Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Binafsi ningependa kusema yafuatayo kuhusiana na dawa ya babu:-

1. Suala la kwenda au kutokwenda kwa babu ni suala la mtu binafsi, matatizo ya afya mtu aliyonayo ndiyo yanayompa mtu sababu ya kufanya hivyo. Tumesikia "wenye afya hawamuhitaji daktari bali walio wagonjwa. Majid ni afya tele.
2. Tusikwazwe na nani anatoa tiba. Imani ya aliyeamua kwenda ndiyo muhimu kwake. Kila mwaka tunasikia watu wanasafiri kwenda nje yya nchi zao na kati ya mambo muhimu yanayofanywa huko ni kurusha mawe kumpiga shetani. Nasisitiza ni imani na sio Abrakadabra kama ilivyoitwa na Majid. Kuna maeneo mengine ambapo hiyo sayansi mnayoijua sana haifit.
3. Tuwe wavumilivu. Kama ni uzushi, utapeli ulaghai au abrakadabra ni mara ngapi yametokea na hatujayashikia bango kama hili la babu? Kulisemea hili sana ni kutaka kujilaumu baadae yatakapokuwa ndiyo au siyo. Tuache hili pia lipite kwa amani mwenye kupata apate na mwenye kukosa naye pia. Ni mambo ya wakati tu kila kitu kitakuwa sawa.

Hivi katika masharti ya kujiunga na JF hamna age limit? Manake wengine humu might be underage

Babu anatakiwa awekewe ulinzi pamoja na DR. Maalum kuangalia afya yake asiwe over worked sababu wengi tunahitaji huduma yake foleni ikipungua.

Nimegundua nusu ya watu hapa duniani ni wagonjwa.

hahahahhaha fanyeni mazoezi acheni ujinga wa kuleta heshima za muda mfupi:lol:

Kuna habari zimeshaanza kuenea kuhusiana na dawa anayotoa Babu kule Loliondo kuhusiana na uponyaji wake kama tunavyoambiwa na Babu kua kikombe kile kimoja cha dawa kinatibu magonjwa sugu kama vile Kansa/Kisukari/Pumu/Presha/Ukimwi na pamoja na vidonda vya tumbo. Sasa kuna habari zisizo rasmi kuhusiana na dawa hiyo kwa wale wenye ugonjwa sugu wa Kisukari si mnajua ugonjwa huu unazoofisha nguvu za kiume na kushindwa kuwajibika kwa wanaume kushiriki tendo lile, sasa hivi ni kua eti kwa wale wagonjwa wa kisukari waliopata dawa tayari kwa babu wamedai wameshapima kisukari na pia kujaribu kula vyakula ambavyo walikua hawaruhusiwi kula kutokana na masharti ya ugonjwa huo hususani na kushuhulika vizuri ipasavyo kwa wake zao kutokana na dawa hiyo kutibu vizuri! jamani natumaini hizi ni taarifa nzuri kama kweli ni rasmi kuhusiana na dawa kutoka kwa babu. Nawasilisha.

Mkuu Ndallo, kama sikosei ulienda kwa babu na hukufanikiwa kumwona na ulituahidi utaenda tena, au ndo hizo habari njema ulizotuletea?

Utaratbu wa sasa hivi kwenda kule ni mzuri sana mkubwa! unaondoka leo kesho kutwa alfajiri umerejea nimeshakwenda na nimesharudi lakini hizi habari ni kweli nimezisikia kwa wale waliokua wanaugua ugonjwa huo.

Maggid subiri uugue ndiyo utatambua maana ya TIBA ni nini? sasa hivi una uwezo wa hata kuona unachoandika ndiyo maana unatamba. wewe sayansi ya nini wakati unatibiwa unapona? enzi za bababu kulikuwa na sayansi?

Acheni siasa zenu, mwacheni Babu afanye kazi yake, kama ametumwa na Mungu ni safi, kama hajatumwa kama wengine mnavyodai ni sawa tu ila cha msingi dawa inaponyesha basi.

MAJIDD:
Nani anayefanya kazi kisayansi kati ya hawa wafuatao:
1. Hospital ya Taifa ya Rufaa, Naumwa Goti lakini nikafanyiwa Operation ya Kichwa na kusababisha niwe Chizi
2. Naenda Loliondo kwa Babu kunywa kikombe kimoja tu kwa sekunde na kupona kisukari au ukimwi, au kansa n.k.?

Hospital zinazofanya kazi kisayansi zimeshindwa sasa ni wakati wa kutumia sayansi ya Bw. God

Utaratbu wa sasa hivi kwenda kule ni mzuri sana mkubwa! unaondoka leo kesho kutwa alfajiri umerejea nimeshakwenda na nimesharudi lakini hizi habari ni kweli nimezisikia kwa wale waliokua wanaugua ugonjwa huo.

nashukuru mkuu ijapokuwa umenijibu ki-tekniko!

MAJIDD:

Nani anayefanya kazi kisayansi kati ya hawa wafuatao:

1. Hospital ya Taifa ya Rufaa, Naumwa Goti lakini nikafanyiwa Operation ya Kichwa na kusababisha niwe Chizi

2. Naenda Loliondo kwa Babu kunywa kikombe kimoja tu kwa sekunde na kupona kisukari au ukimwi, au kansa n.k.?

Hospital zinazofanya kazi kisayansi zimeshindwa sasa ni wakati wa kutumia sayansi ya Bw. God

Ndugu Zangu,

ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa ’ wameoteshwa’ na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.

Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na ’ watalaamu’ wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia ’ Babu’ hadharani. Anatishia kumchukulia ’ wagonjwa’ wake! Askofu nae ni ’ mgonjwa’- maradhi yake ni pesa, hatosheki.

