Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Haya mambo ni mazito!, unajua hata madawa huwa ni lazima ya testiwe ili yaonekane kuwa yapo effective na yana reasonable impact ktk uponyaji wa ugonjwa uliokusudiwa kuponywa na kama yakionekana hayafai baada ya vipimo basi they have to be abandoned, tatizo langu ni kwamba nikisikia tu mtu analeta ushuhuda lakini siye yeye ndiye mlengwa huwa napoteza uhakiki na consistency ya habari. Sasa tunataka mtu aliyeponyeshwa azungumze mwenyewe na isiwe hizi bedtime stories za ati rafiki yangu alipona au mfanyakazi mwenzangu alipona na kwa sababu hii i am sorry to cunclude that bado sioni kama babu ni mponyaji due to unreliability and lack of evidences.
 

Tanzania tuna kazi. Yani wanataka mtu asimamishe huduma yake ile watu waendelee na dawa!! Halafu hapo wanafanya bila kuwa na takwimu zozote zile zinazoonyesha negative effect. Huu ujinga tutauondoa lini? Hawa mananga wanaofanya hizi kazi huko wilayani watakuwa wamezuia maendeleo kwa kiasi gani?
 
Babu amefanya tusahau Dowans,katiba maandamano mpaka turudi mda utakuwa umesogea.
 
Inawezekana ni kweli na jinsi wengi wetu tulivyo wasahaulifu!!
 

you have a point
 
it might b, siku zote imekua hivyo, panapokuwa na hoja nzito kuna upepo fulan wa kupumbaza hupita na kutusahaurisha yote! Yawezekana kweli.
 

With this data, its clear now ..an objective scientific follow up can be carried out!!

A group of HIV patients from a well know hospital should be taken to Babu ... and clear management be done ...according to Babu's instruction ..and medical DR .... get it clear and make a follow up ...and we want feedback!!!
 

Yes -- bedtime stories! Na kama serikali kupitia Wizara yake ya afya inamsapoti Babu huyu na tiba yake, basi iwasaidie Watanzania, na hasa hao wagonjwa wenye maradhi sugu kama vile ukimwi -- kwa kuwapa imani kwamba tiba hiyo ni ya kweli. Wizara ifanye hivyo rasmi kwa kuratibu baadhi ya wagonjwa kwa kuwapima kwanza kama wana HIV na wakisha pata tiba ya huyo Babu wawapime tena ili kuona effect ya dawa. Hapo Watz wengi wataamini, kuliko hizi cock-and-bull stories zisizokuwa na uthibitisho wowote rasmi.


 



Kweli kabisa mkuu Zak: Bila ya kufanya hivyo itakuwa ni rumours tu kwamba tiba inaponyesha! Lakini nadhani serikali haiwezi kufanya hivyo kwa kujua fika kwamba itapata negative results -- maana wakipata positive results (yaani kikombe kimoja cha hiyo dawa inaponyesha magonjwa yote sugu sugu yaliyotajwa) basi medani za sayansi-tiba ulimwenguni itapata mtikisiko mkubwa kutoka Tanzania! Na serikali ya TZ ikubali consequences zake na isije ikaonekana inaendekeza sana masuala ya tiba za imani kuliko zile za kawaida!
 
si mnakumbuka ishu za popo bawa?, si mnakumbuka ishu za mtu kupotea salender bridge?. na sasa babu wa loliondo, hivi hizi ishu hazipikwi na usalama wa taifa kudivert mijadala nchini?
 
Mimi nadhani serikali ya CCM inatafuta namna ya kulifanya suala lote hili -- ambalo linaonekana kuwa popular -- kuwa mradi wake katika kujijenga upya baada ya pigo kubwa la kukubalika na wananchi lililotoka kwa PIPOOOOOZ!
 
Amini utapona na usipoamini huwezi kupona hata kipindi cha Yesu walikuwepo wasio na imani kwa hiyo wengi wataamini nakupona na wengi hawatapona kwa kutoamini kwao
 
Mimi nitawalaumu wanaotupa habari na taarifa mbalimbali. Siamini kuwa usalama wa Taifa ndiyo wanawapumbaza watu kwa style hizo alizotoa mtoa mada ila ni ushambenga biashara za magazeti na vyombo vya habari hapa nchini. Usitake kuniambia kuwa yaliyotokea japan ni mpango wa kijasusi kuwasahaulisha wamagharibi yanayoendelea huko arabuni.

Siku zote media zetu zinapenda kucheza na akili za wako kwa hali na mali wakijua ukimwambia mtu fulani anasaidia watu kupata fedha au mali watu wengi watajitokeza kumfuata, ukisema fulani ni mchawi, dowans na matatizo ya kifisadi nchini, sita kasema hivi, lowasa kasema hivi, rostam kasema vile, dr. slaa aamua hivi, serikali yanywea kwa babu loliondo; basi kila mtu atanunua gazeti au atafualilia vyombo vya habari ili kupata habari au ufafanuzi zaidi. Sasa media inakoelemea ndiyo huko watu wanapoelemea kama media iking'ang'ania mambo ya muhimu katika nchi kusingekua paradigm change in the media.

