Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.



Ndugu Zangu,


ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa ' wameoteshwa' na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.

Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na ' watalaamu' wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia ' Babu' hadharani. Anatishia kumchukulia ' wagonjwa' wake! Askofu nae ni ' mgonjwa'- maradhi yake ni pesa, hatosheki.

Na si tumemsikia ' Babu' wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; "Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni "Nabii" ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu."
"Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002"

‘Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu" ( RAIA MWEMA NA: 176)

Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya ' Babu' wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.

Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.


Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,


Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.



Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.


Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)


Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.



Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.



Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.


Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.



Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.


Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.


Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!


Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!

Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia ' Babu' wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa ' Babu' Loliondo yalianzaje? Na je, kama ' Babu' wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?


Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ' Kikombe Cha Babu', kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.


Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa ' Babu' Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.


Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.
Maggid
Dar es Salaam.
Jumatatu, Machi 14, 2011
http://mjengwa.blogspot.com

Holy Crap....Mjengwa...Usinge waka uko ungeishia kwenye uso wa kitabu na blog yako sasa umepost uku dah ona sasa watu umewavuruga akili wanatukana....Hii Watu wanao umwa magonjwa ambayo wanasanyasi wamekuwa wakizungua kila siku kuwa hayana tiba mwisho wao ni kufa tu....Unafikiri akiambiwa kuna tiba afanyaje?
 
Ubarikiwe kwa mtazamo huo. Hakuna upuuzi mkubwa na wa kihistoria tuliofanya watanzania kama kumrejesha kwenye madaraka makubwa ya nchi yetu mtu anayesema hajui kwa nini watu wake ni maskini na wakati huo huo anawaahidi maisha bora kwa kila mtu!!!!!

Alirejeshwa au alijirejesha na sisi kumfagilia kwa kujaza uwanja siku aliojiapisha fasta fasta kabla zengwe halijaanza?
Tunajimaliza wenyewe kwa uzumbukuku wetu na ndio mtaji wa CCM.
 
hapa udom chuo kimefunguliwa wanafunzi hawaonekani wahadhiri siwaoni sijui wameenda loliondo kwa babu
 
Kosa kubwa alilolifanya Maggid ni kujenga hoja yake kwa kutaka kuthibitisha suala la kiimani kwa kutumia sayansi...kosa kubwa...masuala haya hayachangamani hata siku moja. Na maggid utakuwa umefanya kosa hili aidha kwa makusudi ili kufanikisha malengo fulani au kwa kutokujua. Sipendi kuamini kuwa umefanya kosa hili kwa kutokujua au kwa kukosa uelewa , na hivyo kunifanya niamini kuwa una lengo lako maalum kuandika haya ambalo si lingine bali ni upotoshaji wa makusudi.
 
Usiandike tu ili KUSOMWA bali andika with facts,je umewauliza wale wanaotumia tiba za huyu babu wakupe shuhuda zao??
Unaandika kiimani zaidi kua 'its impossible" but one thing,fanya utafiti kisha andika.
Wasalimie Iringa
 
Desperation always calls on desperate measures too. That's fact, or do we need a scientific explanation?

Wanaoenda kwa Babu sio watu wenye mafua, au kikohozi au malaria. Ni watu walio kwenye different levels of desperation, they are suffering from the 'incurables'. Sidhani kama kuna yeyote ambaye anataka kuishi katika maumivu maisha yake yote, hata kama sayansi imemwambia kuwa anachosumbuliwa nacho hakiponi. Desperation!

Mimi sidhani kuwa 'maji' anayotoa Babu ndiyo yanayoponya, desperate people develop staunch beliefs too, on MIRACLE on the impossibilities becoming possible. They are sick, so sick, so sick and yet no cure for them. But they have not given up, they think (or being made to think) that someone somewhere (or something) has the cure. The cure is on the FAITH, HOPE that these people are having. they are ready to go heights and lenghts, and whatever that comes in between

So, maybe Babu is cunning, just like other evangelists and 'miracle' doctors. Maybe this Babu is using this FAITH that people have on the 'possibilizing' impossibilities. And he's using it, just like Kakobe and company are doing.

We all live because there is HOPE (remember whenever you are using the Future tense, means you BELIEVE) the hope that some things may change. And Babu is giving just THAT!
 
Watashuhudia lakini bado hawatasadiki!Huu uponyaji ni wa kiimani zaidi,it cant be proved scientifically!Maono ya kibinadamu hayawezi kufikia maono ya muumba wao.Sumu kwa maono ya binadamu,mungu kasema iwe dawa na imekuwa!Kwa wasioamini ni kweli ile ni abrakadra kwao lakini wanaoamini ile ni tiba na wengi wamepona!Sio kazi ya kila aliyepona kumtafuta mtu kama Magid na kumshuhudia.Unaweza ukalaumu watanzania wanafata sana mkumbo,lakini vipi kuhusu watu wa mataifa mbalimbali wanavyomiminika kupata tiba Loliondo?Unaweza ukaita unabii wa uongo,lakini manabii wa uongo hutumia jina la mungu kupata mali(rejea yule wa mwenge).Huyu babu wala hanufaiki na hii tiba.Anauza 500,kati ya hizo sh.200 inaenda kanisani, sh.200 inaenda kwenye mfuko wa maendeleo ya kijiji na yeye mwenyewe anabaki na sh.100!Kweli huyu nae mwizi?Msioamini bakini na msimamo wenu.Msiwashawishi wengine hata kwa kutumia peni zenu.Acheni wanaoamini wapone!

