Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

kulaleki...sasa kama kweli inaponyesha ukimwi basi kuna kiongozi flani watamkoma ....maana kanyongea kweli siku hizi kwa ajili ya hili dubwana sasa babau kama anaponyesha kweli basi
 
Kwa nini Mungu asiamuru kirusi cha Ukimwi kife duniani kote katika jina la Yesu?

Kwa nini Mungu anapenda kubembelezwa, na hela za dawa na sadaka analipwa?

Halafu Mr. Mungu ameshatawala miaka mingi mpaka anamkaribia Gaddafi, na matatizo ya health care system yake hayaishi, tumuondoe madarakani.
 
Je walijaribu kumpima huyu mgonjwa wa zamani kwa PCR (Polymerase Chain Reaction) kuona kama kweli hana virusi vya UKIMWI? Na je, alishawahi pimwa kabla kuona idadi ya virusi ili kudhihirisha kweli kwamba mwanzoni alikuwa na virusi kadhaa na sasa hana, maana kupanda kwa CD4+ cells sio issue ya kusema umepona, kwani hata wanaotumia hizi dawa za VVU pia CD4+ cells hupanda japo kwa rate tofauti kati ya mtu na mtu.

Na pia tunategemea mtu anayepata dawa za VVU ambaye vijidudu vyake havijatengeza usugu awe na undetectable viral load, ikiwa na maana ya kuwa japo virus wapo hasahasa katika cells zilizojificha ndani ya mwili katika maeneo kama vile ya ubongo n.k. lakini vifaa tulivyonazo kwa sasa vina limit ya kuona virusi, yaani wakiwa kidogo sana vifaa havitaona na hivyo vinasema huna kirusi.

Sipingi dawa hii, tatizo nina wasiwasi kama mchakacho wa kujua mtu huyu kama kweli amepona umefanyika vizuri. Na zaidi, je, ni kweli alikuwa na HIV? Isije ikawa hakupimwa sawa mwanzoni na akaanzishiwa dawa kimakosa.

Pia mashine huwa zina False Positives. Mungu atusaidie dawa ya mzee iwe inafanya kazi, maana naamini watu wengi wataacha kunywa dawa za hospitali na hivyo kutengeneza virusi sugu ambao kama mtu akimwambukiza mwingine tutakosa option za dawa.
 
Ebwana we! Nilikuwa nabisha lakini sasa naanza kuamini endeleeni kutulea ushuhuda.
 
Yaani natamani nibebe familia yangu yote wakanywe dawa hii, lakini ukata unikatisha tamaa. Nikienda peke yangu itakuwa noma. Nikiwachukua wote si chini ya laki sita zitatakiwa. Nifanyeje? Kuna maradhi yanayojificha, mtu unaweza kujiona mzima kumbe kuna kansa inakunyemelea au ..... Jambo la busara ni kunywa dawa hii, wenye uwezo NENDENI!
 
Je walijaribu kumpima PCR (Polymerase Chain Reaction) kuona kama kweli hana virusi vya UKIMWI? Maana kupanda kwa CD4+ cells si issue za kupona, kwani hata wanaotumia dawa hizi za HIV pia CD4+ cells hupanda japo kwa rate tofauti kati ya mtu na mtu. Na pia tunategemea mtu aliyepata dawa ambayo vijidudu havijatengeza usugu kuwe na undetectable viral load, ambapo japo virus wanakuwemo lakini vifaa tulivyonazo vina limit ya kuona virus, yaani wakiwa kidogo sana vifaa havitaona na hivyo vinasema huna kirusi. Sipingi dawa hii, tatizo ni mtu ni kama kweli mchakacho wa kujua kama amepona kweli umefanyika vizuri. Na zaidi, je, ni kweli alikuwa na HIV? Isije ikawa hakupimwa sawa mwanzoni na akaanzishiwa dawa. Pia mashine huwa zina False Positives.
Mtafute Dr Mbosha umuulize maswali hayo ya kitabibu...hata hivyo umeonyesha katika maelezo yako kuwa kuna progress changes kwenye afya ya mgonjwa,hicho ndicho muhimu na wagonjwa wanahitaji bila kujali kimetokeaje mkuu
 
