda mrefu, lakini baada ya kupewa dawa ya mchungaji huyo amepona na hajapata kunywa dawa nyingine.
Dawa inayofanyika pale inaambatana na sala na imani, lakini watu wanashangaa.
Mke wa Askofu mwenzangu Akyoo alikuwa hawezi kutoka, alikuwa akisumbuliwa na kisukari, lakini baada ya kupewa dawa hiyo juzi nilipompigia simu akasema amepona na yupo kwenye harusi, alisema.
Hata hivyo gazeti hili halikufanikiwa mara moja kupata uthibitisho wa vyeti vya baadhi ya wagonjwa hasa wa ukimwi ambao wamedaiwa kupona, kwani wengi wameamua kuwa wasiri kutokana na unyeti wa ugonjwa huo.
Wakati huo huo watu watano wamefariki dunia na wengine kumi na nne kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso katika eneo la Kijiji cha Esilalei, Mto wa Mbu wilayani Monduli, yaliyodaiwa kuwa yalikuwa yakielekea Loliondo kwa babu huyo.
Magari hayo yalikuwa katika mwendo wa kasi kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa dereva alikuwa akijaribu kuwawahisha abiria wake kwenye tiba ya babu huyo.
Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 11:30 alfajiri ya jana katika eneo hilo madereva wa magari yote mawili yenye nambari za usajili T.606 ABU na T. 681 ABX na mtu na mkewe walifariki papo hapo.
Habari za ajali hiyo zilizothibitishwa na Ofisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, zilieleza kuwa ajali hiyo kwa mujibu wa taarifa za awali ilisababishwa na vumbi lililotanda eneo hilo hivyo kufanya madereva wote wawili kukosa mwelekeo na kugongana.
Ni kweli ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo na watu watano wamefariki dunia na wengine kumi na watatu wamejeruhiwa nadhani kwa taarifa za awali tunaweza kueleza kuwa zimesababishwa na mwendo wa kasi, kwani magari hayo mawili moja lilikuwa linatoka Loliondo na jingine linakwenda Loliondo kwa Babu si unajua shauku ya kupata tiba, alisema kamanda huyo.
Kamanda Mpwapwa aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Zakayo Laizer (36) ambaye alikuwa dereva katika gari namba T. 606 ABU na dereva mwingine ni Beatus Morris Kiboa (39), ambaye alikuwa dereva katika gari nambari T. 681 ABX. Wengine ni Raphael Kiboa (65) na mkewe aliyetajwa kwa jina la mama Kiboa (62) na Ismail Ngozi Mohamed (38).
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo na hali zao kuelezwa kuwa haziridhishi ni pamoja na Kordin Silangei (55), Elibariki Raphael (58), Asna Hassan (60), Namayani Legeri (40), Kirita Mediliyeki (65), Ngaisi Francis (38) na Sangau Magalla (90).
Majeruhi wengine ni Estomih Ole Muunyo (54), Erick Lukas aliyetajwa kuwa ni mwanafunzi, Evalyne Lukas (40), Mama Tivae (28), Anord Michael (11) na Elibariki Kiboa (49), ambao kwa mujibu wa Kamanda Mpwapwa majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Serikali wilayani Monduli.
Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha ajali hiyo na kuwaonya madereva kuacha kuendesha gari katika mwendo wa kasi. Tangu kuibuka kwa mchungaji huyo makundi kwa makundi ya watu wakiwamo vigogo wa serikali, viongozi wa dini na vyama vya siasa, wamekuwa wakimiminika kijijini Samunge usiku na mchana kwa ajili ya kwenda kuwahi tiba hiyo.
Marekebisho ktk majina kidogo kwa majeruhi: Korduni Silangei (55), Sangau Meigaro (93).
 
Kweli kabisa mkuu Zak: Bila ya kufanya hivyo itakuwa ni rumours tu kwamba tiba inaponyesha! Lakini nadhani serikali haiwezi kufanya hivyo kwa kujua fika kwamba itapata negative results -- maana wakipata positive results (yaani kikombe kimoja cha hiyo dawa inaponyesha magonjwa yote sugu sugu yaliyotajwa) basi medani za sayansi-tiba ulimwenguni itapata mtikisiko mkubwa kutoka Tanzania! Na serikali ya TZ ikubali consequences zake na isije ikaonekana inaendekeza sana masuala ya tiba za imani kuliko zile za kawaida!