Kwa upande mwingine nikuunge mkono kuwa serikali haipaswi kusaidia au kupeleka misaada mingi kule ila tu kiasi kidogo kama miundo mbinu na kuangalia usafi wa mazingira kama ilivyodesuri ya kulinda watu afya zao na mali zao. Maana itasaidia waganya wangapi? Mbona hawamsaidii Joe David pale Tanganyika peckers, Kakobe, wanamaombi wengine pale Jangwani na kwingineko kunapokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu na wengine watakaokuya kwa kufuata nyayo za babu wa loliondo?

Ushauri wangu kwa serikali yetu. Waziri wa Afya atoe statement akiwaeleza wananchi kuwa watu wanywe dawa ya babu kwa imani zao na serikali haihusiki na wala haitahusika na matokeo yoyote ya dawa tajwa. Hii itasadia hata yakijatokea ya kina kibwetere serikali isilaumiwe kwa lolote na wala siasa isijeingizwa hapo.

Ushauri kwa wananchi. Kama hujanywa dawa ya babu tafadhali usidhubutu kunywa na washauri ndugu jamaa na marafiki wasinywe dawa hiyo. Lakini hapa nashauri kiimani maana dawa yenyewe ni ya kiimani. Nakumbushia mengi ambayo yalishatokea kwa style hiyo mfano Mbeya, Moshi vijijini na bio disc.
 
Marekebisho ktk majina kidogo kwa majeruhi: Korduni Silangei (55), Sangau Meigaro (93).
 

Marks;

Huduma ya afya Tanzania inaendeshwa chini ya Sheria zilizopitishwa bungeni. Ziko za aina tatu.

1. Conversional medicine ...tiba ya hospitalini ..ili kuifanya unahitaji Uwe umesomea.."Academic qualifications"
2. Traditional medicine ... Tiba ya asili .... Haihitaji kusomewa ..ili kusajili ni watu wakuamini tu ..."No academic qualifications " just watu waamini tu na utmbulikane kijijini...hadi wilayani!
3. Alternative medicine..tiba mbadala ...lazima kusomea... MUST have academic qualificaton to practise..eg chines medicine , indin medicine ..nk!!

Babu anaingia hapo kwenye no 2. Hiyo ni kulingana na sheria ya bunge ya 2002.

Kama Tanzania ina mpango mzuri hivyo wa huduma ya afya ...huwezi kusema...TIBA ZA IMANI ZITAZIDI ZILE ZA HOSIPITALINI....

Sheria haitambui ni huduma gani itazidi nyingine...
Sheria yetu haitambui Wazungu wataionaje dawa ya jadi au mbadala kutoka Tz....

.... Tunasheria yetu ifutwe na kuheshimiwa duniani!!!!
 
Taarifa kama za gazeti hili zinasaidia kuwapotosha baadhi ya watu kuhusu matibabu ya "dawa" itokanayo na mmea uitwao "Mugarika". Maelezo ya kutibu yako based on ushuhuda wa watu ambao siyo watalaamu wa tiba au watafiti. Nchi kama hii ambayo tafiti ziinabainisha wengi ni wanaamini ushirikina, stori kama ilivyotolewa katika gazeti itakuwa "proof" kuwa "dawa" inatibu. Masharti ya kwamba utatibiwa kama ukiamini na kwamba mpaka dawa upewe na Babu mwenyewe Mwasapile yana harufu ya mambo ya ushirikina.

Tusibiri ripoti za kitaalamu, uchunguzi sasa unafanywa. Nikodekeze tu huenda Mugarika ipo based on mmea wenye jina la kisayansi Acokanthera schimperi ambao unajulikana kwa matumizi kadhaa mengine kama vile kuweke sumu za mishale. Ni dhahiri kwamba kama "dawa" itaweza kutibu itabidi kuwa na udhibiti mkubwa wa concentration na dosage inayotolewa kufuatana mgonjwa husika. Kitu ambacho itakuwa vigumu kufanyika kama mazingira yanavyoonekana kule kijijini.

Najua ni vigumu kuwashawishi watu wengi kufanya subira. Lakini wakumbuke taarifa kama hizi zimeshatolewa siku za nyuma. Madai ya tiba za maradhi kwa mfano ugonjwa wa ukimwi kama vile MM1 na KEMRON na nyinginezo
yalivuma sana lakini baadae hayakuzuwa kitu. Maswali magumu watu wasitarajie majibu mepesi na ya ajabu ajabu.
 

usisahau kuwa huko aliko pia ni arusha labda useme ahamie mjini kama ingewezekana kitu ambacho nadhani itakuwa hadithi,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…