Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kusema DAWA ya BABU inatibu kwa jina la YESU uko tuendako siko, BABU yeye kaoteshwa na MUNGU wake kuhusu hiyo dawa sasa MUNGU wake ni yupi hapo sijui. Maana kuna miungu mingi duniani, sasa wewe unayeumwa amua mwenyewe kuamini kuwa mungu unayemuamini wewe ndie aliyemuotesha BABU hapo utapona.Lakini kusema MUNGU YEHOVA, NIKO AMBAYE NIKO ndie aliyemuotesha huo ni mjadala wa kibiblia zaidi ukiusubiri muda ili mjadala uanze hadi upite ndio upate matibabu kwa babu unapoteza muda. Amua moja kwenda au kutokwenda kwa mujibu wa Imani yako.
 
Yaleyale tu,maji ya baraka ,mishumaa,udi ,mafuta ya mizeituni,kuungama kwa padri na mapokeo mengine ya kimagharibi ndio yanayotusumbua angekua mkatoloki angekaa kimya
 
kama ni kwa jina la Yesu angewahubiria watu waokoke sio tu kupewa kikombe cha dawa na kuondoka bila wokovu.pole uliyedanganyika. Yesu wetu anataka watu wote waokoke na waijue kweli bwana.

Mbona hatujasikia mahubiri yoyote pale! PALE YESU HAYUKO .IKO MIZIMU YA KWAO NDIYO INAYOTIBU!

Hivi Yesu alikuwa anawaambia watu waokoke au aliwaambia "nenda na usitende dhambi tena"? Kuokoka kwenyewe ni huku kwa Mwingira? Kakobe? Lwakatare? Give me a break,kuokoka ni usanii tupu.
 
Ulimwengu unahaha unaposikia kuwa Tanzania ina Mantidili yanayodaiwa kutibu magonjwa sugu, na kuifanya serikali ya Watanzania kuwa na kiwewe cha kukabiliana na msongamano wa watu unaoelekea kwa Babu Mchungaji Ambilikie Mwasapile mwenye tiba iliyopatikana kwa njia ya ndoto huko Loliondo Arusha.
Ni rai yangu kuwaomba wale wote walikunywa dawa ya magonjwa sugu kama saratani, kisukari, kifua kikuu...na hata UKIMWI kwa Babu Ambilikile katika kijiji cha Samunge, huko Loliondo, wajitokeze katika hospitali zetu popote pale nchini ili kupima afya tena ili kubaini maradhi yaliyowasibu kabla ya kunywa dawa hiyo.
Mchungaji Mwasapile, kwa kipindi hiki ameteka fikra za watu wengi kutokana na huduma yake ya kuwanywesha wagonjwa kikombe kimoja cha imani na chenye dawa inayodaiwa kuwa ni tiba kwa maradhi kama hayo.
Tuuambie ulimwengu kuwa hapa Tanzania yupo tabibu wa magonjwa sugu kama hayo, lakini njia pekee ni hao wenzetu walikunywa kikombe kimoja cha mantindili wajitokeze kupimwa kisayansi, hiyo ndiyo itakuwa njia pekee ya kuvunja utata wa ubora wa dawa ya Babu wa Loiliondo. Ni hayo tu! :behindsofa:
 
Miss, hata wakati wa Yesu watu walikimbilia miujiza na wakati mwingine mikate na vipande vya samaki. cha msingi ni wewe mwenyewe kulijua, kuliishi na kulitenda Neno.

Yesu aliwaambia nini wanaokimbilia miujiza? Je, haukusoma maandiko? .........si kwa sababu mliziona zile ishara mkaamini, bali kwa sababu mlikula mkashiba. Huoni kama onyo hilo laendelea hata leo hii kwa babu? Nyie mwamtafuta babu si kwa sababu mliiona ile miujiza mkamwamini Yesu aliyempatia mafunuo (kama anavyodai), bali kwa sababu mlikunywa kikombe mkadhani mmepona. Kristo anasemaje kwenu? Amin, nawaambieni, kuna kikombe kinachofaa, nacho ndicho kile kiletacho uzima wa milele. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake. Msiifanye migumu mioyo tenu.

Vaa full armour of God upate kumpinga shetani. Neno likujae moyoni mwako, AMEN.