Marks;

Huduma ya afya Tanzania inaendeshwa chini ya Sheria zilizopitishwa bungeni. Ziko za aina tatu.

1. Conversional medicine ...tiba ya hospitalini ..ili kuifanya unahitaji Uwe umesomea.."Academic qualifications"
2. Traditional medicine ... Tiba ya asili .... Haihitaji kusomewa ..ili kusajili ni watu wakuamini tu ..."No academic qualifications " just watu waamini tu na utmbulikane kijijini...hadi wilayani!
3. Alternative medicine..tiba mbadala ...lazima kusomea... MUST have academic qualificaton to practise..eg chines medicine , indin medicine ..nk!!

Babu anaingia hapo kwenye no 2. Hiyo ni kulingana na sheria ya bunge ya 2002.

Kama Tanzania ina mpango mzuri hivyo wa huduma ya afya ...huwezi kusema...TIBA ZA IMANI ZITAZIDI ZILE ZA HOSIPITALINI....

Sheria haitambui ni huduma gani itazidi nyingine...
Sheria yetu haitambui Wazungu wataionaje dawa ya jadi au mbadala kutoka Tz....

.... Tunasheria yetu ifutwe na kuheshimiwa duniani!!!!
 
Taarifa kama za gazeti hili zinasaidia kuwapotosha baadhi ya watu kuhusu matibabu ya "dawa" itokanayo na mmea uitwao "Mugarika". Maelezo ya kutibu yako based on ushuhuda wa watu ambao siyo watalaamu wa tiba au watafiti. Nchi kama hii ambayo tafiti ziinabainisha wengi ni wanaamini ushirikina, stori kama ilivyotolewa katika gazeti itakuwa "proof" kuwa "dawa" inatibu. Masharti ya kwamba utatibiwa kama ukiamini na kwamba mpaka dawa upewe na Babu mwenyewe Mwasapile yana harufu ya mambo ya ushirikina.

Tusibiri ripoti za kitaalamu, uchunguzi sasa unafanywa. Nikodekeze tu huenda Mugarika ipo based on mmea wenye jina la kisayansi Acokanthera schimperi ambao unajulikana kwa matumizi kadhaa mengine kama vile kuweke sumu za mishale. Ni dhahiri kwamba kama "dawa" itaweza kutibu itabidi kuwa na udhibiti mkubwa wa concentration na dosage inayotolewa kufuatana mgonjwa husika. Kitu ambacho itakuwa vigumu kufanyika kama mazingira yanavyoonekana kule kijijini.

Najua ni vigumu kuwashawishi watu wengi kufanya subira. Lakini wakumbuke taarifa kama hizi zimeshatolewa siku za nyuma. Madai ya tiba za maradhi kwa mfano ugonjwa wa ukimwi kama vile MM1 na KEMRON na nyinginezo
yalivuma sana lakini baadae hayakuzuwa kitu. Maswali magumu watu wasitarajie majibu mepesi na ya ajabu ajabu.
 
Hii isiwe ni dogma ... alternative medicine ziko dunia nzima..
..ziko chinese medicine...ziko indian medicine... ziko German medicine... NA ZOTE ZINAHAKISHIKA

Kama ni spiritual healing..Wako Spiritual leaders wangapi wanasafiri nchi nzima...

Inakuwaje yeye awe tofauti na wengine wote?

TUNASISITIZA ATOKE HUKO ALIPO AJE ARUSHA ...
NA TIBA YAKE IWE OFFICIAL TO MEET INTERNATIONAL STANDARDS...za tiba mbadala! What is the big issue on here?

usisahau kuwa huko aliko pia ni arusha labda useme ahamie mjini kama ingewezekana kitu ambacho nadhani itakuwa hadithi,,,,
 
Back
Top Bottom