Tanzania sasa itajulikana ulimwengu mzima na Mungu lazima ana malengo yake kuifunua hiyo dawa hapa tanzania nchi masikini. Ni bahati iliyoje mtanzania kufunuliwa dawa inayotibu maradhi sugu pamoja na ukimwi!! Tumwache Mungu aitwe Mungu.
 
Mtafute Dr Mbosha umuulize maswali hayo ya kitabibu...hata hivyo umeonyesha katika maelezo yako kuwa kuna progress changes kwenye afya ya mgonjwa,hicho ndicho muhimu na wagonjwa wanahitaji bila kujali kimetokeaje mkuu

Mkuu kwa sasa issue sio kumtafuta huyu dk. Mbosha, maana taarifa imeshatoka huwezi rudi na kuwaambia watu tofauti na taarifa ya awali na bado ukaeleweka vizuri na wote. Hii sio siasa ni afya ya kila mtanzania.

Ku declare mtu amepona bila uthibitisho makini kutaweza kuleta athari kwa wengine na wewe ukiwemo hasa ukizingatia vifaa vya PCR haviwezi kupatikana katika primary health care. Athari kubwa ni kama dawa hii haifanyi kazi na watu wameacha dawa hapa pana uwezekano mkubwa wa kutengenezwa kirusi sugu dhidi ya dawa tulizonazo. Maana kutotumia dawa hata kwa siku mbili tatu tu, kirusi anaweza akajitengenea usugu wa dawa husika. Then what? Hatutakuwa na option nzuri za first choice drugs kwa wagonjwa wengi.

Vitu vingine tusivifanyie kiherehere kwa kuwa vimetoka kwenye gazeti tena lililoandikwa na mwandishi asiye mtaalamu wa kipengele husika.
 
Mkuu kwa sasa issue sio kumtafuta huyu dk. Mbosha, maana taarifa imeshatoka huwezi rudi na kuwaambia watu tofauti na taarifa ya awali na bado ukaeleweka vizuri na wote. Hii sio siasa ni afya ya kila mtanzania. Ku declare mtu amepona bila uthibitisho makini kutaweza kuleta athari kwa wengine na wewe ukiwemo hasa ukizingatia vifaa vya PCR haviwezi kupatikana katika primary health care. Athari kubwa ni kama dawa hii haifanyi kazi na watu wameacha dawa hapa pana uwezekano mkubwa wa kutengenezwa kirusi sugu dhidi ya dawa tulizonazo. Maana kutotumia dawa hata kwa siku mbili tatu tu, kirusi anaweza akajitengenea usugu wa dawa husika. Then what? Hatutakuwa na option nzuri za first choice drugs kwa wagonjwa wengi. Vitu vingine usivifanyie kiherehere kwa kuwa vimetoka kwenye gazeti tena lililoandikwa na mwandishi asiye mtaalamu wa kipengele husika.
Mkuu ushauri wako ni mzuri sana,lakini kwa kuwa mimi si tabibu ndio maana nikakuambia maswali yako huyu dr Mbosha angeweza kuyajibu kifasaha kama ametumia PCR au la..suala la ugonjwa ni la mtu binafsi na daktari ndio maana hatusikii mengi kutoka kwa wagonjwa.magazeti ni media tu haihitajiki mwandishi kuwa na weledi wa fani fulani yeye anaripoti matukio na wasomaji wanafuatilia kama ambavyo wewe kwa nia yako nzuri na weledi wako wa kitabibu ulitakiwa utafute ukweli huko na kuja kutujuza sio kubeza
 
Mh! Hapo nilipo red hiyo ni point muhimu sana, tuache ushabiki,tuache mambo ya imani utaalam unahitajika jamani.
 
