Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Tutakuja kumukumbuka Ulimwengu kwa aliyoandika muda si mrefu hapahapa JF,lo siamini watu wenye bongo hapa JF kushadidia tiba ya bau ya utapeli ,hakika sasa nimeamini hapa TZ mjanja unaweza kutengeza hela ya buure,jamani angalieni pia katuni ya kipanya aliyeweka tangazo la dawa ya kupata pesa bila kufanya kazi huenda mkajifunza,hata DECI watu walionywa lakini wapi
 
babu mkalii, babu kaoteshwa kuja kuokoa wabongo jaman, kama heshima imerud ndan ya nyumba hiyo ndo aman inayotakiwa waungwana
 
Watatoa kila ushuhuda mwaka huu...!

This is DECi Plus... Oops! I mean Death Trap!
 
Maggid uko sahihi kabisa
Cha msingi na ninajiuliza huo uchunguzi utachukua siku ngapi? no one know hata ukiliza hawana majibu. Hili ndo tatizo la utendaji wetu.

kigumu nini sasa

  • watu walitumia dawa wapo
  • maabara tunazo
  • watu amboa ni wapya kwa ajili ya sample wapo wtayari kujitolea kutumia dawa hata kama watadhurika wapo
katika hali hii uchunguzi wa awali unatakiwa usichukue si zaidi ya wiki tatu.

Tunasoma kwenye wiki lieak kampuni ya madwa fulani USA ilipeka dawa zake Nigeria kumbe ilikuwa kwenye kuchungza madhara yake. Winigeria wanakujua ile dwa kama wanatumia katika uchunguzi....

Lakini katika hili la babu hata srikali ikisema wajitokeze watu wa kujitolea kuchungzwa bila kulipwa kama yatapatikana madhara hawatakosekana.

Nistahngaa kutosikia report eyote ya kutoa majibu ya awali ndani ya mwezi 1ja..

Gharama za kufanya uhunguzi na mazigira ya uchungzui yote yapo wazi.

So wafanye haraka watoe jibu.
 
inawezekana ni kweli ni abrakadabra lakini hapo inategemeana na uwezo wa kufikiri wa mtu kama wewe
mimi na mwingine, kubwa ni kwamba hiyo abrakadabra kuu ni kuwa na mtu kama kikwete, kuwa
kiongozi wa tanganyika, na abrakadabra nyingine ni maisha ya kila mwanahabari abrakadabra kama
wanahabari wengi wa tanganyika, ambao kwa sababu ya u-abrakadabra wao wanaweza kubeza ama kusifia
kila jambo kuwa ni zuri hasa kwa kuwa matumbo yao wengi yana abrakadabra.

je tunadhani tutegemee nini kwa mtu aliyepanda mnazi harafu ana mategemeo ya kuangua zabibu?
ama je nini basi tukitegemee kwa mtu mwenye mtazamo abrakadabra asione hiyo ya mzee wa Lolliondo
siyo abrakadabra? Mimi nadhani kikubwa ni kutulia na kuanza kuutafuta undani zaidi
kwako maggid...!!!
 
Heshima kurudi maana yake nini?

Kama hujaowa ukiwowa utayaona....au kwa kifupi vuta picha umekaa na mkeo usiku unavuta hisia zote gari haliwaki....kwa mwanamume that is a worst scenerio..inayosababisha msongo wa mawazo.....

Ni heshima kwa saababu mwanamke anapokosa haki yake kwa asili yake huanza dharau ndani ya nyumba ...angalau kitakachobakisha heshima kama mmezaa ni ule ukweli kuwa wewe ni baba watoto..zaidi ya hapo ni kama kaka na dada!!
 
Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa Ulimwengu, nachelea kusema haya ni maswali mepesi kuulizwa naye.Majibu ni kama ifuatavyo

1.Amekataa isiwe tested katika lab sababu hiyo siyo scientific medicine...nadhani unajua huwezi kuprove that God ana-exist in the lab
2.Hata kama dawa yake inatibu Ukimwi au Diabates ambayo ni magonjwa makubwa, siyo sahihi kusema basi watu wasichukue tahadhari ya kupata magonjwa mengine kama kipindupindu.....ni sawa sawa kama wewe uwe na dawa ya Malaria ndani basi ulale tu bila chandarua au bila kuchukua tahadhari yeyote ya kuumwa Malaria sababu dawa ipo

In general, kwa sababu ulizotumia nashindwa kuungana nawe katika doubts zako...
...........as far as this has touched my faith! how about that conclussion?
 
Jenerali ni sawa na Tomaso! ijapokuwa alikuwa na Bwana Yesu kila siku alipokuwa akitenda miujiza mbali mbali lakini alipofufuka hakuamini mpaka alihitaji kuona alama za misumari kwenye viganja vyake ndipo Tomaso aka amini kuwa yesu amefufuka.

Labda Babu angekuwa mzungu labda skeptism za watu zingepungua! halafu kuna swala la imani, babu ni former priest na tiba yake inatokana na imani ya dini yake, hivyo Jenerali hakupaswa ku challenge imani za watu!

Pombe zake zinaonge wala sio yeye.
 
Jenerali shukuru kwa kupata habari iliyokuwezesha kuuza gazeti.

Kama dawa inaponyesha au haiponyeshi hilo wewe halikuhusu.

Wangapi waliokuwa mahospitalini miaka nenda rudi na hawajapona? kuna ubaya gani wakienda Loliondo?

Angegundua mzungu Jeneráli asingeongea haya ila kwa vile ni Babu Mwasapile basi imekuwa nongwa.
Mimi nadhani Jenerali anajaribu kutufunza kujaribu kufikiri kwa undani na kujihoji kuliko kujadili kwa namna ya kundi la nyumbu! Kwamba kwa sababu wote waliotangulia wamepita hapo, basi hapo ni salama, lol! Hajakataza watu kwenda huko, bali kama jamii tujihoji leo, kwamba je akija mwingine naye kwa staili hii na kutapeli wengi je mtasema nini? Kwa maoni yangu kuwe na mechanism ya kupima mambo kama haya kwenye society, vinginevyo mtu awaye yote asimnyooshee Shekh Yahya Husein kutoa ulinzi usio onekana kwenye ikulu ya magogoni!
 
Jenerali Ulimwengu ur nt correct .pastor Ambilikile Masapila was nt proud himself in any media bt still visitors are visiting him for his cure. science can nt interfere God will.

Next time weka kwa kibantu utaeleweka zaidi!
 
Babu amewafanya wale wanaozitegemea akili zao wenyewe kuuliza maswali ya kujikanganya wenyewe na hivyo kuwaweka wazi wanyenyekevu kwamba kiburi ni upumbavu.
Pia babu amenisababisha nikumbuke maswali ya prof, London(Dan brown) katika utunzi wake wa kitabu cha Engels and demons.
Prof kuna kauli aliyotoa kudai kwamba imani haikuokoi, dawa na vitu kama airbag hivyo ndivyo vinavyoweza kukulinda. Mungu hawezi kukulinda, upelelezi(intelligence) ndio inakulinda 'ENGLIGHTENMENT'.
Anaendelea weka imani yako kwenye kitu chenye matokeo ya kushikika, na punde science itaprove miungu sii chochote ila ni vinyago tu.
Alipoendelea kidogo katika muendelezo wa utunzi wake mara akajikanganya na kujidhihirisha kwamba yeye ni mfuasi na muumini wa imani kwa mungu. Alikuwa akiishabikia kauli ya Einstein "GOD DOES NOT PLAY DICE WITH THE UNIVERSE" na pia maneno ya michaelangels Moses "THE GOD PARTICLE THE DOOR OF PHYSICS" pia katika hicho kitabu mwishoni kulikuwa na maneno ya papa Pius xII "TRUE SCIENCE DISCOVERS GOD WAITING BIHIND EVERY DOOR"
Dan brown alijitahidi sana kumkwepa Mungu na Imani lakina hakuwaza maana ukweli ulikuwa ukiitenga dhamira yake kwa nguvu na unafiki wa kujipendekeza kwa walimwengu. Hivyo ni dhahiri kabisa kwamba wasomi weledi na science ya kweli inatambua uwepo wa Mungu na uweza wake unaovuka mikaka ya yanayoshikika kiakili(miracle)
Jenerali nae ni miongoni mwa wanaomkiri Mungu kwa njia ya imani huku akiukana uwezo wake.
Huko ndiko kujikanganya ninikojaribu kukuzungumzia kati ya wasomi(wanayansi) waongo.
.
 
Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa Ulimwengu, nachelea kusema haya ni maswali mepesi kuulizwa naye.Majibu ni kama ifuatavyo

1.Amekataa isiwe tested katika lab sababu hiyo siyo scientific medicine...nadhani unajua huwezi kuprove that God ana-exist in the lab
2.Hata kama dawa yake inatibu Ukimwi au Diabates ambayo ni magonjwa makubwa, siyo sahihi kusema basi watu wasichukue tahadhari ya kupata magonjwa mengine kama kipindupindu.....ni sawa sawa kama wewe uwe na dawa ya Malaria ndani basi ulale tu bila chandarua au bila kuchukua tahadhari yeyote ya kuumwa Malaria sababu dawa ipo

In general, kwa sababu ulizotumia nashindwa kuungana nawe katika doubts zako...


Mkuu nakuunga mkono
 
namuunga mkono Jenerari,huo upuuzi wa mganga wa loliondo ni sawa na DECI,watu tuliwaambia hapo nyuma DECI ni utapeli watu hawakusikia,inashangaza sana tena sana katika hizi zama za maendeleo watu wazima na akili zao wanadanganyika eti na miujiza ya dawa ya Loliondo,na kwa ujinga huo hata serikali nayo imeingia mkenge wa kumruhusu huyo mzee tapeli eti aendeleze tiba,jamani si hapo nyuma serikali ilipiga marufuku hayo mambo ya waganga wa kienyeji.Jamani msiwe wajinga hakuna dawa inyotibu ukimwi au kisukari hivi sasa ,dawa ni kufuata masharti.

pole kwa uwezo ulionao mdogo wa kutafakali mambo
 
He! kila siku babuuuuuu,babuuuuuuuuu, Kweli tutachelewa kuendelea.Waacheni wenye Imani zao waende,Wakipona Faida kwa Taifa wasipopona Hasara kwao.Wenyewe washawaambia ni masuala yanayohusu Imani zao,sasa kinachokuuma ni kitu gani wewe usiye amimi?Watu mnajaza Thred kibaaaaaaaaao,mawazo ni yaleyale. this things so bored.
 
Mussa Juma, Loliondo na Deusdedit Moshi, Dodoma

DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la 'Babu', huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi.

Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Sonjo iliyoshirikisha mamia ya watu. Akizungumza katika ibada hiyo, Mchungaji Mwasapile alisema Lengume ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza kumtibu.

Akizungumza na Mwananchi kanisani hapo, Lengume alisema baada ya mumewe, John Meneyi Lengume kufariki dunia mwaka 2002, aliamua kwenda kupima na kuonekana kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) lakini baada ya kutumia dawa hiyo alisema sasa hana tena virusi vya Ukimwi. Alisema kwa muda mrefu mama huyo alikuwa akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARV) katika Kituo cha Afya Didodigo wilayani Ngorongoro.


Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kupona kwa mama huyo, Dk Mbosha alisema: "Hiki kitu kilituchanganya sana, nakumbuka mimi ndiye nilimpima mwaka jana... ikabidi niwaeleze watu wa maabara Hospitali ya Wasso ili wafuatilie aliyempima awali huyu mama na nilimweleza aache kutumia dawa kwani hana HIV," alisema Dk Mbosha.