Mungu akubariki miss Judith
 
Yesu aliwaambia nini wanaokimbilia miujiza? Je, haukusoma maandiko? .........si kwa sababu mliziona zile ishara mkaamini, bali kwa sababu mlikula mkashiba. Huoni kama onyo hilo laendelea hata leo hii kwa babu? Nyie mwamtafuta babu si kwa sababu mliiona ile miujiza mkamwamini Yesu aliyempatia mafunuo (kama anavyodai), bali kwa sababu mlikunywa kikombe mkadhani mmepona. Kristo anasemaje kwenu? Amin, nawaambieni, kuna kikombe kinachofaa, nacho ndicho kile kiletacho uzima wa milele. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake. Msiifanye migumu mioyo tenu.

Vaa full armour of God upate kumpinga shetani. Neno likujae moyoni mwako, AMEN.

Mungu akubariki miss Judith

amina mpendwa.

namshukuru sana Mungu kwa kutujalia neema ya kulinena neno lake hapa kwa ujasiri bila kulionea haya licha ya upinzani mkali toka kwa wafuasi wa babu.

hakika licha ya kwamba sie tu sehemu ya kundi dogo, lakini hatimaye kwa uwezo wa Bwana, neno litashinda na litasimama daima

Glory to God
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
 
Pole sana mkuu, Mungu awape faraja yake ilokuu. pia senks kwj ushuhuda, na kama kuna m2 alienda kwa babu akapona na aseme sasa, aweke na ushuhuda wa vyeti kabla na baada, habar za kuambiwa si ziamini, nataka nione kwa macho.
 
Pole sana mkuu, Mungu awape faraja yake ilokuu. pia senks kwj ushuhuda, na kama kuna m2 alienda kwa babu akapona na aseme sasa, aweke na ushuhuda wa vyeti kabla na baada, habar za kuambiwa si ziamini, nataka nione kwa macho.
Sio lazima uende kwa babu.
 
Ndo huu msiba wa mke wa ndugu yangu pia au? maana naye alienda na shemeji kwa babu kwa matatizo ya breast cancer, akapata kikombe ila majuzi ametutoka ndo twasafirisha msiba kesho kwa maziko nyumbanii..Jamaniiiiiiii
 
Asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa Mwisho TZ kumwamini huyu babu.
 
AIMEANDIKWA KATIKA BIBLIA 'amelaaniwa amtegemeae mwanadamu"
 
Hakuna mfuasi wa babu kwani babu si imani wala itikadi. Yeye anakupa kikombe unakunywa na kuondoka; hakuna anapokuhubiri eti uingie kweye imani yake ya lilutheri.
Babu anasema yeye si mganga, bali kinachotibu ni neno la Mungu ambalo Mungu mwenyewe ameliweka kwenye huo mti; yeye ni wakala tu wa kukunganisha na hilo neno. Na ameelekezwa kuwa dawa ataitolea hapo na itanywewa hapo. (hii inaondoa uchaachuaji pia)
Kuhusu masharti, naona hiyo imeshaelezwa vizuri zaidi - hata Yesu aliponya kwa masharti.
Wakatoliki wanaukiritimba wa kutambua matukio kama haya na mwisho wake ni kushindwa kutumia kwa manufaa matukio ya namna hii. Kama mtakumbuka kabla ya mauaji ya Rwanda, kuna mtu alitokewana Bikira Maria na akaelezwa kuwa naona damu nyingi inamwagika hapa, Bikira Maria akamweleza kuwa watu wamrudie Mungu nk. Lakini kanisa katoliki lilichelewa sana kuutambua muujiza huo na kuufanyia kazi hadi mauaji ya kimbari ya Rwanda yalipotokea na watu wengi kuuawa ndani ya kanisa alimotokea Bikira Maria; ndipo kanisa liliposhtuka - oo kumbe huo ndio ujumbe aliokuwa ameuleta Bukira Maria! Ujumbe ulisema watu wamrudie Mungu, kama kanisa lingetambua mapema na kuwahubiri sana watu kuwa Bikira Maria ametokea mahali hapa na kuleta ujumbe kuwa tumrudie Mungu; watu wasingeuana kwa kiasi hicho!
Nashauri watu wenye magonjwa sugu wakanywe kikombe kwa babu maana hatujui kikombe kitakuwepo hadi lini.
Suala la tiba kuwa ya muda mfupi - hata Yesu alihubiri kwa miaka 3 tu!
 
