Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.


Pole na msiba MKUU.
 
Mti anaoutumia Babu wa Loliondo unaitwa Carissa edulis na umekuwa published na baadhi ya scientists wa Kikenya March 2006 (Journal of Ethnopharmacology, Volume 104, Issues 1-2, 8 March 2006, Pages 92-99).
 

Attachments

Babu hatibu kifu tuelewane...na waliofariki wakati wao umefika..'kul nafsin dhaikatul maut'.
 
sasa kama babu hana tofauti na hospitali kuna haja gani ya kuhangaika na folenna shida ya usafiri kwenda kwake?
 
Ndugu yangu kifo ni kitu ambacho Mungu alimzawadia kila mtu. Hatujui siku wala saa. Inauma sana tunapoondokewa na wapendwa wetu, lakini daima tukumbuke kuwa baada ya adhabu zote ambazo Mungu alitoa pale Edeni, mwisho ni kifo, hakikwepeki. Muweni na uvumilivu wakati huu, kwani kwa sisi wakristo (hata waislam nadhani maana sina hakika), tunajali sana kuponya roho na kwenda kwa Muumba wetu. Kama hajapona mwili, basi Mungu kamponya roho na sasa anafurahi kwake.
Mlikuwa na Imani hadi kumpeleka kule, lakini kumbuka sote ni wa Mungu na hatuna budi kuondoka duniani wengine nao waje waishi.

RIP
 

Bikira Maria? Who is she? Au ndo yule tunaambiwagwa malkia wa mbingu? Yeremia 7:18.
Sorry, just being curious!
:lol::lol::lol:
 
poleni sana rip ahadi yake ilikuwa imefika kumbuka''kila nafsi itaonja mauti''.
 
anachosema ni kuwa dawa ya babu ime speed up kifo cha shemejie. Kufa kila mtu atakufa hakuna mjadala hapo. si vibaya tukahabarishana na yatokanayo na dawa ya loliondo. kuna mazuri na machungu. Kwa hiyo wale ambao hawajaenda waweza kutafakari zaidi.

Na mimi ninachoshangaa ni kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha babu anatibu wagonjwa karibu 6000 kwa siku. Wanaopona hawajitokezi, wanaopata madhara ikiwemo kufa ndo tunapata taarifa (nafikiri less than 10 kwa siku). Watumiaji wengine wa dawa hiyo wapo wapi?
 
duh! Pole sana ndugu yangu. Hata usipoenda kwa babu kufa lazima it is just a mater of time. Sema tu mi ningeishauri serikali kuwa baada ya kuibariki tiba ya babu na kusema kuwa ule mti ni sumu kali tena unatumiwa na wawindaji kupaka kwenye mishale. Basi waanze kundaa pesa ya kuwalea yatima na wajane.
 
RIP. Kikombe cha Babu haiongezi siku za kuishi duniani, bali kinasaidia kuponya ugonjwa
 
kuna watu mko kny denial-hio dawa haifanyi kazi period.
 
Samahani kuuliza vizuri, ulimpelekeka, ina maana ulienda na wewe?
kama ulienda ulikunywa?
kama ulikunywa unajisikiaje?
lakini pia naomba ukumbuke, kama walivyosema wengine, kifo lazima, hata unywe sufuria la babu.
pili naomba ujue kuwa wanaoenda na wenye stories ni wengi sana, za kupona, kupata nafuu na za kutokupona. Ila bahati mbaya hawaji hapa JF kuposti mambo yao, ni watu wako bize na maisha yao,
 
Kuna gazeti moja la mwananchi wiki ilopita kama sikosei kulikuwapo ushuhuda wa mama mmoja. Hebu google ucheki!
 
Mkuu pole sana maoni yangu ni kuwa hakuna awezaye kuzuia kifo lakini kuna misingi au kanuni zinazokubalika za matibabu,huyu babu ni msanii ambaye atasababisha vifo visivyotarajiwa ,tuwe makini tunywe kikombe na dawa za hospitali tuache ushabiki.
 
POLE KWA KUMPOTEZA MPENDWA WAKO! LAKINI PIA WANGAPI WANAFIA MAHOSPITALINI? BABU ANATIBU "MAGONJWA" SIYO "KIFO" LAZIMA TUJIFUNZE KUTOFAUTISHA HIVO VITU VIWILI MAAKE IMEANDIKWA"BINADAMU LAZIMA ATARUDI MAVUMBINI ALIKOTOKA" SO MUDA WA KUFA UKIFIKA UTAKUFA TU HATA KAMA UMEWEKEWA MASHINE ZA OKSIJENI, KUBADILISHIWA FIGO etc! ENYI WATANZANIA NENDENI MKANYWE DAWA!:hatari:


 

kama babu anatibu tulitegemea huyu ndugu apone kansa alafu afe kwa ajali au tatizo jingine,dawa ya babu ni utapeli tu.
 
Bikira Maria? Who is she? Au ndo yule tunaambiwagwa malkia wa mbingu? Yeremia 7:18.
Sorry, just being curious!
:lol::lol::lol:

huo ni mtego mwingine wa kupelekea loliondo school of thought!

beware brothers and sisters

Glory to God
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…