Dk Mbosha alisema alihamishiwa katika kituo hicho cha Afya cha Digodigo zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alimkuta mama huyo akiendelea kuhudhuria kliniki na kupata ARV pamoja na ushauri wa kulinda afya yake lakini alianza kuona mabadiliko makubwa ya afya yake na ndipo alipoamua kumpima tena.

Aliamua kumpima mwaka jana baada ya kuona 'CD4' (kinga za mwili) zake zinaimarika kiasi cha kutohitaji kuendelea kutumia dawa hizo za kupunguza makali.Aliamua kumhoji kujua siri iliyokuwa imejificha katika mabadiliko hayo ambayo alisema yalikuwa ya haraka haraka mno na ndipo alipomweleza kwamba alipata tiba kutoka kwa Mchungaji Mwasapile.


Lengume alisema licha ya mumewe kufariki, mtoto wao mmoja pia alifariki dunia lakini baada ya kutumia dawa ya Mchungaji Mwasapile, maisha yake ni mazuri na ana mtoto mwingine mchanga anayeitwa Evelyn ... "Namshukuru Mungu na Mchungaji Mwasapile sasa nimepona na ninaishi maisha mazuri tu."Alisema baada ya kuanza kuugua, mchungaji huyo, ndiye aliyemfuata na kumuomba amtibu akimthibitishia kwamba atapona maradhi yaliyokuwa yakimsibu.Hata hivyo, kitalaamu bado haijathibitika kupatikana kwa tiba wala chanjo ya Ukimwi.

Ushuhuda wa Mzee Mtaki

Mwingine aliyejitangaza kupata ahueni kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsibu baada ya kupata tiba ya mchungaji huyo ni aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mzee Ali Said Mtaki.Mzee Mtaki (81) ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mpwapwa katika miaka ya 1980, Mkuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida kwa nyakati tofauti, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mbunge wa Afrika Mashariki na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Usharika Mkoa wa Dodoma, alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kutetemeka kiasi cha kushindwa kutembea na kuzungumza vizuri.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Mtaa wa Nyerere Mjini Dodoma, Mzee Mtaki alisema tangu anywe dawa ya mchungaji huyo Jumanne ya wiki iliyopita huko Loliondo, sasa anaendelea kupata nafuu siku hadi siku.


Akiongea kwa kujiamini alisema sasa anajiona kama amepona na anaweza kuendelea na shughuli zake ikiwamo ya uwakala wa bima... "Si unaona nilikuwa natembea kwa shida, kuzungumza kwa taabu, sasa hali yangu ni nzuri nafanya kila kitu bila kusaidiwa."Akielezea safari yake ya siku mbili ambayo ilimfikisha kijijini Samunge, Loliondo anasema alifuatana na mkewe, Amina Mtaki ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na mgongo. Anasema naye pia amepona.

Anasema safari ya kutoka Dodoma hadi Samunge iliwagharimu Sh60,000 kila mmoja na baada ya kufika huko walikuta umati mkubwa wa watu ukisubiri kupata tiba hiyo. Anasema aliwakuta watu wa mataifa mbalimbali, Waafrika, Wahindi, Wazungu na Waarabu... "Watu walikuwa wengi na kila mtu na matatizo yake lakini Mchungaji alikuwa akiwasisitizia kwamba habagui watu na haangalii dini au uwezo wa mtu."


"Katika mkusanyiko huo nilibahatika kukutana na Askofu Thomas Laizer wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati akiwa amefuatana na mama wa kizungu. Nilikaa karibu na mama yule wa kizungu ambaye sikumbuki jina lake. Nilimshika Askofu Laizer mkono tukasalimiana na kuongozana naye kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile."

"Tulipofika kwa Mchungaji, Askofu Laizer akamwambia mchungaji kwamba ana wageni wake, hivyo mama yule wa kizungu akapewa dawa na mimi pia nikapewa na mke wangu akapewa pamoja na kijana wangu japo yeye hakuwa na tatizo lolote la kiafya."
 
Back
Top Bottom