Pumba Tupu shwain we!! Watanzania tumezoea sana siasa..na ndo inayotufanya maskini wakutupwa...sasa wewe unaambiwa watu wanapona,ndugu jamna na marafiki tunaowajua wameepuka kifo...sasa unataka eti zoezi lisimame kuingiza siasa za uchunguzi wa madahara nk nk...upumbavu mtupu,kitaalam uwezekana wa dawa za herbs kuwa na madhara is almost 0%!....we hayajakufika mwehu
 
sisi ni wepesi kuamini kwa kusema eti uthibitisho wa kisayansi..........lakini hatujiulizi hii sayansi tuliyo nayo na unayoiamini ni nini imesaidia dunia acha watu wakajaribu kwani hata hii ndio sayansi yetu ambayo tulikataa kuiendeleza kwa kuamini kila kitu kutoka magharibi sasa sitoshangaa vipimo vyao vikishindwa kupima ubora na uwezo wa dawa ya babu kwani kwakuwa sayansi yao ni ndogo na hawajaweza kufika huku alipofika babu.
 
Ubarikiwe kwa mtazamo huo. Hakuna upuuzi mkubwa na wa kihistoria tuliofanya watanzania kama kumrejesha kwenye madaraka makubwa ya nchi yetu mtu anayesema hajui kwa nini watu wake ni maskini na wakati huo huo anawaahidi maisha bora kwa kila mtu!!!!!

Mkulu na mama walikunywa dawa kimya kimya. Majjid ni mahili wa kuandika kwa mtazamo wake bila kuwainisha upande mwingine kwa ushahidi. Si mpuuzi bali ni mhafidhina wa mawazo mgando angeweza kwenda kuhoji Babu kwa swali moja Wakubwa wangapi wamekunywa kikombe? Hao ndio angewatatufa wamthibitishie.
 
Kwani ndugu magidd,
haya uanyo andika pia si ni abrakadabra?? hata hivyo si imeshatangazwa waislamu wasiende?? na redio khier cjui radio yao wenyewe? nasisi tumekubali wasiende tuachiwe hili abrakadabra letu!! full stop
 
Kuna habari zimeshaanza kuenea kuhusiana na dawa anayotoa Babu kule Loliondo kuhusiana na uponyaji wake kama tunavyoambiwa na Babu kua kikombe kile kimoja cha dawa kinatibu magonjwa sugu kama vile Kansa/Kisukari/Pumu/Presha/Ukimwi na pamoja na vidonda vya tumbo. Sasa kuna habari zisizo rasmi kuhusiana na dawa hiyo kwa wale wenye ugonjwa sugu wa Kisukari si mnajua ugonjwa huu unazoofisha nguvu za kiume na kushindwa kuwajibika kwa wanaume kushiriki tendo lile, sasa hivi ni kua eti kwa wale wagonjwa wa kisukari waliopata dawa tayari kwa babu wamedai wameshapima kisukari na pia kujaribu kula vyakula ambavyo walikua hawaruhusiwi kula kutokana na masharti ya ugonjwa huo hususani na kushuhulika vizuri ipasavyo kwa wake zao kutokana na dawa hiyo kutibu vizuri! jamani natumaini hizi ni taarifa nzuri kama kweli ni rasmi kuhusiana na dawa kutoka kwa babu. Nawasilisha.
 
Eisee! nimeambiwa na mshikaji wangu kuwa heshima imerudi make sasa hivi mama ameanza kupata haki yake kama kawa.
 
Huduma za Afya hapa Tz ni mbovu sana, zilizo bora watu wa kima cha chini hawawezi kuzimudu.Vifo vingapi vinatokea kwa uzembe, watu wangapi wanakufa kwa magonjwa ya kutibika.Maggid inaonekana hujawahi kuwa na mgonjwa ndio maana unakuja na maelezo yasiyo na msingi

Nafikiri ungeishauri serikali iboreshe huduma ya afya,tupunguze vifo, maisha ya mtanzania yawe salama.Ww utaona huko sijui kwa manabii,wachungaji,maaskofu,wazee wa upako utaona watu wenye magonjwa watapungua kwenda kuombewa.
Mambo ya imani hayapimwi kwenye test tube,yaangaliliwi kwenye x-ray,hapimwi kwenye microscope.
Mbona hao wa kina kakobe,lwakatare wanatumia vitambaa kutibu na hawahojiwi kiasi hiki?
Go ahead babu wewe tibu, ambao hawaamini waache ndugu zao au wenyewe wafe.
 
Safari hii umefanikiwa kumwona babu nini?
Maana umeangaika sana mkuu
Heshma muhimu sana nyumbani naona na mama leo kauso kamechangamka!
 
Heshima, mamlaka, uweza, usultani na enzi viina Bwana Mungu wetu milele amina. Babu ni chombo tuu tena cha udongo kilichopata neema ya Mungu kufanya hayo aliyoyafanya hivyo utukufu unamrudia Yehova Mungu, muumba mbingu na nchi ambae sasa tunamwabudu kwa jina alilotupa la "Bwana Yesu Kristo".
.
 
Lakini mkumbuke wosia wa babu,amesema kama utaendele kutenda dhambi basi ugonjwa ukirudi uponi tena sio kwa ukimwi tu bali ata hayo magonjwa mengine,kwahiyo kupona huko isiwe ndio chanzo kuwa na tabia za kifataki.....ooh ukiuliza eti HESHIMA imerudi,Jogoo anauwezo wa kupanda mtungi muda wote.....chonde chonde wajameni.....!
 
Mwenye afya haitaji daktari,Majjid ungekuwa unaumwa kama wale watu wanaoenda kwa Babu nadhani usingekuja hapa na hii mada yako
 
Back
Top Bottom