Eti babu anaponya!?! Hu ni ubwege wa kiwango cha kusikitisha.
Babu haponyi! kinachponya ni neo la Mungu lililowekwa kwenye mti huo; yeye amepewa kazi ya uwakala wa kuunganisha neno hilo na wewe.
Jamani kila asubuhi saa moja, babu anakuwa na briefing; anaeleza mengi na kuruhusu maswali.
Watu wanapona, sasa wewe isiyeamini kalagabaho; au huumwi. Ungekuwa na pumu kwa mawingu haya unapumua robo pumzi, usingeacha kwenda kwa babu!
Lakini tusishangae, hata wakati wa Yesu, Mohamad SAW na manabii wapo watu tena wengi ambao hawakuamini!
 
Pole sana mkuu, na wala usijali maana Mungu alimpenda mtu wako kuliko sisi....Aidha, ieleweke tu kwamba kwenda kwa Babu na kupata dawa yake sio guarantee kuwa hautokufa au utapona....!
 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania Kadinali Pengo

Kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana alielezea msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu tiba ya Loliondo inayotolewa na Mchungaji Ambikile Mwaisapile kuwa kabla mtu yeyote hajapata tiba hiyo lazima ajiulize maswali manne kwanza kabla ya kuamua kuitumia.

Akihutubia katika Ibada ya Jumapili katika Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoa ya Mbezi Luis, Paroko wa parikoa hiyo Padre Vivian alisema, "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo.

"Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu," alisema.

Swali la pili alilotaka watu wajiulize ni kuwa tiba inayokuja kama muujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti? Swali la tatu alilolitaja Paroko huyo ambaye ni Padre wa Shirika la Wakalmeli ni kuwa, Kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanyekazi Dar es Salaam na kwingineko?

Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

"Ukiisha jiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata unawea kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo. Hivyo ukiliona basi limeegeshwa katika stendi ya Mbezi au mahali pengine na ukasikia wapigadebe wanaita Loliondo Loliondo Loliondo, basi panda ukapate kikombe cha Babu," aliongeza kusema.

Katika siku za hivi karibuni Mchungaji Mwaisapile ameutikisa Ulimwengu baada ya kutangaza kuwa anatibu magonjwa sugu kwa kutoa dozi ya kikombe kimoja cha dawa ya kienyeji kwa gharama ya shilingi 500/ kwa Watanzania na Tsh 1,000/= kwa wageni.

Viongozi mbalimbali wa siasa na dini wakiwemo maaskofu wa madhehebu ya Kikristo wamekuwa wakitoa ushuhuda wa ukweli wa tiba hiyo na kuwashauri wananchi wenye magonjwa sugu kwenda kijijini Samonge mkoani Arusha kupata tiba.

Hata hivyo kwa upande mwingine, baadhi ya viongozi wa makanisa hayo akiwemo Askofu Zakaria Kakobe wa kanisa la FGBF na Mchungaji Christopher Mtikila wamekuwa wakiipinga vikali tiba hiyo.

Source: mbs
Mwenyewe umesema aliyenena hayo ni Padre vivian wa Shirika la wakarmeli, sasa Kardinali Pengo anahusikaje na mawazo binafsi ya Padre huyo mwenye haki ya kutoa maoni kama Mtanzania yeyote anavyoruhusiwa au Padre huyo ndiye msemaji Rasmi wa Jimbo la Dar Es Salaam na Askofu wa Jimbo hilo?
 
mhh suala la kifo haliwezi kubadilishwa kwa kwenda kwa babu,wala haimanishi kwamba uponyaji wa babu siyo wa kweli au ni wa kweli.Unaweza kupeleka mgonjwa kwenye best hospital na kwa best doctor lakini bado mgonjwa wako akafariki.
 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania Kadinali Pengo


Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

Source: mbs

Kwani nyakati za sodoma na gomora ilikuwaje?
Hao waliokuwa wanaishi huko waliumbwa na nani -si Mungu?
Je nani aliwangamiza - si Mungu?
sasa unasemaje; Mungu aliwaumba na kisha kuwaangamiza?
Mapadri acheni unafiki - wakati mnasema hivyo kwa siri mnakwenda kunywa kikombe na mnawapeleka ndugu zenu kunywa kikombe. Juzi niliona gari la archdiocese of Arusha kwa babu - ok labda lilikodishwa!!!!
 
Back
Top Bottom