Mh! Hapo nilipo red hiyo ni point muhimu sana, tuache ushabiki,tuache mambo ya imani utaalam unahitajika jamani.
gazeti halijaripoti mgonjwa kuacha dawa...ila daktari alimshauri aache kutokana na kuwa kinga yake ipo juu na haihitaji tena dawa za kurefusha uhai
 
Isingekua ufisadi unaotumaliza basi Bongo ingepata bonge la Title, swali moja tu, vp redio Khery wanaendelea kubisha? ndio vizuri wasitumalizie dawa!!!! sio jini lile ni Mungu!!!!
 
Mi nawaambia mkatae msikatae mkubali msikubali kwa macho yangu nimeona waliooenda kwa babu wamepona hao ni watu kadhaa na walikuwa na magonjwa unayoyaona kwa macho.

Mmojawapo wa waliopona Ukimwi kaandikwa katika gazeti la mwananchi la leo, ukurasa wa kwanza!
Asiyeamini halazimishwi. Mwenzangu mmoja kapona kisukari kabis kwa dawa ya babu!
 
Ozzie77 ningekuwa Dr ninaeipenda fani yangu ningetafuta mgonjwa mmoja wa hiari au hisani(wapo tele kila mahali) ningempima na pia kwenda nae kwa babu apate kikombe then niangalie maendeleo yake periodically then niwajuze watz wenzangu nilichoobserve....ni research tosha bila kujali matokeo yatasemaje.hapo nitakuwa nimepata jibu na kupambanua science na imani...kuna maajabu tunaona watu vijiko vinawanasa mwilini mbona madaktari hawatuelezi science yake hapo?Usisubiri serikali fanya juhudi zako binafsi uisaidie serikali yako
 
Mmojawapo wa waliopona Ukimwi kaandika katika gazeti la mwananchi la leo, ukurasa wa kwanza!
Asiyeamini halazimishwi. Mwenzangu mmoja kapona kisukari kabis kwa dawa ya babu!
Pia leo mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya Ngorongoro(Wasso hospitali ) amekiri kuwa kuna wagonjwa kadha ambao walikuwa wanaugua UKIMWI na sasa baada ya kutumia dawa ya babu wamepona na vipimo vimethibitisha hivyo!.
Sasa waliokuwa wanataka uthibitisho wa kimaabara wameupata, sijui watatunga sababu zipi tena za kummwaga babu!!
 
Mkuu ushauri wako ni mzuri sana,lakini kwa kuwa mimi si tabibu ndio maana nikakuambia maswali yako huyu dr Mbosha angeweza kuyajibu kifasaha kama ametumia PCR au la..suala la ugonjwa ni la mtu binafsi na daktari ndio maana hatusikii mengi kutoka kwa wagonjwa.magazeti ni media tu haihitajiki mwandishi kuwa na weledi wa fani fulani yeye anaripoti matukio na wasomaji wanafuatilia kama ambavyo wewe kwa nia yako nzuri na weledi wako wa kitabibu ulitakiwa utafute ukweli huko na kuja kutujuza sio kubeza

Nina wasiwasi kama huko anakoishi Dr. Mbosha kuna PCR wala ELISA. Nafikiri kutakuwa na rapid kits ambazo zinatumika kwa preliminary screening tests. Lakini nyingi ziko reliable kwa kiasi kikubwa. Wasiwasi wangu ni kama kweli huyu mama alikuwa ni mgonjwa na sasa amepona kabisa. Kudhibitisha hilo inabidi vipimo vyake vya zamani vipatikane na afanyiwe pia vipimo vya uhakika kwenye maabara kubwa.
 
Ni kweli jamani mungu amesikia kilio cha watanzania, acha watu waponywe na magonjwa sugu na babu wameteseka na vitu vingi kwa muda mrefu njaa, umeme, maji na huduma zingine za kijamii.
 
Back
Top Bottom