Na si tumemsikia ’ Babu’ wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; “Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni “Nabii” ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu.”

“Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002”

‘Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu” ( RAIA MWEMA NA: 176)

Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya ’ Babu’ wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.

Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.

Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,

Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.

Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.

Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)

Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.

Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.

Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.

Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.

Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.

Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.

Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!

Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!

Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia ’ Babu’ wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa ’ Babu’ Loliondo yalianzaje? Na je, kama ’ Babu’ wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?

Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ’ Kikombe Cha Babu’, kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.

Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa ’ Babu’ Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.

Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.

Maggid

Dar es Salaam.

Jumatatu, Machi 14, 2011

http://mjengwa.blogspot.com

hizi ni habari njema mana wengi walikuwa wanatafuniwa sana kama dawa inarudisha heshima bomani safi

Mimi kuna mtu nilikuwa namfahamu kila usiku lazima wagombane na mkewe lakini toka amerudi arusha naona wanajivinjari kwa tabasamu na bashasha kila kona ya daresalama na ikifika saa moja mlango umeshafungwa na taa zimezimwa....

Haya tena Wadau, naona kumekucha kuhusu Babu. Msomeni huyu Jenerali Ulimwengu kuhusu huyo Babu – anaonekana ana wasiwasi naye sana – lakini atoa sababu zake!

Yes we have faith... but placing it wholesale on a bush healer’s beyond being gullible

By JENERALI ULIMWENGU

The herd mentality is once again on display in Tanzania, raising questions as to the sanity of a society that is so easily swayed by hearsay.

This time round, the hullabaloo is about a “retired priest” in the wilderness of Loliondo, Arusha region, claiming to have had a revelation from God, commanding him to heal hitherto intractable diseases such as diabetes and HIV/Aids.

There are reports of endless queues of thousands of people from near and far, including from outside Tanzania, to get this mystical cure that has confounded knowledgeable commentators.

The mysticism surrounding the healer has added to the intrigue.

He apparently insists that one cannot really be healed if one is not sufficiently infused with faith, so that to be cured you must not only take his potion, you must also have faith in God or something.

Also, for the medicine to work, it has to be administered physically by the prophet himself, using the same cup from which every patient drinks.

In other words, no “Do It Yourself” drinking here.

Though this is a rather recent development, the “medicine” man has taken Arusha by storm, and stories abound of people who claim to have been cured by this latter-day prophet who has apparently discovered a potent mix of herbs and faith to produce a wonder drug that has thus far eluded modern medicine.

Is it true that this man can, and does indeed, cure hitherto incurable maladies, or is it that another charlatan has managed to exploit the proven gullibility of the Tanzanian public to make a quick buck?

Gullibility — if that is what it is — is in generous supply here, given declining educational standards, the absence of critical thinking to interrogate phenomena and a generalised desire to cut corners by riding on quick fixes, even if the last time a similar fad came to town it left many people sorrier and poorer.

We have had pyramid schemes which fleeced many of their savings.

We even have had such schemes which were buttressed by some theological mumbo-jumbo about it being a divinely sanctioned economic communion, but every time this kind of thing has happened lessons were there for anyone who wanted to learn. But it would seem as if learning is one activity we avoid at all costs.

Would we be justified to consider the Loliondo story a hoax by a sly conman or a group of them?

Such a thought need not necessarily suffer from the evidence of many senior people in government and ruling circles flocking to Loliondo, for superstition is intimately woven into our governance processes.

Questions have been asked but answers have not been forthcoming.

Why is it that we do not have solid testimonies of people who had proven clinical records and whose fortunes have been reversed by this miracle man?

Why does this bush scientist refuse his drug to undergo lab testing?

More curious was a plea from his assistant to the government for urgent steps to be taken to improve sanitation in the area to avert a disease outbreak caused by the uncontrolled human press. How could anyone with the powers to cure diabetes and HIV/Aids be worried about dysentery?

Still, one’s suspicions of fraud would be tempered by the paltriness of the fee this healer is charging, only Tsh500 (30 US cents).

Surely, that’s not what a man out to make a killing would charge. Only, I was thinking, if he receives a million visitors, the aggregate sum be a tidy sum.

Another thing: What if the real heist is not in the bush but in Arusha, with all the tour operators, the transporters, the caterers, the hotel and guest house owners and… the sex workers, a whole tourism industry built around an enigmatic former priest in the bush, dispensing herbal drinks while waiting for his cut from his Arusha-based principals and co-conspirators?

*Jenerali Ulimwengu, chairman of the board of Raia Mwema newspaper, is a political commentator and civil society activist based in Dar es Salaam. E-mail: jenerali@gmail.com
Source: The East African

Ubarikiwe kwa mtazamo huo. Hakuna upuuzi mkubwa na wa kihistoria tuliofanya watanzania kama kumrejesha kwenye madaraka makubwa ya nchi yetu mtu anayesema hajui kwa nini watu wake ni maskini na wakati huo huo anawaahidi maisha bora kwa kila mtu!!!!!

heshima mbele mkuu!hatukumrudisha ila alijirudisha kwa nguvu!

Jenerali shukuru kwa kupata habari iliyokuwezesha kuuza gazeti.

Kama dawa inaponyesha au haiponyeshi hilo wewe halikuhusu.

Wangapi waliokuwa mahospitalini miaka nenda rudi na hawajapona? kuna ubaya gani wakienda Loliondo?

Angegundua mzungu Jeneráli asingeongea haya ila kwa vile ni Babu Mwasapile basi imekuwa nongwa.

Back
Top Bottom