Inadaiwa kuwa mizizi ya Kitanzaniya ina uwezo wa kutibu baadhi ya maradhi ambayo ni tishio kwa uhai wa binadamu kama kisukari, UKIMWI....Sasa Loliondo kimekuwa ni kituwo cha rufaa, kwani baadhi ya wananchi toka sehemu mbalimbali, viongozi wa vyama na serikali wamekwenda kwa Babu kuonja maji yanayoaminika kuwa yakichanganywa na mantindili watu huponywa kwa magonjwa yanayo wasibu.
Kwa mantindili anayoyatowa Mchungaji kwa kipimo cha kikombe kimoja na kuagiza kuwa imani yako imekuponya enenda kwa msaada wa Mola, huko ndiko tujenge hospitali ya rufaa ili tuache kuruka kwa ndege kwenda ulaya na Asiya ili kupata tiba. Kama hapatoshi viwanja tuelekee hata Sumbawanga.